vijana wa fc vito wakila tizi bichi baada ya kutua finland
FC VITO Wakiwa Nyumbani Nanyumbu Mtwara wakijitayarisha na Safari ya Finland

vijana wa umri wa miaka 11 kutoka mtwara ambao ni wawakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa ya Helsinki Cup wapo finland lakini hawakuweza kuanza vizuri jana, walicheza mechi mbili ya kwanza walitoka sare 2-2 na ya pili walifungwa bao 4-1.

michuano inaendelea mpaka mechi yao ya mwisho ya raundi ya kwanza hapo jumatanoya kesho. magazeti pia ya helsinki yameifagilia sana timu hiyo kutoka Tanzania ambayo ndiyo timu pekee kutoka bara la Africa.

Timu zingine ni kutoka bara la ulaya na Marekani ya kusini. Habari zaidi kuhusu maendeleo yao hawa mabalozi wetu katika michuano hii ya helsinki cup nitakujulisha baadae.

Hii ni linki ya gazeti moja wapo ikiwasifia vijana hao kwa kucheza mdundiko katika ufunguzi wa michuano hayo.

http://www.liike.fi/uutiset/08/img/0707hesari.jpg



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2008

    Vijana wamejitahidi sana sana kuonyesha kandanda safi,ila tatizo lao kubwa ni Ufupi !kilichonisikitisha ni kuwa Helsink kuna watanzania wengi sana na miji ya karibu ila kwa siku ya jana watu walijitokeza wachache sana ,Shime wadau kesho basi tujitokeze wengi kuwapa moyo wadogo zetu na wawakilishi wa Taifa letu.mbarikiwe sana kwa mtakaopata muda wa kufika kesho.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2008

    Oya sema muda basi na uwanja utakaotumika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2008

    safi sana!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2008

    si lolote si chochote!! hawa watoto wametutia aibu ya mwaka! kweli viwango wanavyo ila size ndio shida watoto wa miaka 11 utadhania wa miaka 6 yaani balaa wamekutana na watoto wenzao wa miaka 11 duu aibu kama wanaonewa vile, ndio mechi ya kwanza wametoka 2 - 2 ila ya pili aibu!!! hata sikumbuki ni ngapi wamefungwa ila mara ya mwisho kuhesabu ni 7 kwa 1 maana watoto wetu hata nguvu ya kupiga mpira hawana wenzao wanapiga hata mita 20 wao mita 5 tuu shida naomba hawa jamaa wanaowale hawa watoto wachangue wenye size kidogo sio kama hawa waliowaleta. na leo j 4 wamecheza ila sijaenda maana jana walitutia sana aibu na mapicha yao ninayo nitamtumia bro michuzi azitundike. au labda wamefungwa kwa mambo mengi kwanza ndio hiyo size miaka 11 kama miaka 6 second wametoka mtwara afadhalia hata wangetokea dar 3 kucheza na wazungu na uwanja mzima umezungukwa na wazungu naona pia inawatia uoga ila viwango binafsi wanavyo. ni hayo tuuu ila sio 4 kwa 1 ni kuanzia 7 au 8 kwa 1

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2008

    kwanini watanzania wengine tuko negative sana juu ya vitu vya kwetu. Timu kubwa katika Champions League zinafungwa mabao 7 au 8 itakuwa watoto hawa?

    Badala ya kufurahi kuwa angalau wamejitokeza na kuwaombea wazidi kuendeleza vipaji; mwakani warudi tena na possibly baadhi yao in a few years wawe timu ya vijana, mtu unakalia kuponda na kupaka utadhani mechi ulilipia; kumbe umeangalia bure. We enzi zako ulipokuwa una miaka 11 ulikuwa una umbo kubwa?
    Tukubali kuwa in general watanzania tuna miili midogo ikilinganishwa na hata baadhi ya jirani zetu; and even much more worse ukilinganisha na mizungu inayokulia ktk junk food and genetically modified food. Na zaidi ya hapo; wascandinavia in general ni warefu.

    Isitoshe, wenzetu wengi wanacheza organized sports toka wana miaka 6, au 7 na wanafundishwa hadi matizi ya kujenga misuli; wanafundishwa jinsi ya kupiga mpira uende mbali zaidi; tofauti na sisi tunaochezeaga cha ndimu tu. Sasa we anony hapo juu badala ya kukalia kuponda tu; toa mchango wako katika kujenga soka na michezo mingine Bongo. Sio unakalia kukosoa tu.
    Ndio nyienyie huku Ulaya na Marekani mnaenda kuangalia mechi ya watoto hamchelewi kuanza kupigana na another parent au na refa. Waache watoto wafurahi; the rest follows. For God's sake, they are under-11!!!!! Ulivyowakalia kooni watoto wa watu sijui kama nini. Usikute we hata kupiga danadana 2 huwezi

    ReplyDelete
  6. Good-luck in the rest of the kids. Mahome Boy wangu wanatuwakilisha Wamachinga!! Mtwara yeahhh!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2008

    waambieni hao watoto wasicheze kwenye maji huko kuna sharks. wasidhanie huko ni bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...