mdau, mnara huu wa azimio la arusha unakukumbusha nini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2008

    Uwe kama nembo ya Arusha tu lakini kwa karne hii na maisha ya sasa haukumbushi chochote, karne hii ufisadi kila kona

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2008

    azimio la arusha

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2008

    It reminds of Yanga bovu, maduka ya Ushirika, everybody get it the same, drink the same, dress the same, shit the same. A future of uncertainty but I also must say it works for that just moment, and its envision has been devastating for the Tanzania future and Economy a like till today.

    I am talking about Education system, EConomic system and more importantly a political system which was essential good on words and papers, but will never be in DEEDS.

    We are now seeing those political talk heads in our current government and previous governments who were results of this so called Azimio la Arusha, are primarily affected today as we speak, less knowlegeable, less educated, more polarizing, more predominently politisized. The last has been a huge effects on our todays leaders, they see each and everything on bad political angle rather than more broad views, visions of our future together as a country.

    Therefore there has been a bad, economic decisions, less technological progression, and most important more knowledge about neighbours, foreign countries and others. Back then we saw our neighbours and foreign countries as poisonous mabepari, we need no connections from them, no education from them, no investment from them(this was considered an omen), and most importantly know nothing about them.

    But now, we are opening up, we are start learning hard lessons from the experience. Bad Mines contract, Socialist shown the money gone crazy(UFISADI), our economic experiments on PRIVATIZATION gone sore, and more serious enough we don't understand even the use of Tanzanite, although we are the solely owner of the GEMS in the whole universe. This in itself shows how we are locked out then, and how we learn bad lessons from opening up, because we did not understand opening up then, we did not learn from opening up then.

    It is essential put us BACKWARDS, 50 years, and we the world considered us a fare game, the only way to come out of this is through EDUCATION, and give the country to a new generation just like RWANDA now. Well informed, knowledgeable, and involves all, value every single citizen, and envision the prosperity rather than political gains and bickerings.



    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2008

    unanikumbusha Nyerere na ubishi wake!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2008

    Unanikumbusha Umasikini, njaa, dhuluma na siasa ya ujamaa na kujitegemea iliouwa nchi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2008

    Nothing, ila uonevu wa ubadhirifu wa viongozi wa tanzania toka nyerere hadi hii leo kikwete, mtanzania mlala hoi han ahaki tanzania

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2008

    hauna maana yoyote zaidi ya udikteta wa nyerere kutufanya kuwa masikini uliko nchi yoyote africa mashariki na kati. alikuwa anajijengea umarufuku wake kwa kusaidia nchi nyingine za africa,now tunaona matokea south africa hdi wabongo wahatakiti. but unaleta sura nzuri kwa jiji la arusha

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2008

    Unanikumbusha 'Jengo hili lilizinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka Fulani' (ridiculous!)

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2008

    dah mbona watu wanamtukana hivi nyerere?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2008

    @ any 3:05pm
    Said

    "dah mbona watu wanamtukana hivi nyerere?"

    Sorry, you have been infected by Azimio la Arusha, Ujamaa na kujitegemea, and e.t.c.

    Hauko Huru bado, Hoja hujibiwa na Hoja!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2008

    Huo mnara unanikumbusha noti ya Sh 20 ya enzi hizo...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2008

    Hakuna kitu kinachoumiza kama ule usemi wa "zidumu fikra za mkapa.... sorry mwenyekiti wa ccm" kweli nyerere alituweza wabongo ndio maana nchi mpaka leo maskini

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2008

    Mnara unanikumbusha kwamba Prezidaa na crue yake waliambiwa marufuku kufanya biashara ukiwa madarakani,lakini kama zilivyo marufuku nyingi bongo, marufuku maana yake ruksa we fanya tuu,watakao kusema jua wanawivu wa kipumbavu!

    ReplyDelete
  14. Inanikumbusha enzi zile tunatoroka shule Ilboru na kujichanganya tauni bila magwanda ya skuli. Chifu akikubamba mitaa hiyo, anakupa dozi hapo hapo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2008

    Wengi wenu mnaomtukana Nyerere mlikuwa hata hamjui yanayotokea wakati huo, mnafuata UPEPO tu, kumuongelea vibaya, hata kama mmesoma na kugundua mabaya yake STILL AMEFANYA MAZURI MENGI AND YOU KNOW IT.....AMESHATUTANGULIA MBELE YA HAKI, BE NICE PPL.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 29, 2008

    unanikumbusha (1) noti ya sh 10 ya zamani (2) walimu wanoko wa ilboru wakiongozwa na MEDUKENYA aka MZULU (3) baridi kali yenye ukungu ya arusha - wakati huo tukisema baridi inanyesha (4) vumbi laini la kijenge haswa mwezi wa 8

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 29, 2008

    Ha ha ha...! Taratibu mbavu zangu. KIDO nimekupata vizuri, na ukikutana na Marehemu Mgaya aka machkura au Shemndolwa sijui utachimba mashimo mangapi?!

