Mkuu Michuzi!

Yaani baada ya zogo kwamba JD hakuwa amealikwa rasmi kwenye shoo ya Mandela hapa UK, nimeona leo heri nikutumie kijipande cha gazeti ambacho nimejitahidi kukipiga picha maana nina haraka la sivyo ninge scan.

Ukiaangalia kwa makini kushoto mwa picha utamuona dada JD. Ama angalia wa pili kushoto toka juu, utamuona. Ikumbukwe sio kila aliealikwa alifanya shoo, ila umuhimu wake ndio uliomleta hapo

Nakutumia zote tatu wewe utachagua ipi itaonekana vizuri. Ukiangalia vizuri Jide ni wa tano kutoka kwa Willy Smith (kulia kwake).Willy Smith, kisha wa sugarbabes, mwimbaji mwingine wa sugababe kuna jamaa mweusi halafu Jide.
Asante

Mdau UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2008

    Wewe mdau ndio tumeona picha.kaalikwa ndio sawa....kwa nini haku perform??ama ndio alienda kuuza sura??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2008

    Jamaa mweusi nadhani ni Jimmie Foxx (academy winner).

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2008

    Ali sio ya chakula wala Ali sio ya kulia Kuimba aliimba sema kama ulitizama kwenye tv hawajaonesha live. JD then huyo jamaa pembeni yake aliimba na jamilia pembeni tena Sugar Babes katikati yao WilliamU Smith chini ya Jide ni Jada Pinket pembeni ya mandela huyo mama mzungu ndio aliyeaanda hiyo party muimbaji jina simjui pembeni ya King Mandela ni Leona Lewis. hao ndio nawajuwa mie nyuma ya will smith huyo babu kavaa kofia nyeusi pacha wake issa michuzi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2008

    WEEE ANOMYOUS WA KWANZA UNAELEKEA UNAROHO MBAYA SANA JD HAKUIMBA ILKUA AIMBE NA PAPAWEMBA LAKINIPAPAWEMBA ALINYIMWA VIZA YA KUINGIA UK KUWEPO KWAKE NDO MUHIMU UNAMUONEA WIVU???UNASEMA KAENDA KUUZA SURA JAMANI! HEBU KASOME UTOE UJINGA KICHWANI KUTAKUSAIDIA UTAANDIKA POINT SIO UJINGA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2008

    sio wote waliokuwa pale walialikwa wapo waliojiarika kama JIDE,Kifupi kaenda kwenye shoo za kibongo sio kwa mwaliko wa mandela,hizo picha tu kipi kingine unachoweza kusibitisha alialikwa,,,kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2008

    wewe hapo juu wa kwanza wewe jee ulialikwa???

    acheni roho za kwanini wabongo tumezidi sasa, Jide kaalikwa kutokana na performance zake kwenye sekta ya mziki Africa, sio lazima aiimbe, what matter is, in that gathering amealikwa kwa status yake, sio wewe umekaa hapo unasubiri michuzi aweke picha ili upake 2, Get a Life.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2008

    Thank u very much mdau,lakini bado kuna watu watasema yuko mbali na Mandela ktk hiyo picha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2008

    SWALA SI KUWEPO SWALA NI KU-PERFORM KAMA ILIVYOKADAIWA WAKATI AKIONDOKA BONGO, HANA SIFA ZA KUPERFORM KWENYE GHAFLA KUBWA KAMA ILE, HANA SIFA HIZO ZA KIMATAIFA, BADO SANA, KWENYE PICHA HIYO WATU KIBAO WALIOPIGA PICHA HAPA HAWAKUALIKWA LAKINI WAMEPIGA PICHA HAPO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2008

    waTanzania bwana tunapenda ubishi wa kijinga jinga!! Hatuoni mema tena sansana nyinyi mlioko huko nje ya TZ. Ukiona mwenzio kapata yaani makeleleee!! Sasa wewe unayebisha kwamba JiDE hakwenda, mbona hukualikwa wewe? Tumikia hao wazungu wazee na ukae kimya!!

