Home
Unlabelled
siku ya bajeti zenj leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ha ha ha ha ha ha....! Mbavu zangu jamani lol!
ReplyDeleteNikisema sana "watan TABLE".
Mh! Yale yale
ReplyDeletekwi kwi kwi kwi kwi!
ReplyDeleteutafikiri kuna cha maana humo ndani wakati kaumeme tuu kidogo kamekatika wameshindwa kurudisha mwezi mzima halafu wanategemea waendelee,na wakati huo huo karume anakandamiza wapemba...aibu tupu na sijui anakenua mimeno yake ya nini huyu waziri,budget 75% ni fake na wanasubiri misaada la sivyo itaishia kwenye karatasi tuu,amkeni wazanzibar
ReplyDeleteHivi Viongozi wetu wanajua wanachokifanya?Au wanafanya kazi kwa mazoea tu bila kutafakari athari zake?Lets be serious!Utawezaje kuwa na Bajeti Mbili Tofauti,moja Visiwani na nyingine Bara/Visiwani ambazo hazina mahusiano kabisa kisera(sera za uchumi),Bajeti ambazo kila moja inajitegemea kikamilifu,LAKINI katika pande zote mbili sarafu inayotumika ni ileile moja!Kila upande utatoza kodi zake ili kukusanya mapato ya serikali,LAKINI,miingiliano ya kibiashara na kiuchumi baina ya pande hizo mbili ni mikubwa mno kiasi ambacho kutoza kodi katika kila upande ni kuzidi kuuvuruga uchumi wa pande zote mbili kwa kiwango kikubwa zaidi?Kwanini pasiwepo na Bajeti ya Zanzibar ambayo ikishapitishwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndipo iunganishwe kama sehemu ya Bajeti ya Tanzania nzima bila kubadilishwa lakini Bajeti hiyo ya Pamoja ikiwa na uwezo mkubwa zaidi wa kutilia maanani athari za viwango mbalimbali vya kodi na riba za mabenki pamoja na mikopo na mishahara ya wafanyakazi.Na hatimaye kujenga uwezo mkubwa zaidi wa kulinda THAMANI YA SHILINGI YETU na kuwa na udhibiti mkubwa zaidi katika MAPATO YATOKANAYO NA BIASHARA YA NJE?Kwa manufaa ya Watu wetu wa Pande zote mbili Bara na Visiwani?Najua kama ilivyo desturi Viongozi wetu wakishasoma ushauri huu watakuwa wepesi sana wa kukurupuka na kutamka kwamba,'Aaah We hujui?Haya yote wenzio tulishayajua siku nyingi,na hivi sasa tunayafanyia kazi.Inshallah Mungu Bariki katika Bajeti ijayo pengine mabadiliko makubwa yote hayo utayaona'.Tuache Ujinga.Hakuna kiongozi aliye litambua hili.Lingekuwa limekwisha rekebishwa ndugu zangu!.Mimi nipo tayari kutoa msaada wa ushauri wa kitaalamu kufanikisha zoezi hilo.Naweza kupatikana au tunaweza kuwasiliana kupitia Blogu hii ya Michuuz.Tuache ujinga wa kujifanya tunajua kila kitu.Tukumbuke 'Kinyozi Hajinyoi'.Unaweza kuwa na PhD ya Uchumi lakini yakakushinda haya ninayo yazungumza.Hayakuandikwa katika Kitabu Chochote.Labda kama hatuko serious na maendeleo ya nchi yetu na uchumi wetu.Lakini kwa mtindo huu tunao kwenda nao,hakika tumegeuka Vioja katika Taasisi za Fedha za Kimataifa,na wamesha tutambua kwamba hatujui tunachokifanya.Hatujui nini tunachokusudia kukifanikisha.Kama zilivyo hivi sasa Bajeti zote za pande zote mbili hazina tofauti na 'Shopping List'ya serikali zote mbili,ya Visiwani na ile ya Tanzania nzima!No,it is time we changed!Tutakuja chekwa na Watoto wetu wenyewe katika miaka ijayo.Mungu iangaze Tanzania,Wabariki Viongozi wake na Watu wake ili waione Njia ya Wokovu!Wokovu wa Kiuchumi.'tonny'
ReplyDelete