Pastor Abisalom Nasuwa,wa Dallas Texas anapenda kutangaza kifo cha baba mzazi wa mke wake Esther Abisalom Nasuwa kilichotokea katika hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro juzi siku ya jumatatu saa tatu usiku.
Mipango ya mazishi inaendelea kupangwa huko Moshi.
Kwa kuwa kutokana na sababu mbali mbali pastor Abisalom na mke wake hawataweza kusafiri kwenda nyumbani kwa mazishi,kutakuwa na ibada nyumbani kwao siku ya ijumaa jioni kuanzia saa moja kamili.
Tunapenda kumkaribisha kila mwanajumua aliyeko hapa Dallas na sehemu mbali mbali ambao wataweza kuungana na familia hii wakati huu mgumu wanaopitia.
Anuani ya nyumbani ni;
7311 Otomi Street,
Dallas Texas 75236.
Kwa watakaopenda kuwapigia simu na
kuwafariji namba zao ni hizi;
Pastor Abisalom Nasuwa 214 554 7381
Esther Nasuwa (Mrs) 972 896 6228
Res; 972 780 2668.
Karibuni sana na Mungu atubariki sote.
Mdau


Dah hii wadau haijatulia "...anapenda kutangaza kifo.." ninavyoelewa anatakiwa aseme ...ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO etc etc.
ReplyDeleteAnyway poleni wafiwa
Poleni kwa msiba. Ila kwenye msiba watu hawasemi ANAPENDA KUTANGAZA KIFO, bali tunasema ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO. Msiba si furaha. Nawakilisha.
ReplyDeletePole sana kwa wafiwa wote. Mungu ailaze roho ya merehemu mahali pema peponi.
ReplyDeleteBro Michuzi,swali la kizushi kwako: Pastor Abisalom anapenda kutangaza kifo au anasikitika kutangaza kifo?
Pole Esther, na family.
ReplyDeleterafiki Zanaki and Msange JKT!
Kumbe ile dili ya jeshi ilifaa hadi ikawa endelevu. Hongera sana.
poleni
ReplyDeleteinatakiwa kuwa MNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO
Please rekebisha tangazo
Mchuzi yeye kapewa abandike, kazi yake sio ku edit matangazo, mpeni break kaka wa watu!
ReplyDeletebaba mzazi "ESTHER"?? kidogo nimekwazika na jina au ni mama mzazi? pleni na msiba anyaway!
ReplyDeletePoleni sana wafiwa lakini hata mimi tangazo limeniumiza kichwa kuelewa nilishngaa huyo mkwe aliyefariki ana jina kama lake? Yaani yeye akioa anabadilisha jina anafuta la mkewe? Sikuelewa kabisa "kutangaza kifo cha baba mzazi wa mke wake Esther Abisalom Nasuwa wakati mtangazaji mwenyewew anaitwa the same name...
ReplyDeletePoleni ni wakati mgumu huu lakini naamini Mungu atawapatia nguvu
JAMANI MIE SIONI CHA AJABU AKISEMA ANAPENDA KUTANGAZA KIFO!!MAANA ALIYEKUFA MUNGU ANAMPENDA SANA NDIO MAANA KAMCHUKUA!!NDIO MAANA YA KUSEMA ANAPENDA KUTANGAZA..MAANA MUNGU NI MKUBWA KWA KUMCHUKUA HUYO MZEE WAO...HAINA HAJA YA KUBADILI TANGAZO MEELIELEWA ACHENI KUOSHA VINYWA...POLENI SANA WAFIWA
ReplyDeletePoleni sana. Lakini Jamani wabongo tunazamia mpaka tunashindwa kurudi nyumbani kuzika wazee. Hii mbaya sana. Michuzi toa hii comment yangu usi ibanie. Tumezidi.
ReplyDeletewasamehe bure kutorudi kuzika nikwamba wameoza wakitoka tu kurudi labda mihujiza ishuke na bingu iteremmuke, unajua hawa watu wa majuu wameoza almost wote hawajuhi kuwa mambo yote bongo!
ReplyDelete