.....NA MPIRA UMEIKWIIIIIISHAAAAAAAAAA.....
TAIFA STARS IMETOKA SARE YA 0-0 DHIDI YA CAMEROUN KATIKA MPAMBANO WAO ULIOCHEZWA WANJA JIPYA LA NESHNO...
DAN MRUANDA KAKOSA BAO AKIWA KABAKI YEYE NA WAVU DAKIKA YA 92!!!
MAXIMO KAHOJIWA SASA HIVI NA KASEMA VIJANA WAKE WAME-PRUVU KWAMBA KUJIAMINI KUMESAIDIA NA KWAMBA WANAWEZA WAKAFANYA MAAJABU HUKO MBELENI


nini tena hapo...?ila anagalau mambo yamekuwa ivo si mabaya...tupe listi ilikuwaje leo kaka michu...
ReplyDeleteHongera Bw Michuzi! Umefanya coverage nzuri na iliyo fasaha ya mpira wa leo. Imekuwa kama ile iliyopo BBC Sports.
ReplyDeleteMdau
http://drfaustine.blogspot.com/
SIONI CHA OYEE HAPO.ILITAKIWA USHINDI KUFUFUA MATUMAINI YA KUENDELEA MBELE.HII NADHANI NDO TUNAYAAGA MASHINDANO TARATIBUUU.......!!!!!!!YAANI BILA KUSHTUKIA.
ReplyDeleteHaya! tumeshindwa kuwafunga hapa nyumbani ndo basi tena!!
ReplyDeleteSasa dada zetu wakawaburudishe new africa maana kwao ni kama ushindi. Nasikia kambi wanapiga hapa hapa, kweli?
Sasa taifa stars oyeee kwani matokeo hayo yamewasaidia nini kwenye kundi lao? Wameshindwa kushinda mechi zile rahisi tungekuwa mbali sasa.watu wanalia maximo ,maximo kiko wapi sasa? Wakifungwa kidogo maximo hafukuzwe.
ReplyDeleteSasa Taifa Stars!! Hatukutakiwa kutoa droo nyumbani!! Ilibidi tushinde! Wao ndio wameshinda kwani walikuja kutafuta droo ugenini!! Hebu njoo hapa kaa chini!!
ReplyDeleteYes tunauwezo wa kuwafunga Cape Verde nyumbani, labda tukabahatisha ushindi na Mauritius. Jumla point 6 plus hizo mbili tutakuwa na nane ambazo tayari zimeshafikiwa na Cameroon. Sasa nafasi ya kwenda iko wapiu?? ah mi nshachoka sasa!
Una kiherehere issamichuzi.Umeshaidaka hiyo.Halafu naomba jumatatu post email adress yako kuna question nataka kukuask through your adress.
ReplyDeleteTaifa staaaaaazzzz oyeeee!!!!Ebwana ndo maana hali ilkuwa mbaya kwa kuogopa majina..duh kumbe mpira ni mpira tu!ndo maana uholanzi walimlamba Ufaransa 4-1!
ReplyDeleteMichu big up bro kwa kutuhabarisha live ubarikiwe.
mdau,
l'shi
Duh! Kweli tumeishiwa..yaani tunashangilia SARE??
ReplyDeleteNaomba niwapongeze taifa stars kwa mchezo wao wa leo na pia naomba niwalaani wote ambao kwa namna moja ama nyingine waliikatisha tamaa timu yetu. Najua tuna wachezaji wazuri na tuna uwezo wa kushinda ila tatizo ni kutojiamini kwa wachezaji wetu. Nina imani tukiwa wavumilivu tutafika mbali.
ReplyDeleteWatanzania kuweni wazalendo na muwe watu wa kupenda vyenu badala ya kushabikia vya njee. Naona leo wachawi wa stars wameumbuka. Stars oyeeeeeeee!!!
Shukrani mkuu wa nanihii ya nanihii kwa kutupa updates za mara kwa mara za mchezo wa leo.
ReplyDeleteHongereni Taifa Stars na Watanzania kwa ujumla. Tukiendelea kuiunga mkono timu na benchi la ufundi tutafika tu.
Wale wadau waliotaka kumtosa Maximo na kumkabidhi timu Bendera bado wana mawazo yale yale au wamekubali tuvute subira?
Ok sasa wadau mpira umekwisha sasa hapo kipi kinaendelea tumeshatoka au vipi??Maana mpira wa bongo mara nyingi sana huwa sifatiliii ok mdau anayefahamu zaidi maana mara ya mwisho nilisikia mnasema kwamba inabidi leo watoe droo na cameroon sasa nini kinaendelea hapo jamani????
ReplyDeletesasa nadhani tumekua na losing mentality, droo tunafurahia utafikiri ushindi, hata kama ni cameroon na wana masupastaa wangapi lakini droo sio ushindi, tusiwe kama england jamaa.
ReplyDeleteHabari kutoka tovuti ya bbc zinaonyesha kuwa Malawi wamewapiga bao 1-0 mabingwa wa Afrika, Misri. Malawi tulicheza nao mechi ya kirafiki tukatoka suluhu.
