Serikali imepanga kupata mapato ya jumla ya shilingi bilioni 7,216.130. Kati ya kiasi hicho, mapato ya ndani ni Shilingi bilioni 4, 728.595 na mapato kutoka kwa wahisani ni shilingi bilioni 2,429.535. Aidha, Serikali inategemea kupata shilingi bilioni 58.000 kutokana na uuzaji wa hisa zake asilimia 21 katika benki ya NMB.Na katika mwaka 2008/09, matumizi ya Serikali yatakuwa shilingi bilioni 7,216.130. Matumizi ya kawaida yatakuwa shilingi bilioni 4,726.650 ambayo ni chini ya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 4,728.595. Matumizi ya maendeleo yatakuwa shilingi bilioni 2,489,480.
Katika matumizi ya maendeleo, kiasi cha shilingi bilioni 1,551.100 kitatokana na fedha za wahisani kupitia miradi pamoja na basketi. Kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 938.380 kitatokana na mchango wa wahisani kupitia misaada ya kibajeti, mapato yatakayotokana na mauzo ya hisa za Serikali pamoja na ziada itakayotokana na mapato ya ndani.


mmh..kazi kweli kweli kwa serikali kama yetu, karibu theluthi moja ya bajeti ya nchi inatarajiwa kutoka kwa wahisani. Na je wahisani wakigoma kutokana na ufisadi wetu tutafanyaje? na hicho kiasi cha bajeti kinachotegemewa kutokana na hisa ndio kile kinachoenda kwenye mifuko ya viongozi mafisadi, kwani hizo hisa wanajiuzia wenyewe tena kwa bei poa tu na hazilipwi....kazi ipo kwetu sie walala hoi!
ReplyDeleteHivi hawa Mawaziri wa Fedha, kwani kunakuwaga na ulazima gani wa kuntanyua hilo brifkes juu?
ReplyDeleteKwani wakilibebakama kawaid tu inakuwaje mpaka walinyanyue juu hivyo wanapokwenda kusoma bajeti? Au ni kuiga tu kusikokuwa na ufafanuzi wowote wa maana?
Nahitaji kuisoma bajeti yote ndipo niweze kuona imekaa vipi.Hata hivyo,kwa muhtsari huu inaonekana ni bajeti nzuri ambayo kwa kiwango fulani inalenga kujibu baadhi za kero za wananchi na hasa watumishi wa umma.Kwa mtizamo wangu kwa taifa changa na masikini kama Tanzania,sio mbaya sana kutegemea theluthi moja tu kutoka kwa wahisani kuchangia bajeti ya nchi.Nadhani tunakwenda vizuri kulinganisha na tulikotoka.Muhimu hapa ni uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia makusanyo na matumizi hayo.
ReplyDeleteBajeti ni nzuri na imetengenezwa kitaalaamu kuliko ile bajeti uchwara takataka ya mwaka uliopita.
ReplyDeleteIla serikali inabidi ianze kutengeneza budget inayotoa "incentives" kwa wasomi na watu wa mijini wapende kilimo na kuwekeza kwenye kilimo.
Kupandisha marupurupu (incentives) ya wafanyakazi wa serikali ili kuwahamasisha wapende kufanya kazi kwa juhudi bila kutoa marupurupu kwa wakulima ili wahamasike kulima na wapende kulima kwa juhudi zaidi sidhani kama kutabadilisha sana uzalishaji katika nchi.Tufikirie namna ya kutoa incentives kwa wakulima kuliko maofisa waaandika makaratasi wa serikali.
Kwa ufupi bajeti hii mapato yake itategemea zaidi watu wa mijini kuifanikisha.(CITY AND TOWN CONSUMERS OF GOODS ) ambao ndio wenye hela za kunywa pombe,kunywa soda,kuvuta sigara na kuagiza magari mitumba kijapani ili waendeshe kwa mbwembwe wawakoge wakulima vijijini.
Hii BUDGET ni CITY AND TOWN ORIENTED kwa utegemezi wa mapato.
Lakini kwa Upande wa matumizi naona inaweza kuwa "Rural Expenditure oriented" kama hizo pesa zilizotolewa nyingi kwa budget za barabara zitatumika kujenga barabara za maeneo ya vijijini na mikoa inayozalisha kwa wingi.Lakini kama sehemu kubwa ya pesa hizo za bajeti zilizoko kwa ajiri ya barabara zitatumika kwa ujenzi wa barabara za mijini na vichochoro na majiji kama Dar es salaam hapo hakutakuwa na maana yoyote utakuwa ni uhuni na upuuzi usiosaidia uchumi kufunguka na kuuamsha.Sijajua mchanganuo wake kwenye eneo hilo la ujenzi wa mabarabara ndio maana nimesema yaweza kuwa rural oriented kama........
Kwa ujumla bajeti nzuri serikali imejitahidi safari hii.Hongera Raisi Kikwete.Safari hii sikuzomei nakupongeza.Sasa hivi nadhani wataalamu wa bajeti hawajaangusha.Hata wabunge watakaojadili hii budget wana kazi ya ziada maana akili iliyotengeneza hii budget ni kubwa.Yataka mbunge akitaka kuijadili atafute ma-consultants vinginevyo ataishia kutoa pumba tupu bungeni.
koloboi@yahoo.com