ze comedy wakiongea na waandishi wa habari leo ukumbi wa maelezo, dar. chini ni katika mojawapo ya shoo zao ambapo saa ingine ilibidi iahirishwe kutokana na msongamano
KIKUNDI cha Sanaa za Maigizo ya Luninga nchini maarufu kama 'Ze Komedi' kimeulalamikia uongozi wa East Afrika Television (EATV) kwa kuwazuia kutumia majina na uhusika wa uigizaji waliokuwanao katika kituo kingine cha TV kwa madai kuwa ni hati miliki yao.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ze Komedy Production, Isaya Mwakisyala alisema uamuzi wa Cosota kukubaliana na ombi la EATV kuwa Ze Komedy ni mali yao katika barua walioiandika Juni 9 na kujibiwa na Cosota Juni 10 kuwa ni mali yao si sawa kwa kuwa wao ni kikundi kinachojitegemea.

"Hatukuanzishwa na EATV bali tulikuwa ni waigizaji kipindi kirefu kabla hata hatujaonekana huko, kinatushangaza na kustaajabisha kitendo cha EATV kudai kuwa Ze Komedy ni mali yao, sisi tuanchosema tutaendelea kuwa huru na kubakia vile vile katika uigizaji huo kama kawaida," alisema Mwakisyala.

Alisema mkataba wa uhalali wa kumiliki kikundi cha Ze Komedy waliupata Julai Mosi mwaka 2007 kwa cheti halali baada ya kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) tofauti na EATV ambao wanadai kupewa umiliki wa Ze Komedy Juni 30 mwaka huu.

Alisema endapo kutatokea kutoelewana kokote baada ya uamuzi wao wa kuingia mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) ambao uhamasishaji wa matangazo ulianza jana, watakwenda kumuona Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ikishindikana watafika kwa Waziri Mkuu na hatimae kwa Rais.

Hata hivyo kurushwa kwa vipindi vya kundi hilo TBC1 kutaanza baada ya wiki mbili zijazo kutokana na safari ya kundi hilo nchini Uingereza baada ya kuahirisha ya kwanza nchini Afrika Kusini kutokana na ghasia zilizokuwapo nchini humo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2008

    ze comedy ni production ya East africa.msilete malumbano bila sababu.muwe na shukurani kwa walivyo wapromote
    kweli tenda wema uende zako

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2008

    kama ndo hivo basi tafuteni jina jingine, kwan mkibadilisha jina mtapoteza mashabiki wenu kama wapo wapo tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2008

    sasa kama mlisaini mkataba bila kusoma, waziri atawasaidia nini? ndiyo maana watu huwa wanaajiri mawakiri....tamaa siyo nzuri....na mkivunja mkataba tu, basi mtafirisika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2008

    Tatizo jina?? au swala ni kuwa hata kama watu watawaponda au vipi, NYIE MNA VIPAJI, kipaji ni kipaji hata kama mtaenda wapi!!! -ACHENI MALUMBANO PIGENI KAZI-Haya ni baadhi tu.

    1.ZE KOMEDI
    2.ZEE COMEDY
    3.LI ZE COMEDI
    4.THE COMEDY


    mdau
    canada

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2008

    hata wakienda kwa kikwete haitawasaidia...hayo ni mambo ya copyrights law wapate mwanasheria awa advise vizuri other than that wanajipotezea mda ambao wangekua wanaendelea kuingiza pesa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2008

    Ndiyo maana kwenye nchi zingine vikundi vya sanaa vina mawakili/wanasheria.... na pia kuna field ya kusomea kwenye sheria inaitwa "Entertainment Law".....

    Naungana na mdau "Tenda Wema" hapo juu kuwa ze comedy ni production ya EATV.....hawa jamaa ni waigizaji wazuri lazima masuala ya sheria wawaachie wanasheria...

