baada ya mawasiliano ya muda mrefu na makao makuu ya tawi la mashabiki wa bwawa la maini huko anfield, hatimaye nimefanikiwa kupata waraka (pichani) unaoturuhusu kuanzisha rasmi tawi la mashabiki wa bwawa la maini kwa wapenzi wake wote wa bongo.
ikumbukwe awali niliwahi kudokeza azma hiyo na wadau kibao wa bwawa la maini (ambao ni mamia kwa mamia hapa bongo na nje) walijitokeza na kusema wako tayari kuwa memba wa 'BongoReds' kama ambavyo tutajiita.
hivyo kwa ujumbe huu wapenzi wa bwawa la maini ambao ni wabongo kaeni mkao wa kula. BongoReds hiyo yaja na kinachohitajika kwa sasa ni kupata memba. hivi sasa naandaa rasimu ya muda pamoja na globu ya mawasiliano na matangazo ya shughuli zetu ambayo itawasilishwa kwenye mkutano wetu wa kwanza ambao tarehe itatangazwa karibu na namna ya mdau utavyoweza kujiandikisha itawekwa bayana.
na kwa kuanzia naomba wale wote wana wa bwawa la maini tuwasiliane kwa kupitia bongoreds@gmail.com kuanzias kesho jioni kwa saa za bongo ambapo anuani hiyo itakuwa hewani na tayari kuchukua barua pepe.
YOU WILL NEVER WALK ALONE
Mungu ibariki BongoReds
Mungu libariki bwawa la maini
Mungu Ibariki bongo


Ebwana mie hio na hipinga kaka michuzi kwani haitasaidia soka letu.tunatakiwa tufanye mapinduzi TFF mfumo wa soka ubadilishwe au mjikusanye makundi ambayo yataanzisha timu za vijana tuanzisha ligi yetu wenyewe sio mambo ya bongoreds.
ReplyDeleteduuh ama kweli misupu huna kazi ya kufanya, we kufungwa kote na kutokuchukua chochote miaka yote bado unahamasisha liverpool,ni bora ukisapot mbagala market,,,pole
ReplyDeletesijaelewa..bwawa la maini??somebody please clarify
ReplyDeleteMi bado sijaamini kama kweli umepewa uwakala please ebu onyesha hiyo barua yote, mbona ikekatwa? WHY? KWANINI
ReplyDeleteMichuzi kwa kufanya hivi, wewe, chenge, balali, na mafisadi wengine wote ni mafisadi tuu. Unalifisadi soka letu la kibongo.
ReplyDeleteMkuu wa nanihii ya nanihii vipi unatangaza uzalendo kukushinda tena? Ina maana wewe sio Simba wala Yanga? Wala Taifa Stars?
ReplyDelete