    Inabaki kuwa historia...!

    Mahadhy

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2008

    The picture reminds me one of the most respected statesman in modern African history. Highly charismatic and immensely endowed with prophetic insights. A gifted philosopher who dedicated his entire life for the greater good; namely freeing mankind from mental bondage!!!! the kind of mental slavey that continues to affect even some of the contributors here. Anyone who says Neyrere was a bad leader, he/she should try to compare him/herself with him: and say can I debate him on first values? Give me a name of a politician in the current government who can equal Nyerere?
    If no then you should SHUT UP!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 29, 2008

    anon 3:24 ACHA ROHO MBAYA,NYERERE NI BABA WA TAIFA,BILA YAKE LEO MNGEKUWA NA UHURU NYIE!?MSIJIFANYE KUENDEKEZA FREEDOM OF SPEECH,JUST BIKOZ MKO MAREKANI,NYIE BADO NI WATANZANIA.WEWE NDIO BADO HAUKO HURU,NI MFUNGWA WA MAWAZO!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 29, 2008

    AISEE ilboru si ndio shule yenye watu wenye akili sanaaa.naomba mmoja wenu tuwasiliane basi!

    babygal

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 29, 2008

    inanikumbusha marehemu babu yangu hizo watu wakidumisha fikra sahihi za mwalimu , enzi hii mbele ya mafisadi hizo fikra za mmwalimu sijui kama ni sahihi aam vipi, watu wanaiba sana, miaka kumi ijayo huo mnara watu wautoa wapanue bara bara hapo, mnara huo hauna maana tena, mwalimu hayupo mnara wa nini? no biashara tu mpaka ikulu mpaka kila kila mahali eboo!!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 30, 2008

    Wengi mnaliongelea Azimio la Arusha bila kujua undani wake. Lisomeni kwanza ili muone Mwalimu Nyerere alivyoona mbali. Ukiwa wewe ni mzalendo na mwanamapinduzi halisi utataka Azimio la Arusha lirudi leo. Acheni kumkebehi Julius. Ni nani kiongozi katika hao mnaowasifia nyinyi amefanya makubwa ya kuiendeleza nchi na kuiwekea misingi imara ya utaifa kama Mwalimu? Msomeni.