    Maajabu....msaani wa kikundi, wakati huo huo ni Mkurugenzi, wapi na wapi?.....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2008

    jamani msifanyiane visa ,ila mjipange kutupa vichekesho upya, eatv imewafanya mfike hapo cha msingi tu ni kuhama kistaarabu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 12, 2008

    Aroo Arooo!!embu sikirizeni kwanza!!munarichezea hilo likyombo la serikali bwana..mtaishia pabayaaa nyie jifanyine wadogo tuu!!na mbadilishe rijina bwana...achanagane huko bwanaaa..asanteni arooo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2008

    Nyie mnawalaumu hao Ze comedy bure, kama wao walisajili kikundi chao kwa jina hilo tangu zamani hakuna mtu ana haki ya kuwanyang'anya hilo jina lao, nani kwanza alikuwa anaangalia EATV zaidi ya wapenda muziki wa bongo fleva? Hata hao EATV wamenyanyuliwa na Ze Comedy sio ze comedy peke yao walionufaika. Hao bwana sio wa kwanza kufanyiwa hivyo hata kuna mtu alishawahi kulalamika kuwa alisajili bongo star search, baadae wakamgeuka na kumzunguka, lakini kwa kuwa alikuwa ni mnyonge basi haki yake hakuipata. Hao COSOTA sijui COSATA Kama kweli ni wafuatiliaji, wanamuziki wa Bongo wanalia kila siku kazi zao kuibiwa na wahindi mbona hatuoni wakichukua hatua? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

    Na kama kweli EATV ndio iliwanyanyua hao vijana na kuwafunda na kuwafanya wakawa wazuri, basi wawaache si wameshakuwa, wachukue vijana wengine mtaani waendelee kuonyesha show! Waapi, wengine hao wanavipaji vya kuzaliwa navyo na si mara ya kwanza duniani kwa TV show kuhama kutoka kituo kimoja kwenda kingine lakini kwetu kulivyo na visa na mikasa basi hao vijana wataonekana wameroja na kufanyiwa vitimbi vya kila namna. Watu wanaacha kazi na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine kufuata maslahi, wengine wanahama mpaka nchi itakuwa wao acheni mawazo na roho za kwanini!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2008

    Ndo maana kila leo wasanii wa bongo wanaambiwa wasome! Hiyo haki haitolewi na Raisi wala waziri mkuu! Mambo ya sheria hayo! Hukubaliani mtafute mwanasheria wa hakimiliki,muende mahakamani ukweli ujulikane!

    ReplyDelete
  11. mmmmmmmhhhhhhhhh hapa thiingilii. sina datas

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2008

    kama ni kubadili jina mbona sio tatizo majina yapo mengi tu, au wanataka na majina yenu mliokuwa mnatumia kama masanja, vengu, hamie j mbadili? hata wakitaka mbadili na majina sio nongwa ,masanja jiite maganga maana ni jina la kisukuma pia, na wengine hivyo hivyo.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2008

    MMEKWISHA ANZA VICHEKESHO VYENU SASA, WAZIRI, WAZIRI MKUU NA RAISI HAWANA MAMLAKA YA KUTENGUA HAKI MILIKI. MLIPOKUWA EATV MLIKUBALI KUKIENDESHA KIPINDI CHENU CHINI YA UTHIBITISHO WA HAKI MILIKI YA EATV PRODUCTION SASA KULIKONI? KUMBE UJANJA WOTE HATA KIKUNDI CHENU HAKINA MWANASHERIA! AIBU KATIKA DUNIA YA SASA KWA KIKUNDI KUFANYA SHUGHURI BILA MWANASHERIA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2008

    natumaini wadau wote hamjambo, mimi nakubaliana na mawazo ya wadau wote haswa mdau wa canada amewapa majina yanayofanana na si kama hilo la zamani, chukueni moja mtuletee mambo acheni kubishana haitasaidia tupeni raha WANAWANI, pia hakikisheni mnakuwa na lawyer wenu.
    mimi mdau ETM

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 13, 2008

    Ambao hamjui acheni longolongo zisizo na maana - Ze Comedy ni jina lao walilolisajili 2007 na wao kuingia EATV as that group and with those characters. Mkataba wao ni kwamba EATV watarusha kipindi hiki hewani tu na creativity, characters etc zitabaki kwenye kikundi. Incidentally it is said that they would regularly bring in 45 million TShillings per month through advertisements and other promotions but EATV gave the group only 250,000 - daylight robbery if you ask me!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 13, 2008

