MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D jana amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.
T.I.D mwenye umri wa miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya wilaya ya Kinondoni baada ya Hakimu huyo kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashtaka.
Baada ya kusikiliza ushahidi huo, ndipo Hakimu Kalombola alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi hao wanne ulithibitisha mtuhumiwa kufanya kosa hilo na hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo.
Mara baada ya kusema hivyo Hakimu alitoa nafasi kwa Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi, Benedict Nyagabona ambaye alimwomba Hakimu kutoa adhabu kali kutokana na tabia iliyokithiri ya watu kujichukulia sheria mkononi kama alivyofanya mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Baada ya maelezo hayo ya Mwendesha Mashtaka ndipo Hakimu alitoa nafasi kwa mshtakiwa TID kutoa utetezi wake, ambaye aliiomba mahakama imhurumie kwani alitenda kosa hilo sababu ya ulevi na kuwa familia yake inamtegemea hasa mama yake.
Hata hivyo Hakimu Kalombola alitoa hukumu hiyo kwa kumwambia mshtakiwa "kwa vile huwezi kujimudu ukilewa na huwezi kujizuia kunywa sasa na kuhukumu uende jela mwaka mmoja ujifunze ili usiwe unakunywa hizo pombe"
Baada ya hukumu hiyo ambayo ilipokelewa kwa mshtuko mkubwa na msanii huyo aliyeng'ara sana katika fani hiyo ya muziki wa Bongofleva akiwa na bendi yake ya Top Band, ndugu na jamaa zake waliangua kilio mahakamani hapo wakati TID akipelekwa kwenye karandinga tayari kwenda kutumikia kifungo hicho katika gereza la Segerea.
Wakati akipelekewa kwenye karandinga hilo, TID aliishiwa nguvu na kuanguka mahakamani hapo na kubebwa na wenzake ambao baadhi yao walikuwa wamekwisha hukumiwa na wengine bado wakiwa watuhumiwa na kumwingiza kwenye gari hilo.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Inspekta Nyagabona, T.I.D alimjeruhi Ben Mashiba kichwani na mkononi kwa kutumia chombo cha kuwekea majivu ya sigara 'Ash Tray' na alisomewa mashtaka hayo mara ya kwanza Julai 10 mbele ya Hakimu Kalombola. .
Mwendesha Mashtaka huyo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka jana saa sita na nusu usiku katika hoteli ya Slipway iliyopo maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam .
Kuna habari nyinge michuz sio breaking news na hazitakiwi kuandikwa kwa Wino mwekundu.. kwa imani ya kitanzania ukimuandikia mtu barua na wino mwekundu tunajua ni hatari tena hatari ya kifo..
ReplyDeletekwa leo michuzi umetushtua wengine huku tukijua labda mwenzetu kesha tutoka..
Tafadhali we ni mwandisha angalia habari inayofaa breaking new na isyo faa . na sio kila habari huandikwa na Wino mwekundu..
Kwa kweli watu bado robo tuzimiew kusoma jina hapo juu imebidi nipige kele kaja mtu kusoam hapa ndo akafikia neno lako la kutuhumiwa...lait kama tusingefikia kuhukumiwa yangekuwa mengine..
Breaking news ni breaking news tu.. hata zikiandikwa kwa kalamu ya risasi.... sasa kama we Zaituni una pressure... basi huku siyo mahali pake.. maana mie wala hata sikustuka!!!!
ReplyDeleteHabari ndo hiyo!!!
Ze mdau
Huyu Hakimu atakuwa aliomba rushwa jamaa wakampuuza sasa kaamua kuwaonyesha kuwa yeye nani.
ReplyDeleteHapa kinachoendelea ni kukomoana, nani zaidi kati ya aliyepigwa na Ash tray na TID na nina fikiri aliyepigwa atakuwa aliapa kuwa lazima amfunge( RUSHWA INA NGUVU SANA)
Hili kosa lilistahili jamaa ahukumiwe kufagia vyoo vya CITY kwa miezi sita huku akipigwa picha za CAMERA ili liwe fundisho(community serving). Sasa kumpeleka jela mwaka mmoja si chochote, bora angepiga mvua tano kabisa. Ila hili fundisho lisiishie kwa TID tu maofisi mengi na hasa ya watu binafsi watu wanapigwa mpaka makofi.
So sad. Kama ni kosa la kwanza sioni kwanini wampe adhabu yote hiyo.
ReplyDeleteMngekua mnafuata sehria hivyo hao wauza unga si wangeisha mitaani.
Hii ni kuharibiana vipaji tu. Kwanini huyo alibamizwa asisue tu akalipwa mahela yake ya nguvu na huyu apewe probation tu?
yeah sikatai kuwa kafanya kosa lkini kuna makosa mengine watu wanapewa au wanaachiwa tu nje makubwa kuliko hayo.
Naupenda sana ule wimbo wake wa NYOTA YAKO .....
