Dar es Salaam,
Julai 19, 2008:
Mashindano ya Taifa ya Pool yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager hatimaye yamefikia kilele chake kufuatia kufanyika kwa mizunguko ya mwanzo iliyoanza Jumatano Julai 16 2008 katika klabu kadhaa za pool jijini Dar es Salaam. Fainali zitafanyika kesho Julai 20 2008 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8 mchana.
Akizungumzia shauku kubwa juu ya mashindano hayo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Bw. Fimbo Buttallah alisema, “Hili litakuwa tukio la kihistoria hasa ukizingatia kwamba kwa mara ya kwanza mchezo wa pool umekuwa gumzo. Sasa pool haitazamwi tena kama tu kitu kinachofanywa na watu wasio na mambo mbadala ya maana, lakini sasa hadhi ya mchezo huu imepanda sana. Natarajia washabiki wengi watajitokeza sawasawa na umaarufu wa mchezo huu ulivyo mkubwa.”
Mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa muda wa wiki mbili yalijumuisha pamoja timu toka Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Tanga, Kinondoni 1, Kinondoni 2, Ilala na Temeke. Wachezaji wa timu zote kumi walianza kuwasili jijini Dar es Salaam Jumanne Julai 15 2008 na kuhudhuria semina na shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha mchezo wa pool.
Safari Lager, ambayo ndiyo mdhamini wa mashindano hayo, imetenga zawadi mahususi kwa mshindi wa fainali hizo pamoja na kila timu inayoshiriki. Zawadi hizo ni pesa taslimu kuanzia Sh. 2,500,000/- kwa mshindi wa jumla hadi Sh. 250,000/- kwa timu itakayoibuka katika nafasi ya kumi.
Mgeni rasmi katika fainali hizo ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Leonard Thadeo. Watakuwepo pia wasanii wa kizazi kipya Professor Jay na Hard Guy ambao watakuwa wakiwatumbuiza mashabiki.
Mashindano yalianza Julai 5 2008 katika mikoa kumi nchini na fainali hizo zitatoa pia wachezaji nyota watano watakaounda timu ya taifa ambayo itakwenda Ezulwini, Swaziland kwenye mashindao ya dunia ya pool yatakayoanza Agosti 16 hadi 23 mwaka huu. Mashindano hayo yameandaliwa na Chama cha Pool Barani Africa (AAPA) mashindano ambayo Safari Lager pia inhusika nayo.

Mnaaribu watoto tu mchezo gani kucheza mpaka uende bar. At the end of the day they will be omba omba maana unatakiwa kuwa na hela kucheza, walevi au lazy ass next generation mchezo usiokuwa na mazoezi ya mwili siukubali hata siku moja. The like of basketball, footie, raadha, tennis na mingine mingi ndio real deal hii ushenzi tu akili azitafunguka ever
ReplyDelete