Michuzi nashukuru sana kwa kuweka malalamishi yangu kwenye blog yako kuhusu muungano wa Africa mashariki.
Nilipata comments nyingi sana kutoka kwa wadau na kaaribia zote zilikua zinaupinga muungano. Nyingine zilikua ni zakusikitisha kwasababu walizungumzia swala la lugha na ndiyo maana nimeamua kwandika kwa kiswahili.
Ndugu zetu watanzania hofu zenu za ardhi na ajira ni bure kwa sababu kwetu waganda tunaardhi yakutosha na ardhi yetu ni fertile kwa hiyo ardhi ya Tanzania is the least of our priorities, kingine ni kuhusu ajira, ndiyo kuna matatizo ya ajira Uganda lakini kwa wale ambao hawajasoma vizuri, labda hao ndiyo watawasumbua. Lakini naamini waofisa wenu wauhamiaji wa ujuzi wa kutosa kukomesha wahamiaji harama wanaochukua ajira za watanzania.
Nasikitika sana kwa fikira za watanzania wasiotaka kuishi na majirani kwa sababu huo ni uoga usiyo na msingi.
Labda nijizungumzie mimi mwenyewe kuhusu ukazi wangu Tanzania.Nilifanya kazi kwenye makapuni mengi sana kama Guardian, DTV, Mobitel, Monier, Eastafrican Movies na nyingine na siku zote nilikua nawasaidia watanzania ambao walihitaji msaada wa ujuzi na vingine.
Mpaka leo naichukua Tanzania kama nchi yangu ya pili. Watanzania msiwe na hofu, ila imarisheni idara za Uhamiaji na board ya ardhi and then leave the rest to co-existance. Jamani hivi vinchi vyetu ni vidogo sana (including Tanzania) to be able to compete well in the global economy.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba"Small nations are like indecently dressed women they attract the evil minded". Tusipongalia watatumeza wote. SO fellow Eastafricans hayo diyo yangu, but kindly avoid those alarmist sentiments least you have a scenario like waht happened in Southafrica, however in this case it will be Tanzanians against the rest.
Huu ni ujumbe kwa Waganda na Wakenya wanaioishi na kufanya kazi Tanzania.Jamani wa-Tanzania ni watu wanaopenda heshima na ushirikiano na msiwadharau eti kwa kwa sababu hawajasoma.
Some of the most qualified people i have ever met are Tanzanians.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa Mashariki
Phillip Higenyi Kakuru
ICT Resource/WebdesignICT MOVEMENT
Tel: +256775669099
P.O Box 5772
Kampala
Mr.Kakuru hujajibu hoja,why all the clamouring for muungano with Tanzania,kuna nini hasa mnakiona Bongo?why dont you leave us alone na umasikini wetu,kutokusoma kwetu,kutokujua biashara kwetu etc?why,why,why?
ReplyDeleteASANTE SANA KAKURU KWA UJUMBE WAKO NI MZURI SANA LAKINI UKWELI UNABAKI PALE PALE,WASIWASI WA WATANZANIA BI WA KWELI,"MIMI NI MTANZANIA NINAKAMPUNI INAYOFANYA BIASHARA UGANDA KWAA MIAKA SABA SASA"KWANZA USIWALAUMU WA TANZANIA KWA KUKATAA SHIRIKISHO LA AFRIKA KWA SABABU SISI WA TANZANIA TUMETOKA KWENYE SIASA ZA UJAMAA NA SASA TUPO KWENYE UBEPARI WA SOKO HURIA,TATU NI KWELI NCHI KAMA UGANDA NA KENYA UKABILA UPO KWENYE KIWANGO CHA KUTISHA,AJIRA KWENYE NCHI KAMA UGANDA NI KUBWA NI KWELI KWANZA TUACHE WATANZANIA WAJITAYARISHE HIYO ARDHI UNAYOSEMA UGANDA IPO WAPI???? MIMI NINAIJUA UGANDA YOTE.TUMEONA MAJAMBAZI WANAOTUMIA SIRAHA ZA KIVITA WANATOKA KENYA NA UGANDA HATUKUWA NA UTAMADUNI HUU,KAKURU NAOMBA UWAACHE WATANZANIA WAPEWE MUDA KWANZA HATA MIMI SISAPOTI KUKIMBILIA KWENYE SHIRIKISHO
ReplyDeleteASANTE!!!!!!!!!!
ISMA KABENGO
Hallow my friend from Uganda....
ReplyDeleteI don't understand why you don't answer the question:
1. What are the Deliverables (at least zikaonekana na mtu wa kawaida) with the plans/activities of the confederation?
2. Do we (confederation members) know that there are activities which we could HOLD accountable the implementers of the plans/activities?
2. What is the time Frame so that are we (confederation members especially sisi Tanzanians ambao unafikiri ni waoga wa hiyo confederation) can realize the benefits. What need to be done, when need to be done, when are we (confederation members) going to measure the Intermediate Results..... we need a proper/executable plans and need to be participatory.
3. Do you think we (Tanzanian) not competitive when it comes to international arena....??? Absolute we are very competitive.... and you know it for sure... We are thinking far from where (wewe Muganda) you are thinking.. Tanzanians (some) knows the ultimate consensuses especially kwa ndugu zetu ambao wako kule vijijini na HUKO NDIKO KWETU.... tunahitaji kuwaeleza na kujua the benefits and risks of the confederation before we get into.... WHY RUSH...
4. Some of us (Tanzanians) we have foreseen many risks than benefits that is why we are resistance for the (FULL) implementation of the Confederation of the Strategy.