    Kaka, A-City.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2008

    Wewe anon wa 12:22 unaishi dunia ya wapi hata haufuatilii matukio?. Ufafanuzi ulishatolewa na waandaaji kuwa Jide ilikuwa aimbe wimbo wa HAPPY BIRTHDAY pamoja na Papa Wemba. Na huyo Papa Wemba alinyimwa visa ya kuingia UK. Sasa wewe nataka maelezo gani tena?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2008

    Maelezo ya awali yalisema kwamab ataimba kwenye show..kupiga picha sio kualikwa..yeye aseme alikuwa na shida ya kwenda London

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2008

    we anon hapo juu, sijui uelezwe lugha gani ndio uelewe. "SIO KILA MTU ALIYEALIKWA ALIPERFOM" sio kuabisha tu bila sababu, and if that what you call kuuuza sura sio yeye peke yake aliyeuza sura, most off them did.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2008

    MICHUZI MIE PIA NILIKUWEPO NINAPICHA YANGU NIMETOKEA NA NILIALIKWA LAKINI SIKUWEZ KUFANYA SHOO.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2008

    we bwege si kila aliyealikwa aliperform. waandazi kwa kutambua umuhim wake ndo wakamualika...Mdau wa UK hiyo kazi ya kusafisha nyota ya JD umepewa na Capt Habash? maana nyie kwa ubish siwawezi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2008

    "KUKAA KARIBU NA MAHAKAMA SIO KUJUA SHERIA" Mdau umenifurahisha sana na huu usemi wako!!! Lakini wabongo kwanini mnabishana jambo ambalo haliwaongezei wala kuwapunguzia chochote!!?? Kama hakualikwa au alialikwa hamna msingi wowote, cha msingi ni kwamba alikuwepo. Sasa kama wewe haukuwepo punguza hasira!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2008

    MTAUMWAAAAAAAAAAAAAA NA DAWA HAKUNA KWA WENU UPEKEPEKE NA LITA WACHOMA NA ROHO ZENU MBAYA MAMBO YA ZANZIBAR STAR AYO JD NDIO KASHATOKA HIVYO ENDELEA KUBWABWAJA

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2008

    WATU WENGINE SIJUI WALIZALIWA WAKATI WA MATETEMEKO YA ARTHI??!!! YAANI NA PICHA MMEONYESHWA, MAELEZO MMEPEWA BADO MNANGANGANIA JD HAKUALIKWA.

    KAMA HAKUALIKWA MBONA WEWE HAUPO KWENYE HIYO GROUP PHOTO? HUO WIVU WENU UNAWAZIBIA MAENDELEO.

    JD AMEKUJA LONDON MARA KIBAO, NA AKITAKA KUJA KUFANYA SHOW HAPA ANYTIME; KWA NINI ADANDIE MWALIKO USIO WAKE??!!

    KUBALINI YAISHE, JD ALIALIKWA RASMI, KAMA BADO HAMPENDI TAFUTENI SUMU MKANYWE MTUPUNGUZIE GHASIA KWENYE BLOGU YETU YA JAMII.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 25, 2008

    Jamani mtaka msitake lady jay dee alikuwepo. Naona hao wasiotaka bado wapo wapo tu. Mbona hatuoni mbongo mwingine hata mmoja? au basi na Ali kiba si alikua maeneo si angeenda basi na yeye kuuza sura kama kila alietaka kuuza sura aliruhusiwa kwenda. Wivu utawaua jamani hasa anon. wa kwanza lol. Acheni hizo na si ajabu wakandiaji wengine ni wanamuziki ambao hawajawahi kutoka hapo kwenye vumbi. JIDE paa mwanangu hakuna cha kukuzuia. wameona picha na HABARI NDIO HIYO

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 25, 2008

    Acheni roho mbaya kama wakaanga sumu.Kuenda kaenda kwa mwaliko maalum,ameimba hakuimba haiwahusu mana si nyinyi mliyemlipia nauli.Acheni midomo mirefu Mbona nyinyi hamkualikwa hata tu kuja London kushuhudia?acheni ushamba nyie.
    Miss R. Nyange,London.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 25, 2008

