umati wa wadau ukiwakodolea macho wacehzaji wa cameroun waliotua dar leo tayari kwa mchezo wao na taifa stars jumamosi hii kwenye uwanja wa neshno mpya. katika hapo almaarufu ni huyo mwente rasta ambaye anaitwa alexander song, mpwawe rigobert song

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2008

    we want to see those sexy papas!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2008

    mithupu huyo ni mchezaji wetu the gunners anaitwa alexander song naona huyo benjamin wako atakuwa anachezea bwawa la maini
    mizizi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2008

    huyo sio benjamin song. ni alexandre song billong ambaye ni nephew (mtoto wa kaka) wa rigobert song. anachezea arsenal.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2008

    Huyo ni mtoto wako wake au ni binamu yake? nadhani rigobert ni uncle kwa bwana mdogo huyo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2008

    Huyo dogo mwenye rasta ninavyojua anaitwa alexandre song anachezea arsenal na ni mpwa wa Song mkubwa sio mtoto wake.sasa sijui labda huyo benjamin song mpya manake hio picha ametupa kisogo lakini kichwa cha alexandre song hicho.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2008

    TFF hayahaya mijihela hiyoo imejileta yenyewe.
    Sisi kwetu kama mashabiki suala la ushindi tulishalifuta maana jamaa ni kama wapo home ground si ajabu watu kuishangilia Cameroon kama alivyoahidi Song kwamba watacheza one touch football..Nakumbuka siku tunacheza na Mauritius waTz tulikua tukimshangilia yule striker wa Mauritius pindi alipokua akiichachafya ngome ya stars

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2008

    Duh! Bora TFF wameweka kiingilio cha kufa mtu angalau uwanja hautajaa. Hebu fikiria uwanja mpya ukiwa umejaa nyomi la watu 60,000 halafu wote uzalendo umewashinda? Kina Binya si watatuua?
    Kila la heri Taifa Stars. Kazi ngumu itakuwa katika dakika 15 za mwanzo na za mwisho katika kila kipindi. Mkitulia vizuri hapo mechi itaisha vizuri. Kumbukeni kufunga ni kutoa pasi ambayo hakuna anayeweza kuifikia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2008

    Alexander song, ni binadamu yake na Ribert Song! Kwa kiingereza Cousin brother!
    Taarifa ziwe za utafiti kidogo, sio Mpwaye "like Nephew". habari ndio hiyo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2008

    Mungu awabariki hawa wachezaji angalau wamechangia uchumi wa Taifa letu na hizo Euro zao .Nchi yetu inaheshimika jamaa wameacha kukaa Mauritius wamekimbilia bongo kufanya shopping na kupumzika.Na nasikia baada ya mechi wanaelekea kuangaliavivutio vyetu!(Wizara ya utalii na 'tours' kazi kwenu).
    FOOTBALL.Stars mtulie,hakuna papara chezeni mpira tunaweza kupata matokeo.
    MSAADA KWENYE TUTA:INAKUWAJE HAWA WACHEZAJI WANAISHI HUKO MAJUU KULIKO NA KILA KITU KIZURI, WANAKUJA KUFANYA SHOPPING DAR??KARIBU WANABLOG HASA MNAOISHI HUKO UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2008

    ISSA MICHUZI, hajakosea sijui lakini labda jamaa aliye sema binamu kachunguza zaidi. Huyo Song mdogo anamwita Rigobert Song Mjomba siku moja African Nation Cup European Tv walikuwa wakisema huyo bw mdogo ni "Nephew" wake Ribert Song Si Cuzin Brother kama anavyosema jamaa juu hapo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2008

    Huyo hapo kwenye picha ya chini kushoto,foreground,anachekelea kitu gani???Ndevu ka' sharubu za paka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2008

    kwa mtazamo wangu kwa kuwa timu ya cameroun inawachezaji wengi wanaochezea ulaya basi waTZ utaona watakavyoishangilia cameroun baada ya staz, na hii ni kutokana na ushabiki wa vilabu tunavyopenda kushabikia vya ulaya, kama mtu ni shabiki wa barcelona basi etoo akikamata mpira atashangiliwa tu na kusahau uzalendo,vivyo hivyo na wachezaji wengine. kazi ipo jmosi mie yangu macho
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2008

    JAMANI WATANZANIA,TUWENI WASTAARABU,KWENYE MECHI ZA TIMU YA TAIFA HUWEZI KUSHANGILIA TIMU YA TAIFA JINGINE.HIYO MECHI SIYO YA ASENO/BARCA,MAN U VS YANGA,SIMBA N.K
    OLE WAKE ATAKAYEWASHANGILIA CAMEROUN,VIJANA WETU WATAKUWA WAMETAPAKAA UWANJA MZIMA(UWONGO MICHUZI?) NA BAADA YA MECHI UTASHIKWA MKONO TARATIBU NA KUPELEKWA......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...