Hope unatuelewa wewe Mtoto wa Museven....
I won't spend muda mwingi kujibu agenda za muandishi. Kwanza kabisa Tatizo sio Tanzania law or policy zinazosababisha Watanzania wengi kupinga swala la muungano, bali tatizo ni nchi zinazotaka kujiunga na sisi.
ReplyDeleteUganda hamja challange uongozi wa kifalme wa Museveni. So, kwa nini tuwakaribishe kwenye muungano wakati bado mpo kwenye zama za ufalme?
Kenya, wana strong tribalism and how can they prove that they will not worship Kikuyu or Luo?
Personal i believe Tanzanain can compete with Kenyan and Ugandan shoulder to shoulder.
Hatuogopi ushindani, tunaogopa kukaribisha watu ambao sio part of us, matokeo yake ni ku cripple our social, economical and political values. Tanzania sio nchi pekee inayopinga hizi geo-political partnership, nchi nyingi tuu Ulaya hazija jiunga na EU.
Kingine, kuna wasomi wengi tuu watanzania ambao wako against hili swala, mimi ni mmoja wao. Na naimani asilimia mia moja few or less kenyan wanaweza hata kushindana na mimi kwenye ajira. So, sidhani kama swala ni ajira. Swala ni Uganda and Kenya bado zinaitaji improvement kabla hatujazingiza kwenye federation. so, ushari wa bure ni kuwashauri waganda wenzio waset goals kabla ya kuomba kujiunga. Goal moja wapo ni kumtimua Museven, Kuresolve matatizo yenu katika mipaka ya Congo ambako bado kuna rebells wanapigana, kushauri seriakili yenu kuwa neutral concern other countries politics.
Naweza kuandika more than 20pages why we don't want muungano na either nyinyi waganda au wao wakenya. Nashukuru magezeti mengi yalielimisha kuhusu swala la muungano nightmare. Bado tunapay price ya failure za 1977, why join another Bonanza?
Get a life, Tanzania will stay as Tanzania.
Mdau wa US tawi # 1
tatizo si kwamba watanzania hatuwapendi majirani zetu. La hasha. ila mipaka inayovuja kwa wenzetu wa Kenya na Uganda inaweza kuwaleta watu toka Sudan ya Kusini na Somalia na kuweza kuingia Tanzania bila ya kuwa na stakabadhi zozote na kutuongezea idadi ya wahalifu nchini. Tunapoungana tunashea na mipaka pia. tusafisha nyumba zetu kwanza halafu ikiwa tayari tuongelee Muungano wa East Afrika. Kwa sasa tuendelee na ushirikiano wa kiuchumi kwanza tujenge soko imara la east afrika.
ReplyDeleteUnajua woga wa watanzania umetokana na mafisadi wengi waliojaa humo maofisini. Hawa mafisadi wanaturudisha nyuma mno! Hapa ni kupima advantages na disadvantages za muungano na kuona ni kipi kizuri. Nilikuwa naongea na Mcameroon mmoja namweleza kuhusu upinzani wa waTz kuhusu hili swala la EAC. Yeye akanipa mfano wa nchi yao na umoja wao wa CEMAC au kwa kiingereza 'Economic and Monetary Community of Central Africa'. Anasema mwanzoni waCameroon walikuwa hawataki kujiunga maana wao ndo ilikuwa nchi kubwa na yenye resources nyingi kati ya nchi zote zilizoko katika huu umoja. Lakini wakaja kugundua kuwa kuna advantages na disadvantages za kujiunga. Na sasa wamefikia kuwa na pesa moja XFA (Central African CFA franc) na central bank moja (hii kwa east africa itatusaidia kupunguza mabalali...hehehe) Lakini ndo ivyo wazee. Lazima tuangalia mbele. Tusione shida tu bali pia tuangalia sisi twaweza kupata nini katika huu muungano. Shida lazima zitakuwepo na kweli mmezitambua. Swala ni kuzitafutia solution sio kukimbia ukweli. Sasa Marekani nayo imeunda NAFTA. Huu ni muungano kati ya US, Canada na Mexico. Wewe nikikuuliza tatizo la Marekani kubwa si wafanyakazi kutoka Mexico. Lakini wao hawaangalii negatives...lazima tuangalie mbele.
ReplyDeleteKusema kweli dunia sasa ivi ni hii miungano. EU imekuwa na nguvu sana sasa kiasi inaacha nchi nyingi nyuma. Kuna yule bwana aliyesema kuwa Tz ni mwanachama wa SADC tayari na hatuwezi kuwa wa sehemu nyingine. Basi sasa uamuzi ndo huo. Wape tutakuwa na faida zaidi. Faida nionazo mimi:-
1. Soko litafuata wateja...na viwanda vitafuata resources...ndo wachumi watuambia ivyo. Kwa iyo labda viwanda vingi vitahamia kulipo na resources. Labda Tz
2. Nchi yenye workforce kubwa itaweza kupunguza tatizo lake la ajira, nk
Kwa kumalizia tu mimi kusema kweli ni Mkristo ninayesoma biblia sana. Samahanini ndugu zangu Waislamu kama pointi hii kama itawaboa lakini mimi binafsi naamini katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana inapoongelea kuwa na One Currency na One Leader (Ufunuo wa Yoh 13). Katika kitabu inaongelea kununua na kuuza bidhaa, alafu ndo inaongelea iyo alama ya 666.
Kweli taratibu tunaelekea huko na sio kwa kulazimishwa bali ni kwa idhani yetu wenyewe.
Open to criticism....
Nakubali kukosolewa jamani...
