
Kaka Nchuzi,
Napenda kutuma salamu zangu za dhati kwa wadau wote popote pale mlipo. Mimi Shwari hapa Madridi Spain. Kwanza kabisa kwa kujitambulisha, naitwa Lomagundi Abdalla Nchinmbi toka kule nachingwea. Kwa hivi sana naishi Madrid nikitafuta maisha.
Kwa kifupi ni kwamba, sijazaliwa katika utajiri. Baba yangu hana majumba mbezi, hatuna akaunti yoyote popote duniani. Hata kutuma hela nyumbani inakuwa shida kwa maana wazazi wangu hawana elimu, nikimpata mtu anaenda nyumbani nampa kamzigo kangu kadogo kunipelekea pengine mara moja kwa mwaka au nikibahati kwenda, wazazi wanafunga mkanda hadi nirudi tena.
Elimu yangu ni ndogo, niliacha shule form two Kutokana na ukosefu wa kifedha. Nikaanza kuhangaika kutafuta ajira bila mafanikio. Nimechuuza sana kariakoo, nikaona maisha hayana mwelekeon nikachanja zangu Sauzi-Afrika na hatimaye kuzamia meli ya Kigiriki 2001 na sasa nipo Madrid Spain.
Kutokana na tabia ya unyenyekevu na uvumilivu, nilibahatika kupata kazi ya SUPEVISA ya upishi kwenye meli inayosafiri kwenda Arabuni. Nashukuru mungu kwa kunipa namna ya kujisaidia bila ya elimu.
Ila ninashangazwa sana na tabia zetu wabongo. Tunatabia za ajabu sana, hatupendani wala hatutaki maendeleo ya wenzetu; tunajaribu kila namna ya kuchafua kizuri mwenzetu anachokifanya. Tabia zetu za gengeni tunazipeleka kila tunakokwenda. Tunachekwa na waafrika wenzetu.
Nilisaidia kijana mwenzangu kupata kazi hapa Hispania, bahati mbaya kampora mwajiri wake na kutokomea, bahati mbaya kakamatwa baada ya siku tano. Mimi kama niliye commend, nikawa hatiani, ila kutokana na tabia yangu safi wengi walionifahamu wakanitetea na kuiponyoka gereza na kurdishwa Bongoland.
Kaka Nchuzi, katupa namna ya kuweza popote tulipo tunapata habari za nyumbani kila dakika, matokeo yake wengi wanavijiwe wanageuka kumponda, kutumia lugha chafu sana.wengine kumuita fisadi, rangi mbili, na mengineyo mengi tu.
Dada yetu Manka Mushi pamoja na Jovinata Kileo kwa ujasiri waliyatoa yalikuwa yanawakera, ili tu wapate usaidizi lakini wakageukiwa na kumiminiwa matusi ya kila rangi na kopo. Wakaitwa wachaga bwana. Ingawa ya Manka yalikuwa yamewapita wengi kimo, lakini ni kawaida mtu kuwa na vigezo. Ukishindwa, basi tulia.
Swala la Jovinata lilinitia huruma sana kuona kwamba mapenzi yake kwa mtu mwingine na kujaribu bahati yake inakua kosa mnamtumia barua 6000 za matusi !.
Kunradhi waungwana, tunaelekea wapi, wapi jamani? Mimi sina elimu kama walivyo wengi wenu ambao baba zao wanaisaidia serikali kufanya mahamuzi lakini nadhani nina busara kidogo kutokana na umasikini wangu.Nisipoamka kufanya kazi, kwa lugha nyingine nimeanka kufa, kwa sababu bila jash langu sina cha kula.
Kaka yangu Chibiriti kawaletea habari mpya ya magari ya gesi. Basi mkaponda bila huruma au kwa sababu ni mmakonde kama mimi? Kisa hasa cha kumpondea ni nini? Bei ya mafuta imepanda, kwa hiyo kila njia inayowezekana kutunza mazingira na kupunguza matumizi lazima tuitafakari, lakini yote mkaona kinyesi mkaponda. Kwani haya ndiyo maendeleo. Na Chibiriti kama mtanzania huu ndo mchangowake kwa nyinchi yake " Chibiriti, I am praudi of you my brothezer"
Kaka Mashaka, katuletea habari za busara sana na kutupa changamoto sana ili tuwe na upendo baina yetu kwa ajili ya amani, basi wengi kumuona kijana mdogo anajitahidi hapo mkajaribu kubomoa; wivu na hasira zikatupagawa na kuanzza kuchafua mazingira. Badala ya kukubali amewashinda, mnakataa na kuponda bila ya kutaka kujua kwamba mafanikio yake yamekujakujaje?
Ray-C mlimuita changudoa, hana lolote, kwani nyinyi wapondaji mnanini zaidi yake? yeye ni supasta. Ni maarufu.
