Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Laston T. Msongole kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Uchumi.
Taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi, Mei 10, 2008) Ikulu, Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa Msongole atashughulikia masuala ya Uchumi na Bajeti katika Wizara hiyo.
Kabla ya uteuzi wake, Msongole alikuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Macro-Economy katika iliyokuwa Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji.

Wizara hiyo ilifutwa katika mabadiliko ya Muundo mpya wa Serikali uliotangazwa na Rais Kikwete Februari mwaka huu

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...