Familia ya Victor V. Mujwauzi Karugaba wa Arusha inawashukuru wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumuuguza, kumsafirisha hadi kumzika kaka mpendwa marehemu Valery Valentine Karugaba aliyefariki tarehe 29 April 2008 katika hospitali ya St. Elizabeth Arusha kutokana na "Low Blood Pressure" na kuzikwa tarehe 1 Mei 2008 Dar es Salaam.
Shukrani za pekee ziwaendee madaktari na wauguzi wa hospitali ya St. Elizabeth Arusha, Wafanyakazi na uongozi wa Impala Hotel, wafanyakazi wa University of Dar es Salaam Computing Centre-Arusha branch, majirani, marafiki na ndugu na jamaa wote. Ni vigumu kushukuru kila mtu zaidi tunaomba Mungu awazidishie.
Mpaka mauti inamchukua marehemu alikuwa mfanyakazi wa Impala/Ngurdoto Hotel upande wa mapishi ya kichina. Marehemu pia amewahi kufanya kazi katika Hotel mbalimbali ikiwemo Kilimanjaro Hotel, Hotel Karibu, Walk Guard Hotel n.k.
Marehemu atakumbukwa sana kwa ucheshi na upendo wake hasa kwa wale waliosoma naye Mlimani primary school na sehemu nyingine mbalimbali.Marehemu ameacha mjane na watoto watatu."sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi"
Misa ya shukrani tarehe 10/5/2008 katika kanisa Kuu la Mt. Theresia wa mtoto Yesu- Arusha saa 1.00 asubuhi


Professeur Karugaba,
ReplyDeleteJe l'écris avec les condoléances les plus profondes pour la mort de votre fils. Dieu donne et emporte. Peut Dieu endurer pour toujours. Je prierai pour vous et votre famille
Est Rose
Poleni sana wafiwa,kazi ya mungu haina makosa,marehem ninamkumbuka sana wakati tunaishi pale Ubungo Kibangu,alikua mtu wa karibu yangu sana,Pole sana Victor kwa kumpoteza Brother wako pekee.RIP.Mdau London.
ReplyDeleteHi Victor,
ReplyDeletePoleni sana na msiba, nimestuka sana kusoma habari hizi.
LUZANGO-PTRETORIA.