wadau kunradhi,

nimepata email nyingi zikinitaka nirejeshe tena zoezi la wadau kutuma salamu na picha kwenye globu yetu ya jamii. zoezi lilisitishwa baada ya baadhi ya wadau kuanza kamtindo ka kutuma picha ambazo sio zao na wengine kutuma picha bila idhini ya wenye nazo na kusababisha hali ya hewa kuchafuka.

mie ni mtumishi wenu na nasikiliza nini mnanituma. kwa hiyo naomba kuuliza kama turejeshe tena hilo zoezi ambalo kwa namna fulani huwa gumu kujua endapo picha na salamu zilizotumwa ni za mleta ujumbe.

hii imekaaje nami hupenda sera ya wengi wape. nasubiri amri yenu wadau na maelekezo ya nini kifanyike kuendeleza libeneke hilo ambalo hata mie nakiri lina raha yake kama maadili yatafuatwa.

naomba kuwasilisha...
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 73 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2008

    Michuzi, huyo demu aliyesababisha libeneke la salamu kusitishwa kwa kifupi alikuingiza mkenge!! Hakuna kitu cha mtu kutumia picha ya mtu kwenye blog ili kuharibiana!!! Picha aliweka mwenyewe akitegemea mambo yatakuwa mazuri, na yakawa kinyume chake!! Ndo ikabidi atugeuzie habari. Any way maoni yangu ni kwamba LIBENEKE LA SALAMU/UCHUMBA KWA NJIA YA PICHA LIENDELEE KAMA KAWA.
    Natanguliza shukrani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2008

    HAİNA MPANGO BRO MİCHU BORA TUBAKİ HİVİ NDO BLOG İNAKUA İMETULİA KWA MTAZAMO WANGU

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2008

    Alaa,kumbe hako kamtindo ka salamu na picha kalikuwa kamesitishwa.
    I HARDLY NOTICED.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2008

    Jibu unalo, sisi hatujui, wewe ni kichwa ngumu, watu wanachotaka wewe unakataa watu wakikataa wewe ndio unapendelea. Hii ni blog yako, fanya ufanyavyo, maana wewe kushaurilika mpaka mtu akuite "KAKA MICHUZI". Wau mnapenda kubembeleeeeeeezwa utadhani kuna blog moja! Kwanza kuuliza hivyo ni kutu fool tu baada ya mijadala kuonekana inafifia kwenye blog wala huna lolote!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2008

    Michuzi sisi ni watu wazima acha kutusumbua, kama unataka blog ya salaam acha watu watume, kama hutaki basi, sisi unatuuliza kwani blog yetu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2008

    sasa mkuu umeojinea mwenywewe uchafuzi wa hali ya hewa usio na kikomo hao hao wachafuzi watatuma comments na kusema utaratibu urudishwe halafu watachafua tena ni naona bora ufe tu...we endeleza libeneke tu kaka.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2008

    Hii sasa Michuzi ndio sasa wewe unachafua hali ya hewa. Swali gani hilo?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2008

    i dont think that is a very good idea,mm naona ni muhimu sana tutransform this bloq to a developmental one rather than posting pics...attracting idiot comments.we have so many things to post scholarships,employments and many other positive things sio umbea na ujinga,if u make simple research u will see,those news of great importance receive few comments upumbavu comments mia.

    mdau,UK

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2008

    Poa tu lakini watuma salamu wasije kukulamikia kwa comments zitakazo tolewa na wasomaji wa blog yako kwani humu ni kama baharini kuna viumbe wa aina tofauti. Naomba watakaojitangaza wajiulize mara2 kabla ya kukimbilia kutafuta umaarufu kwenye blog kwani hali ya bahari haitabiriki na yaweza kuchafuka wakati wowote na kuhatarisha utu wao mbele ya waungwana. Nashauri pia watu kutuma picha nzima na siyo kipande ili tuangalie usafiri kama unalipa tehee!! teheee!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2008

    Michuzi wewe kama tarishi au Mesenja naomba usiruhusu hiy hali kwani ni kweli baadhi ya watu hutuma picha siyo zao, na hali hewa kuchafuka. Zuia kabisa kwani tunaharibiana bila sababu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2008

