Kabila la Hadzabe ni kabila ambalo kisayansi ndilo linatambulika kuwa binadamu wa kwanza alikotoka.Sasa Tanzania ilibidi iwaifadhi ,iwatunze na waishi maisha yao yale yale waliozoea ili kutopoteza tamaduni wao..
Kwa kweli huu ni utajiri mkubwa kwa sisi
watanzania.
Wamisri wanapata pesa za kigeni na kuinua uchumi wao kwa ajili ya utalii
[pyramids].Ndugu zangu watanzania ili kukuza uchumi wetu inabidi tusiangalie short term profit ila tuangalie long term profit]kwa ajili ya uchumi endelevu ama kwa kimombo sustainable, economic growth of our Country and Global too.
Tusiwanyanganye ardhi yao hao Wahadzabe.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.Tuishauri serikali vizuri kwa manufaa ya umma.Na serikali isipuuzie ,huu sio wakati wa kupuuzia mambo muhimu ya umma.
Ludigo Mhagama[Environmental consultant]
The Institute Of Research And Environmental Quality[IREQ
P.O.BOX 80259
Dar es salaam
Tanzania
Tel 755 901002.
e-mail Lmhagama@ireq-tanzania.com
www.ireq-tanzania.com


Kama tungewazibiti MAFISADI watanzania wa leo wasingetembea Tumbo wazi.
ReplyDeleteEnvironmental consultant mzima unataka kuwa subject wanaadamu wenzio kwenye karne ya kwanza maisha yao yote? hata wewe una utamaduni wako wa huko vijijini acha uhuo u-Environmental consultant wako uende ukaisha maisha ya kijima huko uhagamani
ReplyDeleteBwana Ludigo kwa mtizamo wangu naona serikali iwachukue watoto wao iwaelimishe kama ilivyotia nguvu kwa kabila la kimasai.
ReplyDeleteKuishi kwao msituni ndio kikwazo cha maendeleo ya taifa letu kwani GDP inapogawanywa kwa population ya Tanzania na hao hawazalishi basi ina-athari.
Mfano mwingine ni kule Australia serikali iliamua kuwasomesha watoto wa weusi waliokuwa wanaishi msituni tatizo lao waliwatenganisha na familia zao sasa serikali yetu isifanye makosa yale.
Juzi nimeona kwenye global hii mmasai amekuja Arusha kujifunza kiingereza na hapo alipokuwa alikuwa anatumia mtandao sasa unaona maendeleo hayo?
Mwisho maendeleo ya Taifa huletwa na wananchi wakiwa wanafanya economic activities na walipe kodi. Huko msituni hawalipi kodi.
Mchangiaji.
Mtazamo duni kama mimi ningekuwa mwajiri wako ningekufuta kazi.
ReplyDeletePia usingeandika hata hizo contact kwa sababu wewe mwenyewe unahitaji msaada nasi kuwa mshauri.
Kwanza umelinganisha pyramid na watu mbona kichekesho. Yaani watu wasafiri toka Ulaya kuja kuangalia watu wanaishi porini?
Mtu anatakiwa awe na access ya matibabu, elimu, apige kura na haki zingine ili aishi maisha ya karne ya 21.
Kama wewe ungekuwa ni kati ya hao ungekuwa consultant?
Je wazazi wako wanaishi maisha kama ya hao kwa sababu umesema ndio asili ya binadamu?
Tuache kudanganyana, usitumie watu wanaoishi maisha kama hayo ku-justify u-consultant wako.
Mdau
I hope JK got the massage, Tanzanian leaders doesn't think about growth strategy. They think about today, and the results will be nightmare in the future.
ReplyDeleteMdau wa US tawi # 1
Jamani hivi kweli serakali inataka kuchukua ardhi ya wahanz...mimi nimefanya kazi ya kuongoza watalii kwa miaka 15 wakati huo niko Tanzania,nimeongeza mataifa mbalimbali kwenda kuwaona hawa ndugu zetu,i mean it maana nimeongoza tuseme maelfu ya watalii kutoka Holland na marerkani na ujerumani...wanalipa hela nyingi tuu kuwaona hawa watu wanakaa nao kwa siku tatu...jamani serakali muwe makini na mambo mnayoyafanya...UFISADI MMEMALIZA AU MNAONEA WANYONGE TUU???
