Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, William Lukuvi (kulia kwake) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei (watatu kulia) wakiwa na wanafunzi watatu wa darasa la saba waliofanya vizuri katika somo la Hisabati mkoani Dodoma katika sherehe za kuwazwadia 9533 wanafunzi waliofanya vizuri katika somo hilo zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Wanafunzi hao kutoka kushoto ni Sharifa Hamisi wa Shule ya Misngi Pandambili, Kongwa , Sharifa Hamisi wa Shule ya Msingi,Mtengete ya Mpwapwa na Said Suleiman wa Shule ya Misingi Karamba , Kondoa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2008

    tatizo langu nikwamba, kuwa wa kwanza sio tatizo bali ni je umejifunza lolote? umeelimika?napia serikali inapotoa takwimu za kupanda kwa elimu ningependa wasitumie vigezo vya watoto wangapi wamefaulu. kufaulu pekee hakumaanishi kupanda kwa elimu.

    Nimeshuhudia watu kadhaa ambao walifanya vizuri kwenye mitihani yao but mukikutana kwenye level ingine unajiuliza. nakumbuka mwaka jana kuna wanafunzi walirepotiwa kurudhishwa sekondali kwakuwa na uwezo usioendana na max, anaenda seco hata kusoma hajuwi.

    nimeyaona pia elimu ya juu, tena huko ndio kichekesho hasa ukizingatia hakuna 'twishen'. utasikia mtu amefika na point tatu AAA lakini hawezi chochote. wanadisco kibao, wanaingia na migi kwenye paper, wasichana wanajikomboa kingonongono!!!! Y kama walikuwa bora hapo before then washindwe level ingine???

    ni hayo tu!! sisemi pia kama wote wanakuwa mbumbumbu! no.

    G7
    UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...