Mtoto
Hi Kakuru,
ReplyDeleteInaonekana unayo insight nzuri ya watanzania na ukarimu wao.
Technique ya kumnukuu Nyerere is almost guaranteed to be a winner, or is it ?
Hata hivyo ,Hauhitaji kuwa na mvi kichwani ama kuwa msomi wa mido skuuli kuukumbuka muungano wa kwanza wa EA .Jinsi ulivyokuwa na jinsi ulivyo wanufaisha kakazetu wa kaskazini mashariki na magharibi.
Hii ni bila kusahau kilichouvunja muungano huo.
No prize for guessing why the cold feet then Kakuru ehe ?
However sisi tumesomea kwenye shule ya 'umoja ni nguvu' na tunalijua fika hilo.
Tunachohitaji hapa ni assurance kwamba what happened then wont happen again.
After all we have enough fisadis for one infertile land and are more than happy to share them with you if have to.
Pili M7 aachie ngazi kwa demokrasia na amani.(tusingependa kuungana na 2nd Mugabe by any chance)
Kama ambavyo kabila la rais jirani yetu wanavyotakiwa kujifunza kuishi na wenzao kwa amani na kwa kushirikiana. We have seen this enough time .
Karibu tena Bongo land K
Mr Dar
Hi Kakuru,
ReplyDeleteInaonekana unayo insight nzuri ya watanzania na ukarimu wao.
Technique ya kumnukuu Nyerere is almost guaranteed to be a winner, or is it ?
Hata hivyo ,Hauhitaji kuwa na mvi kichwani ama kuwa msomi wa mido skuuli kuukumbuka muungano wa kwanza wa EA .Jinsi ulivyokuwa na jinsi ulivyo wanufaisha kakazetu wa kaskazini mashariki na magharibi.
Hii ni bila kusahau kilichouvunja muungano huo.
No prize for guessing why the cold feet then Kakuru ehe ?
However sisi tumesomea kwenye shule ya 'umoja ni nguvu' na tunalijua fika hilo.
Tunachohitaji hapa ni assurance kwamba what happened then wont happen again.
After all we have enough fisadis for one infertile land and are more than happy to share them with you if have to.
Pili M7 aachie ngazi kwa demokrasia na amani.(tusingependa kuungana na 2nd Mugabe by any chance)
Kama ambavyo kabila la rais jirani yetu wanavyotakiwa kujifunza kuishi na wenzao kwa amani na kwa kushirikiana. We have seen this enough time .
Karibu tena Bongo land K
Mr Dar
Unajuwa kunavitu vingi ambavyo watu munaweza kujifunza kutoka kwa wengine na kila siku bado unatakiwa kutumia akili yako kabla hujachukua, na ndio maana huo unaitwa ushauri na sio amri.
ReplyDeleteKuna katoto kamoja hapa kanasema kuhusiana na habari za cameroon. jaribu kuongea na jamaa kubwa ya wacameroon watakuambia athari ambazo wamezipata ukilinganisha na faida.
chukua mfano wa jumuia ya ULAYA nadhani wengi wanapenda kuiona kama kioo. just fuatilia what is happening? wamekataa treaty marangapi? pia ongea na wananchi wa nchi kama Uingereza, wajerumani, wafaransa. wote wanalaani jinsi wanavyojikuta ndani ya nchi zao wanakosa key benefits kama ajira na maslahi kwasababu ya EURO. waingereza mpaka leo hawataki kutumia euro kwasababu ya maslahi yao. Uingereza na ujerumani zinawalaumu wapolish na wahamiaji wa ulaya ya mashariki kwamba wanavamia uchumi wao na prediction ya population mpaka 2020 inaonesha crisis. UNAJUWA MTU MZIMA ALII KWA SAUTI LAKINI UTAMJUA TU.
just imagine walivyo wahutu na watusi hivi unadhani tukiwa nao hapa watabadilika nini? mbona hata wakiwa wakimbizi walikuwa wanatwangana nchini mwetu na kuwaua ndugu zetu?? wakenya hata majuu wanatambuana kwa makabila yao, mkikuyu na mluo. pia kazi wanapeana same na wakija east africa watafanya same.
By the way sio lazima tuwe shirikisho ndio tufanye biashara pamoja. hapana tunaweza kuwa na soko la pamoja kama tulivyoanza ambapo ushuru wetu tunaudhibiti katika east africa standard, but kila mtu na kwao. Tunaweza kuwa na pasport za east africa ambazo zinatuwezesha kuingia popote but sio kuweka makazi huru na kufanya shughuli za ajira bila sheria za nchi husika.
well namalizia kwakusema kwamba waganda wamemshindwa museven, warwanda na warundi ukabila na sawa kwa wakenya. hawatabadilika na ukitaka kujaribu kuchanganya maji na tope ukadhani vitamix milele basi wewe ni mpuuzi.
Lets be friends, wakigombana tunawaamulia, tukigombana watatuamulia na sio mengine.
nihayo tuuuuu.
G7
UK
Kakuru unasema kwenu kuna ardhi ya kutosha si kweli,sehemu kubwa ya ardhi ya uganda ambayo ni nzuri ni kusini mwa Uganda,kaskazini kuna matatizo kibao si ajabu hata wewe hujawahi kukanyaga tangu uzaliwe,soma link hii uone matatizo yenu hayo na sababu za kwa nini kwenu hakukaliki http://www.theirc.org/where/page-28828228.html hii yote ni kwa sababu ya dhambi ya ukabila,Kenya wenzenu pia wakishaweza kumchagua Rais Mjaluo(Luo) waje kifua mbele kutaka muungano.Vinginevyo viongozi wetu kwa ujinga wao watakubali ushawishi wenu,lakini sisi local people hatutaki muungano wa EA.Kwani sababu zilizouangusha mwanzo bado hata moja haijapatiwa ufumbuzi.