    Nyie hamjawaelewa hawa vijana, hii bongo bwana huko kwa waziri au waziri mkuu wanaenda kutafuta haki kwa maana watapata na msaada wa kisheria. Sheria zipo lakini hao wenye 'vijisenti' wanakandamiza sana WADOGO wanajali maslahi yao tu(hata pesa wanayowalipa ni peanut tu.)
    Wakiacha mambo yaende sijui mahakamani yatachukua MIAKA acha wapige njia ya mkato. Mimi pale bongo dala dala ilishawahi kugonga gari yangu kumbe ile dala dala ni ya 'kigogo mmoja polisi' we cha moto nilikiona haki ikawekwa pembeni kwenda mahakamani ile report ya polisi ni noma kesi ikachukua muda mrefu mpaka nika-give up. WE UNAFIKIRI KWA NINI RAILA ODINGA ALIGOMA KWENDA MAHAKAMANI?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 13, 2008

    mimi sioni kama kuna sababu ya kuwavalia njuga hawa ze comedy, wenye tatizo ni hao eatv. Hata wakiwaletea gozigozi ze comedy itabaki kua pale pale tena watazidi kuendelea zaidi...hamna kubadilisha jina wala nn...Ze Comedy oyeeee

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 13, 2008

    Ze Comedy acheni mambo ya kitoto!EATV ndiyo iliyowafanya muwe maarufu na kufikia hapo mlipo sasa.Hizo TV channels zingine hazikujua kama mpo kabla ya kuchukuliwa na EATV?Mkitaka kuanza shows katika TV Channels zingine kuna mawili.Ama muachane na EATV kwa maridhiano ya hiari yenye manufaa kwa pande zote mbili,na ni juu ya EATV kuwakubalia muendelee kulitumia jina la ZeComedy katika TV Channels zingine iwapo kwa kufanya hivyo wao EATV hawata pata hasara yoyote kibiashara na TV Channel nyingine haitanufaika bure bila ya gharama yoyote kwa jitihada na gharama kubwa ilizo zipata EATV kuwa promote na kuwajenga kama kikundi nyie ZeComedy,AU mkubali kutumia jina lingine kabisa na kuanze upya kwa mwelekeo tofauti katika TV Channels zingine lakini siyo kwa style ileile ya kusoma Taarifa ya Habari iliyotumika EATV!That is fair business practice.TV Channel nyingine haiwezi kuitumia EATV kujinufaisha zaidi kibiashara na kusababisha EATV wawe walijiingiza katika gharama za uwekezaji katika ZeComedy kama hawakuwa na akili timamu na kutohua walilokuwa wakilitenda.Hakuna atakaye wazuia ZeComedy wafanye watakacho kitaka.Lakini watumie busara katika kufikia maamuzi.ZeComedy ni jina na mali ya EATV.Infact Uongozi wa EATV unaweza kutafuta vijana wengine wakaendelea kuigiza katika TV Channel yao kwa kutumia jina hilohilo la KIPINDI CHA ZE COMEDY.Waigizaji wanaweza kubadilika lakini Jina litabakia lilelile.Wakiwa katika TV nyingine kina Masanja itawabidi wabuni na kutumia Jina jingine kabisa la Kisanii lakini sio ZeComedy.Kuchamba kwingi mwisho kushika Mavi!Huu ndiyo Mwanzo wa Mwisho wenu.Afadhali mngetuambia sisi wapenzi wenu kwamba baada ya kukaa kwa kipindi kirefu katika EATV sasa mmepata nguvu kifedha na mtapenda kuwa huru na kuanza maonesho yenu kwa kujitegemea bila kurubuniwa na mfanyabiashara mwingine yoyote.Lakini mlipo tuambia kwamba sasa mnafadiliwa na Manji na kwamba mtahamishia show zenu TBC hapo ndipo nilipo anza kuwaona kumbe hamna maana!Poleni sana.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 13, 2008

    Kwanzakabisa ZE Comedy Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
    Pili ni hivi, EATV wana wivu hawa
    wanataka kuwabania wenzao tu... hawana lolote....mm hawa washkaji nilishawajua kitambo tu.... hata kbla hawajaanza kurusha vipindi vyao EATV....
    kwa EATV hawana vipindi vizuri zaidi yailivyokuwa Ze comedy ..... yaan wao ni miziki tu hamna hata cha maana... watangazaji wenyewe mikorogo mitupu mpaka wanaume wamejichubua siwapendi mie....
    Nadhani nimemaliza wadau
    Ila Ze comedy hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
    EATV achen roho za WHY... KWANININIIIIII!!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 13, 2008

    Simple logic. Hivi kama mimi no Consultant nina mkataba na shirika fulani, nafanya kazi yao, nafaidika nao wanafaidika. Nikimaliza mkataba nao, nikienda shirika lingine, nibadili jina nililosajili? Use your common sense people! This is a similar case