ReplyDeleteBro michuzi natumai umzima wa afya tele na pole kwa mishen mishen za summit vipi ujatujulisha kama umerudi salama nyumbani maana tunasikia mara helicoptor mara magari yameleta varaga njiani any way just wanted to say big up for what your doing and keep on holding what ur doing. Mdau Alex Texas.
ReplyDeleteSince I started following news in this blog, this is the first time I am reading such a wonderful thing. It sounds very interesting and educational, as it would boost Tanzania's economy at large.
ReplyDeleteTourists are not just interested in wild animals and mount Kilimanjaro. They would also like to see how these people live. Stakeholders should brainstorm this point, and see how people of this tribe could also be given the chance to explain why they have decided to live in a very traditional way, without accepting other cultures.
That is truu kabisaa ; hiyo habari hapo juu inahitaji kuafanyiwa ufatiliaji hebucjisomee hapa uone kweli tutakavyonunuliwa na matajiri http://anthropology.net/2007/06/10/tanzania-hadzabe-tribe-threatened/
ReplyDeleteHII NI AIBU NA NI KASHIFA KWA KUWAFANANISHA NDUGU ZETU HAWA NA PIRAMIDI ZA MISRI, HIVI NI KWELI SISI TUNAHITAJI TUISHI MAISHA YA ASALI NA MVINYO KUTOKANA NA MAPATO TUTAKAYOYAPATA KUTOKA KWA WATALII WATAKAOKUJA KUWAANGALIA NDUGU ZETU HAWA AMBAO INASHAURIWA TUWAACHE HUKOHUKO PORINI WAKILA ASALI NA MATUNDA PORI? NA KUNYIMWA ELIMU ILI NAO WAWE KAMA SISI! USHAURI HUU NI WAKIBAGUZI.
ReplyDeleteBwana Ludigo umefanya vizuri kuwaonyesha hawa watu aisee. Labda the Sulvan and other member of NGO's will see and emancipate them from this mental slavary. Aisee lakini hapo ndio umewapa Mafisadi chakula. Baada ya siku chache utaona NGO iitwayo Emancipate The Wahazabe. Utaona. Pia naomba serikali na wadau wote wachukua kila liwezekanalo wawachukua watoto wa hawa watu wakasome jamani.
ReplyDeleteMr.Mhagama,nadhani utakuwa umesoma different reactions from wana blog.
ReplyDeleteNadhani hawa watu wanatakiwa kutafutiwa mbinu ya kuwatoa porini wapate,elimu,afya n.k au basi serikali kama inaweza ipeleke services huko huko walipo.Maisha ya karne ya 18 kwa dunia ya sasa hayana nafasi.Watalii waendelee tu kuja kuangalia wanyama na vivutio vingine siyo hawa ndugu zetu.
Bad Idea at wrong place.
Hivi kweli watu wanaishi STONE AGE,halafu tunasema ni urithi wa nchi hii!, wote tulikuwa hivyo sometime ago ila pace ya kubadilika imetofautiana, hivyo ni jukumu la serikali kuwa-modernise watu hawa ambao ni ndugu zetu, kwa sababu the coming world will be very very hostile for all of us, and they can not survive if they are not modernised.