    Mimi naomba zoezi liendelee.Swala la kusibitisha itakuwa rahisi kuna njia mbili.
    1. ufanye kama benki wanavyofanya kumthibitisha mtu.Kila anaeyeta picha ambatanishe na passport yake iliyokuwa scan ile sehemu ambayo ina picha yake,Kama ana passport ascan kitambulisho chake cha kula,AU kitambulisho chochote kinachokubalika.
    2.Watu wajisajili kwa kuleta majina na picha zao na wewe kuziweka kwenye data base yako.Alafu utakuwa unatoa picha za wale tuu waliojisajili kwako.
    By KK

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2008

    kaka misupu kwanza habari yako na hongera kwa kutufanya tujisikie tuko nyumbani kwa kutuhabarisha udaku na nyepesinyepesi za nyumbani tz kila siku na kadri zinavyotokea! mimi nafikiri hili zowezi la salamu kwa picha ni zuri sana lakini tatizo ndio kama vile ulivyosema mwanzoni kuwa watu si waaminifu wanatuma picha si zao na bila idhini ya wenye picha hizo. basi kutokana na hilo bro michu mimi naona wadau wenyewe tuidhinishe kuwa urudishe utaratibu huo na kukuahidi kuwa hakutakuwa na malalamiko namaanisha kwamba kama wadau wenyewe tukikupa go ahead na zowezi hilo na kama ikitokea mtu picha yake imewekwa hakuna kulalamika kwani zowezi tumeliidhinisha wenyewe! kwa hiyo lolote likitokea tena wewe kaka michuzi akha mchanga wa pwani huooooo! haumo au unaiona imekaaje hiyo kaka?
    mdau katelephone! uk

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2008

    Hapana! Kaka Michuzi!Uwanja wa baraza hii upitiwa na wadau wenye lika,wazifa,jinsia mbali mbali,tusengependa BLOG YA JAMII igeuzwe kijiwe cha kuchafuliana
    ali ya hewa,
    Bada yake nakuomba Salam zisiwekwe,bali matangazo ya MISIBA,Sherehe na matukio ambayo wengi watahitaji kupashwa habari,vinginevyo patageuzwa kijiwe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2008

    Mishuzi tafadhali Bana usiruhusu kwani kinachogomba hapo ni picha za watu kutumwa na bila idhini na vile vile hutumia picha za makundi. Mmepiga watu wanne anatuma mmoja kinachofuata ni matusi au kashfa. Suggestion kama unataka kuweka hizo picha hakikisha hawapost maoni.thx

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2008

    wahuni wapo kila mahali, lakini naamini wengi hatuna tabia za kijinga. japo mimi si mtuma salamu, lakini naona hakuna haja ya kuwanyima nafasi wanaopenda kusabahi jamaa zao kupitia hapa,kwa sababu tu ya kuhofia wahuni. Pia itatoa nafasi kupata maoni ya kundi lingine la wachambuzi wa salamu a.k.a "waosha vinywa", ambao sasa wakuwa kimya muda mrefu, lakini madongo yao yanachangamsha pakubwa na kukosoa kama si kuudhi pia.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2008

    Mimi mdau wako Lazaro Mwaipungu,
    hapa London. Tulikutana ktk Diaspora ya London-UK.
    Ebwana rudisha tena ile fursa ya kutoa salaam ktk blog yako.

    Asante sana mzee.

    LM

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 13, 2008

    Sheikh Issa Michuzi, Wewe ni mtu mzima na pengine una watoto, na kama huna inshaallah mwenyezimungu atakupa yeye ndio mwenye uwezo wa maamuzi makubwa, sie maamuzi yetu madogo ila nakushauri ni vizuri watu kutoa salamu, haya ndio unatakiwa kufanya

    1. Salamu ni kitu kizuri kwa waliopoteana.

    2. Sheikh Michuzi wewe ndio mwenye uwezo wa blog, ila sababu unaheshimu watu umewauliza kwa njia nzuri wanadamu wenzako, kuhusu kutuma pic.

    3. Kila binadamu anauwezo wa maoni ila yawe mazuri tu, sababu maoni yawe ya heshima wewe ndio unauwezo wakuzuia maoni machafu yanaotumwa na watu wasiokuwa na adabu.