ReplyDeleteHabari nyingine zinasema Uganda wamewatandika 2-1 wenyeji wa CAN ijayo, Angola. Tukumbuke kwamba Angola walishiriki kwenye fainali za kombe la dunia. Tulishacheza nao mechi ya kirafiki tukatoka suluhu-nusu tuwapige isingekuwa refa msaidizi kuchelewesha substitution yetu. Uganda tumeshawatoa nje kabisa ya CHAN.
Kenya nao wamewapiga bao Niger, 2-0. Wakenya hao hao tumewatoa nje kabisa ya CHAN. Burkina Faso wamejipatia ushindi wa pili mfululizo. Hao tuliwapiga bao nyumbani na ugenini mwaka jana.
Pamoja na kutoshinda leo na kuishia kupata suluhu ya kutofungana na timu inayoongoza kwa ubora wa soka Afrika hivi sasa, nani anasema kiwango chetu cha soka hakijapanda????? Nawasilisha.
Hongera Stars. Kucheza mechi kubwa na mastaa kama Samuel Eto'o, Rigobet Song and wengine na mkatoka nao sare, si mchezo ! mmejitahidi, hii inaonyesha kuwa mkishikamana na kuwa kitu kimoja, huku mkiimba kwani nini wao wameweza na sisi tushindwe tuna nini? basi tutafika mbali. Bravo stars.
ReplyDeleteNjaps
Kutoa sare ndio tunashangalia namna hiyo?
ReplyDeletemmh, hadi draw tunafurahia na huku tukijua bado tupo kwenye wakati mgumu, anyway niwapongeze timu ya taifa kwa kubanana na cameroon hadi dk 90 za mchezo zilivyoisha. Kweli haya mashindano yanaonyesha kwamba kila timu sasa ya africa inataka kwenda kucheza kwenye mashindano ya kombe la dunia na si zile timu zilizozoeleka kila siku, mana naona hadi majirani zetu wa KENYA, UGANDA NA RWANDA wanaendelea kupeta kwa sana tu.
ReplyDeleteHongereni Taifa staaz kwa kweli mmeanza kuiva sasa duuuuu. Leo mmecheza mchezo mzuri sana ingawa hamkupata bao. Kaza buti wajameni. Nawatakia mafanikio mema katika mechi zijazo.
ReplyDeletemichuzi ama kwa hakika vijana wametupa raha leo,sikutegemea kwani nilijua leo tunavuna kapu la magoli hasa nlipokuwa namfikiria etoo,badala yake vijana hakuangalia cha etoo wala nani,bravo stars,aluta continua....mpo juu
ReplyDeletestazzzzzzzz oyeeeeeeeeeee!! hapo tu team yetu imetinga kombe la dunia! hongera maximo au manimo???
ReplyDeletekwa maelezo ya walio bongo tatizo ni UMALIZIAJI. Taifa stars wametengeneza nafasi nyingi za kufunga . .... ikiwamo moja dakika za mwisho kabisa .
ReplyDeleteMichuzi hivi kuna kocha gani anayeweza kumbadilisha Jamie Carragher kuwa prolific striker?????
... NAOMBA KUWAKILISHA TENA HILI SUALA LA KUMJADILI KOCHA BADALA YA WACHEZAJI .
mbona inatosha tu iliyobaki maximo wapange vijana wako ili mkawakomalie nakwao.......niliwaambia watu kule kwa BC nothing impossible maana wengi wali wadharau stars wakajisahau kua mpira unadunda........bigup stars
ReplyDeleteKESHO MAURITIUS AKITOKA SARE NA CAPE VERDE ITAKUWA.
ReplyDeleteITAKUWA:
CAMEROUN 7
CAPE VERDE 4
TZ 2
MAURITIUS 2
Tukiwa wa pili tunaenda Angola au? Au wa pili kwenye makundi yenye timu 5? Maana kuwa wa kwanza hapa ni ngumu na timu tumecheza nazo zote.
Kama kuwa wa pili dili, basi tuwafunge wote.
