Hi Bro. Michuzi.
Sawa nimekupata kwa jibu lako Bro , kuwa hili jambo kuhusu kubadilishana jezi kwa mchezaji wetu wa timu ya Taifa letu na mchezaji wa Cameruni, kuwa wahusika wa swala hili hawata rudia tena, lakini sasa aibu je kwa sisi?
Kwanini hawa watu wasichukuliwe hatua za nidhamu?? Hilo jambo ndo linaishia hapo hapo? Yaani huku ni aibu kweli kweli, tena leo nimelisikia hili swala likizungumzwa kwa mara nyingine, na pia marafiki na jamaa zangu wakiniuliza maswali kibao.
Leo wamezungumzia kuhusu mchezaji wetu kuwa anakipaji kizuri na inasemekana inawezekana Eto'o ndie aliye anza kuomba jezi, baada ya kukabwa kisawasawa, wanasema pia huyu mchezaji jina la utani ni Cannavaro kama beki wao nyota wa hapa.
Sasa inawezekanaje mchezaji mzuri kudhalilishwa? Wanasema tupo dunia nyingine kabisa, mimi ninasema si kweli kabisa Tanzania tukawa dunia nyingine haiwezekani, nchi nyingi sana za Africa zipo nyuma yetu, sasa ni vipi?
Mimi kama mpenzi wa michezo napendekeza hapa sheria ingetendeka kisawasawa, maana ni aibu kwetu na si jambo dogo huku Ulaya litasemwa kwelikweli, sheria ichukue mkondo wake kwa kumdhalilisha mchezaji wa timu ya taifa ili kweli siku nyingine yasirudie mambo kama haya ya aibu.
Tanzania tunaishi dunia nyingine, dunia ya wapi hiyo???
Mdau B.Chibiriti.
Hii inanikumbusha mechi ya kumuaga Mchezaji wa Timu ya Taifa ya TZ Mohamed Chuma.
ReplyDeleteNahodha wa Kenya Jonathan Niva(RIP) aliadhibiwa kwa kubadilishana jezi na Chuma. Wakati huo jezi zilikua adimu sana
Wahusika wawajibishwe. Hii ni kuua morali wa wachezaji wetu. Tunategemea soka itakua kwa myindo huu kweli? Sioni kama Mr. Horoub a.k.a Cannavaro, alifanya kosa. Je kama jezi ingechanika ktk pilka za uwanjani, ingekuwaje? Inawezekana kweli tupo Dunia nyingine, ndio maana viongozi wetu hawayaoni yanayoendelea kwenye Dunia hii. Angalia, mambo mengi yanavyoharibika, wakati zamani yalikuwa yanaendelea vizuri. Ukitaka kuuwa mti, ni kwenye shina.
ReplyDeleteWabongo kweli hovyooo hata wasome mpaka wapi pumba tupu.sasa hio TFF ina wasomi akina Tenga,Magori na sijui Mwakalebela ndo wanafanya mambo hayo AIBU.Nafikiri FAT ya kina El-Maamry,Rage au hata Ndolanga zilikuwa zina nafuu kuliko hawa vilaza.Na pesa sasa ni nyingi toka kwa wafadhili lakini bado mchezaji anadaiwa pesa ya jezi,jezi,jezi!!!AIBU.
ReplyDeleteHebu JK watimue hao vilaza wametuharibia hali ya hewa huku ughaibuni tunaonekana masikini sana kumbe si kihivyo.
Cha chandu-UK
We Cha chandu inaoneka ni msahaulifu kabisa au hufuatilii mambo.
ReplyDeleteChama cha Mpra wa Miguu cha zamani yaani FAT ilimchosha kila mtu hata Ndolanga mwenyewe.
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeondoa michosho yote iliyokuwepo huko nyuma na sasa hivi nafuu tunaiona, nani tena anataka kuturudisha kule nyuma, hata Mzee Ndolanga hatakubali.
Suala la Jezi tayari Rais tenga ameshaliweka sawa. Japokuwa yule Afisa Habari wa TFF alinukuu kanuni za TFF, lakini alitakiwa ajiulize hizo habari anazitoa katika ulimwengu gani, je ni ule ulimwengu wa mwaka 47 au huu wa 'tekelinalokujia'?
Ni muhimu watoa habari wasiwe kama kasuku wanasema kila wachokisia, ni vema wakajiuliza wanayotaka kusema yatakuwa na athari gani kwa jamii na hiyo ndiyo kazi inayomtenganisha na wengine wote pale TFF. Kama hawezi kupambanua hilo basi hajui anachokifanya.
Mimi nakosa hata kauli manake nahisi nikijaribu kuongea naweza tukana bureee...!!
ReplyDeleteHuyo Tenga anaongea kujikosha tuuu baada ya watu wazima kuongea. Yaani wadhamini sijui wamejisikiaje..!!!..?? Manake wanawezaonekana as if hawakutoa mshiko wa kutosha hadi chama kikubwa namna hii kuanza kugombea ka-tshirt cha sh. 10,000/=.
TFF wizi umezidi manake mapato yoooote ya uwanjani bado sh 10,000 inawatoa rohoo...!!!!!!!!! Looooooooohhhhhhhhhhhh...!!
Huu ni ushamba uliokomaaa na ushenzi kama sio ujinga ulikubikwa na upumbavu..!!
Kikwete aseme jambo au awapige warning..!! But nafikiri katika kulinda jina la nchi, ni vema aongee kabisaaa..!!!
Yaaani nimekereka mpaka kum-moyo..!!
Kachumbari na wewe umezidi, mambo kila siku ohh ulaya wanatushangaa , wanatushangaa.
ReplyDeleteHujui kila siku wanatushangaa kama umejua leo?
Mtumie mdogo wako fedha na viatu ananilamikia kila siku.