Nyoshi El – Sadaat mlipomuona, kitu cha kwanza mukaanza kuponda mkorogo wake na wigi, kwani aliwakataza kutokujichubua? Huo ni uhuru wake. Kama ulivyo uhuru wenu kuponda kazi za wenzenu.Nyoshi anapendwa sana na Watanzania walio wengi, kwani ni mmtumbuizaji sio wa kawaida. Hata hapa miziki ya Nyoshi inawaacha wa Hispania hoi. Sasa kuponda wa nini. Basi mkiamua kumponda miziki yake msisikilize.
Nadhani tutafurahi nchi yetu ikibaki pori la wafu, ilhali wachache wa mbezi wanawatuma watoto wao kutafuta (privte pailoti lisence) maisha mazuri ulaya. Watanzania, jamani tuwe wastaarabu. Tuacheni majungu tushirikianeTumieni nguvu za kulumbana kuipinga ufisadi unaoumaliza nchi yetu.
Au tumlete Barak Obama kuja kutumwagia elimu kuhusu change? Tuigeni wakina Mashaka na busara zao ili upendo utawale katika jamii yetu, hawa ndio wanamabadiliko wa jamii. Tuacheni unafiki, Na pia natumai kuanzia leo hakuna wivu kwa kaka Nchuzi
Asanteni wadau Wote popote pale Mlipo,
na karibuni Madrid
Lomagundi Abdalla Nchinmbi
Lomagundi Abdalla Nchinmbi


asante kaka.
ReplyDeleteAsante ACHIMWENE umejieleeza saanaaa utumbo mtupu.. hebu kanywe maji upumzike kidogo
ReplyDeleteNgoja waamke waosha vinywa, yaani gazeti lote hili, kwanza umejieleza uliondokea Posta ya zamani badala ya Kipawa, halafu unawaamsha wajuaji, Misupu, huyu kajipalia makaa. Shauri yako
ReplyDeleteWEWE NCHIMBI KWELI ULIVYOSEMA NI SAHIHI KWAMBA HUNA ELIMU YA KUTOSHA...BLOG SI MAHALA PA KUPATA MKE WALA MUME NA SI PAHALA PA KUPATA ELIMU BLOG ZOTE ZA KILA KONA NI SEHEMU YA POLOJO POLOJO KAMA VILE KWENYE VIGENGE VYA KAHAWA NA KWA SABABU WATU WANA UHURU WA KUONGEA WANACHOTAKA KUMBE UNAPOWEKA COMMENT YAKO EXPECTS NEGATIVE AND POSITIVE COMMENTS USIKATISHWE TAMAA NA MATUSI NENDA AGALIA BLOG HATA ZA LETS SAY SPORTS LABDA YA NEW YORK YANKEES UTAKUTA KUNA MATUSI PIA. SASA IWEJE LEO MTU ANAMTAMANI MTU ASIYE MJUA AKIPENDA AOANE NAYE WATU WASITUKANE? MASHAKA HAMJUI HUYU BINTI NA HUYU BINTI KAMWONA MASHAKA HUMU BLOGINI KAMPENDA HIYO HAINA UBAYA LAKINI UNATAKIWA KUJUA KUNA WATU WATAICHUKULIA KWENYE NEGATIVE SIDE SO THEY HAVE A RIGHTS TO CURSE! YOU DON`T WANT PEOPLE TO TELL YOU WHAT THEY FEEL STOP PUTTING CONTROVERSIAL COMMENTS.MICHUZI MWENYEWE MWENYE BLOG KISHA PATA MITUSI KIBAO HAJAIFUNGA BLOG YAKE IJE KUWA WEWE NCHIMBI,KIBILITI, RAY C AMA JOVINATA? WHEN YOU POST ANY KIND OF CONTROVERSIAL ISSUE YOU WILL CONTINUE TO GET HARSH COMMENTS
ReplyDeleteHi Bro Michu,
ReplyDeleteHahaa huyu Nchimbi vipi mbona haeleweki,yaani hoja yake imelenga sana kumtongoza Jovita kwa kiasi fulani Manka Mushi si haseme tu wazima watamuelewa tu kwa ni watafutaji...!!!.Eti ana mtetea Mashaka...hivi hujui kuwa huyo ni mumwe mwenza wewe Nchimbi au hukusoma vizuri post ya kwanza ya Jovita juu ya hisia zake kwa Mashaka.Nakushauri uwe mu-wazima na bahati picha umeishaituma waambie tu direct watakuelewa mzee....wacha kuzunguka mbuyu...........!!!!.
Thanks brother for your nice suggestions also I salute you for the hardships you have gone through and how you managed to fight back till the point your are now! Big up bro! Nikija suala la watanzania kupendana, ni kweli inabidi tupendane, I agree with you 100%. Ila naomba nitofautiane kitu kimoja na wewe, when you post somthing on the blog, newspaper, or anywhere in public, expect positive and negative comments! We human beings are not the same, even the five fingers of the same hand differ in size and length. I'm very concerned with the situation of my dear sisters Manka & Jovi, ni kweli kuna watu walitukana may be kwa sababu ya wivu/chuki au kutokuwa na qualifications,etc but on the other side I believe all the mails the received sio zote za matusi, at least asilimia 5 should be genuine mails, with really good intentions. Kama kaka yetu Michuzi anaweza kusoma mails 2000 kwa siku na kuweza kuchambua pumba na mchele, na wao they can go through those mails carefully, I'm optmistic at they end they will emerge out with something! and as you know something is better than nothing. Kaka yangu huu ni mtazamo tu! God bless my country, Tanzania!
