jk (saba kulia) akiwa na viongozi kibao wa nchi za afrika wanaohudhuria mkutano wa yokohama, japan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2008

    Njaa zinawasumbua

    ReplyDelete
  2. Sijawahi kusikia viongozi wa Afrika wakikaa kujadili masuala ya uchumi.
    Nadhani badala ya kwenda ugenini kufanya hivyo, ingekuwa vyema Waafrika tukaangalia jinsi tutakavyoweza kukuza biashara ndani ya bara letu.

    Mdau
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2008

    mafisadi oyeee

    maana naamini ufisadi haupo bongo peke yake!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2008

    HAKUNA UFISADI BONGO MSIWE MNAWAZUSHIA VIONGOZI LAWAMA HII NCHI BADO CHANGA NA VIONGOZI WETU KUPITIA CHAMA CHETU CHA CCM WAMEFANYA MENGI SANA MAJUMBA MAKUWA YA KILEO MAHOTELI YA KITALII TUMEKUWA NA SIMU ZA MIKONO NA HATA UTAMADUNI WETU UMEKUWA UNABADILIKA KWA KASI HAYO YOTE NI MATUNDA YA VIONGOZI WETU HAPA TANZANIA NINGEWAOMA KAMBA HIYO HIYO IPO SIKU TUTAISHI MAISHA YA NCHI ZA MAHARIBI SIO MUDA MREFU HIVI

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2008

    kaka wewe ni ccm unafikiria kila wakatin watu wanakuandama hizo ni fikira potofu ufisadi hauna chama nitabia ya watu wachache na imeonekana ccm wapo wengi ila mdau kabla yako kasema anaimani mafisadi hawaapo bongo tu kwa taarifa yako majumba unayo yaona bongo mazuri ni asilimia 10% ya watanzania asilimia 90% hawana ujanja huo wapo vijijini sasa unaongoza taifa lipi?10% wenye uwezo wakunyonya kodi za hii asilimia90% au90%?kazi kwenu wadau tuache uchama tupambane na mafisadi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2008

    we anon 4:48 ambaye ni mwana CCM damu damu,please tafadhali nielezee kuhusu ishu ya vijisenti chenge, basil mramba,gray mgonja, na fisadi Benjamin Mkapa bila ya kumsahau Balali, since wewe unaelewa sana mambo haya sio? SASA TOA MAJIBU,AU KUBALI KUDHALILIKA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2008

    sisi tuna rasilimali nyingi kinachohitajika sio misaada bali mbinu za kutufanya tujitegemeee..
    =================
    Pateni kichekesho cha mwaka
    +++++++++++++++++++++++++++++
    mzee mmoja fisadi anayeishi Masaki aliamua kumpeleka mwanae kwa babu na bibi yake kijijini Tanangozi.walipokuwa njiani wakielekea huko mzee akamwambia mwanae lengo la safari ni kumwonyesha jinsi walivyo matajiri. akamwambia sisi tuna nyumba nzuri mfano wa nyumba la kifalme yenye kabwawa ka-kuogelea,ka-bustani kenye miti,kajibwa,gari n.k.safari ilikuwa nzuri na kijana aliifurahi sana. waliporudi kwenye jiji la Kandoro mzee akataka kujua jinsi kijana alivyojionea hali ya umaskini kule bush. Mazungumzo takawa hivi:
    Mzee: kijana naona feedback ya safari yetu?
    Kijana:akaanza kwa kumshukuru mzee.pili akashukuru kwa kumuonyesha jinsi wao walivyo maskini kule babu na bibi yake kule kjjini.
    Mzee: alihamaki akauliza kwa vipi sie tu hohe hahe?
    Kijana:akajibu sisi tuna kibustani lakini kule nimeona msitu mkubwa,sisi tuna kajibwa lakini wao wana mbwa nyingi,sisi tuna bwawa lakini wao wana mto ambao sikuona hata mwisho wake.
    Kijana akamuuliza mzee niendeleee ,mzee kuona hivyo akabaki mdogo wazi meno 32 nje!!haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    by Mnyaluko!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2008