    CHAMA CHA MAPINDUZI
    AZIMIO LA ARUSHA
    NA
    SIASA YA TANU JUU YA
    UJAMAA NA KUJITEGEMEA
    Imetolewa na Idara ya Habari,
    TANU, Dar es Salaam, 1967
    1
    SEHEMU YA KWANZA
    Imani ya Tanu
    SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA
    IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII
    Kwa kuwa TANU inaamini:-
    (a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
    (b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
    (c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
    kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
    Mikoa hadi Serikali Kuu;
    (d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
    yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
    wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
    (e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
    hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa
    mujibu wa Sheria;
    2
    (f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
    kutokana na kazi yake
    (g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
    wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
    kwa vizazi vyao;
    (h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
    sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
    muhimu za kuukuza uchumi; na
    (i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
    kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
    kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
    mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
    na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
    na siasa ya watu wote kuwa sawa.
    MADHUMUNI YA TANU
    Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama
    hivi yafuatavyo:-
    (a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;
    3
    (b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara
    kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu.
    (c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya
    watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist;
    (d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika
    vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
    (e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa
    kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;
    (f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na
    kudumisha vyama vya ushirika;
    (g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa
    katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;
    (h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
    wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;
    (i) Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,
    vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;
    4
    (j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara
    njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo
    itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
    (k) Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika
    Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
    (l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama
    ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.
    5
    SEHEMU YA PILI
    SIASA YA UJAMAA
    (a) Hakuna Unyonyaji:
    Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
    ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya
    chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
    watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
    kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
    hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
    aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
    hayapitani mno.
    Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
    kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
    ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
    kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
    kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.
    Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
    chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
    vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
    ikapanuka na kuenea.
    6
    (b) Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya
    kazi:
    Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
    kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
    zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi
    wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
    vyao vya Ushirika. Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama
    kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.
    Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
    maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
    usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
    biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
    simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
    ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
    kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
    mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
    katika viwanda vikubwa.
    Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa
    zinamilikiwa au kutawaliwa na Serikali ya Wananchi.
    7
    (c) Kuna Demokrasi:
    Nchi haiwi ni ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au
    zote za uchumi hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti
    Serikali iwe inachaguliwa na kuongozwa na Wakulima na
    Wafanya kazi wenyewe. Serikali ya Makaburu wa Rhodesia au
    Afrika ya Kusini ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi, hiyo
    itakuwa ni njia ya kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta
    Ujamaa. Hakuna Ujamaa wa kweli pasipo na Demokrasi ya
    kweli.
    (d) Ujamaa na Imani:
    Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani
    Ujamaa ni imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini
    na kufuata kanuni zake. Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na
    Wajamaa wenzie, yaani waamini wenzie katika imani hii ya
    kisiasa na uchumi ni wote wale wanaopigania haki za wakulima
    na wafanyakazi katika Afrika na po pote duniani. Wajibu wa
    kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU, ni kutii
    kanuni hizi za ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na
    hasa mwana-TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu
    mwingine au kufanya jambo lo lote ambalo ni la kibepari au
    kikabaila.
    8
    Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na
    siasa ya ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa
    ni imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya ujamaa
    ikiwa hawaikubali imani hiyo.
    9
    SEHEMU YA TATU
    SIASA YA KUJITEGEMEA
    Tunapigana vita:
    TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na
    kulitia katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa
    Tanzania (na wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhiki na
    kuwa katika hali ya neema.
    Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha,
    na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya
    tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi;
    mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena.
    Mnyonge hapigani kwa Fedha:
    Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
    silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
    unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
    sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
    vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
    yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha ndiyo msingi wa
    maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo”!
    10
    Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
    kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
    mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
    wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
    Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
    mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
    wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha
    tutaendelea, bila fedha hatutaendea”!
    Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake
    kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu
    tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, “Katika miaka
    mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili
    kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000”. Kama tumetaja na
    tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja
    kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha
    kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.
    Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu
    yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa
    shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
    kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.
    Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina
    barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?
    11
    Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao
    mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au
    hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa
    huyo - kwa FEDHA.
    Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya
    chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba
    wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo
    kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
    mishahara na kujenga majumba bora - KWA FEDHA.
    Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana
    ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa
    kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko
    tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa -
    wa FEDHA!
    Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya
    mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za
    mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu
    wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!
    Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya
    makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo
    kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na
    12
    Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni
    Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
    maendeleo. Wizara zinapoleta makaidirio yao ya matumizi huwa
    zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
    Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake
    awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha.
    Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa
    kupunguza Makadirio yao ya matumizi.
    Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
    itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo
    ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge
    na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba
    Serikali haina fedha.
    Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
    Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
    walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
    shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
    Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
    tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
    zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
    Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
    kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
    13
    zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
    bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
    kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
    Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
    kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi;
    kwamba hata ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
    au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
    yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
