Michuzi,
Pole na kazi ,naomba sana wadau wasaidie katika hili , ni kwamba siku hizi wafanya kazi wa Tanesco wamekuwa na tabia ya ajabu, kama kumetokea tatizo la umeme na labda ikasemekana kuna nyaya zinameanguka chini.
unapowaita wakija na kukuta ni kweli kuna tatizo la umeme lakini nyaya zilivyokaa labda wao wanaona hazitasababisha hatari kwa maisha ya binadamu basi wanakwambia umewasumbua na hawakurudishii umeme.
wanarudisha nyumba zingine wewe uliyewaita wanakuacha mpaka baada ya siku mbili ukilalamika tena ndipo wanakuja kukuunganisha.
Wanadai wamekupa adhabu wa vile umewasumbua.Je wanaruhusiwa kutoa adhabu??
Mdau


Hao TANESCO wajinga ndio maana hata walidanganywa kiurahisi na Richmond. Wafanyakazi wengi wa Tanesco hawajui wapo kwenye biashara na mteja ni mfalme badala yake wanafikiri wanatoa msaada kwa watumiaji wa huduma yao. Kazi kweli kweli! Nafikiri hii ndio sababu iliyomfanya Kikwete amteue Dr. Idris kuwa mkurugenzi ili awasaidie kuwabadilisha hiyo attitude ya mwaka 1947
ReplyDeleteWaruhusiwe kutoa adhabu kama nani? Ndo matatizo ya kuwa na monopolies hayo! Watafanyakazi kibabe sana tu. Wanasahau kuwa bili yako ndo inawalipa mshahara...kweli kuna watu wa ajabu sana!
ReplyDeletekha!wapuuzi eeeh??HOW DARE THEY..hii ni ishu ya kupelekwa magazetini ili wakuu wao wapate kusikia,ili tabia hii ikomeshwe! hata kama ipo kwenye nafasi ambayo haihatarishi maisha,its still wise to call them to fix the problem! this tanesco people are very weird!am dissapointed
ReplyDeleteKWA KWELI NI ISHU YA KUPELEKWA GAZETINI HII ... HAYA HABARI IMEFIKA KWA MISUPU NADHANI ITAPELEKWA HUKO MAANA YUPO KARIBU NA HAYO MAGAZETI... JAMAA WANABOA SANA
ReplyDelete