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 13, 2008

    Hivi nyie mnaowalaumu ze comedy ni wadau wa EATV nini? Eti EATV ndo imewabeba na kuwafikisha hapo walipo, mbona hamsemi wao pia wameipandisha chati? Mnashangaza sana! Mimi ninahisi wote mnaotoa maoni ya kutetea EATV na kuwaponda ZE COMEDY ni walewale watu wa EATV, mnataka kuonyesha kwamba sisi wananchi wa kawaida ndo tunatoa maoni hayo. Acheni zenu hizo. Mbona hii inajionyesha wazi kabisa, sababu hapa ni ubahiri wenu, mnataka kujinufaisha peke yenu kwa jasho la wenzenu. Kama kweli mlikuwa mnapata milioni 45 kwa mwezi na kuwalipa laki mbili na nusu tu kwa nini wasiwakimbie? Hata kama ningekuwa mimi nisingekubaliana na UFISADI huo. Kwanza wengine tulikuwa hata hatuangalii kituo chenu cha TV, tumeanza kuangalia baada ya kuanza kurusha kipindi cha ZE COMEDY. Hivi hamjui kuwa sasa kuna ushindani kibiashara? Ninyi mlilewa faida mliyokuwa mnajilimbikizia kwa kuwanyonya ze comedy mkajisahau kuwa hata wadau wengine wanawalilia na wangetamani kufanya nao kazi? Poleni sana EATV kwa umbwiga huo. Acheni kuwaonea vijana hao kwa kung'ang'ania kisicho halali yenu, hiyo yote ili tu muwakomoe?! Mshindwe na mlegee katika jina la YESU. Acheni ufisadi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 13, 2008

    Ze comedy production ni mali ya EATV, kama ilivyo Late Edition ya Wolf ni mali ya CNN au 360 ya anderson cooper ni mali ya CNN. Anderson akiondoka haondoki na 360.please mjifunze sheria
    Masanja kuwa na shukurani...almost na sisitiza ALMOST nobody knew u guys. EATV ili amini vipaji vyenu ikawapa platform mmejulikana kote.Muwe na shukurani,Kuna wasanii wengi wamekufa na vipaji vyao
    IWAPO NI KWELI MMENYIMWA HAKI YANU YA MALIPO NENDENI MAHAKAMANI(Najua ni uongo, walipewa hela zao zote, ndio maana wakaweza kuishi samaki mbezi beach na kunywa pombe kila siku kwa semboja)
    Nawaamuru muondoke kwa usalama, mitake malumbano.MTAPOTEZA umaarufu.na sasa mnaanza kuwakumbatia maadui wa EATV.poleni mnatumiwa

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 13, 2008

    Kuna watu wengine humu globuni nahisi wanakaaga mitaa ya nywagwa kwa pale nyuma,

    Kama ni mambo ya kupandihsna chati hata EATV nao wamepanda chati kupitia Ze Comedy,

    Arusha huwezi kushika EATV bila ungo,

    Kuna rafiki zangu kadhaa walinunua ungo kwa ajili tu ya Ze comedy,

    Fine, ni biashara ya ungo ndio imefaidika na sio EATV lakin kabla ya Ze Comedy wala hata walikua hawajishughlishi na EATV, at least sasa wanaijua.

    Pili pengine hatujaelewa, tusiwalaumu sana EATV pia,

    labda "Ze Comedy" ni ile show na sio kikundi, kwamba kikundi kilikua kinafanya kazi aitha bila jina(???!!) au kwa jina lengine ambalo halikuvuma (labda!!!??)

    Ni kama ilivyo "Planet Bongo" Salama adai ni ya kwake.

    Sasa hao COSOTA, EATV na Ze Comedy wake chini waangalie cha kufanya,

    Ikiwezekana basi waige ushauri wa jamaa hapo juu kua majina yako mengi yenye kufanana,

    Hata Ze Comedi poa tu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 13, 2008

    Hakuna anaye wang'ang'ania ZeComedy wewe mshamba!Tunachosema ili kuepusha mgongano wa kimaslahi huko watako kwenda kufanya maonyesho yao kupitia TV CHANNELS nyingine wawe huru kutumia Jina lingine la Utambulisho kibiashara lakini siyo tena la ZeComedy ambalo tayari EATV wanalitumia na hivi karibuni waigizaji wapya wataanza kuonekana katika kipindi hicho hicho!Simple.Simpooooooooooo!Na kwa taarifa yako mimi siyo mfanyakazi wa ITV wala Radio One wala EATV wala CAPITAL TV!Na sijawahi kutuma application huko ya kuomba kazi.Bali ni utetezi wa masuala ya kimsingi tu.Niwape jina jingine hao jamaa,wajiite ZeZobaaz! mnaonaje mashabiki?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 13, 2008

