mama wa mitindo asia idarous akionesha ubunifu wake wa mavazi ya harusi
mkongwe khadija mwanamboka anaonesha mamodo wake wa kiume katika mavazi ya harusi huku khadija kopa (shoto) na sabbah muchacho wakiimba wimbo wa 'kimasomaso mwanangu msimuone"
mustafa hassanali akionesha ubunifu wake wa mavazi ya harusi
mamodo wakiwa katika mavazi ya harusi yalobuniwa na rose valentine

safi wamejitahidi, nimependa nguo za khadija mwanamboka
ReplyDeleteMz. Michuzi asante sana kwa kutubandikia picha hizi. Nimefarijika sana kuona kwamba tunaanza kujikomboa kiutamaduni na kuondokona na KASUMBA iliyotawala miongo kadhaa sasa kuwa vazi murua la harusi ni lile lililobuniwa huko "ULAYA"!!!! Ninawapa pongezi wabunifu na kuwaomba waendelee na ubunifu wao kwa kasi mpya na kwenfa nje ya mipaka ya harusi. Nani anajua, pengine wanaweza kuja na ubunifu utakaotutoa kwenye unifomu ya mikoti na mitai ya ulaya, na kutuweka kwenye vazi ambalo tunajisikia raha na bado tunaonekana kuwa watanashati na waungwana katika mijumuiko rasmi ya kitaifa na kimataifa.
ReplyDeleteHongera wabunifu,
mkereketwa wa utamaduni
Hongereni sana.
ReplyDeleteNimependa vazi la Rose Valentine.
Natumaini next maonyesho wabunifu wote mtaondoa huo U-Nigeria kwenye mavazi mbuni kitu pekee kidogo
Wapi Africa Sana???
ReplyDeletevazi la rose valentine ndo bomba sana wengine bado sijaona kitu hapo,jaribu tena baadae.
ReplyDeletendugu anony wa hapo juu, kumbuka kwamba ubunifu ni pamoja na umairi wa kuchanganya vitu kutoka vyanzo mbalimbali. Katika dunia ya sasa ya utandawazi tusitarajie kuwa wabunifu wa kitu cho chote kile wataanzia kwenye zero. Bali watachukua hapa na pale kutoka vyanzo mbalimbali nigeria, south africa, ulaya, india, china, congo, uganda, nk. huo ndio utamaduni hai na endelevu na umairi ni jinsi gani mtu anavyochagua na kuchanganya.
ReplyDelete