    OYA AKINA MATONYA!! Nadhani hawa jamaa hawana tofauti na matonya isipokuwa hawa wanaomba huku wanakula kiyoyozi wakati matonya analala barabarani lakini afadhali ya matonya kuliko hawa kwani bili ya hivyo viyoyozi wanayolipia kupitia mlango wa nyuma ni kubwa sana na ina athari kubwa sana kwa chumi zetu kila siku kwani hawa wamekuwa watu wa kupangiwa sera na mabosi wa nchi zilizoendelea.
    Tatizo la Afrika ni kwamba kuanzia viongozi mpaka wananchi hatujui nini tunataka na nini tufanye ili tuweze kuwa na chumi bora katika nchi zetu. Afrika siku zote inaendeshwa na nchi zilizoendelea na ndizo zinazotoa maelekezo ya nini kifanyike katika sekta zote kwani wao ndiyo wanaofanya tafiti zinazoaminiwa na kutumiwa na nchi zetu na wanajua namna ya kuzitumia hizo tafiti ili kuiyumbisha afrika. Mfano ni ule mpango wa kuondoa ruzuku kwa wakulima, afrika tulitekeleza kwa haraka sana na kusababisha umasikini mkubwa sana kwa nchi yetu lakini wao kwao wanatoa ruzuku ili bei ya chakula isipande na chumi zao kuwa imara. Ni aibu kwa viongozi na waafrika kwa pamoja kubaki kuwa masikini katika ardhi ambayo ina kila aina ya neema za asili kuendelea kuwa masikini huku viongozi wetu wakibadilisha suti kwa ajili ya safari ya kwenda kuomba misaada. Nadhani hii ni laana kwani hata wengine wanaukana uafrika kwa kujichubua ili wawe weupe kama wazungu lakini wanasahau bado ni waafrika tu. Hapo si ajabu ukasikia kwamba mwezi ujao wapo paris ili kutangaziwa mikakati ya kisaidiwa afrika na seikali ya ufaransa na mwezi mwingine wapo uk, mara ujerumani (walishaenda china, india na sasa japani). Hao ndiyo viongozi wetu na huo ndiyo uafrika. Hapa nilipo waniita Afrika kama bara leusi, hii siyo kwa ajili ya rangi za watu wake bali ni uduni wa maendeleo na kifikra walionao waafrika. Na wengine pia waanamini afrika hatutumii dawa za binadamu kama hizi wanazotumia wao kwani wanamini sisi ni binadamu ambao ni tofauti sana na wao. Nawashauri viongozi wetu wa afrika wawe na mipango yao ya maendeleo inayojitegemea ili nchi zetu ziwe imara na pia kutuondolea aibu tuliyonayo kuitwa akina matonya na pia kupunguza madhara mabaya yanayotokea kwa raia wao kama ambavyo tunashughudia watu walioenda kutafuta maisha SA wanavyouawa. Viongozi wakumbuke kwa staili yao ya kutembeza bakuli hawatofanikiwa hata siku moja kuinganisha afrika kuwa moja kwa staili hii.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2008

    japan ndiyo wanatupa msaada ila masharti wanayotupa siyo kabisa kwanza magari lazima tununue kwao iv angalia magari yote tz kisha jiulize tumewaingizia japan kias gan,pil japan wanachukua mchanga zahid ya makontena kupeleka japan nahis uo mchanga ndan kuna madin siyo mchanga tunaoujua yan na siri nying nikisema hapa mtalia sana,yan ni rushwa juu ya rushwa