ReplyDeleteMdau,
Sweden.
Dah Kaka nchimbi ningevumilia lkn utovu wa adabu juu ya wazazi wako sitokuwacha na mavi lazima nikunawishe, inakuwaje unawadharau kiasi hicho hata kama hawakwenda shule ina maana hata hiyo posta ya kuchukulia pesa na kupata usaidizi kwa wafanyakazi waposta na kupata fedha zao pia elimu hiyo wamekosa? nilikuwa tu nikisikia wazamia meli akili zao ni pumba lakini lkn leo nimeamini endelea kuuza vumbi hapo spain sio upishi kama unavyodanganya.
ReplyDeleteunachekesha kweli wewe nchimbi umeibukia wapi na maelezo yote hayooo?!!! wakati wa hizo hoja za watu wote hao kwa nini haukutoa maelezo yako? hayo ni matumizi mabaya ya muda. Bro Michueee maelezo kama haya yasome tu mwenyewe kisha yadiliti
ReplyDeleteHAYA KAKA NCHIMBI,,UMELIWASHA MWENYEWE..NGOJA WA2 WARUDI KUTOKA KWENYE BOX,,HALAFU UTAONA STRESS ZAO WATAKAPOZIMALIZIA KWAKO...OOKK..??
ReplyDeleteHa ha ..Fani ya utongozaji, you are genious man, lakin umefuja ndefu sana kukuamini, ungeachia pale pale penye resume yako, halafu ukamtetea chibiliti, lakini ulipoanza kuongelea Jovinata, Ray c, na wengine UMEFUJA..lakini good try.
ReplyDeleteSAWA NDUGU YETU MBONGO.nakuunga mkono kwa hoja yako ya Wabongo kutopendana nchi za watu,Tena hawana maana kabisa.Majungu yao ya Bongo wanahama nayo.Wanaofanya kazi za maana ni Asilimia moja tu.Wengi wao ni Mafagio,kuchamba na mabox.Simaanishi kukandia hizo kazi.Tuwe na mifano kama Wanigeria au wakenya.Sawa wanigeria ni matapeli lakini wanamtapeli nani? Wao nawasaidiana sana "HIS MY BRODA".wAKENYA WAKO MBALI SANA na wengi wao wana fanya professional jobs,wana makapuni binafsi mengi sana hadi wana Bank yao London.KENYA COMMERCIAL BANK.Wabongo zao ni kujadili jinsi ya kumchoma mtu na nani karudishwa.
ReplyDeleteNakutoa maoni ya matusi kwenye Blogs.
we kweli umande uliuogopa sasa gazeti kubwa kweli nimejitahiji kutafuta ujumbe sijapata
ReplyDeletesiku nyingine jitahidi kusamaraizi
Michuzi najua hii haihusiani ila wewe una influence kubwa...Naomba usaidie kuhusu utaratibu wa blogs hapa Tz..maana kuna blog ya "Theutamu"...kitu inachofanya sio haki na inaharibia heshima za watu..watanzania wanashindwa elewa utaratibu unakuwaje.maana picha nyingine zinachukuliwa bila hiyana..sasa sijui Watanzania tufanyeje?hamna umoja wenu mmpe adhabu au mmushauri..Au Watanzania wachukue sheria mkononi wamuaribie!?Naomba usaidie hilo kaka!
ReplyDeleteMIMI SIMO UMEAMUA MWENYEWE KUMPIGIA MBUZI GITA SASA NGOJA HUONE MATOKEO YAKE.
ReplyDeletebrother nami ni Mtanzania niliyeko Spain (Barca). Umenigusa na mawazo yako nawasilisha 697636001
ReplyDeleteAisee, wewe kaka nchimbi, umepandia Posta ya zamani badala ya Uwanja wa kimataifa, alafu unashindana na wakina Masjhaka, Mwenzangu, kweli utayaweza. Kubali yaishe, sema ummemaindi Jovinata sana, lakini rafiki yangu kwa zari aliyopata na upishi wako melini rafiki yangu, pole sana. Naye anatafuta dhaabu kama ulivyo wewe hapo, heri ungejiita mashaka unepata email to ka kwa jovita..... Hivi uliota jana huko nachingwea nini?
ReplyDeletebwana Nchimbi ione blog kama shule fulani. watu wote hufanana na zaidi huwa kama watoto. wanapenda kuongea utani na hata matusi. unapotoa maoni tegemea positive na negative comments.
ReplyDeletenawapa pole wote walioingia humu bila kujua kanuni za mchezo huu, kama vile Jovi.
usiwe mwanasheria wa mtu yeyote.