    Papa Wemba kanyimwa visa ya UK? Anaihitaji kweli? Yeye mkazi waFrance. Toeni sababu nyingine

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 25, 2008

    Hoo sijui ataimba na papa wemba!!mbona hata papa wemba mwenyewe haonekani!!jide mwenyewe anaonekana karukia picha..inaonekana alikuwa kwa mbali tena anapita alivyoona watu wanapiga picha na mandela akakimbilia...mualiko unafikiri mchezo!!!JIDE KARIBU NORWAY JAMANI..

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 25, 2008

    JIDE SONGA MBELE!!!! USISIKILIZE
    MAONI YA WANAFIKI!!!!
    Kuna baadhi ya watu hawapendi kusikia wasanii wa Tanzania wakifikia au kufunika kimataifa,baadala yake wamekuwa watu wakuzusha hoja zilizo jaa fitina na majungu na kudhalalasha
    wanamziki!
    Sasa kuna faida gani?ya kutaka kumdhalilisha Bint Machozi,wakati pale katuwakilisha wabongo,
    Heti baada ya kufuraia na kujisikia fahari baadhi ya watu wamekuwa na roho za kwanini!ambazo
    hazina faida yoyote

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 25, 2008

    jambo la kujiuiza ni kwamba waliomuimbia mandela wamepata nini??
    au ukimuimbia ndiyo utakua maarufu?? basi mimi mtu ninaejua ni maarufu wa mziki ni michael jackson na hakuchukua shit kwenda kupoteza mda wake na mtu kama mandela asiedhamini wa afrika wenzake badala yake wanawachoma kama nyama nyie fikilieni na muone vitu vya kuoneana wivu hii ni pumba tu!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 25, 2008

    Jide go my girl. Hakuna wa kusema wameshaona picha wameishiwa maneno mara ooh papa wemba anaishi france atakosaje visa ya uingereza, hivi kwana kuna asiejua papa wemba alipatwa na kesi ya kuingiza wahamiaji haramu? sasa cha ajabu kunyimwa viza nini? Bwana mtaka msitake ndio keshaenda na siku hazigandi.. Jide anatisha yuko juu sana. Huo ni msumari unawachoma moyoni na machoni yaani kote kote...(Jahazi moden taarab)

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 25, 2008

    Duh,Hii kali wapi PAPA WEMBA kanyimwa viza,JIDE hakualikwa bali huu ulikuwa MCHONGO WA JIDE Kuingia UK,Kwahiyo kausheni msichonge mpaka UBALOZI wa UK ukajua.mkamfanya asije tena kututembelea,mi ndio niliyempokea jide,,mi nilikuwepo na sikuwa na mwaliko.
    MR.UK

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 25, 2008

    MDAU ULISEMA PAPA WEMBA NI MKAZI WA FRANCE, ALIWAHI KUKUONYESHA PASIPOTI YAKE YA UFARANSA?? AU UKISIKIA MTU ANAISHI FRANCE NI LAZIMA AWE RAIA WA FRANCE. UBISHI MWINGINE HAUNA MASHIKO, TUWEKEE HAPA KOPI YA PASIPOTI YA PAPA WEMBA YA FRANCE INAYOTHIBITISHA NI MFARANSA NA KUWA HAHITAJI VISA KUJA UK, NDIO UJE KUSUTA WATU KUSEMA PAPA WEMBA HAHITAJI VISA.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 25, 2008