ReplyDeleteWadau nadhani wengi mmeipokea hii habari kwa jazba. Mimi namuunga mkono bwana Mhagama kuhusu hifadhi. Msimamo wangu nikuwa Wahadzabe kama walivyo binadamu wote, wanahitaji hifadhi ya maisha yao na heshma ya utu wao. Pili nakubaliana na wadau kuwa waliokasirishwa na ujumbe wa mhagama kuwa cha msingi siyo pesa, bali maendeleo yao. Mwisho, ikiwa mtapenda kunielewa, hawa wahadzabe wanayo haki ya kujiamulia mustakabli wa maisha yao. Serikali inapaswa kuwatambua, kuwasaidia katika kufikia malengo watakayokuwa wamejiwekea kwa ajili ya kile wanachoona wao kuwa ni maendeleo. Na hapa tunapaswa kuwa na tahadhari kubwa ili kuepuka mambo yafuatayo: assimilation, cultural genocide, na discrimination. Hakuna mtu mwenye haki ya kukupangia namna ya kuishi ilimradi huvunji sheria. Katiba ya Tanzania inasema kuwa kila mmoja wetu tangu kuzaliwa ni mtu huru. Na anastahili hifadhi ya maisha yake toka kwa jamii. Ninapinga kwa nguvu zangu zote kuwafanya wahadzabe kuwa sehemu ya maliasili ya nchi [kuvutia watalii] na pia napinga kwa nguvu zangu zote kuwalazimisha wahadzabe wafuate taratibu zetu ambazo kwao hazina manufaa [nyingine tunaipachika majina "maendeleo"]. Tunapowaangalia wahadabe tuzingatie sana utu/ubinadamu wao na haki zao za msingi.
ReplyDeletenaomba kuwasilisha
ni mimi ndugu yenu - kipimautu.
Hii ndiyo topic yenye akili kwa siku za karibuni kwenye JAMII BLOGU!
ReplyDeletemawazo yangu ni kwamba hiki kizazi cha watu waishio msituni ni lazima kiachwe huko huko maporini ili kisije kupotea. hatari ya kuwaindoa bila kufanya utafiti ni hatari kwani tunaweza kuwatokomeza kabisa. mfano miili yao haina resistance na magonjwa kama siye kwani haijana chanjo za magongwa yoyote kama sisi.
Hivyo ushari wangu kwa wachangiji ni kwamba ikiwekwa topic jiulize kwanza kabla ya kuanza kurusha lawama kwa mtoa mada.
Nawaombeni msome zaidi kwenye link hizi muone watu wanaoishi kwenye vinyumba vya barafu (IGLOO),eskimo wa misitu ya Kongo na KHOISAN wa Botswana na Afrika Kusini, jinsi gani wameachwa au wamefukuwa kwenye makazi yao!
http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/1356570.stm
http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/4554221.stm
http://www.survival-international.org/
....mimi sijasema!!
TUBADILIKE TUELIMIKE!!!
kama unataka maelezo zaidi
bipu vodafasta 078656565122
Video toka Brazil za watu ambao wanaishi pori.
ReplyDeletehttp://youtube.com/watch?v=Ur-HOcnCg84&feature=related
KABLA YA KUWAENDELEZA HAO WAHADZA KUNA MAMBO MENGI YANAYOTOKEA AMBAYO NI KICHEKESHO KUNA TOUR OPERATOR MMOJA AMEJIMILIKISHA KIJIJI KIZIMA CHA HAO JAMAA UKITAKA KWENDA KUTALII HUKO INABIDI UENDE OFISINI KWAKE ARUSHA UKALIPIE NDIO UENDE, MBAYA ZAIDI MTU MWENYEWE "MDHUNGU" DOROBO TOURS
ReplyDeleteWanatakiwa waende shule lakini maisha yao yawe vivlevile kama wale wa south africa na wamasai amabao watu wengi sasa wanakuja hapo.Hilo kabila lina watu wasiozidi 25,000.Hata kama hawatafanya kazi wataingizia serikali pesa za kigeni kuliko kabila lolote lile barani africa na kuinua GDP.Kwani hao watu watakao kuja watalala kwenye hoteli na watakula chakula na watanunua vitu vingine.Na madhumini yao ni kuja kuona hilo kabila kwa hiyo unaweza jusema hao wanaitia hasara serikali?.Hivyo vitu hao watu watakavyo nunua na hotel watakazo lala ziataongeza GDP.Nitakueleza kuwa ni copy ngapi za DVD's zinauzwa Duniani kote?Tunabidi tuwe makini na kuweka sera nzuri ili kuingizia pesa serikali yetu.Hapa sio mchezo kaka michuzi hii mada ni nzito na ina maana sana sana kwa maendeleo yetu.Hilo sio kabila kubwa ukifikiria na makabila mengine.Hiyo ndio eco-tourist tulioongelea pale arusha [sullivan summit].