Kunanuka shombo humu ndani, kuna mpishi karibu nini...
ReplyDeleteGo do what you do best brother, ka-SUPEVISA wapishi melini...
ReplyDeletemimi chichemi. kijana nchimbi ametoa maoni ya busara, lakini akumbuke kuwa blog ni kijiwe. washiriki wana uhuru wa kusema waliyo nayo moyoni. kwa mfano, kuhusu suala la jovinata, sikuona matusi yo yote bali ushauri kwa mitindo mbalimbali ya matumizi ya lugha, na huo ndio utamu wa kijiwe.
ReplyDeleteMtakumbuka rais wetu wa awamu ya pili alipoambiwa ukweli na mzee punch wa mlimani (kiaka hiyo) akafunga chuo eti ametukanwa matusi ya nguoni!
kachamambo
We Nchimbi bin Chimbo usituletee siasa zako za kizushi,Jovinata humpati ngó ingawa gia yako ndo hiyo unazungukia kwa kina Chibiliti na nani sijui..hapa tuko huru tunatoa comments zozote ilimradi hatuchafui hali ta hewa kwa lugha chafu.Sasa umeweka ujumbe wako humu lazima tukukosoe pale ulipokosea na kukupongeza pale ulipopatia sasa unaogopa nini...Hii ndio jamii ya kitanzania mzee learn to live with it kama Chibiliti
ReplyDeleteWe mi sio mmakonde mwenzako, mimi ni kabila jingine kabisa, watu tu huwa wananitania humu ndani, hawajui mimi ni kabila gani. Usiniingize kwenye umakonde, ingawa nawapenda sana wamakonde sina shida nao kabisa, ila mimi sio mmakonde. Kuhusu swala lako hapa watu wanaruhusiwa kutoa hoja zao maana tupo nchi huru, ila tu matusi hayatakiwi maana ni blog ya jamii hata watoto wengi wamo humu, ndicho hicho tunacho ombwa kila siku na Bro.Michuzi, yaani tuwe wa staarabu, Michuzi anasisitiza sana hilo, si kwamba watu wasitoe maoni yao. Pia kuhusu swala ulilosema kuhusu gari ya gesi, yaani nilivyo uliza, si kweli watu wamenitukana, wamenijibu vizuri tu mpaka sasa maoni 12 niliyo pata hamna matusi, mimi napenda ukweli Bwana ukiongea kinyume lazima nikwambie, kuhusu hilo umedanganya, ukumbuke pia maadili mazuri ni kusema ukweli. Unisamehe kama nitakuudhi kwa kukwambia ukweli, mimi napenda sana ukweli kwenye maisha yangu ninayo ishi. Ninakutakia kila lakheri huko Madrid, na ninakusalimu sana sanaaa...!!!!!
ReplyDeleteCHIBIRITI.
Duhh naona umeandika utenzi mreefu, mie nlijuwa utenzi wakuomboleza kifo cha karume! Hapo ndo umeonesha tofauti ya mtu aliekwenda shule na asie kwenda shule...ahsante kaka kwa ku-prove failure! Criticism ndio mfumo wa maisha! Asili ya maisha ya mwanaadamu ni challenge, ngoja nikuuingize shule kidogo; Nianze na asili uone kwamba hata wewe upo baada ya challenge kuubwa (1)Ili yai la kike liweze kurutubishwa millions of sperms huotolea kutoka
ReplyDeletekwa baba lakini nimoja tu ndio inayo fanikiwa kupenya "zona pellucida" na kurutubisha yai, jee unajuwa kwamba wewe uli "compete" na millions of sperm ndo ukawa wewe, kuanzia hapo asili ya maisha yako tegemea upinzani tu ! Jee wajuwa kwamba unatembea kwa maringo juu ya ardhi hii kwa sababu ya nguvu ya upinzani (friction force)..ha ha ha! Bila upinzani inaamana usinge fika hispania...lol
Kaka yangu "in a nutshell" nikwamba Kanuni ya maisha inaonyesha bila upinzani hakuna maisha! Ndio, lazima tupingane na tushindane! Hivyo silazima unachokiona wewe sawa na mimi nikione sawa "common sense is not so common" Kwa hiyo hao akina manka,jov, mashaka, wewe, mimi, n.k madhali tupo duniani lazima tupingwe na tupinge pia, kama hutaki kupingwa tafuta sayari ya peke yako ukaishi! Wanasayansi wanatwambia kuna sayari 9, moja ndio hii watu wanayoishi kwa kwakupingana, nyengine ni mars washapachika bendera zao marekani na Urusi, zimebaki 7 chagua yoyote ukaishi...ruhsa!
Umenisoma....?!
"Lazima tukubali kutokukubaliana"
Bwana Nchimbi, watu mnapaswa kuelewa kuwa hayo mnayoyaita matusi yapo katika kila lugha hapa duniani na yaliwekwa ili watu waweze kukemea mambo ambayo hayaendani na jamii.
