kikao cha bunge cha bajeti kimeanza leo asubuhi hii huko dodoma ambapo inatarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali pamoja na bajeti ya mwaka wa fedha 2008/2009 itayosomwa siku ya alhamisi na waziri wa fedha mh. mustafa mkullo
Home
Unlabelled
bunge la bajeti laanza leo dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SIO WAZIRI WA FEDHA NI MH. WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI KWANI MR MICHUZI HUJUI KAMA WIZARA YA FEDHA ILIUNGANISHWA NA WIZARA YA MIPANGO NA UWEZESHAJI NA KUWA Wizara ya Fedha na Uchumi. Tafadhali rekebisha
ReplyDeleteNASUBIRI WABUNGE WATASEMA NINI KUHUSU che Nkapa!
ReplyDeletethithemi hapa msije mkapata mistuko ya moyo uko bungeni kuleni kuku tuu. hii taarifa kuhusu bunge sitaitoa leo. it is still clissfyied information. sijui declassfication yake itafanyika lini. ila wazee wa longo longo mna hali mbaya sana . kuna bunge la mwaka 2090. wabunge hawata kuwepo tena kutakuwa na madakaka shinani. yaani cheo kikubwa ni malkia kinachofuata ni balozi wa nyumba kumikumi. ingeweza kuanza hata kesho ila tumeonelea kizazi hiki kimalizie mazoea. kutakuwa na zero budjet. charity start at home mkikataa nitahamia hata cape verde maana n-b-i hakubaliwi nyumbani. kila kitu kitakuwa kinaitwa tanzania starndard sio usa wala uk.
ReplyDeleteacademia Tumaini geofrey Temu
MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA MAMBO YAKE YAWE MEMA. AMINA
ReplyDeleteSamahanini. Nje ya Mada na Msaada kwenye Tuta. Hivi TBC1 ilikuwa si waonyeshe live michuano ya EURO? Mbona hakuna kinachoendelea???
ReplyDeleteKaka nimeipenda sana hiyo title ya Mz yaani Mzalendo. Mz Isssa Michuzi Mz. Dun'gani Nang'orunye Nikaiyodongo. Swali langu nini tofauti ya Mz wa kike na Mz wa kiume?
ReplyDeletemmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhh haaaaaaaaaaaaaahaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeletekumbe. do sjjjjjjjjjjjui oooooookk
Tunaisubiri kwa hamu sana ili tukaijadili kwa makini kwenye Bunge letu (Jamii Forum) kuona hatua tuliyopiga na mapungufu ambayo bado yanatukabili hasa kuhusiana na Uduni wa Pato la Mtanzania kwa upana wake ihali Mafisadi bado wanatamba kwa jasho letu wananchi.
ReplyDeleteUNIVERSITY OF DODOMA!
ReplyDeleteWaTz tusitegemee lolote jipya, viongozi wamezoea kupanga kwanza matumizi makubwa na ya anasa yasiyo ya lazima ndipo wanapanga namna ya kuyalipia, hapo wanaishia ktk kulazimisha mapato na kutayarisha bajeti ya kuumiza wananchi ili wao wafaidike na matumizi. Wanaishia kila mwaka kupandisha mafuta, vinywaji, usajili wa magari n.k huwezi kusikia lolote kuhusu mapato kutokana na mali asili na madini tuliyonayo na sababu sasa tumezifahamu baada ya mitandao kuanika kila kitu. Hakuna mwenye uwezo wa kubuni vyanzo vipya vya mapato.
ReplyDeleteyale yale, hamna la kuomba wala kushangilia hapa. nasemaje, YALE YALE
ReplyDeletemz. sekila
Ndugu zangu inawezekana nisieleweke ila sioni haja ya kuwa na wabungu wasio watetea wananchi wao. Hivi vikao bajeti vipo tu kila mwaka na tunavisubiri kwa hamu saana. Baada ya mwaka ukiuliza nini kimefanyika? hakuna; madeni, ufisadi, Dar es salaam kunafurika hata manyunyu yakidondoka, mawaziri wanatuwakilisha wanazidi kuneemeka na walalahoi hawawezi kupanda hata daladala.
ReplyDeleteHivi tutalia mpaka lini??
Bunge letu ni kama kikao cha harusi kwani mambo mengi ya matumizi ya fedha zinazopitishwa ni kwa ajili ya matumizi ya anasa kwa watu wachache na walio wengi tangu nchi ipate uhuru mpaka leo wanashughudia mbwembe za wanavikao (wabunge) pamoja na kamati zao lakini hakuna kinachobadilisha maisha yao. Wapiga kura wenzangu nchi yetu inahitaji mageuzi ya wanavikao(wabunge) kwani naweza kusema wote waliopo hawafanyi kazi kulingana na mshahara tunaowalipa(wanafanya kazi chini ya kiwango) na wapo kwa manufaa yao.Pia tuweni macho na hawa wabunge hasa wakati huu tunakaribia 2010 kwani kila 1 atataka aongee japo ni pumba ili wapiga kura tuone yupo nasi ili tumchague tena. Kimsingi wengi hawana jipya kwani kuwepo kwao muda mrefu bado hakujainasua nchi kutoka kuwa omba omba licha ya utajiri uliopo huku wao wakijineemesha kwa semina na vikao. Hali hii inaifanya nchi ikonde lakini wabunge na viongozi wanaota viriba tumbo (vitambo au kero za wananchi kwa maneno mengine). Tuwang'oe wote ili tuanze upya kama vile nchi ndiyo inapata uhuru wake leo kwani tumechoka na misamiati kama bangusilo n.k
ReplyDeleteKatika historia ya Danganyika kwa mara ya kwanza hatutatoza Kodi kwa bidhaa yoyote ile.Kuanzia Juisi,Oxygen hadi Maji ya Barafu.Wote mtakubaliana nami kwamba tumepata mafanikio makubwa sana ya kiuchumi.Uchumi wetu unakua kwa kasi sana.Mfumuko wa Bei umeendelea kushuka na Shilingi yetu sasa ni imara vya kutosha.Bajeti yetu mwaka huu imepungua utegemezi kwa pasenti kubwa.Kiwango cha umaskini nchini sasa kimeshuka sana.Upo umaskini tu ule wa kujitakia.Rasilimali zipo tele.Ukichimba tu umeramba dhahabu.Njaa ya chakula labda kwa wale wapenda Wali au Npunga.Lakini magimbi na mihogo pamoja na makunde yamejaa bwelele kwenye masoko yetu.Bei ya mafuta nadhani kuna matatizo ya mawasiliano tu.Lakini tunayo mafuta mengi na ya kutosha.Kukabiliana na ukosefu wa madawati mashuleni tumeamua katika mwaka huu wa fedha tutagawa mikeka milioni 500 katika shule zote za msingi ili watoto wetu wasikalie vumbi madarasani.Tuna mipango mingi sana ya maendeleo.Kinacho takiwa hapa ni kuwa na Subira tu.Kama mnavyo jua Mvumilivu Hula Mbivu na Haraka Haraka Haina Baraka.Asanteni sana kwa kunisikiliza!Sasa nitawaombeni kwa kauli moja muipitie hii Shopping List ya Serikali na muipitishe ili tuanze kuchapa kazi mtindo mmoja.Kila mtu ameguswa kwa namna yake katika Shopping List hii.Wengine wanaiita Bajeti sijui!Eeh ndiyo Bajeti.Sawa.Whaaaiiiiii?
ReplyDelete