ReplyDeleteHapo naungana na Njonjo wa Kenya aliyetamka wazi kwamba hautaki muungano na hautatokea tena yeye akiwa hai.
Wanaolinganisha mafanikio ya EU na east africa wanapotoka kwa maana EU hakuna kabisa matatizo ya ardhi kama huku kwetu,mfano ni majuzi tu mwaka 2007 Kenya ilitokea vurugu ya kugombania ardhi maeneo ya mlima Elgon ikiacha watu 150 wakifa na wengine 60,000 wakikimbia makazi yao.
Comment yangu imebase sana kwenye ardhi kwa sababu nchi zote hizi zaidi ya 80% ya wananchi wake wana tegemea kilimo.Pia ukabila ni doa ambalo hawa jamaa hawajalitibu,walitibu kwanza ndio waje kwenye muungano.Japo viongozi wetu wanapumbazwa na suala hili ukweli utabaki palepale kwamba muungano hautufai,sisi tunajua muungano kuliko wao na tunayafahamu matatizo ya muungano kuliko sehemu yoyote ile duniani,ukizungumzia nchi huru,hakuna mjinga yoyote atakaye weza kutufundisha uzuri na ubaya wa muungano,kwa sababu tayari tupo kwenye muungano na tunaona utamu na uchungu wa muungano.
Kwa kumalizia ni kwamba muungano huo wanaoulilia una athari nyingi sana kuliko faida kwa sababu mbili
1.Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi sana na ukuaji wa uchumi katika mazingira yaliyopo hivi sasa hautoendana na ukuaji wa idadi ya watu,hivyo suala la ardhi litabaki palepale kwamba ni tatizo,ukizingatia kwamba kwa sasa zaidi ya 80% ya wanaEA wanategemea ardhi
2.Suala la ubaguzi wa kimakabila pia limeonekana kwamba ni kikwazo cha maendeleo kwa nchi zote(Tanzania ina unafuu) hakuna ukweli kwamba watu hawa wakikaa pamoja eti haitatokea wakagurugana ,si kweli,na hii inaonesha ni kwa kiasi gani viongozi wa nchiza EA wanavyoligwaya hili,Kenya hawapo radhi kutawaliwa na Mjaluo,
Uganda wao wanalilia muungano wakati historia yao inaonesha hakuna hata kiongozi mmoja aliyeingia madarakani kwa ridhaa ya wananchi(bila kutumia bunduki).Si ajabu kuona ni kwa nini Museveni haachii madaraka.
Niishie hapo tu,matatizo yapo mengi mno,mi nimeongelea tena kiasi tu kuhusu ardhi na ukabila tu
In the first place I don´t understand why Mr.Kakuru is bringing this argument now. I wish angeleta pindi akiwa bado yuko Tanzania. May be angeogopa kufukuzwa nchini. Kwanza sijui hata kama alikuwa akiishi na kufanya kazi Tanzania legally. Now he is criticizing our country because he has already left. He is treating the country as a damped girl friend of his. In swahili tunasema `` Shukrani ya Punda ni mateke´´.
ReplyDeleteSo Mr. Kakuru after reaping all that, is that what you can say about Tanzania? Shame on you.
Generally I hate Kenyans and Ugandans who come to Tanzania looking for jobs, and because they can speak Swahili and have some family names resembling some of our tribal names in Tanzania, they falsely claim to be Tanzanians. Some companies knowingly they illegally employ them.
I have a good example of an Ugandan guy who claimed to be from Bukoba because his family names resembles the HAYA names; he managed to secure a job, even got a scholarship for his masters degree while in Tanzania. To be more smart he got married to a Tanzanian woman.
I have much experience of meeting Kenyans and Ugandans who come to Tanzania looking for job. It is a fact that Tanzania have more resources than any country in East Africa. Our good political atmosphere coupled by a peaceful mentality among Tanzanians make this country a good place to live. People love one another, we don´t have such a stupid and primitive caste problems like our counterparts, Kenya and Uganda. You guys, just learn from us, but we are not ready to see our freedom a and opportunities taken by foreigners.
East African community sounds like a forced marriage, I don´t give it a damn, I personally don´t need it. May be for the sake of good neighborhood and trade relations we can have it, but issues like individual state´s resources, jobs and other privileges constitutionally conferred to citizens should not be availed to foreigners, Kenyans and Ugandans.
Thanks. A CONCERNED TANZANIAN.
Mi,i mi mtanzania, na niko proud tya kuwa Mtanzania. Lakini ina niogopesha kuona watanzania tunaanza kuugua ugonjwa wa Exnophobia. Ukweli nikuwa, just kwa sababu tulikuwa wajamaa basi tuna haki ya kuwa suspicious wa kila kitu, nadhani itafikia mahali sisi watanzania tutakiogopa hata kivuli chetu na kuwa na wasiwasi nacho. Naamini Confederation of East Africa, ndio solution pekee ya kuweza kuzifanya serikali zetu kuwa accountable kwa kila jambo watakalo lifanya. Michuzi, Na kua advice kuna comments ambazo jamaa wana zitoa ni za kujenga chuki, ingekuwa vyema uka zichuja comments za namna hii ili Blog yako iwe kweli Blog ya kifamilia. Nita muonyeshaje mtoto wangu blog ikiwa ina ruhusiwa kujaza hates comments. Pili English, English wadau wana haribu lugha ya wato vibaya mmno
ReplyDeleteKuna mada moja iliwekwa kwenye Blog hii inasema kuwa Watanzania "eti ni waoga ku-take chances....." Hivi ninyi mnaoandika tuuuuu kila kukicha huwa mnatafuta statistics za ku-back-up your statements? Akaendelea kusema kuwa "....eti hata ukiwapa wa-Tanzania chances mpaka uwasukume.... inasikitisha sana....."