    4.Issa Michuzi hasa wale wanaaooandika na number za simu na mail bila sababu za kujuwa je ndio wao hao fanya kama mtu unamjuwa na unahuwakika naye. msalimie fundi mussa mwambie kawachakupiga kiwi kandambili pia. from mbele Torres na fabiano au Torres na Villa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2008

    Brother.
    To be on the safe side na kuendelea kulinda heshima yako bora ungeacha tu.
    Maana wachafuaji hewa ni weng, wanatuma picha za watu wengine na kuwadhalilisha.
    Wacha tu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 13, 2008

    Zoezi zuri watu kufahamiana, kuwasiliana na vitu kama hivyo tatizo ni wale wanaochafua hewa. Na kama ulivyosema ni ngumu kujua kama picture ni mwenye kutuma salaam. Mtu ana hasira na mtu, labda alipigwa kibuti anambandika humu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 13, 2008

    Rudisha ila za kutafuta wachumba na kazi hapana!Hapa ndipo kwenye uchafuzi wa hali ya hewa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 13, 2008

    michu, achana kabisa na mambo ya picha labda wadau watume salam bila picha, watatuibia picha zetu,

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 13, 2008

    anaekutumia picha lazima atume picha mbili tatu alizopiga na jamii ili kuhakikisha kama ndio yeye mwenye picha.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 13, 2008

    KAKA MICHUZI SWALA DOGO SANA LISIKUUMIZE KICHWA.
    USHAURI WANGU NI KWAMBA WATU WANAOTUMA SALAMU TU AU WALE WANAOTAFUTA WACHUMBA, WEKA SALAMU ZAO HEWANI BILA PICHA KWANI HATUJUI KAMA PICHA NI ZAO AU HAPANA.KWA NJIA HIO WATU WOTE WANAOUTUMA SALAMU AU WANATAFUTA MCHUMBA WAWEKE EMAIL ADDRESS ZAO AMBAZO WADAU WATAKAO PENDA KUWASILIANA NAO WAWASILIANE KWA EMAIL NA HUKO NDIO WATUMIANE PICHA WENYEWE.
    SASA KWA VILE WATAWASILIANA KWA NJIA YA EMAIL,CHA KUFANYA WEWE KUEPUKANA NA WACHAFUA HALI YA HEWA BLOCK COMMENTS ZOTE.USIWEKE OPTION YA KUTOA COMMENT KWENYE POST YOYOTE YA SALAMU AU YA KUTAFUTA MCHUMBA,WAACHE WAWASILIANE KWENYE HIZO EMAIL UTAKAYO WEKA KUAMBATANA NA SALAMU.
    mdau mzawa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 14, 2008

    Haya kaka naona akina Manka wamemiss kujitangaza na sasa wanarudi kwa staili nyingine.

    Mie sina pingamizi kabisa. Waruhusu wadau wajirushe maana wengine umaarufu wameupatia hapa hivyo itakua vibaya kuwabania wengine wasipitie njia hiyo.

    Najua kuna watu watakua wanatumia vibaya lakini hiyo isiwanyime uhondo wadau. Hebu fikiria yahoo/gmail/msn wangeamua kufunga mail zote kwa ajili kuna watu wanatumia vibaya (scam).

    Warushe warembo tuwaone, tunaweza kuwa waume watarajiwa.

    Ignorant, Jeremani

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 14, 2008

    Kusema kweli libeneke la salam lilikuwa na raha yake. Maana tangu lisitishwe hata wakina-Chibiriti wameadimika kabsaaaa.

    Kwa maoni yangu ni vyema lirejeshwe ila sijui ni nini kifanyike kudhibiti fitna za wachafua hewa.

    Mdau- Amsterdam

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 14, 2008

    Go ahead and unleash the fire, post those pix's n greetings koz i m missin all the krazie, unsuspected comments by wana glob. Michu keep knowin those comments usually make our day, to some of us.
    Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 14, 2008

    Anzisha libeneke hilo, we r waitin kwa hamu hehehehehehe

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 14, 2008

    Kaka Michuzi wewe ni Mwandishi wa siku nyingi sana mimi nakusihi kwamba jambo hili sio la wengi wape ni jambo la sheria na masilahi yako na wadhamini wako kuweka salaama kwa picha ni jambo zuri lakini pia zingatia kuwa kunawatu ambao huweka picha ambazo sio zao na wewe hujui au huna jinsi ya kuthibitisha sasa katika ulimwengu huu wa sheria unaweza kupata matatizo ya bure ya kushitakiwa kwani wewe nawadhami wako TIGO wote mko liable kisheria kuhakiki kama mweka picha ni yeye na kwa kuwa uwezo huu huna BASI MIMI USHAURI WANGU NI KWAMBA USIWEKE HIYO NAFASI BALI UNAWEZA KUWEKA SALAAM BILA PICHA KWANI UJUMBE UTAFIKA.
    BY JUDGE USA 2008