ReplyDeleteSidhani kama kuwatumia hawa watu kupata utalii ni good idea. Kwa nini yeye huyo consultant harudi kwao alikokulia babu mzaa babu yake watu wakatalii as well?
ReplyDeleteTusiige mambo ya wazungu eti igloo na hizo website za bbc hawa bbc wapi wamewaacha watu wao waishi maisha ya karne ya 16?
Sasa hivi watu wana zungumzia technologia ndio inayoleta maendeleo.
Tanzania ni tajiri hela zote za ufisadi zikirudishwa na mianya ya ufisadi kuzibwa.
Kijana.
Nashukuru kutujulisha kwamba wapo ndugu zetu hapa njini ambao bado wanaishi hivyo, however, sidhani kama ni vizuri kuwatumia kwa Tourist Attraction, that's what Museums are for. Their life style and culture can be preserved in many different ways without encouraging to remain this way. We need to bring hawa ndugu zetu to par with the rest of the society we are in today. Hata watu weupe kwa maendeleo walionayo leo, hawakuamka siku moja asubuhi wakawa wamevaa suti na tai na kutumia vijiko na uma, wao vile vile they changed and evolved thru the years. Wao vile vile walivaa ngozi za wanyama !!
ReplyDeleteLast time I checked, hakuna watu huko Finland au Norway ambao wamehifadhiwa(preserved) for show and tell !! Even the Native Indians in the USA, the so called Red Indians - they no longer ride on horses in the wild and shooting arrows and eating berries, they are homogeneous with rest of the Americans and yet their history and culture is much in evident and is there for anyone to learn and see.
Let's bring our brothers and sisters to par with rest of Tanzania.
Mdau -Atlanta-USA
Shule inaendelea......
ReplyDeleteYUMKINI tunaelimika na blogu Jamii!
Kuna mwana kijiji hapo juu naitwa Anony...kasema watoto wa hao Wahadzabe waondolewe porini. Ndio twaweza waondoka lakini siku moja watadai walidhalilishwa na kupokonywa haki yao ya kuishi maishi yao yenye utamaduni ambao wanaufurahia.
sina ujuzi wa haki za binadamu..lakini uwelewa mdogo ni kuwa ni haki yao kuishi maisha ambayo wanayafurahia. Kikubwa ni kuwaendeleza pale walipo.
Sisi hizi haki ni nyingi mfano akina dada ukiwaambia wasivae vimini,Je mtaelewana?
Bofya hapa kusoma kesi ambayo ipo Canada:
http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/7438079.stm
mwenye kiti naomba kuwasilisha mada hii!!
Mungu wangu! Siwezi kuamini kuwa kuna watu wanatamani binadamu wenzao waendelee kuishi maisha ya tabu na ya ajabu ili wao wafaidi. Hivi kweli tunaweza kuwafananisha binadamu wenzetu na wanyamapori? This is more than ufisadi, naapa!
ReplyDeleteSeve
Mdau wa June 11, 2008 2:12 PM, ni kwamba kosa sio mzungu ni pumbafu lidas wanaofikiria mishikaki na bia na tujisenti wakidhalilisha utu wao na elimu zao,huyo mzungu sio chizi akulupuke tu na kumiliki kijiji,Back to the point naunga mkono hoja ya mdau wa June 11, 2008 12:40 PM,waacheni binadamu waamue wenyewe maisha wanayotaka kuishi,kuwalazimisha waanze kuvaa jinsi wakati hawapendi ni kuwanyima haki zao,ni sawa na leo watoke watu huko watulazimishe tutembee uchi bila nguo je mtaona poa?
ReplyDeleteJamani kuna hili swala eti kila mtu anauhuru wa kuishi popote anapotaka. Wapi???