    zaidi.
    Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?
    Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri
    kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za
    kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
    (a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure
    tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo.
    Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au
    Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya
    maendeleo.
    (b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
    kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.
    Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
    14
    Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
    maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
    kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
    (c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
    kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
    yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
    mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
    kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
    shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
    Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
    kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
    wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.
    Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
    nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
    la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
    viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
    za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
    ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
    viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
    neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada
    hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda
    kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda
    kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au
    15
    shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara
    hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo
    hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza
    mazungumzo ya neema!
    TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO
    Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
    kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
    Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
    kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
    nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
    Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
    zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
    ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
    viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
    Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
    zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
    msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
    katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
    zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
    Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
    kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
    16
    maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
    matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
    mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
    yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
    kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
    Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
    huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
    Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.
    MISAADA NA MIKOPO
    VITAHATARISHA UHURU WETU
    Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
    kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
    hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya
    Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au
    mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji
    kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi
    yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini
    kwa Uhuru wetu na uzima wetu.
    Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
    nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada
    17
    unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza
    maswali.
    Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
    “bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada
    itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha
    jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
    kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya
    kukuwezesha kuulipa.
    Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
    Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
    tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu
    maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni
    kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa
    walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.
    Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka.
    Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni
    wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia
    yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi
    inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama
    italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila
    vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali
    mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata
    18
    kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
    hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji
    katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
    Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
    Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
    mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
    kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
    uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
    faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
    kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
    wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
    tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu
    Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?
    Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
    misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha
    uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
    ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na
    Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila
    kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu
    wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
    Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
    ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
    19
    maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka
    nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata
    fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
    tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
    siasa nyingine za nchi yetu.
    TUMEKAZANIA MNO VIWANDA
    Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la
    pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema “Bila Fedha
    hakuna maendeleo,” ni kama twasema pia “Viwanda ndiyo
    maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo”. Hii ni kweli siku
    tutakapokuwa na fedha nyingi, tutaweza kusema kwamba
    tumeendelea. Tutaweza kusema, “tulipoanza mipango yetu tulikuwa
    hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha ulitupunguzia
    nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka zaidi. Lakini leo
    tumeendelea na tunazo fedha za kutosha”. Tumeendelea,kwa hiyo,
    tunazo fedha za kutosha”. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na
    maendeleo.
    Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema
    kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata
    viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu
    yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha
    viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha
    20
    zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa
    tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje kuja kuanzisha
    viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata
    fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia
    viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba hata kama tungeweza
    kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza kukapotosha siasa
    yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari kuja kuhozi
    viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote
    tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila
    labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi
    kujenga Ujamaa.
    TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI
    Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie
    zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha
    za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa
    kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika
    kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila
    kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi,
    fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa
    katika miji.
    Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
    hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
    21
    zilipwe. Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha
    zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda.
    Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu
    tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi
    na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje.
    Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa
    ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka
    mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na
    viwanda vyetu.
    Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni
    haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini
    hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi,
    basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu
    ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na
    fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika
    zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.
    Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi
    za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini
    wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.
    Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo
    sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha
    za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao
    hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika
    22
    miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama
    mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni
    wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao
    ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na
    maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu
    yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida
    kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na
    jasho la mkulima. Tusisahau jambo hili.
    Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa
    bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo
    na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza
    kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande
    mmoja; na wafanya kazi na wakulima upande mwingine. Pia
    twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa
    vijijini upande mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa
    wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.
    WANANCHI NA KILIMO
    Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha.
    Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji
    vitu vine: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora.
    Nchi yetu ina zaidi ya watu milioni kumi na eneo la eka 362,000.
    23
    MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO
    Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya
    kutosha. Nchi yetu inaweza kutoa mazao ya aina mbali mbali
    ambayo tunayahitaji kwa chakula na kwa fedha.
    Mazao ya chakula (na fedha kama tukiyatoa kwa wingi) ni
    kama vile mahindi, mchele, ngano, maharage, karanga n.k. Mazao
    ya fedha ni kama vile mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto,
    chai n.k.
    Pia nchi yetu ni nzuri sana kwa ufugaji wa ng’ombe, mbuzi,
    kondoo, kuku n.k. Pia twaweza kuvua samaki katika maziwa, bahari
    na mito.
    Wakulima wetu wako katika sehemu ambazo zaweza kutoa
    mazao haya, kama si yote walau mawili matatu au hata zaidi. Kila
    mkulima wetu aweza akaongeza mazao haya ili ajipatie chakula kingi
    zaidi au fedha nyingi zaidi. Na kwa sababu nia kubwa ya
    maendeleo ni kupata chakula zaidi na fedha zaidi kwa ajili ya
    kujipatia mahitaji yetu mengine, ndiyo kusema kuwa jitihada ya
    kuongeza mazao ni jitihada, na kwa kweli ndiyo jitihada peke yake,
    ambayo italeta maendeleo, yaani chakula zaidi na fedha zaidi kwa
    kila mwananchi.
    24
    MASHARTI YA MAENDELEO
    (a) Juhudi:
    Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi
    anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja
    kubwa ni JUHUDI. Twendeni vijijini tuzungumze na wananchi
    kuona kama inawezekana au haiwezekani wananchi kuongeza juhudi.
    Kwa mfano, katika miji, mfanyakazi wa mshahara hufanya kazi
    kwa saa saba na nusu au nane kutwa kwa muda wa siku sita au sita
    na nusu kwa juma. Tuseme saa 45 kwa juma, kuondoa majuma
    mawili au matatu ya livu, katika mwaka mzima. Ndiyo kusema
    mfanya kazi wa mjini hufanya kazi ya saa 45 kwa juma kwa majuma
    48 au 50 kwa mwaka.
    Katika nchi kama yetu muda huu ni mdogo kwa kweli. Nchi nyingi
    hata zilizoendelea kutuzidi – hufanya kazi kwa muda mrefu zaidi
    kuliko saa 45 kwa juma. Si jambo la kawaida nchi changa kuanza na
    muda mfupi kama huo. Jambo la kawaida ni kuanza na muda mrefu
    zaidi na kuupunguza kila nchi inavyozidi kuendelea. Sisi kwa kuanza
    na muda mfupi huu na tunapodai muda mfupi zaidi kwa kweli tunaiga
    nchi zilizoendelea. Na kuiga huku kunaweza kukaleta majuto. Lakini
    hata hivyo wafanya kazi wa mishahara hufanya kazi ya saa 45 kwa
    juma; livu yao kwa mwaka haizidi majuma manne.
    25
    Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi kwa
    saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi mno
    ambao hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa
    mshahara.
    Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi.
    Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana
    livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye
    yote katika Tanzania. Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina
    mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni
    ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi
    sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na
    kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo
    ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri.
    Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda vijijini
    na kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na kwamba ni
    wajibu wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na faida ya Taifa letu.
    (b) Maarifa:
    Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi
    kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia jembe kubwa
    badala ya jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa na ng’ombe badala
    26
    ya jembe la mkono, kutumia mbolea badala ya ardhi tupu,
    kunyunyizia dawa ili kuuwa wadudu, kujua ni zao gani lifaalo
    kupandwa na zao gain lisilofaa, kuchagua mbegu vizuri kabla ya
    kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, wakati wa kupalilia n.k.,
    ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa mazao mengi zaidi.
    Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni fedha
    na wakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko fedha na
    wakati mwingi tunaotumia katika mambo mengi tunayoyaita
    maendeleo.
    Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka
    mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni ile
    inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. Pamba, kahawa,
    korosho, tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka sana
    katika muda wa miaka mitatu iliyopita. Lakini ni mazao ambayo
    yameongezeka kwa sababu ya juhudi na uongozi wa wananchi, siyo
    kwa sababu ya fedha.
    Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au
    msaada kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo huko
    vijijini. Wamejenga shule, dispensary, majumba ya maendeleo,
    wamechimba visima, mifereji ya maji, mabwawa, mabarabara,
    wamejenga mabirika ya kukoshea mifugo na kujiletea wenyewe
    27
    maendeleo ya aina mbali mbali. Kama wangengoja fedha
    wasingeyapata maendeleo hayo.
    JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO
    Mipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna mingi
    ambayo imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya
    upungufu wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele za fedha.
    Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba
    tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama
    kubwa za kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga
    safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika
    kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya
    kuleta maendeleo kwa kila mtu.
    Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala
    hatutajenga viwanda au kufanya mipango yo yote ya maendeleo
    inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea
    wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu.
    LA, SIVYO. Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata mwaka
    tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina mbali mbali
    kuzidi mwaka uliopita. Kwani hiyo itakuwa ni dalili moja ya
    maendeleo yetu.
    28
    Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini
    ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU,
    ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo,
    fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo.
    Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala
    ya kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda vitakuja, na
    fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na
    hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea. Kwa hiyo
    basi, mkazo wetu na uwe:-
    (a) Ardhi na Kilimo.
    (b) Wananchi.
    (c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na
    (d) Uongozi bora.
    (a) Ardhi:
    Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea
    kutegemea kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha
    maisha yao barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa
    matumizi bora ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya
    binadamu kwa hiyo Watanzania wote waitumie ardhi kama ni
    raslimali yao kwa maendeleo ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni mali ya
    Taifa, Serikali ni lazima iangalie kuwa ardhi inatumiwa kwa faida ya
    29
    Taifa zima na wala isitumiwe kwa faida ya mtu binafsi au kwa watu
    wachache tu.
    Ni wajibu wa TANU kuona kuwa nchi yetu inalima chakula cha
    kutosha na kutoa mazao ambayo yataleta fedha nchini kwa kuuzwa
    katika nchi za ng’ambo. Ni wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika
    kuona kuwa wananchi wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi
    unaohitajika katika kilimo na ufugaji wa kisasa.
    (b) Watu:
    Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni budi
    wajengwe moyo na shauku ya kujitegemea. Wajitegemee katika
    kuwa na chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali pazuri pa
    malazi.
    Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi na
    uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika upande
    wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka waliomo
    nchini ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje wenye nia
    mbaya ya kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari kulilinda Taifa
    inapolazimika kufanya hivyo.
    30
    (c) Siasa Safi:
    Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya
    Ujamaa ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye kazi
    na aishi kwa jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta usawa wa
    kugawana mapato ya nchi ni lazima kila mtu atimize wajibu wake
    kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Asiweko mtu wa kwenda kwa
    ndugu yake na kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi kwa sababu
    atakuwa anamnyonya yule ndugu yake. Vile vile mtu ye yote
    asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo mijini au vijijini bila kufanya kazi
    ya kumwezesha kujitegemea mwenyewe bila kuwanyonya ndugu
    zake.
    TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi aweze
    kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na wananchi
    wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu wote. Ili
    kudumisha Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara ni budi
    kujitegemea kwa kila hali bila kwenda kuomba misaada nchi zingine.
    Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi.
    Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa
    tawi zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegemea kwa Wilaya
    ambayo ni kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote ni
    kujitegemea kwa Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.
    31
    (d) Uongozi Bora:
    TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo
    ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa
    hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu
    mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili
    waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe
    mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia.
    32
    SEHEMU YA NNE
    UANACHAMA
    Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na
    wanachama wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania vita
    vya kumng’oa mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU kufanya kwa
    wakati huo. Lakini sasa Halmashauri Kuu inaona kuwa wakati
    umefika wa kutilia mkazo kwenye imani ya Chama chetu na siasa
    yake ya Ujamaa.
    Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye
    Chama kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye Chama kifuatwe na
    ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei kuwa anakubali imani,
    madhumuni na sheria na amri za Chama, basi asikubaliwe kuingia.
    Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni Chama cha wakulima na
    wafanyakazi.
    33
    SEHEMU YA TANO
    AZIMIO LA ARUSHA
    Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika
    Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka
    29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
    A. VIONGOZI
    1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
    mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
    kikabaila.
    2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
    3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
    4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
    5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
    6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
    ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
    vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya

    Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha
    Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye
    vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
    kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).
    B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE
    1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwisha chukua
    mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.
    2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue
    hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama
    ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.
    3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
    kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na
    wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za
    ng’ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya
    miaka mitano. Halmashauri Kuu ya Taifa inaazimia mpango
    huo urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.
    4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali
    hayapitani mno na yale ya wafanya kazi Serikalini.
    5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 30, 2008

    Ha ha ha...nakuunga mkono Kido
    huwa mnara unakumbusha Ilboru na headmaster mzee Bino, nakumbuka ukifika hapo ushaingia A town bila unifomu kilichobaki ku'check gari ya headmaster tu...

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 30, 2008

    muungwana acha kuchemsha!! mwalimu alikuwa na short coming kibao, mojawapo ni hiyo ya azimio la arusha, ngoma hiyo ilikuwa plain failure bila ubishi. ingawa alifanya mambo mazuri mengi.azimio killed the speed and potential we had.

    ReplyDelete
  25. Mnara huo unanikumbusha kuwa tumemsaliti Seth Benjamini Mpinga aliyetembea kwa mguu mpaka akafa na kuwa mhanga wa kuliunga Azimio la Ujamaa na Kujitegemea la Arusha lililobatilishwa na Azimio la Ubinafsi na Kutegemea la Zanzibar!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 30, 2008

    Maoni yaliyotolewa na mchangiaji nimeyapenda wewe una akili sana, uko wapi nikupe uwaziri manake unaelewa chanzo cha uchumi kuwa mbovu Tanzania,nahisi hautakuwa fisadi.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 02, 2008

    this reminds me why bongo is the dumbest country in africa, 45 years of peace but nothing except poverty,ignorance etc, some people here turned nyerere into a cult figure worthy worshiping, wengine bado tunavaa vipicha vya nyerere, kumbukeni mlikuwa mnavaa wakati alipokuwa hai na sasa bado mnavaa bado, somebody smart mentioned seth benjamin huyo ndio anastahili tuvae picha zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...