Dah nasikitika mshkaji wangu TID kufungwa, inanishangaa hakuna fine wakati ni kosa la kwanza, sijui sheria labda wanasheria tusaidieni jamani kama hukumu ilikuwa sawa maana inawezekana ikawa ni kumkomoa sababu ya kuwa na showing offs nyingi, kama ni kumkomoa basi hukumi hiyo ime muonea.
ReplyDeleteIla tatizo TID kainga kwenye anga mbaya, usicheze na famila ya mwana usalama, utalala jela , kwanini washkaji haakumshauri akapige magoto kwa mama wa jamaa aliye umiziwa mtoto wake? yani hakujua hawezi shidana nao au alileta kujua sana?.
Damn homie ! Thats messed up.
ReplyDeleteSegera is a messed up joint dude. Wanavyosema, malipo ni hapa hapa duniani.
Pole sana.
naungana na zaituni jaman michu umetushtua sana mimi nilikaa kimya kidogo ndipo nikavuta punzi nikaanza kusoma kwani nilijua kabisa TID amefariki kumbe amehukumiwa
ReplyDeletejamani bro siku nyingine usifanye hivyooooo
Anonymous hapo juu umesema ukweli kabisa. Mimi nilikuwa ofisini wakati nasoma hii habari. Niliposoma tu hapo BREKING NYUUUUZZZZ na kuona picha ya T.I.D nguvu zikaniishia nikapiga yowe la ajabu na kusababisha boss wangu kushikwa na ugonjwa wa moyo na kuzimia hapohapo.Sasa hapa nilipo kibarua changu kipo matatani. Michuzi, umetuzoesha kuwa breking nyuuz zote huwa ni habari za msiba, so naomba hizi habari zingine uzitafutia kichwa kingine cha habari. Pliiiiiizzzz.
ReplyDeleteMmmmh this's sad.....kwa nini hakimu hata hakutoa option ya kulipa fine? Kuhusu kutumia neno breaking news na rangi nyekundu naona michuzi umefanya kitu sahihi kabisa kwani hii sio habari nzuri na ni ya kusikitisha pia ikimuhusisha msanii mwenye umaarufu kwa kiasi fulani kwa jamii ya watanzania..
ReplyDeleteNaungana na huyu jaji kumfunga jamaa kifungo cha mwaka mmoja.Na nafikiri pia angepewa adhabu ya kuchapwa viboko.Hivi mtu na akilizake timamu anawezaje kusema kuwa nilifanya kitendo hiki nikiwa nimelewa.Halafu eti ahurumiwe kwa kuwa ana watu wanamtegemea.Huo ni utetezi gani?
ReplyDeleteHuyu jamaa alijiona maarufu kwahiyo akaamua kufanya kitendo hiki akidhani kuwa atakuwa juu ya sheria.
Halafu inakuwaje mtoto wa Kiislamu kwenda kujiingiza katika mambo ambayo Allah kaharamisha kama vile pombe.Kifungo hiki ni jaza kutoka kwa Allah.
Akitoka jela ama aache pombe au atapata bakora nyengine zaidi ya hii.
Mithupu ehhh, hizi comments nyingine uwe unabania bwana zinachafua hewa ahhhlaaah.
ReplyDeleteSasa huyu dada analalamika hiyo sio breaking news kivipi? au yeye anajua breaking news ni tangazo la kifo?
Endelea kutupeperushia kama kawa.
Acha nigeuze kibao kwa huyu TID, kwanini hakumalizana na hawa jamaa nje ya mahakama wakafuta kesi? alikuwa na uhakika wa kushinda au ni kutojali? Maana mapato yake ya mwaka mzima na adha atakayopata ya kuwa dada jela bora angemalizana nao tu, kwa maoni yangu.
Mdau wa NY.
Ukweli ni kwamba TID anawakilisha jamii ya wasanii wa kizazi kipya toka tanzania ambao wana jeuri na discipline ya hovyo sana mbele ya jamii lakini bila kuwa na uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina. Inawezekana kuwa adhabu ile ikawa kubwa sana lakini hayo mambo yalitakiwa kuisha bila hata kufika mahakamani kama sio kiburi chake penginewe. Alitakiwa akutane na huyo jamaa na kuweka sawa hiyo issue na kuomba msamaha mapema sana kabla hizo habari hazijawa kubwa kabisa. Maringo na kiburi haivitawafikisha popote wasanii wa bongo kwa kweli. Na sielewi kwanini msanii mwenye jina kama yule anashindwa kuwa na Lawyer wa maana wa kumtetea kwa kweli. Hapa ndipo tunapojua kuwa maringo yenu mtaani kumbe hamna akili hata kidogo. Nadhani watu wamsaidie kupata Lawyer wa maana ambaye atamsaidia TID kutoka huko Lupango maana nako hakufai kabisa haswa wakati wa hizi zama za Ukimwi na wabakaji. Sisemi kwa ubaya ila naomba iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaoendekeza maringi na kujifanya wako juu ya sheria siku zote na naomba jamii impunguzie adhabu TID maana sidhani kama ana lolote la kutegemea zaidi ya mziki kwa kweli. Ruge na Kusaga msaidieni bwana mdogo huyo wazee wa mjini.