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 14, 2008

    Nafikiri ni vizuri kwa watu kutuma salamu zao lakini wabongo inabidi tuendelee kidogo kwani sio kitu cha ajabu ni kama vile ilivyokuwa kwenye radio zetu za bongo lakini kwa kutumia mtandao. Kuwe na masharti kwamba iwe ni salaamu tu kwa ndugu, jamaa na marafiki na sio kutafuta wachumba au kazi au kujionyesha wewe na maendeleo yako unless iwe unanufaisha jamii nzima ya watanzania. Wenye nia hizo wanaweza kuanzisha blog zao au kutumia zile ambazo ziko kwa ajili hiyo bwana Michuzi nafikiri umenipata. Kwa hiyo mimi naunga mkono libeneke la salamu kuambatanisha na picha liendelee ila tuwe wastaarabu na kuona ni kitu cha kawaida sio kuwadhalilisha watu wengine kwa sababu zao binafsi. Awe mbeba box au chibiriti hii ni sehemu ya kutakiana mema hasa kwa wale ambao wako mbali na jamaa zao.
    Asante Ndugu Michu

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 14, 2008

    Liendelee

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 14, 2008

    RAHISI SANA:

    1. Blog ni kioo cha jamii husika (washiriki)

    2. Kama watu wengi wanatoa maoni kwenye mambo kama salamu ni vema

    3. Kama watu hawatoi maoni kwenye masuala ya maendeleo ni sawa

    Hitimisho:
    Kama watu wengi wanapenda 'kuchafua hali ya hew' kwenye salamu, na kutoa maoni mengi 'kwenye mambo ya kijinga (kama mdau mmoja alivyosema hapo awali) Ina maana hii ndio jamii tuliyonayo. Ndivyo tulivyo.

    Kama watu hawapendi kutoa maoni kwenye masuala ya 'maendeleo' basi hapa si mahali pake, kwani ndiyo jamii husika inavyoonyesha.

    Takwimu za maoni zinaonyesha hivyo, na wewe (Michuzi) kama mmiliki wa blog, wape kitu wana jamii yako wanapenda kuchangia.
    Au?

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 14, 2008

    Salamu na picha ni vizuri sana, lakini hayo maoni ya kuchafua hali ya hewa ni wewe unaekubali kuweka, na kama kila mwenye maoni machafu hapati nafasi ya kuwekewa maoni yake basi nina uhakika kila anaetaka kuchafua hali ya hewa hatosubutu kwasababu anajua kuwa maoni yake hatabandikwa.
    Pia nakulaumu sana michuzi kwa kubandika maoni ya wachafuwa hewa. Nashangaa kwanini unaweka mwenyewe maoni hayo machafu?.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 14, 2008

    Michuzi, wala usipoteze muda. Wabongo wapuuzi kweli. Kitu kizuri wanaharibu. Wivu tele! Acha itapunguza usumbufu na bugudha!

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 14, 2008

    HAPANA HAPANA, TUNAPIGA PICHA NYINGI KWENYE SHUGHULI MBALIMBALI, na PICHA ZETU ZIKO KWA NDUGU NA JAMAA MTU ANAWEZA KUFANYA CHOCHOTE NA HIZO PICHA ZETU BILA IDHINI YA WAHUSIKA . no picS , no picS.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 14, 2008

    bwana michuzi mi naona bora ilo zoezi liendelee,humu kuna watu wa aina tofauti usiwabanie matakwa yao,wakichafua hali ya hewa kivyao na mitazamo yao,na ukiangalia kwa makini salamu za hivo ndo zilikua zina comment nyingi kuliko.
    kwa hiyo kaka ENDELEZA LIBENEKE LA SALAM NA PICHA.hata mimi nimemiss sana yani tangu ustopishe hilo zoezi hata sijawahi kucheka.R.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 14, 2008

    Bro michuzi, hii blog ni yako na kwa ajili ya kuhabarishana. Watu wamechezea vibaya nafasi ya kutuma salam na sirahisi kwa ww kugundua kama anyekutumia picha ni mhusika anaetaka salaam zake ziende. Idea ya Salam naipinga. Kwanza zitajazana salaam nyingi na habari chache.
    Kwakifupi salam NO