    EATV acheni mambo yenu ya aibu..inashangaza sana kuona kampuni kubwa kama nyie mnawabania vijana kama hawa wanaotafuta riziki..Au ni chuki binafsi za watu wachache?? Kama walikuwa wanawafanyia biashara kwanini msiwalipe vizuri nao wakajikomboa kimaisha??? Na comment nyingi za kuwaponda hawa vijana mnazituma nyie nyie wafanyakazi wa EATV...acheni tamaa na chuki binafsi jamani!! Waacheni vijana waendelee kujifutia risiki!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 13, 2008

    Kama Mdau wa Canada alivyo washauri Change the name sligthly. Wao IPP walikuwa na Kesi na IPS, na wakashinda IPP= Industrial Product Promotion wakati IPS = Industrial Produst and Services kama sija kosea.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 13, 2008

    Wadau, mimi nawapenda Ze Comedy, kama wanavyojulikana sasa, lakini nitawakumbusha tu kuwa kabla wao hawajaitwa rasmi Ze Comedy, kipindi hicho kilikuwa kunawashirikisha wasanii mbalimbali, kama kina Zembwela, wengi tu na kilikuwa kinaitwa Ze Comedy. Hivyo hiyo hata wakienda wapi ni mali ya EATV na sio wao. Mara baada ya wasanii wengine kuacha kuigiza, walibaki wao na bla kuangalia vizuri unaweza kudhani wao ni Ze Comedy, lakini si kweli. Ze Comedy ni jina la kipindi cha EATV an sio kikundi cha maigizo. Tafuteni jina jingine hapo mmenoa, pleaseeeeeeee!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 13, 2008

    Watu wengine bwana vitu vingine havihitaji hata darasa la awali! hii issue ni two way trafic kwa sababu eatv imewapromote na ze comedy pia imeipromote hiyo tv.Nani alikua na muda wa kuangalia hiyo eatv yao? na kama kuna mahali wanaweza kupata takwimu ya watu wanaoangalia eatv vipindi vingine walete mtandaoni, lakini mimi nina uhakika namba kubwa itakua ilikua alhamisi tu kaajili ya ze group! acheni ze comedy wetu watoke acheni wivu na viroho vya kwa nini kwa watoto wa wenzenu! eatv haooooooooooooooo, anzeni mbele huko acheni vijana washughulikie visa zao!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 13, 2008

    Jamani acheni kuwaonea the comedy yaani nyie EATV amuoni hata aibu mnyonge mnyongeni lakini haki yake mumpe, kumbe mlitaka waendelee kuwatengenezea hela tu wakati wao hakuna wanachonufaika nacho? huu ni wakati wa ushindani wana haki yakuamia wanapoona maslai yapo kwani nao wapo katika harakati zakutafuta maisha kama nyie mnavyofanya,niko pamoja na comedy katika kutetea hili jamani ufisadi mpaka lini hata kwa watu wanaotumia nguvu zao ili wapate kitu kidogo mnataka pia kuwakamua,kuweni na mioyo ya kibinadamu hata kidogo.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 13, 2008

    Jamani huu ni mkakati wa EATV, wote tuliotoa comments hapo juu kuwapinga Ze Comedy ni sisi wafanyakazi wa EATV. Mkakati wetu ni kukisambarisha hicho kikundi. Na nyie mnao watetea Ze Comedy,mjue mtashindwa tuu,ni sawasawa mnampiga konzi kinyago.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 13, 2008

    Kudadeki!,Michu mbona unatubania maoni yetu?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 13, 2008

    Kuna mtu ameniambia,chanzo cha matatizo ya Ze Comedy na EATV kuwa ni mtangazi mmoja anaitwa Salama. Je ni kweli?

