mwanamama anayesadikiwa kuwa mzimbabwe akisimama na kuzoza juu ya zimbabwe wakati makamu wa rais anahutubia. chini ni mtu mwingine ambaye pia alitoa kauli za kulilia tanzania iingiliea mambo ya zimbabwe. hapa wanausalama wanakula nae sahani moja na kumtoa nje
jamaa kadhaa wanaosadikiwa kuwa ni watu wa zimbabwe walivamia mkutano wa diaspora hapa london leo na kutaka kuanzisha vurumai kwa kupiga kelele za kudai wanachodai haki yao huko zimbabwe na kuomba jk aingilie kati. wakati huo makamu wa rais dk ali mohamed shein ndio kwanza alikuwa amesimama kuhutubia. hata hivyo makamu wa rais aliutuliza umati wa diaspora kwa kusema hii inaonesha tofauti ya wabongo na watu wengine kwa tabia ya amani na demokrasia, na kuwataka wahudhuriaji waachane na hao walalamikaji wanaoshukiwa ni kutoka zimbabwe na kuendelee na mkutano wetu kwa amani na furaha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Lakini hata hivyo ujumbe ulifika. Nahisi jamaa wa Uingereza walichekelea kichinichini
    m3

    ReplyDelete
  2. what a shame jamani,kweli kama ni kufundwa watanzania tulifundwa na hayati nyerere tangu zamani,ingekuwa mtz hapo angeamua kuondoka kimya kimya au angesubir mda ufike amwage sera zake na sio kwa kuropoka kama hivyo,amani yetu idumu Tanzania
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  3. Hapana tatizo wazimbabwe, tanzania tutakusaidieni, tutaleta ndugu zetu waje wapigane vita vyenu, wauawe na kulemaa ili mupate muradi wenu, muishi kwa raha, watakaobahatika kurudi nyumbani tutawaambia "HATUNA CHA KUWAPA ILA AHSANTE" nanyi msahau msaada wenu. Msishangae tumezoea hayo ni juzi tu tumepeleka ndugu zetu commoro. Sisi ni mahodari sana kuingilia ya watu ingawa yetu wenyewe ya zanzibar yanatushinda!!

    ReplyDelete
  4. Jirani yako anapohitaji msahada, ni vizuri ukamsahidia. Iko siku nasi tutakuwa matatizoni na tutahitaji kusahidiwa. Shida haipo kwa nchi 1 milele...ipo siku yanayowapata wenzetu yanaweza pia kutufika sisi.
    Ukimya wa Rais wetu na viongozi wa Africa kuhusu shida za Zimbabwe ni udhaifu mkubwa...kulindana huku kutakuja kutufikisha pabaya.

    ReplyDelete
  5. watz ni waoga jeuri hiyo hatuna,ingekuwa nchi nyingine tungeshapigana tayari kutokana na mambo ya ufisadi.

    ReplyDelete
  6. Naelewa frustrations za Wazimbabwe. Inasikitisha kuona kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Africa anaye conderm kitendo cha Mgabe isipokuwa Desmond Tutu aliyesema kwamba inawapashwa waafrica wote tuone aibu kwa kutokuchukua hatua yeyote dhidi ya manyanyasiko ya ndugu zetu.

    Naaelewa kwanini viongozi wa Africa hawadhubutu kusema sababu ni kwamba hakuna aliye clean! huyo Mbeki hana hata aibu kusema kuwa Zimbambwe haina crisis yoyote anataka mpaka hali iwe je ndiyo a admit kwamba hali ni mbaya?

    Kusifu kwamba Watanzania tuna amani ngojeni nasisi iko siku tutachoka hivyo vitendo vya viongozi wetu vya kuiba mabilioni ya wananchi kwa manufaa yao wenyewe na hakuna anayesema chochote itafika wakati na watanzania watasema enough is enough!!!!

    ReplyDelete
  7. Aisee hiki kimama kinajiamini vipi. Sijui itakuwaje!??? maskini sijui watamnanihii!
    We Misupu utaweza haya? Fanya hivyo kama hawajaku-kombelia kama sio kukuKolimbalia mbali huko.

    Masaai halisi

    ReplyDelete
  8. watanzania ni waoga na wanafiki wenye kupenda kujipendekeza kwa viongozi hii ndo tofauti lakini sio kwamba wabongo ni special sana ktk africa, nchi yetu inayumba halafu bado tunafikiri tuna amani kalaghabao,

    ReplyDelete
  9. Nafikiri ilikua ni relevant message to the right people (Shein). Inamaana Shein hajui kama Kikwete ni mwenyekiti wa AU?

    Labda kama Michu useme walitukana...