ReplyDeletena huyo mtu aliyesEma kuwa msilamu apigwe viboko..blablabla zako hizo ww utakuwa shedadi wa aliyepigwa au ulikuwa na bifu na TID.ACHA BLABLABLA
ReplyDeletekwa kweli hapo tz ndiyo tunapochekesha kweli kesi ndogo hiyo toka mwaka jana sasa ukiua inakuwaje
ReplyDeleteKuhusu kusema jamaa hawe fundisho kwa watu wengine wanaochukua sheria mkononi mbona hamkumfanyia hivyo marehemu ditopile mzuzuri?
ReplyDeleteMbona mafisadi hawaukumiwi hata mmoja hili wawe fundisho kwa mafisadi wengine ? Nchi hii inauonevu kwa raia wakaida ambao wanakula kwa jasho lao.nina huakika kuna kiwango cha fedha kingetosha kabisa kulipia maumivu alioingia huyoo jamaa aliyepigwa kuliko kuamua kwenda kumrudisha nyuma kijana ambaye anategemewa na ndugu zake kwenye nchi yenye maisha magumu kama tanzania.na hawa malawyer mnao waropoka ropoka kila siku wako wapi?
Na kuhusu michuzi kutumia wino mwekundu ,breaking news ni breaking news tu wewe msomaji ndio unatakiwa uchukue mda wako kosoma habari hio kabla ujajipa mapresha.
Mdau mzawa
inatia huzuni jamaa kupewa kifungo cha mwaka mmoja.nadhani miezi 3 ingetosha sana tu haswa ukichukulia huyo aliyepigwa nadhani hakujeruhiwa vibaya.lkn kwa upande mwingine,hii tabia ya kuchukua sheria mkononi imetapakaa sana kwa mastaa wa bongo.sasa bado huyo DUDUBAYA.sijui kama kashaacha tabia ya kukong'oli wenzie.
ReplyDeleteSO SORRY TID, MY PRAYERS ARE WITH YOU... YOU WILL SURVIVE,BE STRONG....
ReplyDeleteHuku majuu ma-celebrity hawafungwi..wanapigwa tu faini kubwa..he he he..!! Si unaona Wesley Snipes ilikuwa afungwe kwa kutokulipa kodi ya miaka sita...mbona hawajamfunga? Lol..nimesahau za Tyson na akina Martha Stuart...Mhh...kumbe kifungo ni kifungo tu....Si wamchape tu viboko kadhaa halafu wamuachie akatumbuize wananchi...Usijali TID utawatumbuiza huko lupango...labda utaongoa roho za watu huko...
ReplyDelete!! Kila la kheri..tunakusubiri kwa hamu.
oya kwani TID nani bwana ma star wabongo wanafikiri wao wapo juu ya sheria weka dani hakim mbona papy kocha yupo ndani nafikir papy na TID wataanzisha band jela kama wajela jela. wasalimie wote huko tid
ReplyDeleteHapo sasa ndio nimeona kwamba nchi yetu mtu ukiwa chini basi huwezi kufanikiwa kabisa sasa hapo kosa lipi la maana la kuweza kumfunga mtu??Au ni kumkomoa tu sijamaanisha kwamba namsapoti TID hapana bali inabidi saa zingine hawa ma lawyer warudi darasani maana hiyo sio kesi ya kumfunga mtu mwaka 1.Mbona wa madawa ya kulevya hawajawafatilia na wanawashika alafu wanawaachia nchi yetu imejaa rushwa sana tena sana mafisadi wakubwa mimi nimemaind maana vitu vidogo wana vitolea macho alafu kesi zingine hawashoboki kabisa ila kesi kama hizi ndio macho mbele mbele alaa mtaishia hivyo hivyo maana sasa hivi mnafanya vitu kwa kukomoana....Michuzi nawakilisha ukinibania ni sawa sio mbaya maana nimemaind sana kosa gani la kumfunga mtu mwaka mmoja??waambieni warudi darasani wakasome upya
ReplyDeletewasanii washamba washamba wa hapo dar gerezani ni mahali pake, amepata milion kumi kwenye ankount kichwa mlima....kuna wasanii kichwa maji hapa usa wako gerezani vilevile au wanakesi ...huwezi ukachukua pistol ukaanza kushoot ovyo(t.i.d gangstar hana hata bunduki) eti kwa sababu unatokea kwenye magazeti ya gozi sport la majid.sheria ni sheria. unahatia unatiwa gerezani. bongo mnaukosefu wa ma-star. basi aende huko akashike mike za wanaume huko sengerea. kazi nzuri hakimu.