ReplyDeleteUnajua wewe Kakuru kama ulisoma Tanzania, ukafanya kazi Tanzania, ukaishi Tanzania isiwe tabu ya kusema kuwa "......tunaogopa... challenges..." we (Tanzanians) are able and very competitive... na tunauwezo wa kufanya kazi popote pale kwenye ulimwengu huu...
Tunafikiria kama "....ukimkaribisha mgeni ujue umefungua milango....nzi, mbu, vumbi, harufu mbaya vyote vitaingia ndani...." so who would like to have all those mess kwa nyumba yake????
After all Mr Kakuru... hebu tuambie kwa maneno ya kawaida sana tu ".....what is the contribution (japo moja tu....) of your country kwenye confederation kama sio kuwaamulia vita kati yenu na huyo Kony...."
Jamani kama Tanzanians wameona haifai ujue "kwao haifai...." watakapoona inafaa wataingia kwenye confederation in full force...
Naomba ujue kuwa we are NOT WORRIED OF ANY COMPETITION..... IWE.... AJIRA, MASOKO, ELIMU... sasa msitulazimishe kuingia kwenye mashindano....
Mdau kutoka Iraq - Baghdad
BWANA KUTOKA UGANDA,
ReplyDeleteSIS WATANZANIA TUNA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, BADO UNA HITIAFU NYINGI, TUNA UHUSIANO MKUBWA KATI YA BARA NA VISIWANI LAKINI MPAKA LEO WAZANZIBARI WANALALAMIKA ,,BASI NI BORA TULIMALIZE HILI KABLA YA KUANZA MENGINE.
PILI HUU MUUNGANO WA EA ULIKUWEPO , UKAVUNJIKA , BASI TUJIFUNZE KWANZA KWA NINI ULE WA MWANZO ULIVUNJIKA..
HAKUNA ANAYEKATAA KUWA UMOJA NI NGUVU, LAKINI LAZIMA UWE UMOJA ULIOUNDWA VIZURI LA SIVYO TUTARUDIA MAKOSA.
KAMA WALIVYOSEMA WASEMAJI WENGI, UGANDA NA KENYA BADO ZINAMATATIZO MENGI, UGANDA NI KAMA NCHI TATU KATIKA NCHI MOJA, KENYA NI KAMA NCHI MBILI KATIKA NCHI MOJA, BASI SAWAZISHENI HAYO HALAFU MTAKUWA NA NAFASI NZURI YA KUJADILI HAJA YA KUUNGANA,
HALI KADHALIKA TANZANIA , YAPO MAMBO AMBAYO NI VIZURI YAKAANGALIWA KABLA HATUJA INGIA KWENYE MUUNGANO.
MATHALAN, JE VIJANA WETU WA ELIMU NZURI KUWEZA KUPATA KAZI KATIKA SOKO HURU LA EA, JE VIWANDA VYETU VINA UFANISI KUWEZA KUSHINDANA NA WENZETU NA MENGINE MENGI,
HIVYO KWA JUMLA NI JAMBO LA HATUA KWA HATUA.
AHSANTUM
Sasa nitasema kama Nyerere Mpende msipende muungano lazima utakuwepo! (lakini yeye alisema Mkapa atakuwa rais wenu) Ipe miaka 20 tu...lazima EAC itakuwa inadunda! Unajua hapa ni kama kumpeleka mtoto shule mara ya kwanza. Ataanza kwa kugoma goma alfu taratibu atazoea na kupenda ile mbaya! Toeni mifano sijui ya failure ya EU...lakini EU is seen as a success. Wewe hata tajiri akijenga nyumba ukiangalia kwa nje utaisifia...ndani yeye bado anaona nyufa. Sijui umenipata G7 hapo.... Lakini sifa bado zitafurika kutokana na uzuri wa hiyo nyumba uonekanao kwa nje. Ninachosema ni kuwa hamna kilicho perfect. Hata siku moja huwezi kufaidisha/kufurahisha kila mtu. Wa EU wengi watapiga kelele sana. Their currency has surpassed the dollar (US). Ujerumani hii wanaita Autobahn inajengwa na funds kutoka EU. Not everyone sees the success. People measure success differently and most of the times is in an individual scale. Katika mfano wako...Wengi wanapima success on them getting employed. How sure can they be that they would have had jobs if their country was not part of the EU? U always look at the majority bwana! How many jobs the economy as a whole is creating or losing. And I would argue EU is a success! It does so much more than what u see publicly. Wewe unaongelea huu mkataba wa Lisbon kukataliwa?
ReplyDeletemtoto
Sawa bwana Kakuru..manake naona jamaa wamejieleza unatuona wote Mazuzu...sio?