ReplyDeleteMtu anapokuja humu lazima afahamu kuwa si kila analoliongea litakuwa na maana sawa kwa kila atakayelisoma, wengine wataudhiwa, wengine watafurahishwa, wangine hawatachukua upande wowote. vilevile majibu yatategemea na uwezo na uelewa wa mtu wa mada husika bila kusahau kuwa watu watatumia lugha waliyoizoea na ambayo itawafanya waonekane wamesimamam upande gani. Hivyo basi kuponda wataponda, kusifu watasifu, kudharau watadharau na kutusi pia watatusi. Jovi au Manka na wewe na mimi ni kina nani hasa tusitusiwe, iwapo huyo Mkapa, Kikwete na wenzao wajapo hapa Washington, DC wabongo huwaponda waziwazi mbele ya macho yao tena kwa kuwaonesha vidole, waulize watakwambia.
Watu wamechoshwa na upuuzi wa wabongo, vilevile watu hawawezi sifia au kubaliana na mambo yasiyo sawa, wanaokubali mambo ambayo hayako sawa hawa ndo huitwa wanafiki na si wale ambao wanaokemea mambo hayo.
Ukiongea utumbo, ukileta upuuzi humu watu watakuchamba tu, hivyo nawaomba wabongo kabla ya kuanika mambo yenu hadharani, chagueni ni yapi ya kuyazungumza si kila kitu na issue gani tulete kwa wadau. Iwapo tutawaletea maozo watayanukisha tu.
Kwa hiyo msilalame mnapopondwa wakati mmewapa watu pointi za kuwaumbua.
Nirudi tena katika issue ya hawa kina dada hasa huyu Jovi. Hivi kweli mtu ushindwe kukonekti na watu wote uliokutana nao maishani mwako, umuone jamaa kisa msamaria ukaanza kutangaza unataka akuoe, humjui hakujui, interest zenu hazifanani, inakuwaje? Kwa sababu huyu jamaa Mashaka ni mtu ambaye yupo tayari atoe dolar 6000 kwa masikini ilihali yeye asibaki hata na senti mfukoni. Je atayaweza au ndo kaolewa leo kesho anaanza kulalama maendeleo hatuna, jamaa anagawa hela kwa watu bila mpango. Au mbaya zaidi baada ya ndoa tu jamaa anabadili kabisa uelekeo wa maisha, anakuwa bahili kupindukia, kisa mwanmke anabana hataki jamaa afanye kama mwanzo, mbona yeye Jovi hatujamsikia kusaidia hata rafiki yake tu.
Jovi na Manka watambue kuwa hali waliyonayo sasa inatueleza mengi zaidi ya wanayoyaeleza wao na huo ndo unitwa usomi, uwezo wa kutambua
yaliyojificha katika maelezo yaliyopo.
Halafu kuhusu watu kama Nyoshi, hupaswi kuwatetea, hawa ni watu wenye mfadhaiko wa akili, mwanamume unashida gani ya kujichubua bwana, ili iweje, unapotoa mfano wa Michael Jackson hujakosea, sasa huoni yule jamaa ni matatizo makubwa, mwanamume gani kamili anaaibu kama demu wa miaka 12? Na ndo sababu kashindwa hata kutongoza mademu ingawa walikuwa wanamlilia mno kiasi cha yeye kuwa na uwezo wa kuvuta na kuchapa, kashindwa akaamua kubaka vitoto vya kiume. Huyu ni mshenzi tu, hivyo watu kama hawa kina Nyoshi, kweli wanaweza kuwa maarufu lakini ni shida kwa jamii ndo maana mkewe Rukia watu wanamvuruga hovyo kila guesti hous na mpaka tumemuona kwa Utamu, usiteteee ujinga huu.
Huyu Ray C, watu wanmjua, kuimba si issue ni kipaji, haimaanishi kama anaimba na ni maarufu basi ni mtu safi, mbona Sir Elton John ni mtu maarufu tu lakini choko. Sasa wadau wanawajua watu hawa na matatizo waliyonayo, hawawatukani wanataka wajirekebishe. Wadau wasitetee ushenzi hata mimi ninawaomba.
Jiulize Jovi anahitaji wanaume wangapi, 6200? Si kweli, Si ni mmoja tu. Kama hawezi kupata mmoj katika pile hiyo hafai kuwa mke huyo.
Samahani Bwana Nchimbi, napenda kujisahihisha kosa, kweli kuna mtu mmoja ndio kanisaga, lakini hamna shida. Mimi niliuliza swali ili nipate kujua, pia ni kuelimishana tu. Nafikiri huyo jamaa hakuelewa kabisa maelezo yangu, hayo magari yalishatoka miaka mingi sana na wala sio sasa, halafu ni magari ya kawaida kabisa kama tunayo tumia bongo, ukiamua unaweka mitungi ya gesi na kuweka sistimu yote, si kitu cha ajambu sana, na mimi nilitaka kujua kama unaweza kupata gesi Bongo, yeye kanijibu ovyo, lakini ndiye yeye pekee aliye nijibu ovyo, na kuingiza mada zingine kabisa zisizo na misingi yoyote. Mimi ninamuunga mkono Bro.Michuzi kwamba kila mtu anaweza kusema awezavyo ila asijafue hali ya hewa tu, basi ndio hayo tu. Nisamehe Bwana Nchimbi sikuona vizuri.