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 14, 2008

    wewe ni mpiga picha halafu hutaki picha?? silipati hili. unajua kabisa rating yako imeshuka tangu usitishe picha. picha zaongea zaidi ya maneno .kama unataka kuizika hii blog basi sitisha picha.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 14, 2008

    Nafikiri kukata kabisa huduma hii utakuwa unaumiza wengi. Siamini kuwa iwapo samaki mmoja akioza, basi wote tuwatupe. Nafikiri kitu kizuri ni kuangalia nani anatuma hizo picha/ujumbe. Iwapo mtu ana sign anonymous wakati wote, mie nisingetundika picha zake. Iwapo mtu ni blogger au anatumia jina ambalo linalolingana na e-mail anayotumia kukutumia hizo picha/ujumbe, then tunaomba uweke huzo picha. Naelewa kuwa kufungua new e-mail account sio kazi, ila hiyo itapunguza spidi ya wagonga vichuguu waletao matatizo yao ya vichwa humu.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 14, 2008

    Hivi nyio wote mlochangia hamjui nini maana ya Blog Hata huyo michuzi mwenyewe hajui ..anataka kufanya hii blog kama ni ya kitaifa au inaendeshwa na serikali .. nini wewe bwana acha ushamba hapa ni kijiweni toa picha yoyote hata ya muheshimiwa akiwa na madhambi, ndio maana ya blog ni kijiwe cha watu kuongea utmbo na mazuri .. tena wewe Michuzi hii Blog yako unaendesha kwa sera za CCM TUMESHATOA MAONI KIBAO KUHUSU CCM HUYATOI.. unachuja habari ,, kwa taarifa yako blog ..za huku Marekani unapotuma maoni yanakwenda moja kwa moja .. hakuna hata haja ya wewe kuyapitia.. Hii ni Internet news ,, ndio maana unaona kuna ponno sites humu ..

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 14, 2008

    MISUPU MI NAPENDEKEZA LIBENEKE LIENDELEE TU,ILA MAONI YA KUDHALILISHANA USIYAWEKE
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 14, 2008

    Mambo ya long time hayo mirojo achana nayo kama salamu siwapigiane simu. tunataka habari za maendeleo siyo habari za kutumiana salamu unaweka na picha yako hahahahaaaaaaaa.
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 14, 2008

    Zoezi liendelee kwani matusi ni kitu cha kawaida, kama siyo hivyo utajuaje kuwa hayo ni matusi. kuna wengine tunapata raha kwa kusikia waosha vinywa wanavobweka. endeleza!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 14, 2008

    BWANA MISUPU SASA NAONA KUWA HAUNA MSIMAMO KABISA .MTAZAMO WANGU UNGEKUWA MAKINI SANA KABLA YA KUKURUPUKA TU NA KUANZA KUTOA MAWAZO HAYO YA KUSITISHA KUTUMA PICHA NA SALAM KATIKA BLOG HII MUHIMU.NASHAURI TU BORA UACHANE NA HUU MTINDO MAANA IKITOKEA TENA HALI IMECHAFUKA ,HAUONI KUWA UTAKUWA KWENYE WAKATI MGUMU SANA NA ITAPELEKEA BLOG YAKO WATU WAILAZIMISHE IFUNGWE MAANA INAONESHA KWA MTINDO HUU ,KUNA KAUFISADI KWA MBALI KANAKOOKANA NA UTUMAJI WA PICHA NA SALAMU
    KUWA NA MSIMAMO MKUU WEWE NI MTU MUHIMU SANA KTK KUENDELEZA LIBENEKE AMBALO WENGINE WANATAKIWA WAIGE
    MDAU
    SWEDEN

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 14, 2008

    Kaka Michu,
    Hapo tu umeuliza wadau kwa heshima tayari mtu keshakuandikia upupu, hao ndio wachafuzi wenyewe.Mi naona kama kurudisha iwe ni salamu bila picha. Kama haiwezekani zoezi lisirudi kabisa. Manake wachafuzi wa hewa wako tayari kufanya mambo usiwape nafasi.