    ReplyDelete
  33. ZE KOMEDY RUDINI NYUMBANI HARAKA HIYO BIASHARA SIO MAIGIZO NI MADAWA YA KULEVYA UMEWAONA WENZENU WAMEKAMATWA . FANYENI HARAKA. MSHIKO WA MADAWA USIWAZUZUE. MUNGU ATAWABARIKI MTAKUWA MATRILIONEA KIHALALI

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 13, 2008

    Mdao aliyesema kwamba Ze Comedy ilikuwepo tangu enzi za akina Zembwela ni muongo na mnafiki. Kina Zembwela walikuwa wanaigiza kwa jina la MIZENGWE na siyo ze comedy. Hapa inaonyesha kwamba mnataka kuwauwa kisanii hawa madogo lakini hamtoweza kwa sababu hawa wote walijulikana katika maigizo kabla ya Ze comedy na tayari wana wapenzi wao. Acheni roho za kimasikini kwani kama ipo ipo tu.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 14, 2008

    mtafute
    1. jina lingine je ZOZO BOZO COMEDY? itawafaa
    2. mwanasheria
    3.mkurugenzi mwenye uwezo wa kuelewa dynamics za corporate na global business.Awe KICHWA
    sasa mnajishusha chati kwa kuonekana hamna ueklewa wa kutosha wa biashara
    ZE COMEDY ni mali ya EATV.msipoteze muda wa wadau wa vitu ambavyo ni obvious na trival. Hii blog iwe ni mahala pakupata ufumbuzi wa matatizo mazito(strategic) ya jamii hasa yanayohusiana na siasa,biashara, elimu, afya na ,masuala ya jamii

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 14, 2008

    SI KWERI KUWA EATV WAMEWAPA JINA ZE COMEDI HAPO NGOMA DROO NA HAO EATV PIA WAMETIZAMWA NA WATU WENGI SABABU YA ZE COMEDI,ILO LIWE FUNZO KUBWA KWA WASANII WENGINE SASA WAMADILIKE WAJITAHIDI KUWA NA WANASHERIA WATAKAO WASAIDIA KTK MAAMUZI MAZITO KAMA HAYO,NA PIA WATAWASAIDIA HAKA KTK MAMBO YA MALIPO STAHIKI YA KAZI ZAO,NACHO WASHAULI ZE COMEDI WAACHE MALUMBANO MUDA AUWASUBILI UNA YOYOMA,WANAONEKANA NI WASANII WENYE VIPAJI WATAFUTE JINA NA STAHILI INGINE YA KUTOKA NAYO,MAAMA HATA STAHILI YAO YA KWANZA AWAKUTEGEMEA NAZANI KAMA ITAWATOA,HIVYO TOKENI KIVINGINE

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 15, 2008

    SASA MNAONA BEPARI NI BEPARI TU HATA KAMA NI MZALENDO, ANATAKA KUWAUA HAWA WATOTO WA WATU NA NJAA NA NI HUYU HUYU MZEE ANAYETAMBA KUTETEA MASIKINI WAJIKWAMUWE NA UMASIKINI, WAKATI UMEFIKA SASA WATANZANIA WA KUSIMAMA NAKUSEMA UKWELI JUU YA MASWALA YA JAMII, AACHE UTAFIKI WA KIPIGA VITA UMASIKINI KAMA ANAKANDAMIZA HAWA WATOTO WA WATU BILA SABABU YA MAANA. HIVI EATV ILIANZISHA ZE COMEDY NA KUTAFUTA WACHEZAJI AU AU HAWA WACHEZAJI WALIKUWEPO NA KUFANYA MKATABA NA EATV, HAPA NI VITA KATI YA MANJI NA TBC UPANDE MMOJA NA EATV WALA SI KATI YA WATOTO WA WATU NA EATV, EATV INA ROHO MBAYA ANATAKA KUWATUMIA WATOTO WA WATU KWA KUINGIZA PESA ZA MATANGAZO NA WADHAMINI, ACHENI HIZO. KAMA HALI INAKUWA MBAYA BASI EBU TAFUTENI JINA LINHGINE NA NINA AMINI MTAKUWA JUU KAMA KAWAIDA, MBONA WAO WANATUMIA MAJINA KARIBU YOTE YA BIASHARA ZAO YAPO DUNIANI KOTE NA BADO WANADAI NI ZA KWAO. WAACHE HIZO ZA KIBEPARI, HIVI WATANZANIA WATAFUTA UMASIKINI KAMA NI HIVYO. MANJI NA TBC WASAIDIENI WATOTO WA WATU WAONDOWE UMASIKINI, ACHANANI NA HUYO BEPARI UCHWARA. KWANI VITA HAPO NI KATI YA MANJI.TBC NA EATV NA SHIRIKA MAMA ITV. UKWELI NI HUO