ReplyDeleteHaya Kaka Nchimbi, hivi kati ya hao jamaa wawili katika hiyo picha wewe ni yupi? Maana umetoa salaam na picha halafu hujasema kuwa wewe ni yupi hapo. Kama ungelisoma ungelijua umuhimu wa vielelezo, si kosa lako.
ReplyDeleteNa pili, huyo jamaa mwingine umemleta wa nini? Ulimuomba akakubali umtumie?
Elimu ni pamoja na kutambua issue kama privacy na kuplan ahead. Wewe umeibuka tu na picha ulipiga na rafikiyo, ukaamua kuipaisha hewani ukitetea jambo pengine huyo jamaa halifagilii, inakuwaje?
Kwa nini usingeli edit hiyo picha ukaweka yako tu, na kutoa salaam hizo. Hapo tusingelikuwa na shida ya kutambua nani ni nani.
Najua utakuwa umenielewa, siku nyingine hutofanya hilo.
Umesema mwanangu!!! watasema sana lakini ujumbe umewafikia. yaani kweli nakuunga mkono best wangu.Watanzania wanatakiwa wabadilike kwani wanatabia kama za kichawi vile.
ReplyDeleteHAKI YA NANI, KWELI ATAIPATA HUYU NCHINMBI WAOSHA VINYWA WAKIAMKA...NYIE SUBIRINI TU NA MTAONA COMMENTS...HEY, HIVI KATIKA PICHA NCHINMBI NI YUPI, NI HUYU WA RASTA?
ReplyDeletehuyu mkulima sijui kaibukia wapi naye? hivi wewe unajifanya kufagilia Jovina na Manka unafikiri wanaweza kukupenda mtu hata shule huna na hueleweki,pole sana labda Jovina maana anaonekana mbabaikaji sana anaweza kukufikiria,next time ukija humu hakikisha umesoma kidogo hata cha form 4 labda tutakusikiliza,na wewe michuzi naona sasa unatuharibia blog yetu kwa hizi story za watu wasioeleweka kama hawa na kina Manka na jovina bila kumsahau yule mpenda ujiko asio kuwa nao mashaka
ReplyDeletesawa kaka habari ndiyo hiyo tumeipata.sasa ndugu yetu nchimbi kwenye hiyo picha wewe ndio huko wapi maana kuna wa2 wawili hapo...au ndio huyo mwenye suti?
ReplyDeleteHaya kaka mi naenda kulala... hii nitasoma nikitoka kwenye mizunguko nishachoka nicheke nikisoma Comments tuu. aza waizi maelezo marefu umezunguka sana point ila umeeleweka na wenye akili wamejua umelenga nini.
ReplyDeleteKila la heri!!
sasa kati yenu yupi Nchimbi , huyo mwenye suti ya kipaimara ? au aliyeshika glasi ya maji? .wewe
ReplyDeleteNchimbi tunajua janja yako unamtaka Jovita.. si useme tu usingie na kisingizio cha kujifanya kukandia watu wanavyoandika comments zao , hapa sio kanisani wala msikitini .. hichi ni kujiwe cha watu wenye hisia ZA KISHENZI NA KIUNGWANA.
kaka vipi? napenda kukwambia kuwa watu huwa hawatukanai wanaongea kile cha kweli we mchumba anapatikana kwa michuzi mi mwenyewe ni msichana ila naponda sana kwa hilo haifai kabisa na wewe unajidai kuwatete hao wadada waoe basi uone kama manka atakukubali na hiyo cv yako. na jovinata anampenda mashaka shauri yako wewe mpishi wapi na wapi!!!!!!
ReplyDeletedah!umejaribu kuelezea kama gazeti lakini umeboronga,pumba nyingi kuliko mchele,au uliona chibiliti anafaidi kuonekana kwenye blog na wewe ukaona uuze sura?kidhungu chenyewe chpela,thijui kispanish kama unajua,maana sentensi yako nainukuu i am praudi of you my brothezer, duh hapa matope tupu.
ReplyDeleteG-KUBWA
JAMANI TUACHE MIHASIRA HAINA MAANA BRO MICHU KAANZISHA BLOG KWA NIA NJEMA ILA SISI WATUMIAJI TUNATAKA KUIHARIBU NAKUIPOTOSHA ILE NIYA YA BRO MISOSI( MIMI NAPENDAGA MNAVYO ZOZANA NACHEKA HADI BASI) SIS ZANGU JOVINATA NA MANKA INABIDI WAKUBALI TU KUWA PENYE WENGI PANA MENGI NA PANA MAZURI NA MABAYA HILO WALIKUBALIS O WAKUBALI MATUSI NAPIA NAAMINI YAPO MAZURI WANAYOYAPATA ILA HAWATAKI KUTUAMBIA WANAYARIPOT YALE MABAYA TU.