Mi angalau nimeridhishwa na matokeo,ila kimchezo Stars tuseme ukweli safari ni ndeefu,ndefu mno na mimi sijaridhishwa nao.Tumepata suluhu kwa sababu Cameroon haikucheza vizuri nadhani japo wengine watakereka lakini ukweli ndio huo.Sababu za kutoridhishwa na uchezaji wa Stars ni kama ifuatavyo
ReplyDelete1.Nilikua naangalia mechi jukwaani lakini sikuweza kuhesabu pasi zikafika 4 bila Cameroon kuupata mpira!Hii inaonyesha timu bado ina matatizo katika kumiliki mpira.Ikumbukwe kwamba kumiliki mpira ni njia inayokuwezesha kutengeneza nafasi za kufunga na pia ni silaha nzuri ya kuzuia msifungwe
2.Timu yetu ilikua na tatizo la kuunganika,wachezaji bado ni wazito sana kufunguka pindi wanapopata mpira,ama wanapoanzisha mashambulizi. Hii imesababisha mchezaji anayekua na mpira kutumia muda mwingi akitafuta Options za wapi apeleke mpira.Sijui ni kwa sababu wachezaji wengi wametokea viwanja vyetu vya uswazi ambavyo pitch ni ndogo?maana wanashindwa kutanua kabisa uwanja,hali iliyopelekea kina Alex'Song kupora mipira kirahisi katikati.Na athari za kupoteza mpira kirahisi ni kupoteza nguvu nyingi mlizotumia kuutafuta mpira,hivyo kuathiri ubunifu
3. Viungo wetu wanatatizo la namna ya kupiga pasi za mwisho. Hii pia inaweza kusababishwa na strikes kutojua namna ya kuonesha njia,au kukaa kwenye nafasi.Tatizo hili limejionesha wazi kwa Ngasa ambaye alicheza kiungo mshambuliaji wa pembeni.Mchezaji huyu ana pace nzuri,ana footwork nzuri lakini anatatizo la kupiga pasi za mwisho.Bado anahitaji msaada mkubwa wa namna ya kuelewa ni wakati gani apige krosi ndefu,na wakati gani apige square pass ama ni wakati gani aendeshe,"cut inside".Maana alikua akifahamu wazi kwamba Bikey na Song ni warefu kumzidi Mrwanda lakini alishindwa kupiga hata krosi moja ya chini.
4.Kuhusu strikes ni kwamba hatuna strikers,ukweli ndio huo jamani.Na hili si tatizo la Tanzania pekee!.Huwezi nishawishi kwamba Dan Mrwanda ni centre striker,amepungukiwa sifa nyingi sana(my view)
5.Back line pia bado ina kasoro nyingi,ni Shadrack Nsajigwa pekee namkubali,lakini Amir Maftah na Nadir? sijui!
6.Kuhusu kipa mmh,tushukuru mungu zile mistakes mbili hatukuadhibiwa,nadhani hapa Yanga wanajibu zuri tu kuhusu kipa
Kuhusu kocha sina comment nyingi,ninachoweza kusema ni kwamba "progress is a slow process" pia "looking for more alternatives is also the best way of solving the problems"
gEoRGe
Wanaoshangaa tunaoishangilia sare niwafahamishe ninachoshangilia mimi. Timu inaonyesha kuwa katika mwelekeo sahihi wa kutisha katika ulimwengu wa soka.
ReplyDeleteNi mwaka 2002 tu tulikuwa tunapigwa 5-0 na Kenya. Sasa hivi Kenya hawatupi homa tunawatandika na hata Cameroon na Senegal tunatoa nao suluhu tukiwa kwetu. Tukiendelea na mwelekeo huu baadae kidogo Cameroon nao tutakuwa tuna uwezo wa kuwapiga na kuweza kutoa sare na kina Argentina, Brazil na Uholanzi. Kisha baada ya hapo tutakuwa na uwezo wa kuitandika timu yoyote ulimwengu huu. Ndicho tunachoshangilia. Soka inahitaji muda. Hata elimu ya msingi inachukua miaka saba kuhitimu.
Taifa Stars oyeee.
Wewe Anony June 14 11:35 pm hapo juu.Wewe ni mziray nini?Bado tuna safari ndefu tunakubali.Lakini usiseme Cameroun hawakucheza vizuri.Nani alikudanganya kwamba Cameroun hawakucheza vizuri(Stars ilidhibiti formation yao ndo maana unasema hawakucheza vizuri).Mimi nadhani Siyo vizuri kwa sasa kutaja majina ya wachezaji wetu humu mmoja mmoja.Hii inaweza kuwakatisha wachezaji wetu tamaa
ReplyDeleteYou got to remember hiyo Stars haina professionals kama ilivyokuwa Cameroun.Professional players wanasaidia,angalia Kenya na Uganda wanavyo perform.Bado tuna safari ndefu ni kweli,so pole pole tutafanikiwa nadhani.Hata hivyo naheshimu mawazo yako.Una uhuru.Samahani kama nimekukera.
hapa hamna cha kufanya vizuri au kutoka kidedea wala nini manake hii mechi ilikuwa ya taifa stars kushinda. draw unatoka ugenini sio nyumbani. angalia uganda wamewafunga angola nyumbani, malawi wamewafunga egypt nyumbani, rwanda wamewafunga morocco nyumbani. hizi ndo gemu tutakazokuja kujutia kwa nini watukushinda
ReplyDeletewabongo tumezidi unafiki sana, watu walitabiri tutafungwa 8,10 n.k kiko wapi? shame on u haters starz walicheza kwa kweli, cha msingi tuipe moyo timu yetu na sio kuikatisha tamaa
ReplyDeleteMs Bennett
Taifa stars oyeeeeeeeeeee!!!! mmejitaidi bwana kutoa droo na mataita
ReplyDeletebig up maximo,
Cameroon international Jean Makoun has left Lille to join another French club Lyon in a deal worth US$21.6m.
ReplyDelete