    Kazi njema
    Mdau Moshi

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 14, 2008

    Matusi hayaui .... Infact zile salamu ni part of entertainment ... Zirejeshwe haraka iwezekenavyo lakini kuwepo na masharti katika utumaji wa picha kama wadau wawili watatu walivyoshauri hapo juu

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 14, 2008

    MICHUZI MIE NATOA MAONI KUWA PICHA ZA WATU WAZIMA USIWEKE,HILA PICHA ZA WATOTO WANAOTOA SALAAM KWA NDUGU NA JAMAA AU BIRTHDAY ZA WATOTO PLEASE PLEASE WEKA,LAKINI MTU KUOMBA KAZI NA KUWEKA PICHA NOOOO...UCHUMBA HAPA SIO MAHALA PAKE..KAMA MTU ANATAKA MCHUMBA AENDE KWENYE
    www.match.com asante ni hayo tuu

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 14, 2008

    Ama kweli kazi ya jamii si mchezo.Nikienda str8 to ze point naomba usirudishe salamu zina kera.Kitu pekee ambacho sina kinyongo nacho ni ile ya kutafutana.Ukirudisha SALAM tuta-doubt uimara wa misimamo yako.nakumbuka ile mail ya kusitisha salamu ilikuwa kali mno sidhani kama umesahau machungu yale.Napongeza hatua yako ya kutushirikisha

    USIRUDISHE SALAMU...

    Mdau wa Mayfair

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 14, 2008

    WATANZANIA NI WAVIVU SANA WA MAMBO YA MAENDELEO.MMEWEKEWA POST YA MAMABO YA SULLIVAN SUMMIT INAFANYIKIA NCHINI KWENU LAKINI HAMNA COMMENT HATA MOJA! UMBEYA TUUUUUUU WA LIBENEKE LA SALAMU!!HOOOVYO!!!

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 14, 2008

    mimi naona haina mpango mambo ya kishamba mtu kutuma picha yako binafsi umepiga eti uko na mchumba wako, naonelea ungekuwa unaweka picha ulizopiga wewe mwenyewe au toka kwenye kampuni yako, hata ikiwa ya tu na mchumba wake kwani kwa kufanya hivyo lazima utakuwa wewe michuzi wamekupa ridhaa yao wenyewe uso kwa macho na masikio.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 14, 2008

    maoni ya namna tofautitofauti yatakuwa mengi lakini muamuzi wa mwisho ni wewe mwenyewe kwa kuzingatia MALENGO na NIA yako kuanzisha hii blog.i believe you have your objectives and you knew that there might be "kuchafuka kwa hewa". blog hii ni kama chombo kingine cha mawasiliano; kwahiyo sidhani kama wadau wanaweza kuwa wanakuamuru nini ufanye na nini usifanye. mfano: sidhani kama wasomaji wa gazeti wanaweza kumuamuru mchapishaji awe anachapisha nini kwa kuzingatia wao wanavyoona ubaya au uzuri wa hicho wanachokitaka.
    ushauri wangu: kaa na fikiria kwa makini, ukipenda washirikishe na watu wako wa karibu/wanaokusaidia kuendeleza libeneke, kama unae mwanasheria mshirikishe pia bse kwa huko kuchafuka kwa hewa I sense somthing like tortious liability which may face you ingawa najua unazo kanuni na taratibu za kuendesha blog yako.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 14, 2008

    Blog itapooza kwani wengi tunapenda mambo ya maendeleo sio salam

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 14, 2008

    Michuzi,

    Jaribu kukaa chini japo kwa dakika chache ukiulize ni kitu gani kimeifanya blog yako kuwa maarufu haswa kwa wadau wa ughaibuni. Kwa maoni yangu ni picha ulizokuwa ukiweka za nyumbani pamoja na current news! Don't be distracted.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 14, 2008

    Hao wanaoomba hawana mema. Kwani kama mtu ana internet connection home si atume salam kwa e-mail au chatting. Sioni sababu hawana jema kwa kifupi.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 14, 2008

    Haina maaana

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 14, 2008

    Nini nia na malengo ya blog yako? Mission and vision of your blog?

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 14, 2008

    We nawe michuzi umechoka kweli, Kwani kunalazima gani mtu kutuma salamu aweke na picha? hizo salamu haziendi bila picha? kwani wale wanaotuma s alamu redioni wanatuma na picha? asa kama unataka hali ya hewa iendelee kuchafuka ruhusu picha humu ndani maana mtu anatuma comment yake kaongea pumba alafu anabandika na picha y ake macho yanamatege watu wataacha kusema kweli?