ReplyDeletekuuliza si ujinga Hivi huyo nchimbi ni mwanaume au mwanamke? kwa picha na hoja zake nashindwa kumwelewa .Wale mnaoelewa kuangalia hoja na picha niasaidieni.
ReplyDeleteTuache utani Nchimbi amependeza sana ila kavaa nguo na viatu vya mitumba.
ReplyDeleteYaani Pamoja na kukaa Ulaya bado anavaa mitumba?
OYO MCHIMBI MBONA UMEDATA SAAAAANA! TOA UPISHI HAPA. NEXT TIME COOK! SEEMS LIKE SUPERVISING DEM COOKS LEAVES U SO IDLE TO POST AUS A LONGFUL MAIL SHIT! PIKA!
ReplyDeleteMULOX.
maaalimu michuzi naomba msaada wako maana kidogo wewe umetembea, hivi hiyo suti aliovyaa ndugu yetu hapo sio zile zinazotumika kwenye maombolezo....!?
ReplyDeletebraza posa yako kwa jovi imefika vigezo unavyo ila kimoja kinahitaji huruma ya jovi nacho si kingine `MASTA' hauna
ingawa kuna vi point point ila bado nafikiri inabidi uende shule maana hiyo supervision job yako itakufa siku moja na kupata nyingine huku Europe itakuwa mbinde!
ReplyDeleteUshauri wa bure nenda shule kaka in Europe kama shule haijapanda watakutema siku moja hata kama unamnanihii bosi!
Ukiwa na shule yako hata wakikutema utapata kwingine!Usimaind!
lol WEWE BANGI MTU KWELI.
ReplyDeleteJAMANI EEEH NCHIMBI NI HUYO MWENYE MILIPS YA BANGI(KUSHOTO)
ZOOM HIYO PICHA UICHEKI VIZURI
LOL
Mengi uamesemwa hapa, lakini alolisema Anon Apr 8, 8:34 am. sentensi yake ya mwisho tu Mh! karibu na ukweli. Ngoja nitoke nikapate lunch niingie tena hapa kijiweni kuajabia maarifa ya kishenzi, maana ya kiungwana nilifundishwa na mama na baba nyumbani.
ReplyDeleteMchezea pembeni
Unasikia bwana kaka nchimbi!so kama vip,ulivyoeleza mengine fresh mengine hayahitajiki mahala hapa!unajianika flan!!usilaumu watu kwa tabia yao ndo mazingira waliyokulia hata wewe ulikuwa huku,umeona changes coz uko ughaibuni!pia watu wanatofautina kwa mapokeo namtazamo wa mambo mbalimbali(kimsingi "Perception")we tafuta maisha yako bwana! achahna na mambo ya watu!una mambo mengi ya kufanya hujayamaliza!!
ReplyDeleteWee mwana Bhagheeee Nchimbi, unatukaribisha Spain wakati mwenyewe umefika kwa kunyatia (KUZAMIA)unataka na sisi tuwe kama wewe. Halafu kama unataka kuoa, acha kutumia gear hiyo wewe sema tu sina kigezo cha Masters, wasichana watakufikiria.
ReplyDeletePamoja na kuzamia bado kimakonde kimo mdomoni, angalia Michuzi ulivyoiandika mwishoni, eti kaka Nchuzi. Lol! Kwanza wewe muongo unasema unapika sijui unawasimamia wapishi, hakuna hilo! Mchafu hivyo utampikia nani ale, kwanza mirasta hiyo nani atakubali, duh.
ReplyDeleteMdogo wangu, nilikuambia ngoja waamke wenye hasira na maisha, sasa, kama mwanaume, toa e mail yako upate mitusi kama Jovita, si wewe unajifanya Bangi ziko kichwani, hii itaziondoa zote! Teheteheteheteheteh
ReplyDeleteACHEMWENE NCHIMBI!
ReplyDeleteUFANYE KILA NJIA UTAPATE WAFADHILI WA KUWALETEA MITEGO YA KUNASA SIMBA
NACHINGWEA NDUGUZO ! WANALIWA NA SIMBA TENA MCHANA WA JUA KALI!
NA SIKU INGINE UWE NA ADABU SIO
UNAKURUPUKA NA KUANDIKA PUMBA NDANI YA BLOG HII YA JAMII
Mi huyu mshikaji nimetulia na hiki kiswahili chake tu, pamoja na kukaa nchi ya watu lakini bado lafudhi yake ni ilele ya "kunyumba" huyu kweli katokea mtaa wa congo.
ReplyDeleteTupendane vipi wakati wewe umeshaanza kuwaponda 'watumishi wa serikali' wenye nyumba Mbezi! Halafu unatuletea mambo ya kutaja makabila ya watu; huo sio utamaduni wetu. Je, kwa nini unadhani ni muhimu kutuambia 'hujahudhuria shule' unapotoa maoni?