ReplyDeleteUkweli utabaki pale pale...jitahidini kubadilika,nimefurahi sana kuwa wewe binafsi umeishi Tanzania na umeweza jionea tofauti zilizopo kati ya Kenya na Ugandan people kwa watanzania...ni jamii tofauti..tulijifunza kwenye muungano wa kwanza,ambao ulikuwa na maedeleo mazuri kupita kiasi..nani alikuwa chanzo cha kuvunjika kwake...????
sisi tunajua na kuielewa hali yetu ya kimaisha na kimaendeleo,nawe pia unaifahamu..maendeleo hayaji tu kwa kuwa na pesa au utajiri..sababu lukuki pia zinatakiwa,chache ya hizo ni amani, utulivu,kuaminiana, kuvumiliana, na kukubali hali halisi...mtatuambia nini kwa yale yanayotokea Kenya (kwenye siasa) na hali ya utulivu iliyopo Uganda...hauoni tofauti na Tz?je tz ndo iwe kimbilio lenu baada ya kugundua kuwa kwenu ajira zenda kwa kufuata ukabila na udini?
jisafisheni kwanza ndo mje kula na sisi, hali ya Uganda ilivyo haiko mbali na kuwa ya Mugabe na Zimbabwe..una/mnalijua hilo? Kenya nako ndo hivyo huyo mzee hataki na madaraka yake,kisa eti katumwana Kabila lake asiachie ngazi...!!!!
utatuambia nini hapo? achaneni na sisi....
Nyaningedere
Well mie nasikitikia kwa nini watu wa kutoka jirani zetu wanang'ang'ana kutakamuungano na sie well kiuchumi wazee hatutaki kuungana na nyie kwasababu kimaendeleo kenya mna heavy industry nyingi. Vilevile kwa uganda kuna kitu gani sijui maybe mafuta (kama yapo). Kwa tanzania kumejaa natural resources kibao mkitengeneza muungano utasikia wakenya watadai kwakuwa sie tunaviwanda basi uzalishaji ufanyike kenya. Hivyobasi rasilimali inatoka tanzania inaenda kenya kuzalishwa faida wanakataka gharama zao tanzania mnabakia maskini. Uganda hali ya hewa ni nzuri investors wote watafungua ofisi zao huko haya sie tubakie na nini? Mbona hamuwaulizi UK kwanini hawajajiunga hadi leo EU wanajua kuwa watayumba kiuchumi. Kuhusu wasomi mie ni mmojawapo wako wabongo kibao wasomi si hoja ya kweli hivyo mie Mr Kakuru sikubaliani nawe na hoja yako kwamba tunafaidika kwa lipi?
ReplyDeleteAcheni zenu kae kwenu hatutaki rasilimali zetu ni zetu. Tanzanite yachimbwa tanzania Kenya ndo the biggest supplier si wizi huo????
Hello Mr.Kakuru! Osibyetano Ssebo?
ReplyDeleteFe abbe Tanzania tubtya nyonyonyo mwe abe Buganda ne' Kenya! Mr. Kakuru to my opinion I don't fear Ugandans or Kenyans at all especially on the issues of competitiveness in education, jobs, language, etc. But my biggest worry when we join you guys is the political instabillity of your countries. Since I was born, I have been hearing stories of war in Uganda till now when I'm writing this e-mail, why? e.g Joseph Kony has refused to sign the peace agreement! our fellow Kenyans same thing, tribal tensions are there to stay! Always I hear tensions btn Kikuyu vs Luo, Kikuyu vs Kalenjin, etc Worse enough when one is in power in either Uganda or Kenya getting him out of power there must be bloodshed! Take a current example of M7, and he has already started 'campaigning' to become the first president of the Federation, lets take an example M7has become the president of the federation, when his term/s ends will he leave peacefully or will we have to take up guns and fight him out? Some opinions you have read here seems to come from angry Tanzanians, have you asked yourself why? Why Tanzanians are angry with you guys? I will give other reason apart from what I have mentioned, it's because of the attitude of some Ugandans and Kenyans towards Tanzanias, some few guys from your countries tend to show openly that they are better than Tanzanians and worse enough they do that while they are in Tanzania,this is high level of disrespect! what do you expect? ofcourse hatred if not xenophobic elements takes place slowly. I'm a Tanzanian and I have been around the world almost in every continent, I strongly bet that my fellow Tanzanians are very polite people! but that does not mean that they can be abused/disrespected and stay quite! So my dear friend Kakuru, first stabilise your political system, change your attitude and show respect to Tanzanians then will sit on the same table to negotiate the terms of Federation.
Mdau,
Scandinavian countries.
KWANZA NA MJIBU NDUGU YANGU ALIOKOSOA WAGANDA KWAMBA WAMESHINDWA KUTOKA KWENYE UFALME WA MUSEVENi,hata sisi watanzania tumeshindwa kujigomboa kwenye ufalme wa ccm.
ReplyDeleteSASA NARUDI KWA MGANDA,KITU KIKUBWA TUNACHOKATAA MUUNGANO NI KWASABABU SISI WAOGA WAKUPIGANIA HAKI YETU PALE TUNAPOTAKIWA.VIONGOZI WETU NDIO WALIOSABABISHA UMASKINI WETU HUU NA KILA TATIZO LETU.VIONGOZI WETU MALIMBUKENI WALISOMA KWENYE MFUMO WA KUKALILI NDIO MAANA NCHI YETU YENYE UTAJIRI MWINGI IMEWASHINDA NA KUAMUA KUIBA PESA HILI ZIWALINDE WAKITOKA MADARAKANI.
Sasa wewe mganda kama sisi watanzania tumeshindwa kupigania haki yetu kwa serikali moja tu ya ccm TUTAWEZAJE KUPIGANIA HAKI YETU TUKIUNGANA NA NYIYI {kenya na uganda} ? MUUNGANO WA AFRIKACA MASHIRIKI MTU ATAKAYE NYANYASIKA ZAIDI NI RAIA WA TANZANIA AMBAE MUOGA WA KUPIGANIA HAKI YAKE.