ReplyDeleteMwache afungwe, maana hana lolote.
ReplyDeleteAkikaa wiki mbili ndani ndo ataelewa kukaa na wakubwa na kuheshimu sheria.
Wamefungwa akina Fundikira, Ismail Aden Rage ambao walileta ya maana TZ iwe huyu chalii.
Hata kama nje ya nchi kuna sheria za kufuata watu kweli wanazifuata, sio hapa bongo. Watu ugomvi wanautaka wenyewe unakuta mtu unatukwana MS***e bar halafu unapigana hovyo. Acha mabouncer wako wapigane kwa ajili yako wewe uende kuwatoa kwa dhamana.
Baada ya wiki mbili akitoka ndani kwa msaada wa Lawyer ndo atajirekebisha.
Pia elewa visa ya Australia na Canada unaweza kosa kama uliwahi fungwa kwa makosa kama haya ya kutumia nguvu na chupa katika baa.
TID AMEKWENDA JELA KWA KUVUNJA SHERIA, HIYO NI FACT..FACT NYINGINE SHERIA NI MSUMENO.
ReplyDeleteMY TAKE:
DHARAU IMEMPONZA, ANGETAKAKIWA KUTUMIA KILA SENTI ALIYONAYO KUMLIPA LAWYER WA MAANA ILI AMSIMAMIE KWENYE HII KESI...AU AMALIZANE NA HUYO ALIYEMJERUHI NJE YA MAHAKAMA...SASA MARINGO NA DHARAU ZAKE ATAZIFAIDI VYEMA HUKO SEGEREA.
ONYO KALI KWA MABISHOLOLO WENGINE WANAOJIONA WAKO JUU YA SHERIA BAADA YA KUTOA SINGLE MOJA.
Hili kweli ni fundisho kwa wasanii wa bongo. Naungana na mdau aliyesema wasanii wanafikiri wako above the law, alafu kibaya zaidi amekubali kosa na kudai ni pombe.
ReplyDeleteMara ngapi tumesikia wasanii nje wakihukumiwa kwa mambo kama haya...
ReplyDeleteHuyu TID kajidai yeye mbabe kamtwanga mwenzie na Ash Tray na kuendeleza ubabe labda kwa kutoomba radhi au msamaha kwa mshikaji aliyempiga.
Chukulia mfano wa Dudubay na Mr Nice...msela aliomba radhi yakaisha, TID anajidai yeye ZEZE analeta mijidharau.
Kwanza naona mwaka mmoja haumtoshi, hakimu muongeze miwili.
Toto la Kiislam, uanaharam tuu, tena unasema mipombe (nililewa)....pumbavu zako.
na kujivalisha mihereni,na miurembo...Segerea wazee lazima waburudike.
Hii iwe fundisho kwa wengine.
Top Band,onesheni mambo bila TID msife moyo.
sikio la kufa halisikii dawa.huyu bitozi mwaka juzi tu alikuwa na kesi ya kubaka na akaponea chupu chupu kwenda jela lakini nadhani hakuweza kujirekebisha.kumpiga mtu ni 'assault',sio kesi ndogo kwani angeweza kuua.nchi za watu angechukua hata miaka mitano kwa kesi kama hiyo ya kuhatarisha maisha.
ReplyDeletedu, wabongo hamna huruma, uyu ni superstar jamani. muoneeni huruma. huenda alizinguliwa kweli. kwani akiringa si anaringia kipaji chake. ata wewe ungekua na kipaji si ungejiona na kudharau na kuringia wengine. tena alikua na pesa. wabongo cheni kuponda mastaa wetu. ata wamarekani wanaringa.
ReplyDeleteAnastahili na viboko juu!!!!
ReplyDeletetatizo la wasanii wabongo wakipata pesa wanajiona kuwa wapo juu ya sheria na hakuna zaidi yao sasa we unaenda maeneo ya kishua afu unaleta fujo za kinondoni,he was mistaken kule ni masaki bwana,kuna watu na hali zao wanaendakujipumzisha,na hii ni mara ya pili anakua CONVICTED si mnakumbuka ile rape scandal yake,na nivizuri amejijua kua kuna watu wanamtegemea katika familia yake mana madoido aliyokua anafanya kitaa utadhan wazazi wapo mtoni,hili liwe fundisho kwa wasanii wengine hivyo viela mnavyopata msione ka hamna watu wenye nazo zaidi yenu kuna watu wanaVIJISENTI na hawana fujo.mwache aende kumpa kampani PAPII na Q chilla usipopunguza misifa utafata.mana ela za ukubwani zinawazingua vijana
bado kalapina, chidi benz na dudu baya
ReplyDeleteNENDA KAKA, NENDA SUPERSTAR WA BONGO, NENDA KACHEZEE MIC ORIGINAL. ULICHOKIPANDA KWA MUDA MREFU, HATIMAYE UMEKIVUNA. TULITEE PICHA ZA UNAVYOCHEZEA MIC SEGEREA KAMA ZILE ULIZO ZISAMBAZA ZA MLIBWENDE WA BONGO KATIKA MAGAZETI YA UDAKU. UKIRUDI UTAKUWA NA FANI MBILI
ReplyDeleteTo be honest naona judge amemuonea TID. Kuna watu kama Kinje Ngombale Mwiru ambaye ameshaua mtu kwa kumgonga na gari na pia huyo huyo Kinje ameshawahi piga bastola juu katika baa yake, lakini yuko huru na bado anatamba akisema nitaua mtu na kudai kuwa hatofungwa. Sasa kuna vitu serious ambavyo majudge hawavioni na wanaviachia. TID angepewa community service kupaka rangi shule, kufagia barabara au kusafisha vyoo na fine juu yake.