    ReplyDelete
  10. Hebu jamani nisaidieni mie na umbumbu wangu sasa huko Zimbabwe watu wataingiliaje? Kenya ilikuwa rahisi maana matokeo ya uchaguzi yalicheleweshwa lakini yakatangazwa na watu wakayapinga na kukawa na vurugu. Hapo unaingilia uansema unaenda kuokoa maisha ya watu. Au huyu naye atangaze matokeo ageuze nyuma mbele, mbele nyuma ajiseme yeye mshindi halafu wakina Tsvangirai walianzishe, hapo ni rahisi kuingilia, sasa kakaa kimya kama jogoo kuchi hebu nambieni unaingiliaje hapo maana na sheria za kimataifa ziko wazi, upeleke majeshi ulimabiwa kuna vita au unataka kuvamia nchi ya watu.

    Huwezi kulinganisha na hata Comoro huko Anjuani, kwa hali halisi ilivyokuwa ya anjuani. Sasa sio kutubebesha mizigo kupeleka majeshi ni pesa.Wa South walikaa kwetu kula na kulala bure na nyumba nzuri nzuri walipewa, na hata ardhi ya kuweka makambi yao walipewa, hao hapo wanatusaidia nini zaidi ya kuja kukomba Tanzanite na utajiri mwingine. Wameshindwa hata kutusaidia kwenye maafa ya Mererani mpaka walipolazimishwa. Tulishafunga mikanda wee kwa ajili ya Obote mpaka leo imekaza. Wazungumze wamalize na ya Wazimbabwe watamaliza wenyewe Wazimbabwe ila ushauri kupewa wapewe, na kama kusuluhishwa wasulihishwe.

    Na ya Wapemba na Waunguja wanajua wanachongambania tangu wakati wa Mapinduzi, mambo yao ya mie bwana huyu mtwana na huyu kidagaa watayamaliza wenyewe. Hata kama ikisainiwa miafaka 20 kama roho zao bado zina visa na kutu ya tangu enzi ile ya Sultani basi hiyo miafaka haitafaa kitu!

    ReplyDelete
  11. injustice anywhere is a threat to justice everywhere(mrk), mugabe turn to be bullish to his own people, leaving his own people dying with AIDS, dont care , depressing his own people everywhere, dont care, pushing back the development reached to the point zero, dont care....and no body among the african leader finger point the ruthless ruling of mr mgabe.....why? mungu ilaani africa

    ReplyDelete
  12. Amani na upendo vidumishwe ili wenye nchi waendelee kufaidi vijisente

    ReplyDelete
  13. During the UNO security council meeting in New York, the issue of Zimbabwe wanted to be discussed but was quickly put down bu the AU chairman, JK, that it is an Afrikan issue and SADC will take care of it.

    So, we wait for SADC to take care of the Zimbabwe issue.

    Hao waliovamia mkutano nadhani wanaona haki wafanye hivyo kwani TZ ilishiriki kikamilifu kusaidia ukombozi na wanaangalia sasa watu wanakufa na njaa Zimbabwe na "mkombozi" wa kusini mwa Afrika, Tanzania, tunafanya mikutano ya diaspora in relative peace (issue ya Zanzibar I sometimes think tunaijua sisi wa Tanzania tuu)

    ReplyDelete
  14. Well nawapa pole sana wazimbabwe kwani matatizo yao yamekuja wakati mbaya sana. Kitu pekee ambacho kinanifanya nisiwalaumu hawa jamaa ni suala la kwamba TZ ni mwenyekiti wa AU sasa. lakini kuhusu kuingilia mambo ya zimbabwe nadhani imefika kikomo kwani moja ya sababu ya umasikini wa tanzania ni kujishebedua kwatu na nyerere wetu katika kusaidia nchi nyingi za africa kupata uhuru ikiwemo zimbabwe na mustakbari wao. musidhani ni mchezo mdogo tuliofanya na nikiongea na hao tulio wasaidia huku nje sioni kama wanashukurani zozote mbali ya kusema tz is poor and kukebei kiswahili bila kujua kwamba wao wanaongea lugha za colonial masters.
    Gharama zilizotumia uganda, mosambique, angola,burundi na rwanda, south africa, cameroon, ghana ivorycoast. zote zinadumaza uchumi wetu. Halafu kwani mbona zimbabwe geographically haipakani na TZ na kwanini watake msaada wetu sio kenya, uganda and others!!

    Nasema hivi, enough is enough.

    hao wapemba na waunguja wataendela hivyo mpaka waache kubaguana nje ya siasa kwani wamezidi kujitoa utu. nashangaa hata kidini sio safi kwandugu kuasmiana.

    all the best bongo tukitulia tunachance yakuwa great nation,MUTANIKUMBUKA.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  15. Sasa hawa wanataka Tz iingilie upuuzi wao kama nani?Hata kama Jk ni MWENYE-kigoda wa ze UA ugomvi na matatizo ya Zbw hayatuhusu.Tuna matatizo kibao ambayo hawa mabwanyenye waliotuomba kura zetu wanashindwa kuyatatua na ila wanazidi kutuongezea(richmondi & co)Halafu wa-Zbw wanataka kutulea vumbi zao.Ushauri wa bure Wazimbabwe wanatakiwa kuuza misuba nasikia misuba ya zimbabwe ni kasheshe.
    NB-Hongera Anon wa 3 toka juu comments zako kali kaka.