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2008

    Afrika bado ni Bara la Kutangatanga halijatulia bado.Na wanaotufanya tutangetange ni Viongozi wetu.Hivi karibuni tu India iliwakaribisha viongozi wa Bara la Afrika katika mkutano wa Ushirikiano wa Kibiashara na Uchumi kama huo wa Japan.Viongozi walipofika kule Kazi ya kwanza ilikuwa ni 'KUSHANGAA'.Safari hii imekuwa ni Japan.Pia kazi kubwa kule ilikuwa ni 'KUENDELEA KUSHANGAA'.Nina uhakika watakuwepo viongozi wa kiafrika ambao pengine ilikuwa ni mara yao ya kwanza kupeana mikono na kufahamiana wakiwa ugenini Japan.Lakini walipokuwa hapa hapa katika Bara lao wenyewe hawakuwa na mpango huo wa kufahamiana.Nchi nyingi za kiafrika bado hazishirikiani kiuchumi na kibiashara.Lakini zitaona fahari kuwa na mashirikiano makubwa ya kibiashara na kiuchumi na nchi za Ulaya na Marekani au Mashariki ya Mbali kuliko baina yao wenyewe.Nchi nyingi ni masikini na tegemezi kithiri.Nyingi haziheshimu misingi ya utawala bora na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.Nyingi zimekuwa chini ya utawala wa 'mkondo uleule wa kifikra na kiitikadi'uliojikita toka enzi za miaka ya 1960 nchi nyingi barani Afrika zilipo pata uhuru wa bendera.Utawala wa Ubabe wa Kimawazo bado umekithiri katika nchi nyingi za kiafrika.Katiba za nchi hazibadilishwi hadi shinikizo litoke kwa Wahisani na Wafadhili wa Maendeleo kutoka nchi za Nje.Viongozi wengi bado ni Vibaraka wa Mataifa Makubwa kwa namna moja au nyingine.Kila Kiongozi ana mwelekeo wake wa kisiasa,kitamaduni na kiuchumi.Ni nadra sana kukuta viongozi wa kiafrika wakikutana mara kwa mara kuzungumzia mustakabali wa Bara lao la Afrika katika Biashara,Uchumi na Siasa.Siyo ajabu kwa nchi yenyewe kutojua rasilimali zake zilizomo ndani ya nchi yake yenyewe mpaka ije izinduliwe na mataifa ya nje yatakayo dhamiria kuivuna rasilimali ile.Siyo ajabu kwa nchi moja ya Afrika kutojua nchi ya jirani yake inazalisha bidhaa za aina gani,zipi inaweza kuzinunua badala ya kuziagiza kutoka nje ya bara la afrika na zipi inaweza kuziuza katika nchi zingine za afrika.Makovu ya ukoloni wa miaka mingi bado hayajapona.Sijasikia nchi yoyote ile ya afrika iliyo tayarisha mkutano wa kimataifa na kuzialika nchi zote za magharibi na mashariki zilizo endelea zaidi kwa viwanda.Kwa lengo ya kukuza biashara miongoni mwao.Licha ya Utajiri mkubwa wa Rasilimali iliyopo barani afrika lakini sisi wenyewe hatujui nini cha kufanya ili kunufaika zaidi na rasilimali hiyo kwa kutumia akili zetu wenyewe.Baadhi ya viongozi kwa kukosa akili ya kufikiri wamesikika wakiiomba serikali ya Japan ifikirie kuanzisha viwanda vya kutengeneza baadhi ya bidhaa vitengenezewe katika nchi za afrika.Japan ikifanya hivyo,viwanda vyao vikauze wapi bidhaa zake?Na hata wakikubali kuja kuanzisha baadhi ya viwanda huku afrika kisha wenyewe wakaamua warejee makwao Japan,nani ataviendesha viwanda hivyo wao wakiwa hawapo?Je,afrika ina rasilimali watu wenye uwezo huo kiteknolojia?Au Japan viongozi wetu wame enda kutembeza Bakuli Tupu,na Matonya mwenyewe walimsahau mjini Morogoro? Viva Matonya!The symbol of our Prosperity!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2008

    mwanaccm kakimbilia wapi mbona hajajibu maswali?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2008

    Magairi ya Japan yamejaa bongo lakini sbb si kwamba wanatupa masharti bali magari yao ni bei nafuu, yanadumu, yanavikorombwezo vingi na yanaspea nyingi. Si bongo tu bali hata ulaya magari ya japan yamejaa.

    lakini hiyo picha ya ombaomba walioaimamishwa na PM wa Japan ni tusi la kutosha. Ningekuw ndo mimi (rais toka afrika) nisingeshiriki. Kweli akutukanaye si lazzima akuambie kk*****oo. NAwezakukuonyesha tu usivyo na akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...