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 15, 2008

    NENDENI MAHAKAMANI MKASOME HUO MKATABA, NA PIA EATV HAINA HAKI YA KUANDAA KIPINDI KAMA HICHO KWENYE TV YAO KWA VILE HAO VIJANI NDIO WALIOKUWA WAHUSIKA WAKUU EATV INASEMA KUWA ZE COMEDY NI MALI ILI WAANZISHE KIPINDI KAMA HICHO TENA, NA MTU MMOJA ANSEMA JUU YA CNN HII SI SAWA NA CNN ANDREW COOPER NI MWAJILIWA WA CNN, WOLF PIA NI MWAJILIWA WA CNN HIVYO HANA HAKI YA KUTUMIA JINA LAKI AKIENDA TV INGINE NA PIA CNN HAINA HAKI YA KTUMIA MAJINA YAO ONCE WAKIACHA KAZI CNN. ZE COMEDY HAWAKUWA WAAJILIWA WA EATV WALIKUWA KWENYE MKATABA WA MAONYESHO TU. NA WALA EATV HAIKUANZISHA ZE COMEDY KWANI HAIKUWEPO KABLA YA HAO VIJANA KUANZA KUIGIZA HUMO. MAHAKAMANI NI MAHALA PAZURI PA KUPAMBANUNUA JAMBO HILI.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 16, 2008

    Jamani watanzania tutoe maoni ki-professional kama wasomi si ukongea tu kwa sababu michuzi kakupa nafasi.
    Hapa point si nani alimsaidia nani ( Commedy au EATV). Point ya msingi ni copyright---- Kipindi kinaitwa Ze comedy na si Kundi linaitwa Ze-comedy. Hivi mnakumbuka Kaole walianza ITV na Kipindi cha Maisha? Lakini nini kilitokea baada ya wao kuondoka ITV? Maisha iliendelea kama kawaida. Hivi ni vipindi vya television na ndo maana pale chini huwa wanaandika copyright EATV. Hata leo akina Masanja wanapoondoka EATV bado EATV wana haki ya kuendelea kuonesha vile vipindi vyao vya zamani.
    Tusiwe watu wa kuoneka tunaonewa kumbe hatujui sheria zinasemaje? Ndo maana tumekuwa tunaingia kwenye mikataba ya ajabu, kumbe ni sheria tu ndo zinatusumbua.

    ReplyDelete
  40. hili ni jambo rahisi kwa mtu yeyote kulielewa.ze comedy walikuwa wakifanya kazi lakini mwenye hakimiliki ya ze comedy ni EATV.na ndiyo maana kila mwisho wa kipindi kulikuwa na maelezo kuhusu umiliki halali kisheria wa show hiyo.watu wasiwamislead wasanii hawa.pengine kosa lao ni kuwa vipofu wa kisheria wakati wakiingia mkataba na EATV.
    kwa sasa hakuna msaada, labda kama msaada wanaouhitaji uwe ni wa kuvunja sheria.
    hili ni sawa na sakata la Athuman Idd, kipindi kile alilazimika kutocheza mpira msimu mzima kwa sababu ya umbumbumbu wake kisheria na kupokea ushauri kutoka kwa watu wasiojua sheria.
    si lazima kuwa na mawakili kama uwezo wa kuwamudu haupo.lakini si jambo gumu kwenda kwa wanasheria na kutafuta ushauri wa kisheria kabla ya kufanya mkataba na baada ya kufikiria kuuvunja.
    tutatumia muda mwingi kuwapa vichwa vya bure.ni kweli ze comedy wanafanya kazi nzuri kweli.nami nakiri ni shabiki wao mzuri sana,huahirisha hata ratiba zingine niwawahi hao.lakini napenda kuwashauri wawe makini na mikataba ya kifisadi maana uzoefu unatuonesha wasanii wengi wanaathiriwa na mikataba wanayoisaini pasipo kuielewa lugha yake kisheria.
    ni hayo tu kaka Michu na wadau wengine wote.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 16, 2008