    ReplyDelete
  16. If my memory still serves me, there was a female student at University of Dar in 1991 or 1992 who was very furious at male students at that time and compared them with male students wearing skates!! I remember that she called their behavoiur "Ukondoo". Very unfortunate, I forgot her name. She was very caurageous woman. It is a naked truth that most of Tanzanians are cowardy, honestly. We cannot come forward and critize our leaders in public. We like to chat about our economy, policies and then go to bed.

    Chatting has been our greatest hobby and it will be so many years to come.
    1. Tanzania has bought a useless radar. A british MP resigned because she was not happy with this transaction. A poor country like TZ buying that piece of expensive equipment. None is using it now! I heard it has a full of corrosion right now. As usual, we chatted about it and life goes on
    2. IPTL; as usual, we chatted and life goes on
    3. Richmond; as usual, we chatted and life goes on
    4. Central Bank; As usual, we chatted and life goes on
    5. Vijisentigate; As usual, we will chat and life will go on.
    6. President Jet; As usual, we chatted and life goes no



    Let's wake up and demand change in Tanzania. The change that we can believe in. If we believe that we can bring change, change will become true. I recently heard that we are 3rd country in Africa for Gold production. We are the only country in the world producing tanzanite. We have great rivers & lakes, but having problem with electricity. Our leaders are letting us down. This is the fact. How can they enrich western countries by taking our money and deposit to their bank? Do not they know that by depositing money to their banks, they are actually helping them economically?

    ReplyDelete
  17. narudia tena....what a shame michuzi! umejiabisha wewe na waandishi wa habari wote wa Kitanzania.
    nashangaa kuona umeshindwa kuweka msg yangu just kwa kuwa nimekupa ukweli kwamba umejishushia hadhi kwa kumwita mtu anaedai haki yake kwa kuzungumza ukweli MWENDAWAZIMU!
    kwa maana hiyo mtanzania pia atakapodaia haki yake na kuwataka mafisadi kurudisha mali zetu na sie ni WENDAWAZIMU!
    kwa kweli ni aibu kusikia lugha kama hiyo inatoka kwa mtu mwenye akili, anajitapa kuwa amepitia mambo mengi, na kuijua siasa na ilipotoka.
    cha kushangaza zaidi ni kuona umeweka maoni ya watu waliokuunga mkono wewe, lakini kwa kuwa mie nimekuandikia maoni ya kukumbusha ukweli umeyatia kapuni.
    na nafkiri kwa msimamo wako ulionao basi tanzania tunawendawazimu wengi tu, kama vile kina Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Dr Slaa, na wenginewe wengi kutokana na kusimama kidete kupigania haki zao pamoja na ZAKO
    all ni all kama hali ya mzimbabwe aliyevamia mkutano, ujumbe wangu UMEFIKA japo ukiamua kutoudhihirisha. kwa nafsi yako umeshafika

    ReplyDelete
  18. Mdau Apr 20 8:06am poa moto...Hata mimi nilidhani anasema hawa watu ni wendawazimu lakini nilituliza kichwa nikarealize aliposema Wazim alimaanisha Wazimbabwe... ndio maana ni vyema kulifikiria jambo vizuri badala ya kurespond kwa pupa!! Keep doing a great job Michu.

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete
  19. Huyu mama hakustahili kutolewa nje. Huyu ni binadamu mwenye mwenye machungu makubwa ambaye hajui wapi akayamwage. Hapa mmekwepa debate kubwa sana kuhusu jinsi ya kuwsaidia wanzetu.Hapo hamja tatua tatizo bali bado limelimbikizwa. Namfananisha huyo mama na mlemavu mmoja aliyekua mshika mguu Nyerere huko kiwira baada ya kuona hasaidiwi na walinzni walipomkataza Mwl Nyerere aliwaambia mwacheni tu.Akasema shida yake akaahidiwa kusaidiwa. Na huo ndio utanzania Shein alikua na haki ya kumsikiliza kwani hakua na bunduki alikua anatoa mawazo sasa hiyo demokrasia yetu iko wapi manyangaĆ u sisiiiiiiiiiii eeeeeeee?

    ReplyDelete
  20. WABONGO bwana!mkiambiwa ukweli OOh mzimbabwe,ooh mganda ooh mkenya!!acheni mambo dada kaona mnamzengua tu maneno kibao halafu nchi mwaiuza kwa wadosi na wengineo:

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...