Hi Issa,
Big Up for the good job you are doing. Your blog connects tanzanians all over the world! That is very great! Now here comes my help request on the "Tuta" (jamani tuta kwa inglish ni nini?)
Wapendwa watanzania nimepata bahati ya kushinda "Special Immigration Visa to the USA"Sijawahi fika USA wala sina ndugu wa karibu huko.
Just for your information hapa nilipo nina kazi nzuri, nyumba na naishi maisha ya kawaida. Najua kuna watanzania wengi huko na ni watoto wazuri nina imani mtanisaidi kwa maswali ya fuatayo: -
Kwanza kabisa faida za kuja huko nikiwa na green card
- Ni state ipi nzuri kwa kuishi yaani kwa wageni?
- Huduma za afya nasikia si rahisi huko how does one go about?
- Watoto wa kisha kuwa shuleni, shule zina health insurance?
- Procedures za kupata kazi
- Mengine mengi ambayo napaswa kujua/kujitayarisha kabla sijaja huko.
Thanks in advance for your input.
Love you all!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2008

    Wewe kama unataka kwenda nenda tu ukapambane na maisha wala usitegemee maajabu, ni vigumu sana mwanzo labda hadi ukiwa umekaa kwa muda hivi na kusowea mitaa na maswala mbalimbali ndo utaanza kuona mambo yanaenda vizuri lakini mwanzo asikudanganye mtu yoyote ni mgumu sana hasa maswala ya kazi kwa mtu anayetoka nje na accent ya kiafrika unajuwa tena wazungu wanajali sana uweza wa kuwasiliana/communication watakuambia hatukuelewi mara hili mara lile, hivyo wala usitegemee kupata kazi kama hiyo uliyonayo hapo nyumbani kwa siku za mwanzo, wewe fanya kazi yoyote ile inayokuja machoni pako kwani mungu ni mkubwa huko kazini unaweza kukutana na watu wakakuonyesha njia sio lazima wawe watanzania, cha msingi usiwe muoga be talkative and inquistive, na msingi ni uvumilimu kwani itachukuwa muda kufika level ungependa ufikie, na pia ujuwe USA si kama kwa mfano UK ambako kuna social benefits, I mean if you dont I have a job in UK and you are citizen au mkimbizi au una indefinate stay unalipwa vijisenti kadhaa na familia yako na matibabu bure, kitu kama hicho hakuna USA inabidi ugangamale mwenyewe, mimi kwa ushauri wangu wewe nenda na familia yako yote kama ulivyoorodhesha katika hiyo green card cha msingi na ambacho familia itafaidi ni kusoma kwani mutalipa/pay kama raia and you have some benefits as any other USA citizen na hilo ndo la msingi nendeni mkasome kama vichaa hivi kwani elimu itawasaidieni siyo huko tu mahala popote pale duniani ambapo mnaweza kupata kazi, msije mkaa bweteka na starehe za USA badala ya kuwekeza kwa namna moja ama nyingine kwani kuna uzee, kwani sidhani USA ama Ulaya yoyote ile inafaa ukiwa mzee hasa kwa mtu wa kuja kama sisi, kwani watu wako busy hakuna atakaye kutazama na uzee wako, uongo bongo mjomba, shangazi anweza kukuletea maji ya kunywa. USA is an incredible and fantastic country nimekuwa huko mara kadhaa wenzetu wako peponi, lakini pia kuna masikini kama Tanzania na maisha yao ni mabaya afadhali hata masikini wa bongo ambao wanaweza kwenda kwa mjomba na kunywa maji, but it is an awesome dream country na mara nyingi wageni hufanikiwa kwa wao wamekwenda kwa kusaka mafanikio kwa wale wenye akili zao za maisha, hivyo wewe ukienda usifanye mchezo kakazane kwa ajili ya familia yako, mara nyingi hii si siri watanzania wwengi tukiwa nje huwa naweza kusema hatuna muda na wenzetu sasa sijuwi ni kwa sababu gani pengine u-busy wa maisha na kuhangaika,wapo wachache wazuri si wengi hivyo nakushauri usitegemee sana watanzania, sikatai wapo wazuri unaweza kuwa na bahati yako ukakutana nao na kukusaidia, lakini ukweli tuko tofauti sana na ndugu zetu wa West Africa, Kenya na Uganda huwa wanasaidiana sana kuliko sisi wakiwa ugenini, hayo ni maoni yangu na experience yangu na ndivyo nilivyoona mimi. State nzuri USA hii inategemea na wewe unataka nini na uwezo wako wa kipesa kwani kuna States ambazo ni nafuu kimaisha hasa maswala ya nyumba na chakula. Lakini kwa mgeni kama wewe vitu vya kuzingatia ni State yenye kazi nyingi ambako unaweza kubahatika kupata kibarua kwa urahisi au unaweza kuanzia popote pale unapoona nafuu na mfuko wako baada ya kuzowea unaweza ku-move on kutokana na taste yako, lakini hii pia unaweza kuulizia hapo ubalozini wapo watu wanaweza kukupa mawazo mazuri na mwanga, pia hali ya hewa zipo states zinabaridi sana hasa sisi watu nchi za joto pengine zinaweza kuwasumbueni kidogo lakini mnaweza kuzowea pia, Tafuta information kwenye internet tumia google.com jaribu kuangalia NEW YORK, WASHINGTON DC, CARLIFONIA, TEXAS kuna states zingine ni maafa kila siku ya mafuriko na vimbunga pia hiyo ni factor ya kuangalia.

    Mwisho mimi naushauri uenda tena na familia yako yote, kama una asset zozote hapo nyumbani wewe ziweke sawa tu zitakuja kukusaidia.

    Mwisho hongera sana na mungu akusimamie huko uendako mambo yaende kiulani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2008

    KAMA UMESHINDA VISA/GREENCARD HIYO PACKAGE WALIYOKULETEA INA MAELEZO YOTE/INAJITOSHELEZA. NA KAMA UNATAFUTA KAZI POSTI RESUME YAKO ONLINE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    Sasa wewe na shule yako nzuri na kazi nzuri unaomba visa za bahati nasibu ili iwe nini sasa?kama unataka kazi usa soma vizuri omba kazi huko kama unafaa utapewa tu work permit na utafanya kazi hata ten years then utarudi home,kma akina balali na wenzie wengi,mambo ya bahati nasibu waachie ambao wamekosa otpion so they are tossing.sasa utaenda huko usa na familia ukaanza e kusoma then utafute kazi yaani watu wengine mwe ,haya nenda holiday,nauli wanakulipia?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    Kama kweli ulikuwa unataka ushauri wa dhati huyo anonymous wa kwanza kabisa June 18 10:43 PM amefunga kazi.Nilikuwa nasikia duniani kuna watu wenye GOLDEN HEART basi huyo Brother/Sister ni mmoja wao.Hii inadhihirisha bado katika dunia yetu hii ya leo iliyojaa wivu,uhasidi na roho mbaya bado kuna watu wachache wenye ubinadamu.May God bless him/her na Good luck na mipango yako.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2008

    Asante WARYA, mimi ni wa kwanza hapo juu sikutaka kuweka jina langu hapo kwa vile watu humu ndani hutukanana sana sijuwi kwani? najuwa sababu lakini singependa kuisema hapa hivyo ni bora wanitukani bila ya jina. Nawe WARYA mungu akubariki, binadamu tusaidiane na tupendane.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...