    Kuna lingine hapo juu ndio kubwa jinga kabisaaaa.eti "papa wemba kanyimwa viza ya uk kwani yeye anahitaji yeye na raia wa france".usiwe pumbavu wewe kunyimwa visa haichagui maskini wala tajari,haichagui wewe raia wa wapi wala nini.alinyimwa visa ya uk snoop,alinyimwa visa ya marekani amy winehouse.visa unanyimwa na record yako iko vipi na kama unakumbuka vizuri papa wemba alikuwa ana kesi ya kuwazamisha watu.
    Hilo swala la jide kinachowasumbua ni roho ya korosho na nyinyi ni vijana wadogo haina haja ya kuwa na wivu wakijinga jinga kwa mtu ambae aingilii hata kidogo kwenye maisha yenu.mkianza kuwa na roho za korosho kwenye umri mdogo matokeo yake baadae msipofanikiwa wengi wenu mnaanza kujiusisha na mambo ya kishirikina.
    Tujifunze kujali maisha yetu wenyewe na sio kutolea macho maisha ya watu wengine.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 25, 2008

    Wabongo sijui kwanini KAMWE HAMTAKI KUKUBALI UKWELI. JD au JIDE atajijua mwenyewe lakini UKWELI NI KWAMBA 'HAKUALIKWA' KAMA ANGEALIKWA NA KUWA NA UMUHIMU WOWOTE LAZIMA ANGE-PERFORM... OK? Ukweli ndio huu. Nakubaliana tu na mdau mtoa maoni kuwa ilikuwa a-perform na huyo mwanamuziki wa KIZAIRE ambaye apparently alinyimwa VISA kuingia Uingereza. Labda kwa kutegemea kuingia nae ndio angepewa mwaliko rasmi kama wengine, lakini sio yeye mwenyewe tu JIDE because no one knows or care about her. Ila nampa POLE.
    KUTOKEA KWENYE PICHA YA WENGI HAPO SI HOJA, KWANI NIMEONA MANDELA MWENYEWE HAKUWEKA RESTRICTION YA NANI ARUHUSIWE KUPIGA NAYE PICHA NA NANI ASIRUHUSIWE. MANDELA IS VERY HUMBLE, NI MTU WA WATU NA ANAPENDA WOTE MASIKINI NA TAJIRI, KWA HIYO HATA MIE NILIPATA HII FURSA YA KUPIGA FOLENI NA KUPATA SNAP. Halikadhalika ndivyo alivyofanya huyu JIDE na siyo hiyo tu baadae nikamwona walisogea pembeni akafanya juu chini akutane na WILL SMITH, NA EDDY GRANT AKAWAOMBA WAPIGE NAYE PICHA. Kama mnavyojua nao hawana noma kabisa.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 25, 2008

    jamani wabongo wanapenda sana kuongea,Mimi nilibahatika kuonana na JIDE london walifikia hotel inaitwa marlyland ipo oxford circus,nilkutana naye ajiri kuna rafiki yangu alikuja pamoja na group la celtel kwenye birthday.sababu kubwa ya kutokuperfom jide ni kuwa ilikuwa hapeform na papa wemba ila wemba alikosa visa hivyo ikashindikana,mbona wabongo mnakuwa mnatafuta tu vijineno ili mwongee tu.
    mdau LSC,uk.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 25, 2008

    MHH WABONGO MPO DUNIA GANI NYINYI MTAISHIA KUPIGWA NA VUMBI KWA MAMBO YA KIJINGA...KUNA MDAU KASEMA ETII UTAISHI KULE WAZUNGU WAZEE WEWE UMEFANIKIWA KUTOKA NJE YA TANZANIA HAYA SASA MUULIZE HUYO ANAYELEA WAZEE KIASI CHA HELA ANAYOPATA KWA WEEK NA FANANISHA NA HELA YAKO UNAYOPATA KWA MWEZI ALAFU ANGALIA MAISHA YA HUYO MLEA WAZEE NA MAISHA YAKO YANAENDANA ACHA KULOPOKA KAMA UMEKUNYWA MAJI YA CHOONI SIO VIZURI USIMUANGALIE MTU KWA KUMUONA....PIA JAMANI WAKINA DADA NA WAKINA KAKA TUJARIBU KUANGALIA MIDOMO YETU OR TUJARIBU KUICONTROL MIDOMO YETU...kuna kitu kinasema kwamba ficha upumbavu wako usifiche hekima yako SASA HAPO JIANGALIE PUMBNA GANI UINAZOONGEA NA ZINAKUSAIDIA NINI KATIKA JAMIII NA WENGINE JARIBUNI KUTUMIA AKILI ZENU ZA DARASANI MSITUMIE AKILI ZA MTAANI JAMANI AU SIO MAANA MTU UKIANGALIA COMMENT HAPA INAONEKANA WATANZANIA KIASI GANI HATUJASOMA TUSIWE NA WIVU WA KWANI ILIBIDI TUMSAPOTI MTANZANIA MWENZETU JAMANI SIO KUANZA KUMPONDA KAMA UNATAKA NA WEWE TAFUTA KAZI YAKO AMBAYO ITAKUTANGAZISHA ILI UWE KAMA J DEE AU SIO PAMOJA....