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 14, 2008

    Michuzi, sio wazo zuri, wanataka kuchafua jina lako, 4 sure

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 14, 2008

    Kama ni moja ya lengo la blog yako endelea. But binafsi sidhani kama nia yao ni njema, especially kwa jinsi ulivyosema kuwa kuna kipindi walichafua hali ya hewa.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 14, 2008

    VERY BIG NO

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 14, 2008

    Wape masharti magumu.
    Mfano:
    1. Picha iambatane na ya wazazi wake kama wapo hai. Na kama ameoa picha ya mkewe na Kama ana watoto picha ya watoto wake.

    2. Anafanya kazi wapi na address ya ofisini kwake.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 14, 2008

    hamna mpango kabisa

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 14, 2008

    Mr. Michuzi, labda nianze na kwa kukuuliza wewe mwenyewe kwamba, kama ingekuwa ni wewe ambaye picha yako bila idhini yako umeikuta kwenye blog hii ikiwa na ujumbe mfano wa kuomba kazi, kutafuta mchumba au ina ujumbe wowote ule kinyume na anri yako, utajisikiaje? Tena basi ujumbe wenyewe uwe wa kashfa au ambao utapelekea wadau kuchangia kwa kashfa na huku watu wengine wakijua kabisa ile sura na jina ni la kwako, hivyo wakaamini ni wewe ambaye umepeleka ile picha na ujumbe wakati siyo, je utafanyaje?

    Nimeanza kwa kukuuliza maswali hayo ili na wewe ujiweke kwa muda tu katika nafasi ya hao ambao imeshawatokea kwa kupitia blog yako. Be fair, ngoja nikujibie katika hili. Bila shaka ungejisikia vibaya sana. Na hata ukija kukanusha na kuweka ukweli, haitaweza kutibu vidonda vilivyokwishatokea katika ajali hiyo. Huo ndiyo ukweli na hali halisi.

    Bila shaka umeunda blog hii kwa nia njema. Hivyo, una wajibu pia kuilinda isije ikawaumiza watu ambao ni innocent. Tafadhali sana. Uwe mwangalifu usije ukajitengenezea maadui na watu wasio na makosa kwa kuwaumiza bila sababu. Hata kama ingekuwa ni mimi, ningekuchukia wewe, pamoja na blog yako. This is more serious kuliko unavyofikiria. This can cost someone's entire life kwenye jamii anayoishi kwa kumfikiria visivyo. So, please, please, be very serious kuhusu hili. JIBU NI MOJA TU, TAFADHALI USITOE PICHA ZA WATU NA UJUMBE BILA YA KUHAKIKISHA KUWA NDIYO WENYEWE WALIOKUTUMIA, PLEASE. HAPA NDIYO KIPIMO CHA WEWE KUKOMAA KATIKA MAAMUZI AMBAYO KIMSINGI YANAWEZA YAKAATHIRI WATU WENGINE.

    Kwa kukusaidia tu, kama ni lazima kutoa picha ya mtu na anaomba iwe na ujumbe mbali ya zile za misiba, basi alete yeye mwenyewe kwako na wewe utaihakiki picha hiyo na yeye kuona kuwa inaendana na sura yake na kisha ujiridhishe. Hii iwe kama ile ya kwenye passport tunaposafiri. Huwezi kusafiri na passport isiyo na picha yako. Never. Kwa wale wa mbali itabidi watafute hata ndugu zao na pia msainiane. Let it be legal kuliko madhara yatakayokuja kukupata kwa nia yako nzuri. Watu hatuaminiani siku hizi.

    Hata kwa hizo tunazosema za misiba, ni kwamba ndugu yangu unatake risk tu bila kujijua. Tumeaminiana sana. Umeshafikiria siku ambayo umeletewa picha ya mtu na kuambiwa kuwa amefariki na kutoa mpaka ratiba na mahali pa mazishi huku habari hiyo ikawa si ya kweli? Labda tu ni mtu amemchukia kupindukia na hivyo kumfanyia hivyo! Utafanyaje? Think aloud, think big. Huo usumbufu utakaokuwa umeusababisha kwa kupitia blog yako, utakuwa umewaathri wangapi wakati mtu atakuwa ni mzima wa afya? Kwa kweli tufikiri kwa upana zaidi suala hili kuliko tunavyoliweka.

    Ndugu yangu, nimeandika sana, lakini ushauri wa bure ndiyo huo. Ipo siku tu utajikuta unakuwa implicated na issues hata za kisheria kimzahamzaha hivi hivi. Maoni yangu na ushauri wangu ndiyo huo.