ReplyDeleteMsouth
Mbona hiyo adhabu ni kubwa sana, jamani iwe fundisho kwetu ukiwa celebrtity kuwa na personal lawyer. Kuna uwezekano huyu jamaa hakuwa na mtu wa kumteteta na pia hakutaka haya mambo yaishie nje (i.e. reaching out) ya mahakama kwa njia ya compensatio
ReplyDeleteMbona hiyo adhabu ni kubwa sana, jamani iwe fundisho kwetu ukiwa celebrtity kuwa na personal lawyer. Kuna uwezekano huyu jamaa hakuwa na mtu wa kumteteta na pia hakutaka haya mambo yaishie nje (i.e. reaching out) ya mahakama kwa njia ya compensatio
ReplyDeleteWengi mmeongea lakini jamani "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni". Nakubali TID amekosea lakini adhabu aliyopewa haiendani na kosa lake. Wengi mnamchukia kwa vitabia vyake vya dharau na kujidai mimi nikiwa mmojawapo,huyu jamaa simmaindi kabisa ila kwa hapa ameonewa sio haki kabisa kisa ben baba yake yuko serikalini ndio iwe tabu????? HONGO itaisha lini bongo??????!!!!! inasikitisha sana. Bwana mashiba sio ubinadamu huo acheni kutumia ubabe. Bro michuzi naomba upost comment yangu tafadhali.
ReplyDeleteDear all,
ReplyDeleteMi nadhani ndiyo sheria ni msumeno.lakin "NO ANY OFFER IS ACCEPTED WITH A DRUNK PERSON".Kama alikuwa mlevi,wangempa adhabu ya kawaida.jaman pombe si chai.hii ni kuua vipaji.wanasheria wanaotetea haki za wanaoonewa jitokezeni.Mbona DITO aliua akato? Na aliyemshtaki naye si mzalendo,mwaka mzima una hasira na mtu?
Ulaya izi ni ishu za kawaida zakumalizia nje.
Kafaidika nini mwenzake kutumikia jela? SIO MZUKA KABISA
POLE SANA TID NA FAMILIA YAKO POLE WASHABIKI WOTE WA TID,POLE KWA TOP BAND,HII NDIO INAITWA DUNIA MAPITO TUNAPITIA MAMBO YA FURAA NA HUZUNI PIA KWA KWERI INATIA SIMANZI,LAKINI HAPO TUELEWE SHERIA NI MSUMENO NA AINA SUPER STAR,NAWAPA USIA WANANGU WOTE WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA KWA SASA MSHIKO MNAO JIWEKEENI UTALATIBU WA KUWA NA WANASHERIA MAANA NAISI TOP IN DAR ANGEKUWA NA MWANASHERIA ANGEPATA MUONGOZO MZURI WA KISHERIA NAZANI ASINGEFIKIA HAPO,PIA MUACHE MAJIGAMBO KAMA HAYO YAKUPIGA WATU ADHARANI,KUHUSU BREAKING NEWS DC.WA TEGETA AUJAKOSEA NA ENDELEA NA UTARATIBU HUO BREAKING NEWS SIYO TANGAZO LA KIFO TID NI SUPER STAR NA ALISTAHILI BN.
ReplyDeleteSuper star bongo? wapo kina salman khan na sanjay dut india, walifungwa lakini hatimae walikaa siku robo tu ndani, wakatolewa na kupigiwa saluti na maafande.
ReplyDeleteHawa ndio supppaar staaaarrrrr sio huyo TID,
Nasubiri remix ya NYOTA YAKO , TID feat BABU SEYA sasa
NAONA VIJANA WANA CHUKI NA T.I.D HAPO JUU.WANAOSEMA KAONEWA SIO KWAMBA WANAMPENDA T.I.D LA HASHA TUMEKUSANYA MATUKIO YALIOPITA KESI KUBWA TU WATU HAWAJAhUKUMIWA LAKINI KWA VILE HUYU MASKINI KAMA SISI WANAJITESEA HILI WAONEKANE WANAFANYA KAZI.NA KWA VILE WATANZANIA WENGI SISI NI WAJINGA KAMA HAPO JUU WANAOSEMA KAVUNJA SHERIA MBONA HAWAJIULIZI KUHUSU MAFISADI? MNASEMA WASANII WANAFIKIRI WAKO JUU YA SHERIA JE VIONGOZI WENU WANAFIKIRIA WAKO JUU YA NINI?