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 26, 2008

    Mkuu wa nanihii alishasema, wabongo kama senene. JD alikuwepo kwenye sherehe ya Madiba. Tujiulize walikuwepo waalikwa wangapi wanamuziki? Sherehe ilikuwa ya muda gani? Kila mwanamuziki aliweza kutumbuiza?
    Hata kama JD hakutumbuiza, kuwepo kwake kule ilikuwa ni nafasi nzuri kubadilishana mawazo na watu kutoka kona mbalimbali za dunia. Tusingekuwa senene basi tungejitahidi kupata mshindonyuma kutoka kwake badala ya kupigapiga jungu.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 26, 2008

    Martha Stewart, mamarekani bilionea alinyimwa VISA iwe Papa Wemba.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 27, 2008

    KWAHIYO JIDE HAKUWEZA KUIMBA WIMBO PEKE YAKE KWA KUWA PAPA WEMBA HAKUWEPO,,NDIO KUSEMA MADIBA HAKUIMBIWA NYIMBO YA HAPPY BIRTHDAY SABABU PAPA WEMBA HAKUWEPO, HACHENI UONGO JIDE HAKUALIKWA

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 29, 2008

    Unajua kuna aina mbili za ku appreciate mafanikio ya mwenzako....ya kwanza ni kukubali na kumpongeza then kuchukua hayo mafanikio kama changamoto.......Ya pili ni kukataa mwenzako hawezi kufanikiwa na kudhani kila alichopata ilikuwa ni kamati za ufundi au kujaribu ku justify in negative critics kuwa jamaa hastahili.

    nikisoma maoni ya wote hapo juu naona kuwa sote tunakubali maendeleo ya ya Lady jaydee ila katika hizi approaches mbili nilizozitaja hapo juu.

    Wengi wetu tuna hulka ya approach ya pili....ambayo ni ya kijinga na ya kishamba kupita maelezo.....na huu ni ukataji tamaa tu wa maisha tena wa kijinga..siku zote mpambanaji hawezi tumia hii aproach atahangaika na yeye a fullfill dreams zake ili pia watu wamuone(soma vizuri motivation factors kwa nguri Manslow)...

    Na kwa wale wanaojifariji kuwa wanakusanya paund nyingi ulaya huku wakiishi maisha kama ya njiwa kisa wanapata paundi nyingi nadhani pia wamesahau kulinganisha gharama za maisha za bongo kwa kiasi kile kile kidogo wanachopata na gharama za maisha za Uk na kwa paundi hizo(nyiiiiiingi) wanazopata. na pia wamesahau kulinganisha utu wa kusafisha na kulea wazee na utu anaoupata mtu akiwa na kazi yake bongo. dont get me wrongo, si wabongo wote wanaobeba box Uk..wapo wenye kazi zao nzuri lkn hawazidi 5%..trust me, I have been there....na juzi tu gavana wa central bank of england kasema wameshindwa ku control gharama kubwa za maisha zinazozidi kupanda ndani ya UK....sawa kote maisha uwe bongo au ulaya..ila msijechekwa ujinga kwa kudhani mpo bora kuzidi nyumbani..na si kwamba Lady Jaydee alikuwa na shida sana ya kuiona congestion city such as London..si angechagua paris au miji mingine isiyo na magofu kama london!