Kwahio muungano hatuutaki kwani nchi yetu bado haijapata viongozi ambao wenye uchungu wa nchi yetu na wakaweza kupigania haki zetu wakati wa muungano huo.
SWALA LA ELIMU NAWAPA HONGERA NDUGU ZANGU WATANZANIA WOTE KWA KUPIGA HATUA KUBWA SANA YA ELIMU TUOMBE MUNGU TU MFUMO WA KUAJIRI UBADIRIKE yani kutoka kwenye kuajiriana kwa kujuana kwenda kwenye kuajiriana kwa kiwango cha elimu wa vigezo vya kazi yenyewe.
Mdau mzawa
Bro Michu acha kuwajaribu wadau hapo hakuna cha mganda wala nini. Itakua jamaa tu anafanya tathmini yake.
ReplyDeleteJamani,
ReplyDeleteInaniuma roho kuona ni jinsi gani sisi Watanzania bado tuna mawazo ya kijamaa, mimi ninapinga watu wanaomshambulia huyu kijana mwenye mawazo yanayoona mbali. EA as a block needs not to wait further in joining hands with our fellow neighbours and get a louder voice towards todays world of globalisation.
Kwanza TZ is the most less fertile among the all EA countries in the region so neither of our neighbour will want our land! you can google it
Naomba niwaambie kitu kimoja hivi nchi kama Ujerumani ambayo ina kila kitu ina-export more than what it export inataka nini zaidi mpk ku-forge an economic block na vi-nchi kama Bulgaria hebu ask youself? hii tunaita as Europe wana jaribu ku-protect masoko wanaungana na vi-nchi vidogo wana-improve infrastructure halafu ili kuwawezesha kuwa na uwezo wa kununua na kwa kufanya hivyo uchumi wao unakuwa as a block.
Mungu wangu hivi naomba kuuliza? tushawahi kupigana hata mara moja na hawa majirani zetu (ukiondoa Uganda ambayo inatushukuru kwa kumuondoa Nduli)? mbona wao wana imani nasi?
Naomba niwaambieni siku zote maskini wa Kijamaa/kikomunisti, anamawazo ya kupinga maendeleo kisa hawezi ku-fit na maendeleo hayo na hafikirii kwamba anapaswa kuji-switch aendane na hayo maendeleo. Nawapa mfano, hivi karibuni wanataka ku-float shares za NMB kwa wananchi, kuna mwandishi m1 wa Daily news aliandika kama NMB ina tengeneza faida kwa nini iuzwe na pia akasema ikiuzwa watu wa vijijini hawatakuwa nauwezo wa kununua kwa hivyo isiuzwe! sasa nauliza hivi kweli leo hii tuko kwenye Free Market economy tunafikra kama hizi? tuko in a right direction kweli?
Mtu mwenye fikra za kitajiri na busara angesema hivi pamoja na kuwa Benki ya NMB inatengeneza faida serikali inapaswa kuiuza kwa vile mpaka sasa haieleweki hizo dividends zinazoenda kwa serikali kila mwaka zinafanya nini? Serikali hii kuendelea kumiliki makampuni ni kuipa mianya ya kufisadi mapato . Nchi zilizoendelea serikali zinajihusisha na kutoa huduma tu kujenga barabara, afya, usafiri, majia na kadhaliak !Pili hata kama maskini hataweza kununua hizo share basi ataajiriwa na huyo atakayenunua hizo hisa akiwa Mtanzania mwenzake. Maskini hawezi kumilikishwa kampuni hatamudu jamani. Kinachohitajika hawa wasiojiweza wapewe basic needs kama foundation ya wao kuja kuwa na uwezo baadaye.
Kurudi kwenye EA topic, nawaomba tuache kufikiria ya kuwa sisi tuta-loose tuache kutojiamini, na tuache kuchukiana hata sisi wenyewe hapo Tanzania kuna ukabila na matabaka na ukada wa chama kupata deals serikalini hata kama unavigezo, angalia jinsi Watanzania wenye uwezo wanaponyimwa tender kwa vile hawatoi Hongo, sitaki kuingia kiundani hapa.
Naombeni niwaase tunahitaji ushindani ili tuamke, unapomuona Mkenya au Mganda anakuja kufanya kazi TZ, furahi kwa vile anakuja na ujuzi mpya jifunze kielimu tuko nyuma mbali ya Baba wa Taifa kutaifisha shule badala ya kujenga mpya sijui alisaidia au aliharibu wewe unalo jibu!! matokeo yake tunaona enterprenuer wakubwa kama wa kina Sameer group wako Kenya leo au Mehta Bro.s wako Uganda hawa wote walikuwa TZ kwa vile ikumbukwe towards Independence ni Tanganyika tu walikuwa wana uwezo wa kufanya biashara kwa vile ikumbukwe Waingereza walikuwa ni waangalizi kwetu na sio Wakoloni parse huko Kenya na Uganda walikuwa wanabaguliwa! majengo yote mjini kuanzia ya NHC, IPS building, Tambaza, Zanaki yalikuwa yao na tukijiuliza kuyataifisha ilitusaidia au ilitulemaza kwa kutaka urahisi badala ya kufanya hime kujenga shule zetu na makazi wewe unalo jibu! Vyama vya ushirika viliuwawa kwa makusudi kwa vile ilionekana haviendani na sera za kijamaa kwa hiyo lazima uangalizi wa karibu wa serikali, sasa hebu tujiulize kama KNCU iliweza kujenga Ushrika College na hata KCMC Hospital au Mawenzi tower leo tungekuwa wapi kama serikali isingekuwa na fitna za kijamaa na ku-support na kuhimiza vyama vingine vya Bukoba na Mbeya viige mfana na pia mikoa mingine zaidi kufanya hivyo.