ReplyDeleteSAAA NYINGI NIVIZURI KUWA REASONABLE WATANZANIA WENZANGU SIO MNAPAYUKA TU KAMA WANYAMA.
TUSIPOUNGANA SISI MASIKINI NDIO MAANA WAKINA CHENGE WANACHOTA HELA ZA NCHI NA BADO WANATOA MANENO YA KEJELI,YULE SASA NDIO YUKO JUU YA SHERIA.WALIONDESHA SHITAKA HILO WANASEMA HAWE FUNDISHO KWA WALE WANAOCHUKUA SHERIA MKONONI,MBONA HAWAKUMTUMIA DITOPILE KUWA FUNDISHO KWA WENGINE BAADA YA KUMUUA YULE DEREVA DALADALA?
tukijitenga sisi wenyewe hakuna anayeweza kututtetea na sheria itaendelea kumnyonga maskini tu.
Hata kama akikaa jela siku moja, aftermath yake itakutana naye almost popote atapo omba visa, hasa nchi za Europe au USA.
ReplyDeleteUkishakuwa na Criminal Record hawa wazungu wanakuona hufai kabisa kungia nchi zao
Zaitun, itabidi basi awe anaziita HABARI MSHTUKO labda itakusaidia.Maana mshtuko si lazima iwe ni kifo tu...........!
ReplyDeleteHapo sasa ndio nimeona kwamba nchi yetu mtu ukiwa chini basi huwezi kufanikiwa kabisa sasa hapo kosa lipi la maana la kuweza kumfunga mtu??Au ni kumkomoa tu sijamaanisha kwamba namsapoti TID hapana bali inabidi saa zingine hawa ma HAKIMU warudi darasani maana hiyo sio kesi ya kumfunga mtu mwaka 1.Mbona wa madawa ya kulevya hawajawafatilia na wanawashika alafu wanawaachia nchi yetu imejaa rushwa sana tena sana mafisadi wakubwa mimi nimemaind maana vitu vidogo wana vitolea macho alafu kesi zingine hawashoboki kabisa ila kesi kama hizi ndio macho mbele mbele alaa mtaishia hivyo hivyo maana sasa hivi mnafanya vitu kwa kukomoana....Michuzi nawakilisha ukinibania ni sawa sio mbaya maana nimemaind sana kosa gani la kumfunga mtu mwaka mmoja??waambieni warudi darasani wakasome upya.....
ReplyDeleteNIMEONA KATIKA COMMENT NYINGI SANA WATU WANAMUONEA WIVU KISA ANALINGA HIVI NA HIVI SIO HIVYO KILA MTU ANA HAKI YAKE...LAKINI SASA PIA WATU WENGI HAPA INAONEKANA ELIMU HAKUNA NDIO MAANA WANAONGEA BILA KUFIKIRIA MNAONGEA NINI FIKIRIA KABLA YA KUTENDA...PIA ANGALIA JE HILO NI KOSA LA KUMFUNGA MTU MWAKA MMOJA??ALAFU PATA JIBU SIO MNALOPOKA KAMA HUNA ELIMU USISAPOTI KITU AMBACHO HUJUI...ALAFU MNASEMA TZ TAMBARARE NANI KAKUAMBIA TUWE NA USHIRIKIANO HIVYO VITU VYOTE VITAKWISHA TUSIJIGAWE JAMANI SHAURI YENU MTAISHIA HIVYO HIVYO....
Kila mtu atalipwa kufuatana na matendo yake. TID analipwa kwa jeuli yake mwacheni akachezee MIC za segerea akitoka huko atakuwa amejifunza.
ReplyDeleteALIYE SEMA WESLEY SNIPES HAJAFUNGWA NANI? HUKUMU WESLEY SNIPES KASHAHUKUMIWA SEMA SIKU YA KUINGIA GEREZANI NDIO BADO. KUHUSU T.I.D naona KWELI WAMEMUONEA ILA PIA FUNDISHO TUSIJIONE SANA HUJAFA HUJAUMBIA PIA HUFI DUNIANI BILA MACHUNGU YA DUNIA NDIO HAYO. INSHAALLAH ATAJIFUNZA.