    camon guys muamke sasa sio mnalalamika tu kama watoto wa kambo...she deserved it, rudi mama utupe burudani na machozi band..wabongo ndio maana hawaendelei huko ughaibuni..wataishia kuwaona wanaijeria na mataifa mengim=ne ambao wapo aggressive.

    mdau wa Doha

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 29, 2008

    baadhi ya watz ni wambea sana na wapumbavu, asa hicho ndo kitu cha kujadili hivyo!ujinga mtupu! kwenye habari za albino kuuawa ahaa-a mko kimya tu! watu wachache wamechangia pale, ila ubongo wenu umekuwa active mlivoona ishu kama hii isiyo na maana... mtaishia kuuwa wenzenu kwa umaskini wa kufikiri!
    michuzi ukitaka bana, ila lazima wajue ukweli watu kama hawa! bure kabisa! inafaa nini kwa taifa kuwa na upupu wa watu wasiojua ishu za kuchangia?

    ReplyDelete
  36. USHAURI KWA JIDE Na WASANII BONGO
    NIKIANZA NA JIDE MUSIC NI FANI KAMA FANI NYINGINE, HIVYO KUIBORESHA INATAKIWA MUENDE SHULE
    MAMBO YA KUSHINDWA KUONGEA ENGLISH WAKATI MNATAKA MUUZE KIMATAIFA NI KUTWANGA MAJI KWENYE KINU NA MAISHA SIO TU KULA NA KUVAA NA MISIFA MNAYO PEWA NA WABONGO.
    MSOMEE NA MUWE COMMITED SIYO NYODO NA NA DHARAU HAZITAWASAIDIA HATA MJE ULAYA MARA 100, HIYO SIYO DAWA MRUDI SHULE ILI MUWEZE KUSUIT KATIKA FANI ZENU NA KATIKA USHINDANI WA KIMATAIFA.
    KWANI MOST OF BONGO FLAVA MUSICIAN WHEN THEIR COME TO PERFORM EUROPE THEIR JUST PERFORM IN THEIR WARE HOUSE EVEN THE GOVERNMENT THE DONT RECOGNISE BECAUSE MOST OF THEM THEIR COME WITH VISITOR VISA INSTEAD OF WORK VISA LIKE OTHER MUSICIAN. IS VERY SHAME AND RISK
    SO WAKE UP AND GO BACK TO SCHOO IFE IS NOT ONLY EAT AND SLEEP.

    ReplyDelete
  37. jamani tatizo hapa watu wanabishana kwa lengo la kubishana maana hao wanaosema kuwa Papa wemba hakuwepo nao si wafuatiliaji wa habari.

    Mimi niliituma hii picha kwa michuzi si kuonyesha kuwa JD aliimba la hasha. Ikumbukukwe kuna jamaa alisema kuwa alikuwepo katika eneo la tukio na hakumuona JD, na kama watu mnaobishana hapa kuwa Papa wemba hakuwepo kuna habari zinasema Papa Wemba alikuwepo pia.

    Waalikwa walikuwa wengi na lile lundo la wanamuziki waliomuimbia HAPPY BIRTHYDAY lilikuwa kubwa si rahisi katika Luninga yako kumuona mtu kama Papa Wemba ama JD. Ndiyo maana wengine hapa walithubutu kusema walikuwepo pale ingawa ulikuwa uongo ninachojua mimi waliangalia katika Luninga.

    Sasa pitia katika mtandao huu
    http://news.bbc.co.uk/2/hi/entertainment/7475717.stm

    na huu pia.
    http://www.gmanews.tv/story/103829/Stars-gather-for-Mandelas-90th-birthday-in-London-concert

    Wakosoeni na hao pia wanaopata access kubwa. Msipende kubisha bila kufanya research.

    MDAU UK MTUMA PICHA

    ReplyDelete
  38. Oyaa wabishi nyie angalieni hili lundo la wanamuziki hapa katika gallery pitia

    http://www.46664.com/136/gallery

    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...