    Siki njema kaka.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 14, 2008

    Michuzi rudisha libeneke la salamu, kwa wale wanaotaka habari za kitaifa wanaweza kutembelea website za ippmedia,mwananchi, raimwema,tanzania daima, etc na kwa habari za kimataifa wanaweza kwenda cnn.com, bbc.com, deutchwelle,etc. Mimi ninavyoelewa ni kwamba blog ni kama kijiwe, kuna mambo ya KIUNGWANA na KISHENZI na unapoingia huko ujue uko tayari kukutana na mojawapo kati ya hayo mawili. Sasa nyinyi mnaomwambia Michuzi aweke news tu, kwa ufupi ni kwamba atakuwa anafanya duplication/copy and paste ya habari zilezile. Mfano ni habari kuhusu mkutano wa Sullivan, no comments kwa sababu tumeshazisoma habari zake kwenye magazeti na kuziona kila station ya TV. Kwa ushauri wa bure ndugu yangu Michuzi, ni kwamba anayetuma salama aambatanishe vitu vifuatavyo:
    1.Copy/scan ya passport/kitambulisho cha kazi/kupigia kura etc
    2.Picha kutoka kwa ma-anonmy marufuku
    Kwa mtindo huu sijui kama kuna atakayethubutu kutuma picha ambazo sio zake.
    Mdau,
    Sweden.

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 14, 2008

    kaka liendee kama kweli unasikiliza mawazo ya wadau wako

    dalali

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 14, 2008

    HATUNAMDA NA WASHAMBA WA PICHA KWANI MMEAMBIWA KUTUMA SALAMU MPAKA PICHA. ZILE ZILE ZA KALAPINA MNALETA! MULOX

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 14, 2008

    Salam na picha viendelee kama kawada Michuzi!!ila usizi-release coments za wachafuzi wa hali ya hewa!! mdau sweet wa arusha naomba tutafutane(hoseasichone@yahoo.com)

    Mdau,Arusha.

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 14, 2008

    Mi kwa ushauri wangu Libeneke la Salamu liendelee kama kawa.

    Tena kwa kuonyesha msisitizo hapa hapa mi naliendeleza,

    Kwanza kabisa napenda kumsalimia mchumba 'angu Nyaso akiwa Kinondoni,

    Na dada 'angu Janeth Mushi akiwa maeneo ya KIA

    Pili My bro Shebby akiwa Dom,

    Mpwa Ibrah nae pia wa Dom,

    pia napenda kumsalimia Thomas Mwaki-P na Salimu Ahmed wote wakiwa Precision-Air DSM

    Tatu ni kwa Wafanyakazi wote wa Engen Petroleum kurasini DSM

    Bila kuwasahau Wanachuo wote waliomaliza chuo cha CBE Account-division mwaka 2006-June.

    Mwisho kabisa ni kwa wana-libeneke wote wa blog yetu ya jamii,

    Ujumbe; Libeneke la Salamu liendelee kama kawaida, si mnaona navyojiachia kwa salam.

    Posted by ; Jamaa
    Date Posted ; 14/05/08

    ReplyDelete
  68. jamaa yako chibiliti ushauri wake alio kushauri unakutokea puani sasa bro!

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 14, 2008

    Brother Michu, libeneke la picha na salama liendelee kwani tangu limekamishwa tumekosa uhondo, wengine tulikuwa tunaburudika kwa kusoma comments za watu za kuchekesha hapa blogini, ila watu wasitumie fursa vibaya na kuanika picha za watu waweke zao....
    Mdau Tehran

    ReplyDelete
  70. AnonymousMay 15, 2008

    Mkuuu kazi nzuri nashukuru sana kwa kunipiga kapuni lakini sioni kibaya nilichoandika zaidi ya ukweli.

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 15, 2008

    HIVI WATU WAZIMA NYINYI NI KWELI KABISA MTU HAWEZI KUTUMA SALAMU BILA PICHA KIASI CHA KWAMBA MNAPOTEZA MDA WENU KIASI HIKI?
    MICHUZI KAMA HUWEZI KUHAKIKISHA PICHA UNAYOTUMIWA NA MTU SIO YAKE HUWE TAYARI KUWAJIBIKA KWA LOLOTE LILE BAADAE.

    ReplyDelete
  72. AnonymousMay 16, 2008

    Misupu upooooo! Saaalaaaaaaam hapoo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...