ReplyDeleteNi kweli kaonewa kwani adhabu hiyo ni kubwa kuliko kosa alilofanya. Simfagilii T.I.D na wengineo kama yeye wasiokuwa na adabu au kujawa masifa, au wale wenye kuchukua sheria mkononi. Lakini hakimu anaonekana hakutumia haki kwa kumhukumu adhabu kubwa kuliko kosa lenyewe. Watanzania tunachekesha, hivi mjaua hakuna sheria yoyote ya kumshitaki dereva aliyesababisha ajali hata kama imesababisha mauaji ya makumi ya watu? Isipokuwa dereve huyo huhukumiwa na Jamhuri ya Muungano na kupigwa faini isiyozidi hata milioni 2? ....kana vile wanoukufa ni kumbi kumbi, lakini kijikosa kama hiki ambacho kinaweza kutolewa faini tu, inashangaza kuona kwamba kunachukuliwa jazba na chuki na mahakimu kujifanya wanafuata sheria sasa, na kutoa hukumu zinazozidi kosa. Mbona Ditopile yuko nje? Mbona mafisadi wezi wa mamiliaoni ya walala hoi wanaendelea kutesa? au wauzaji madawa ya kulevya? Watanzania tuamke jamani!
ReplyDeleteLakini kuhusu hawa macelebrity wa bongo kinachowaponza ni kukosa elimu, ndio maana kila siku nasisitiza masupa staa mkishawini hivyo vimilioni rudini shule ili mzidishe maarifa na wala si kuacha shule kama Mr. Blu. Sasa T.I.D kaka bado hakijaharibika kitu, ukishamaliza kuzimia tia akili kichwani, kata rufaa, tafuta lawyer mlipe vizuri kile ulichonacho, ili akusadie ushinde rufaa na usikae sana lupango! shauri yako kama hutaki kusikia yangu, basi kama walivyosema wengine, angalia mwaka mmoja huo wasikufanya dada!
Jirani Mdaku
hapo ndo utagundua umuhimu wa shule vile vile.we utaendaje mahakamani bila wakili wa kukuwakilisha na ukijua kweli ulijeruhi mtu.ndo mjifunze,kama unahela tumia lawyers celebrity mbuzi weee!! ukisikia usidhalau mahakama ndo hivo.
ReplyDeletekuna watu wanachonga hawajui kula jera ipo kwa kila mtu,ipo siku mnaweza mkasikia MISUPU ndani 4 life, dah T.I.D hakustahili adhabu kama hii,hii ni komoa,yaani bongo hii kumpiga mtu chupa jera 1yr,,,May GOD bless tid,,
ReplyDeleteRANGI NYEKUNDU SI KIFO KWA WATALAAMU WA RANGI EBU FANYA RESEARCH NA UTAONA KUWA RANGI NYEKUNDU SI KIFO, I KNOW WHAT IT MEANS READY COLOUR, BUT I CAN NOT SAY ANYTHING HERE I WANT YOU TO DO SOME LITTLE TINY BIT RESEARCH LAKINI UKAE UKIJUWA KUWA SI KIFO.
ReplyDeleteNyie manaosema kaonewa, mfahamu kuwa sheria hakutungwa jana. Cha msingi mkiona sheria ni kali ni kuomba watunga sheria wafanye ammendments na sio kumlaumu hakimu. Lakini hata ivyo TID hajaonewa coz anaonekana kuwa na record ya uhalifu, toka kubaka, bangi mpaka kumtwanga mtu. Anaesema Ben katumia nafasi ya babake serikalini basi atumuie mwanya huo kumshauri TID akate rufaa.
ReplyDeletemi nakubaliana na wana blog mnaposema hamna mtu ambae tupo juu ya sheria lakini wanablog that is too THEORETICAL ila PRACTICALLY kuna watu wapo juu ya sheria,we sababu Kinje anagonga watu na magari au Dito alipiga mtu bastola na wewe mtoto wa mkulima unakunywa pombe za msimu unataka kupiga watu tena mbaya zaidi maeneo ya KISHUA ka yale ambayo watu wa mbingu ya saba wanajipumzisha mana wengine tunaendaga kubahatisha tu tukizidaka.sasa Bro TID ilikua lazima aitambue hali yake sio mpaka ulivyofika mbele ya Hakimu ndo UNACONFESS kuwa mama ako anakutegemea,that was guff!!sorry bro 4 being experimental animal 4 such behaviour ya vijana especially wasanii ambao mna background ya kutoka familia maskini,namaliza ka nilivyochangia pale juu Q chilla nawe jirekebishe mana i know u guyz(and TID)mnasifa za kijinga.Tchao
ReplyDeleteWEWE MSAUZI, TOFAUTI YA KINJE NA TID NI KUWA KINJE AKIFANYA MADUDU YAKE HUKO HUWA HAFANYI DHARAU JUU YA SHERIA, ATAWEKA WAKILI NA KUPOZA ALIOWAKOSEA. LAKINI HUKU BISHOLOLO TID ALIFANYA DHARAU NDIO MAANA YAMEMKUTA HAYO.
ReplyDelete1. ALISHINDWA KUMALIZANA NA ALIYEMJERUHI KABLA KESI HAIJAENDA MAHAKAMANI. ALITAKIWA AKAMPIGIE MAGOTI KUOMBA MSAMAHA.