ReplyDeleteUlaya sehemu zote ziko surveyed na hakuna nyumba inayojengwa bila ku-husisha council. Acha kujenga nyumba ile iliyopo ukitaka kuirekebisha lazima uombe kibali.
Sasa hao ndugu zetu consultant anashauri waishi mazingira magumu ili nchi ipate hela!
Wale wanahitaji msaada waishi katika mazingira yanayolingana na haki za binadamu kama access ya huduma muhimu matibabu,maji safi na MASHULE.
Mdau
We anon wa June 11 at 1:36am, cha ajabu kipi watu kutoka Ulaya kuja TZ kuangalia wanaoishi porini mshamba wewe, mbona hapa US watu wanaenda porini kuwaangalia Red Indians wanavyoishi??
ReplyDeletemoja ya sababu,iliyofanya maendeleo yachelewe kufika afrika,ni wakati wenzetu,wanadomesticate wanyama,na kuacha maisha ya wandering,hatimaye kutokana na kutulia,wakawa na organisation na division of labour.sisi africa tulipokuja kustuka na kutulia,others were well ahead,sasa in this day and age,hawa wahadzabe are being condemned to remain behind for the sake of heritage.this constitutes a crime against the hadzabe,and believe me,iko siku watakwenda mahakamani kudai haki yao citing years of neglect by the tanzanian government
ReplyDeleteEti ooo maisha ya tabu na dhiki... eti waendelezwe...
ReplyDeleteWAENDELEZWE KWA LIPI?
SEMA, KWA LIPI..?
- HAWANA UKIMWI
- HAWANA KIPUNDUPINDU
- HAWANA FOLENI ASUBUHI
- HAWANA KELELE
- HAWANA SHULE (FORMAL)
- HAWANA DEADLINES
- NA ORODHA INAENDELEA...
Kama wanaishi kwa Amani.. waacheni.. Kha!
Maisha gani haya ya raha... bia za kudandia weekend?
Au kitimoto cha juzi?
HII NGUMU WADAI YAANI KUNAWATU WAANAWAAMBIA WENGINE KWAMBA WAO WANAMAENDELEO KULIKO WAO. KWAMBA MAISHA YENU SIO BORA , UNATAKIWA UNA MAISHA BORA. KUANZIA LEO UKIPITA HAPA WEWE UTASHITAKIWA (TRSSPASS) HURUHUSIWI KULIMA HAPA MPAKA UWE NA KARATASI, MAANA HAYA MAENDELEO YAMEHAMISHIWA KWENYE MAKARATASI. KILA KUKICHA WATU WANATEGEMEA MAKARATASI. DU AKO KAKOLONI KALICHOVUMBUA MAKARATASI KANAAKILI. ALICHUKUA MADINI YA WATU YA THAMANI KAMA GOLD NA ALMASS ALIPODAIWA AKASEMA' KARATASI HILI NDIO MALIPO YA VITO VYA SAMANI' BASI BINADAMU WAKAKIMBILIA MAKRATASI YANAITWA PESA, USIKU HAWALI WANATAFUTA PESA, AKATOKEA MJASIRIAMALI MOJA AKASEMA UKINILETEA HIKI KILE CHA ZEZUZERU UNATAPATA PESA, SASA WAZUNGU WETU AMBAO NDIO WAWEKEZJI ASILIA WANAUWAWA. SASA HAYA MAENDELEO MNAOJIKOMBA NYIE VIBARAKA WAMAMBO LEO WASHIKAJI WENU NA VIJITEMINOLOGY VYENU SIJUI SAP AU GDP HAYO NI MAMBO YA ZAMA ZA MAWE , MSITULAZIMISHE TUWEKE UJINGA WENU WA KUSEMA HAKUNA MUNGU, KWANZA MAENDELEO YENU MNAYOJIVUNIA YAKO HEWANI. HUWEZI KUMILIKI ARDHI AU NYUMBA UNAMILIKI MORTAGE, HUWEZI KUNUNUZ GARI UNAKUWA NA LEASE. HUWEZI KUWA NA CASH UNAKUWA NA MIKOPO CREDIT. NA HII CRDIT NI MITEGO HYA KUWAFILISI WATU.WADAU MANAOISHI HUKO USIKUBALI KUSAIN CHOCHOTE HAWA JAMAA NI PROFFESSIONAL PLASTIC SMILERS. MAENDELEO NI KUISHI MILELE TUU HAMNA UJINGA MWINGINE
ReplyDeleteHayo maendeleo yanayotajwa ni maendeleo ya watu au vitu?
