Shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi wa Dar es salaam International Conference Centre ulioko PPF Tower. Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Dkt. Stergomena L. Tax.
Imetolewa na:-
Afisa Mtendaji Mkuu,
Chama cha Hakimiliki Tanzania,
S.L.P 6388,
Dar es salaam.
Simu: +255-22-2125981
Nukushi: +255-22-2125982
Barua pepe: cosota@intafrica.com
Tovuti: www.cosota-tz.org
Angalau sasa Alhamdulilahi safari imeanza.Wasanii wetu watapata hata hamu ya kuzidisha ubunifu wakitarajia kunufaika na jasho lao.Lakini kilio changu bado kipo palepale kwamba Mgao huo bado mdogo sana hauridhishi na wala haumotishi wasanii.Kuwa Msanii mahiri uliyekubalika na jamii siyo kazi rahisi kama tunavyo ichukulia.Ni kazi ngumu sana.Ndiyo maana kutokana na mapato duni na hali mbovu ya maisha wasanii wengi hutumbukia katika ulevi uliopindukia au hata madawa ya kulevya wakati mwingine kutokana na msongo wa mawazo uliokithiri.Bado lipo tatizo kubwa hapa nchini la 'Piracy of Copyright'wizi wa kazi za wasanii bila ya ridhaa yao na kuzikuta kazi hizo zikiuzwa madukani bila ya wao kunufaika lolote na zikiuzwa katika ubora hafifu na hivyo kuwaharibia soko lao.Nashauri tu zikaribishwe Kampuni Binafsi na isiwe moja yenye Monopoly tatizo litabakia palepale,ili Kazi za Wasanii zikiingia katika soko ziwe na ulinzi wa kutosha 'security marks/stickers reflective'ambazo siyo rahisi kwa mtu tu wa kawaida kugushi.Nafikiri nime eleweka.Tunathamini kazi za Wasanii wetu.Wanahitaji support yetu ili tuweze kuendelea kufaidi vipaji vyao.Lakini tutakapo shiriki katika kuwaibia mapato yao hakika tutaichimbia kaburi Fani ya Sanaa iwe Muziki au Maigizo au Kwaya na kadhalika.Nawapongeza Cosota kwa hilo,si haba.Niwaache na ujumbe mmoja tu usemao,'Be not afraid of growing slowly,be afraid only of standing still'.tonny.
ReplyDeleteMichuzi shauri yako, umetundika majina ya watu, tena kiasi cha pesa kabisa!!!
ReplyDeleteSIYO SAHIHI KUTUN DUKA PESA ZA WATU HADHARANI BILA IDHINI YAO EBU ONDOA KABLA HAWAJAKUSHITAKI NA KUWALIPA FIDIA NONO AU KWA VILE HUKO BONGO WATU BADO NI WAJINGA HAWAJUWI HAKI ZAO INGEKUWA HUKU MAJUU WANGEKUSHITAKI NA KUWAONGEZEA PESA ZA BURE, EBU ONDOA UPESI nakupenda sana, usije ukapiga mnada kibanda chako ili ulipe fidia.
ReplyDeletemichuzi una tabia mbaya, na ina sikitisha kuwa wewe hujijui!
ReplyDeleteyaani hata wiki mbili hazijapita watu kulalamika kuhusu kuweka majina ya wenye passport sasa umeamua kuweka majina na malipo ya watu!
nahisi nia yako ni kutaka kulazimishia kuwa blog yako ni kituo cha taarifa, lakini naona unaingilia privacy za watu....tena unaziingilia vibaya sana
kuna siku mtu atakushtaki.....shauri yako
wewe michuzi issa jounir senior.. unajipenda kweli!? stop being idiotic,nakushauri utoe this data..sio jambo jema kabisa. na waliosema huko juu ni kweli,huku ulaya ungeshitakiwa. this is confidential matter.
ReplyDeleteHebu acheni hizo kama iko kwenye gazeti yeyey anahuru wa kuweka huku...Mmezidi na nyie sasa....Hata hayo majina ya pasi mwenye kuhukumiwa ni hao waliompa na sioni hata shida ni ipi...mmmezeidi....Michuzi hayo ni macho ya chura tu .....wala usijali kaka yangu
ReplyDeletewatu tuwe na lugha ya heshima na ustaarabu. Hata kama una point ya maana ya kushauri, ukimuita mtu mjinga (idiot) unategemea atasikiliza point yako? We Anony wa July 19, 2008 6:01 PM, hebu kuwa na heshima bwana. Michuzi kakustahi sana kwa kuweka hata comment yako hapa, maana angeweza kuifutilia mbali. Usikute mtu mwenyewe ni katoto ka mwaka 1990, Michuzi anaweza kuwa baba yako. Maana ungekuwa mtu mzima usingeandika upuuzi kama huu.
ReplyDeleteMwishowe, msimlaumu Michuzi, walaumu hao wanaomletea habari aweke. Ye amefanya kuweka hapa kama hisani. Sasa kama hao COSOTA/Ubalozi/etc wanaweka personal info za watu katika press release zao Michuzi afenyeje? Au mnataka aanze kukataa kutuwekea matangazo hapa?