    TBC isiwe kituko na kufanya mahala pa kuwakilisha mambo binafsi ya mtu na mtu tulisha oona vita vimefanyika kwenye vyombo vya kutunga sheria na kutafsiri sheria na ukweli na haki ukadhihiri sasa bado tu watu wanaendelea zaidi mpaka wanaingiliana kwenye sehemu zao za biashara ! .Sawa kama bado kuna upande mmoja unaendeleza libeneke basi kaa chini na ujipange vizuri kinachofanyika sasa ni vita za kitoto ! kabisa tunaona mifano mingi sana nje kwenye TV Production companies actor anatoka kutengeneza movies/drama/series! Na hakimaliza hapo na kwenda kwenye company ingine huwa aendelei na jina lake la kuigiza ila linabaki la asili basi na huwezi sikia Rambo kamaliza urambo wake na kwenda kwingine na kujiita Rombo ! itakuwa ni ujinga .Mfano hata hapo ITV kulikuwa na Drama inaitwa jahazi na kikundi kinaitwa Kaole lkn walipotoka na kwenda TVT wakaanza na majina ya kuigiza mapya kabisaa !! na wamendelea mpaka leo na hatukusikia kokoro yoyote sasa leo ni vioja vitupu ! Ze Comedy natumai lilikuwa ni jina la kipindi sina hakika kama ni jina la kikundi na Production ilikuwa ni ya EATV ! na kama wamemeliza mkataba na kwenda kwingine kwa ajili ya masilahi basi huyo anayewasimamia awe ni mtu amkini basi ! tafuta majina mapya ! tafuta jina la kipindi ! sababu jina la Ze Comedy sio Hirizi ya kufanyia kazi ! je isingelikuwa EATV kuanzisha Ze Comedy msingelijulikana ? Mlijaribu kuteka hisia za watanzania na wakawakubali na mkawa ndio mnaangaliwa kwa wingi na watu wa rika lote kwa wingi kupita kipindi chochote ! sasa naona mkajisahau kabisa na sasa sawa mnatafuta maslahi zaidi sawa ! basi msijiaibishe kwa kuleta malumbano yasio na msingi zaidi ya kijiporomosha kiusanii ! msidanganywe kuwa wadanganyika hawataoona kuwa mnafanya upuuzi kwa kugombania jina ! anaye washauri hivyo nadhani ni kwa maslahi yake binafsi na anawafanya nyinyi ndio wajinga ! mwaweza poteza umaarufu ndugu zetu ! kaeni chini na mtoke na kitu cha maana .TBC tulitegemea kuna watu ambao ni watauluma kwa kazi zao za TV Production pamoja na Adminstration sasa mwaleta kitu cha ajabu na kuishushia heshima. TBC ! hau ni chombo cha maslahi binafsi kimekuwa sasa ? tunawaomba sisi wadanganyika wenye hiyo TV msituaibishe kwa upuuzi huu ! na tunajaribu kuliona kuwa ni la kiutawala zaidi sababu hapa kwetu tumezoea kuona wana taaluma huwa hawasikilizwi na wakubwa zao wa kazi na hupelekea mara zote kuleta matatizo mbeleni ! acheni hii tabia mbadilike ki ukweli kweli kama tulivyotegemea na si kufanya mambo ambayo si mazuri.Tunawapenda sana nyote TBC ni ya kwetu na waigizaji hao ni wadogo zetu na kaka zetu.Mungu ibariki Afrika ! Mungu ibariki Tanzania.(usiibane michuzi wakilisha !)
    Mzushi !

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 17, 2008

    Hivyo ZE COMEDY ni jina la KIPINDI si jina la KIKUNDI kama hivyo sawa EATV wana haki ya kukataza lisitumiwe na mtu mwingine, lakini kama ni jina la KIKUNDI EATV haina haki ya kukataza kutumika jina hilo na hao watoto ni hao watoto tu ndio watakuwa wenye haki ya kukataza mtu mwingine kutumia jina lao, pia majina ya waigizaji kama walikuja nayo EATV ni yao hamna haja ya EATV kuwakataza kuyatumia hayo unless EATV ndio iliyowapa hayo maji kwa ajili ya kipindi chao cha ZE COMEDY, lakini ni kama majini yao walikuja nayo EATV ni yao EATV haina haki ya kuwanyang'anya. Hata hivyo kama EATV hiyo ZE COMEDY ni yao tafuteni jina lingine tu na yako mengi tu na mtapa wapenzi kama kawaida cha msingi ni kufanya kazi kwa nguvu na ubunifu nyinyi mnatafuta maisha kama EATV inavyotafuta maisha, hamuwezi kuinngiza Tshs 45,000,000.00 na kupewa Tshs 250,000.00 huo ni wizi wa kimachomacho. kuna majina haya chini hapa mnaweza kuyafikiria MICHUZI wapelekee.

    1. TZE MOB
    2. TZE INCREDIBLE
    3. TZE INKREDIBO
    4. KOMEDE
    5. TZE FANTANCY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...