2. ALISHINDWA KUWEKA WAKILI AMSIMAMIE HII KESI.
3. ALISHINDWA KUMSHAWISHI DEMU WAKE AMBAYE NDIYE SHAHIDI WAKE PEKEE ASIENDE SAFARI ILI AHUDHURIE MAHAKAMANI KUMTETEA. (au pengine demu naye ni sista duu zaidi; dharau kama TID mwenyewe.)
4. ALISHINDWA KUTAFUTA USHAURI WA NAMNA YA KUMJIBU HAKIMU, MATOKEO YAKE ANAKUJA NA SABABU ETI "NILIKUWA NIMELEWA"!!!
YOTE YANAONYESHA NI JINSI GANI ALIVYODHARAU HII KESI.
MWACHE AKAWAPE WANAUME STAREHE HIKO SEGEREA.
ANGALIA MITANZANIA ILIVYOKUA MIJINGA HAINA UPEO WA KUFIKIRI MIJINGA NDIO ILIWAO,BADALA YA KUSHABIKIA MAFISADI WAFUNGWE MAANA WANAHUJUMU NCHI,HAWANA TOFAUTI NA MAJAMBAZI YANAYO VAMIA BANKI NA SEHEMU NYENGINE KUPORA MALI,NAKUWATIA UMASKINI MNASHABIKIA TID KUFUNGWA,HII NCHI IMEOZA KESI KAMA HIZI NI ZA FAINI NA SIO MTU KUFUNGWA MWAKA,TUKIFUNGA MTU KWA KESI KAMA HII MWAKA JE NAMAFISADI TUWAFANYE NINI?BADALA YAKE TUNAWAACHA WANADUNDA MTAANI TU,WHY?KWANINI?MAHAKIMU WAWE WANAWEKEWA WATU WA UTAWALA BORA ILI KUEPUSHA RUSHWA NA UPENDELEO!!WAKIGUNDULIKA WAPEWE ADHABU KALI ZA RUSHWA!!HIVI UNADHANI TID ANGEKUPIGA WWE ANGEPEWA ADHABU KALI HIVI?UNAJIDANGANYA KAGUSA MTOTO WA FISADI!!BUT KUMBUKA HII NI KAMA AJALI MAFISADI WAMETUZUNGUKA KILA KONA KESHO WATAKUA KWAKO MSHABIKI NA UTAKIONA BAADA YA KUNYIMWA HAKI ZAKO
ReplyDeleteMwacheni akachezee MIC za kina Babu Seya labda atajifunza, kwani hakuna aliye juu ya sheria. Kwani wakati anampiga mwenzake alikuwa hajui kuwa na yeye ana watu wanaomtegemea. Angeua ndugu zake wangepata wapi msaada? Nenda Segerea ukajifunze kuishi na watu.
ReplyDeleteJamani mnamlaumu hakimu kwani sheria inasemaje au la wasipofungwa hao mafisadi sie tunaopigwa na kudharauliwa tusishitaki hadi mafisadi malizwe kufungwa. Ndio maana wakasema sheria ni msumeno mafisadi nao wakifikishwa mbele ya hakimu watalimwa kama kawa. Poleni wapenzi wa TID lakini habari ndio hiyo. Kwanza nyota yako ule wimbo aliuiba akashitakiwa, akashitakiwa kubaka na hiyo mibangi akaponea chupuchupu sidhani kwa tabia za TID ndio mara ya kwanza kupiga mtu na ila pengine pia kachukua demu wa mwenzie na midharau juu. Hiyo miezi sita ya mchana na usiku itamtosha. Nyota yake itaenda kung'aa jelaaaaah kwa kina T-bag. Pole TID huwezi panda maharage utegemee kuvuna mahindi. Wamefungwa kina Tyson, Paris Hilton na Lil kim sembuse wewe. Tuliza kichwa utunge verse.
ReplyDeleteBreaking news kutoka Segerea ni kwamba TID agombewa kama mpira wa kona.
ReplyDeleteWanaume Segerea wagombana kwa ajili ya TID, kila mmoja akisema ni wake.
ReplyDeleteANON WA Tarehe July 24, 2008 3:38 AM, Mtoa Maoni: Soames..UNAJUA KWELI KUELEZEA NIMEIPENDA ILE YA MWISHO....WANAPOTOA "SINGLE MOJA"
ReplyDeleteHiyo ndiyo stahili yake, akirudi atakuwa na adabu.
ReplyDeletei hope THIS will sends a message to other artists what can be done with fame and fortune - fanyeni vitu vya maana kwenye jamii na sio kuleta ubishoo isiokuwa na mpango. so to any other artist out there, superstar or whaterver the hell you think you are, hope you know what TIME IT IS. closed mindedness, negative attitudes , arrogance and narcissism ndio kilichomponza TID.
ReplyDelete