ReplyDeleteNi dhambi kuyatumia maisha wanayoishi Watanzania wenzako kama "zoo" ili uweze kujipatia kipato eti cha kuinua GDP.
Hawa watu inapaswa wasibughudhiwe na wazungu wanaoenda kuwashangaa wanavyoishi maisha ya asili. Badala yake inapaswa sisi Watanzania wengine tujifunze kutoka kwao jinsi walivyoweza kujinyambulisha na mazingira yao. Kwa mfano, hawana hospitali lakini wana namna zao za matibabu. kwa kujifunza wanavyotibu tu tunaweza kuinua GDP. Mambo kikoa. Tutengeneze mazingira ambapo na wao wanaweza kujifunza kutoka kwa Watanzania wenzao kile wenzao wanachokifahamu. Tujichanganye nao, sio kuwatenga na kuwatumia kama njia ya kujiongezea GDP binafsi.
LIcha ya vyama vingi, ukweli wa kuwa binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshima ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake bado upo.
Ndugu environmental consultant, kama unataka kuwaonyesha viumbe hai wageni kuna mbuga zetu zina wanyama na mimea ambayo haipatikani sehemu nyingine duniani. Vinginevyo unaweza kujionyesha mwenyewe kwa wageni wako hao wakupe vijisenti.
Hatupaswi kuigilizia kila kinachofanywa na wenzetu. Kuna mweusi mwenzetu wa Congo alishawahi kuwekwa kwenye zoo huko New York. Tusifanye kosa hilo.
HIVI NYIE MNAOLALAMIKA OHH WAONDOLEWE WAPELEKWE WAPI??KUNA WANANCHI WANGAPI MIJINI MAISHA YAMEWASHINDA!!HAWA WAKITOLEWA HUKO WAPELEKWE WAPI??SI NDIO KUWAUWAA TUU..NI SAWA NA WEWE NIKUTOE HAPO MAREKANI ULIPO NIKUPELEKE MANZENSE KWENYE NYUMBA AINA HATA FENI WALA UMEME..UTAWEZA KWELI?MIE NAONA WAACHENI NA MAISHA WALIYO NAYO,MAANA HAKUNA MTU MMOJA ANAYEWEZA KUWASAIDIA HAWA WATU..AFADHALI WATALII WANAENDA KUWATEMBELEA NA KUWAPA HELA NA MATUMIZI MENGINE MENGINE.
ReplyDeleteno way pple shud live prem life in the 21 century,sudden changes will not bring a fair result but it is important for them to get education at least,welcome tourist but these pple shld not be treated like animals
ReplyDeleteYaani wahazabe waendelee kuwa wajima kwa faida ya nani?
ReplyDeleteSiasa na Historia vyakubali ujima ni hali duni kabisa ya maisha katika nyanja zote.
Kwa hiyo wewe unawashauri watanzania wawafanye wenzao maonyesho na kishangao kwa faida ya walioendelea, kwa maana nyingine, wahazabe wawe wajitoe muhanga wa kiuchumi.
Hata kama mafisadi wasingekuwepo, wazo hili ni chafu na waliolileta wana uja uzito wa mawazo, uviza wa ubongo huo. Ubaya wa wazo hili angalia kwamba utumwa ni bora zaidi ya ujima kimaendeleo, kwa nini tuung'ng'anie ujima ikiwa utumwa ni mbaya kama tunavyofahamu.
Soma notes zako ujue kuchagua kitega uchumi.