ReplyDeleteJAMANI MWACHENI KAKAAANGU!! KWANZA NAKUPONGEZA SANA...WEWE KWELI UMONA MBALI!
ReplyDeleteHIVI WATU MMEWAHI KUJIULIZA KWANINI NCHI YETU HAIENDELEI NA USHIRIKINA UNAZIDI???
KWASABABU WA NYOYO HIZO!!!! BINADAM TUNATAKIWA TUPENDANE NA MKIMUONA MTU ANAEPATA UJASIRI NA MAENDELEO, UNATAKIWA UPATE HASIRA YA KUWA NA MAENDELEO NA WEWE!!
KAKA NAKUPONGEZA KWA KUISHIA KATIKA MJI MZURI KAMA MADRID, MIMI NIMEKAA SANA BARCELONA NA MADRID POTE PAZURI!! NA HONGERA KWA MANENO YAKO LAKINI ... IF YOU ARGUE WITH A FOOL... SI UNAJUA TENA!! HUWEZI BADILISHA WATU!!!
Bro Michu,
ReplyDeleteMimi tangu mwanzo nimesema huyu ndugu yetu nchi pamoja na kuzamia melikebu bado ana mambo ya kishamba sana,anatumia migongo yetu wanablog kuwatongoza dada zetu Jovita na Manka..eti tumewatukana kume mzushi tu.Angalia hata Bro Chibiliti mwenyewe alisema tumemtukana amemkana kuwa hatujamtukana bali tulimwambia ukweli.Mtu anaambia ukweli kutokana na maelezo yake,kama wewe Nchimbi umeambia ukweli be open,go straight away kwa Jovita japo hauna vigezo maana hata kuondokea Bongo umeondokea Kurasini wakati watu twaoondokea Kipawa....!!!!!.Ndiyo maana watu tunampenda Bro Chibiri maana anakubali kukosolewa...!!!.But You young guy,you are too rigid and primitive..!!!
Mzee Lomag umetema point nyingi ambazo mimi nakubaliana nazo kabisa. Najua wabongo washakutukana na kuongea utumbo lakini at the end maneno yatawaingia tu. Hata mimi nimewasapoti hao madada Manka na Jov kwa kuposti matakwa yao. Sielewi kabisa kwanini watu wamejibu maneno mengi ambayo si mazuri. Ningalikuwa singo ningepeleka application maana qualification karibu zote ninazo.
ReplyDeleteNa wewe Chibiriti hebu onyesha ustaarabu kidogo.. unamwita mtu muongo, hukufikiri kuwa labda amepitiwa tu kidogo... Hongera sana Mzee Nchimbi kwa hatua uliyofikia kimaisha na Inshaallah mwenyezi Mungu atakuongeza.. ps. suti imetulia hiyo usiwasikilize wazushi.
Mdau - Boston, US
Michuzi hacha kubania Comments"Watu wanajaribu kuwa amasha wa Tz unajua wa Tz wengi hawajaelimika so unapo bana Comments haisaidii,si mtu unakulupuka tu kumfagilia mtu bila kujua kunawatu wapo after Pesa,kama mwana Kijiji au Mashaka wanachofanya always kutafuta Njia za kutoka kupitia migongo ya watu.
ReplyDeleteNTWARA OYEEEEEEEEEEEEEE!!! BAH UCHICHAHAU ILE NYIMBO YETU HATA HAPO ULIPO MANEMBO. KILA MUTU AVE NA KWAO. WAKO BINGWA WA CHALAMU AFIRIKA MACHARIKI NA MANGARIBI - JINA LANGU NI
ReplyDeleteTIRENI NTIMBO NA NNERO - MAHUTA SHIMONI, NEWALA , WAPE HAII MANEMBO WOTE WA UGAIBUNI --- CHIBIRITII UPOOOOO!!!
mijitu mingine bwana hata ufanye nini hayataelewa. Jovi alisema anataka mtu mwenye masters na sio mwenye ku-master wapishi wengine.
ReplyDeleteVyakula vinaungua wahi kapakue.
Kukaa kwako ng'ambo sio kigezo kama umesahau kutongoza rudi kwenu ukaozeshwe.
MWANAWANE
baaah,kwali jaje bwana wewe?unaacha kwenda kulima ntama na ulanga huko unaingilia vijiwe vya watu humu,sasa umekoma utarudia tena?
ReplyDeleteasiingilie vijiwe vya watu kwani yeye sio mtu,ebuuu hapa eti ntwara aliyewambia nachingwea iko mtwara ni nani.Mi nadhani nyie hata jiografia shule ya msingi hamjasoma .Mwacheni nchimbi au sababu mtu wa kusini ndo asiende Spain hata kama kazamia,mbona wengine wamejifanya wakimbizi tofauti iko wapi.Eti kupikaaa si bora huko kuliko kuchambisha vizee.Kakangu usjijali ucharike tusaidie ndugu zetu kwetu Nachingwea.YES WE CAN.
ReplyDelete