Mobhare Matinyi,
Washington DC
Cape Verde imeichapa Mauritius bao 1-0 kwa penalti huko huko kwao visiwani Mauritius. Ushindi huu unaiweka Cape Verde katika nafasi ya kuipiku Taifa Stars - timu hatari kuliko zote Afrika Mashariki na Kati lakini isiyokuwa na wafungaji.
Kwa matokeo haya Cape Verde sasa ina pointo 6 na magoli 2 ya kufunga na kufungwa 2; Tanzania ina pointi 2, imefungwa goli 1 na imefungwa 2. Cameroon ina pointi 7, imefunga 5 na haijafungwa hata goli 1. Mauritius ina pointi 1, imefunga 1 na imefungwa 5.
Wiki ijayo Cape Verde inaikaribisha Mauritius nyumbani kwake na iwapo itashinda, itafikisha pointi 9 na idadi ya magoli itakayojulikana baada ya mechi. Tanzania iwapo itakwenda suluhu, itafikisha pointi 3.
Ili Tanzania iipiku Cape Vede itabidi iifunge Dar es Salaam na pia iifunge Mauritius kwao, hapo itafikisha pointo 9, na hapo tofauti ya kufunga na kufungwa itaamua mshindi kati yetu na cape Verde.
Utabiri wa kimazoea unaonesha kuwa Cape Verde itaichapa Mauritius Jumamosi ijayo na Tanzania itafungwa. Iwapo mambo yatakwenda hivi ndiyo tutakuwa tumeshatoka.
Kwa maana nyingine dua letu liko zaidi kwa wenzetu kututengenezea mambo. Iwapo maajabu yatatokea na tukaifunga Cameroon, na pia Mauritius ikaifunga Capa Verde kwao, shughuli itakuwa imekwisha; Tanzania itafikisha pointi 5, Cape Varde itabaki na pointi 6, Mauritius itapata pointi 4. Mpira si hesabu - tusubiri.
Hata hivyo, kuna haja ya Maximo kuwarejesha washambuliaji wa zamani waliostaafu ili kuokoa jahazi, japo kuwachezesha kwa dakika 20 za mwisho. Mohamed Hussein 'Mmachinga' na Madaraka Suleiman na Duwa Saidi wanapaswa kujaribiwa.
yapo mataifa yaliyowahi kufanya hivi na kufanikiwa, ingawa wameshapumzika sana lakini wana afadhali kuliko vijana wetu wanaokosa kona 18, mashuri 20 na penalti moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2008

    Huyu jamaa bwana! mtu kaandika vizuri comment yake halafu mwishoni analeta mambo ya mzaha. Come on man you should be serious in serious issues. Sasa wazee hao watacheza nini au unadhani soccer ni sawa ni ngoma ya kwenu eeh?

    Big Sam

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2008

    Haya Watanzania,La Kudoda hilo!Issue hapa ni Upangaji wa Timu.Oooh hatuna wafungaji hatuna wafungaji!Nani aliyekuambia kwamba Tanzania haina wafungaji?Basi siyo vizuri kuendelea kulaumiana hivi sasa,Kama ni marekebisho ilikuwa yafanyike kitambo.Lazima tukomae lakini tusijidanganye,nafasi yetu iliyobakia ni finyu sana!Sisi sio watu wa kufungwa na Mauritius na Cape Verde.Hilo mimi nakataa kata kata.Endeleeni na Ubozi wenu.I know it will be very difficut!But will play to the Limit!You know Cameroon not only Continental Players BUT International playing worldwide.So,if Taifa Stars to win everybuddy come to the pitch to shout so Taifa Stars to win!Tanzania Love this country!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2008

    Big Sam hapo juu, je ni nani amekwambia huyo mwandishi anatania? Kila mtu ana maoni na mawazo yake...kulikoni weye unadhani analeta utani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...