Pili tujiulize kama hatuna skilled people kwa nini tusiajiri wao ambao wako cheap na si South Afrikans au Westerners. Tuangalie UAE inajengwa na wageni kwa hiyo sioni ubaya tatizo tunaogopa ushindani na hatuwezi kuendelea na madudu tunayofanya makazini. Lazima tupate ushindani.
Mbali na hayo tusife moyo bado tuna watu wanaoweza ku-compete na big businesses in Kenya na Uganda in case ya Integration, foristance Technogroup, ZEK group, Ernst & Youngs Tanzania, Precisionair, Sumaria group, IPP group, serengeti Breweries, Bhakhresa Group, Quality Group, Azania group, Mkono Advocates na wengineo wengi ambao ni waTanzania tukiwa kwenye Community watauza huduma na bidhaa kwa watu 120 mio. na sio 40 mio na pia watakuwa na uwezo hata wa kuexpand na kushindana na makampuni ya Sauzi, Nigeria na hata Egypt. lets look far watu kama hawa ni Watanzania na wako tayari kutu-represent kama TZ brand hebu ona juzijuzi hapa tumeona makampuni 1200 ya TZ yamejisajili na the New EA Quality Brand hii ni achievement tumejiandaa vya kutosha. maswala yao ya vita si tatizo la kusema tusiungane nao kuhusu ujambazi mipakani si wao tu wanaiba hata sisi huiba kwao mbona hawa-react kama sisi tuache kuwa emotional bila sababu za msingi na pia hakuna Mkenya au Mganda anaeiba bila ya kushirikiana na Mtanzania. hii ni kazi ya Polisi jamani. Nawapa Mfano France, Uk, Germany na Spain wamepigana mara ngapi hebu tujiulize kila Europe civilization history utaona wamepigana mara mia kidogo lakini leo hii wameungana na wanakula matunda.
Ndugu zangu tuache uwoga, tupiganie asasi za serikali zijisafishe na pia tupiganie serikali iuze kila kampuni inayomiliki kwa wananchi tukianzia na ATCL kwa vile kinachoendelea sasa ule ni mradi wa watu kula pale! Angalia jinsi mikataba mibovu inavyofanywa jamani geuzeni macho kwenye Oil Exploration licences, mtatoa machozi! Tukiacha Ufisadi tuingie kwenye EA tukiwa Most Efficient and clean member. Tutakula matunda bila tatizo
Hime jamani lets do it now so to be able to benefit from the other sleeping African countries tukianzia na West africa. Lets create billioneers now. Lets do pamoja East africans tuache chuki hatujapigana na hawa majirani zetu jamani. ni Ukomunisti unatu-haunt us
Mdau ulioanzia na {jamani} comments yako ndefu lakini imekwenda shule mno.nakupa hongera na unaonekana msomi sio wasomi fake kama mdau wa usa tawi #1.msomi akiandika kitu unaona tofauti.
ReplyDeleteDid I read something like free movement of People? Sasa wahamiaji haramu utawapataje?
ReplyDeleteA LAND LOCKED COUNTRY IS CRYING FOR...ILI MTUMIE BANDARI BURE!
THOUGH TANZANITE YACHIMBWA BONGO KENYA NDIO WENYE TRADEMARK KWANINI WASITAKE SHIRIKISHO? TUANZE KWANZA NA COMMON CURRENCY KAMA YA SHIRIKIHO (si na sisi kaela ketu katanyanyuka au ya Waganda itatushusha?)
Mr kakuru
ReplyDeleteNaona watu wanakushambulia sana humu ndani.
Mimi ni Mtanzania na nafahamu matatizo ya jumuiya ya East Afrika mpaka ilipovunjiaka kwa sababu tu ya Marehemu Iddi Amini miaka ya 70 kama sijakosea ni 1977 na ni sababu hizo ndizo zinafanya watu wahoji uhalali wa kuundwa tena jumuiya hiyo.
kama mwanzo ilikufa kwa sababu tu ya ujinga wa kiongozi mmoja, je safari hii waganda na wakenya wamewahakikishia nini watanzania kwamba jumuiya hiyo haitafunjika.
Hilo ndilo swala ambalo watanzania wanataka kufahamu na sio tu viongozi wakurupuke na wasema tunaunda jumuiya.
Angalia mfano European Union mpaka leo kuna mambo ambayo hawajakubaliana, sasa ndugu yangu kuunda jumuiya sio mchezo wananchi na vingozi wao wanabidi wakaee na kuelimishana na kuhakikisha hakuna ncchi ambayo inamuelemea mwenzake au inafaidika sana na jumuiya hiyo kama wakenya walivyo faidika kipindi cha nyuma na kudai Mount Kilimanjaro upo Kenya na kufanya Tanzania ikose Fedha nyingi kwa sababu watalii wote walikuwa wanashukia Kenya na mpaka leo hii Tanzania inastruggle kuelimisha Ulimwengu kwamba Kilimanjaro ipo Tanzania.
Kuunda jumuiya sio kazi raisi kama unavyofiki wapeni muda au viongozi waangalie ni jinsi gani watatengeneza sheria kwa manufaa ya yote na sio kukurupuka na kuunda jumuiya baada ya siku chache inavunjika
KENGE