Wadau wapendwa,
Hakika hili limenisikitisha sana na sina pa kulisemea zaidi ya hapa.
nilipoteza wallet yangu8 tarehe 21 ikiwa na id's zangu pamoja na ATM card yangu, sasa nikaenda bank niblock account yangu. Nikaambiwa haiwezekani hadi niende polisi nipewe lost report.
Hapo bank wakanipa form ya kunitambulisha huko polisi kama mteja wao. Nikaenda police pale Udsm mlimani , wakaandika maelezo yangu then nikaambiwa inabidi niende kituo cha magomeni au oysterbay nikalipie shilingi mia tano (500) kwa sababu wao hawana mhasibu pale, nipewe risiti niirudishe pale polisi ndio wanipe hiyo lost report ili nende bank kublock account yangu na kuanza process ya kupewa ATM mpya.
Kwa kuwa ilikuwa jioni definately nisingemkuta huyo mhasibu, nilivyoenda oysterbay nikaambiwa hawana risiti zimeisha niende magomeni, nikaenda magomeni nikaambiwa risiti zimeisha niende baada ya siku tatu au niende msimbazi, (kumbuka siku zinapita sija-block account yangu hapo), mchana huu nimeenda msimbazi, nimeambiwa risiti hakuna.
Sasa nikauliza inakuwaje kwenye ishu kama hii wananizungusha hivi na account yangu inaweza kuibiwa wanasema there is nothing they can do.
I am so mad hata sijui nfanyeje, tena bila aibu polisi huyo ananiambia rudi kule mlimani wabembeleze wape chochote wakuandikie lost report ndo hali ilivyo" can you imagine?
Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 nimetembea vituo vyote hivyo vya polisi na hakuna nilichokipata, sasa jamani kwa hali hii mtu anafanyaje? Je hii nchi haina kabisa utaratibu wa maana zaidi ya mlolongo mrefu usiokuwa na kichwa wala miguu ukitoa mianya ya rushwa?
Na sasa ni lazima kuwe na process ndefu namna hii kwenye huduma ambayo ni haki yangu?
Mdau Mwenye Usongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2008

    Na mimi nilipoteza kadi yangu ya CRDB tangia 2003 mpaka leo sijaifatilia baada ya kukumbana na sokomoko kama lako. Kuna laki 2 zangu huko bado. Inaudhi mno kwamba unapoenda kujiandikisha benki hauambiwi upeleke taarifa ya polisi, lakini unapokwenda kuripoti matatizo ya account yako unaambiwa uende kwanza polisi.

    Nchi zilizoendelea ukipoteza ATM ama credit card yako hakuna haja hata ya kwenda uko benki kuripoti icho kitu. What you need is just to call the credit card/atm card issuing company and ask them for a replacement card. You will get the new card in 2 business days.

    Kwanini kitu hiki kisifanyike TZ? - Sina jibu la kukupa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2008

    baada ya kusoma hii msg imenikumbusha mwaka 2004 nilikubwa na tatizo hilo, mie cha kunishangaza baada ya muhudumu wa benk kuniambia niende police hakunipa hata hiyo barua, nafika police kujieleza police anasema WEWE HUJUI SHERIA UNATAKIWA UJE NA BARUA YA BENKI, then kwa ufupi nikawa naambiwa nenda hapa pale usumbufu mtupu,baada ya kufanikisha kupata hiyo barua kurudi police ETI POLICE ananifanyia interview swali lake ULIPOTEZA VIPI KADI , NILISHANGAA SANA, ARE THEY for real!!!sasa issue ikawa kuchukua pesa nilikwenda na pasi yangu uwezi amnini walikataa kunipa pesa, now nimeamua sina tena ac ndani ya tz, bora niweke nje.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2008

    Benki ndiyo wa kulaumiwa, block account kwanza then mengine yatafuata, mabenki mengi ya Kibongo yanamuona mteja kama ni mtumwa!!! Na hii serikali yetu toka ianze kukumbatia mafisadi basi na mapolisi nao wameamua kuwa mafisadi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2008

    Pole mdau, haya ni mambo ya aibu. Kuna shida gani kwa benki kuizuia kadi ya zamani na kukupa mpya, hata kama inabidi uilipie badala ya kuanza kudaiana taarifa za benki?
    Wenye mabenki mnasikia kilio cha wadau? Rekebisheni hili!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2008

    inabidi uwe mwangalifu, sasa bank na polisi ni wapi na wapi jamani bongo. Benki inapofungua akaunti yako inatakiwa iwe tayari imeshakutambua kwa vitambulisho sasa kwenda polisi ya nini tena? yaani ku-block ckadi tu? Tuna safari ndefu..yaani mtoni hata benki kwenyewe huendi. Unaiua simu tu na kuzungumza na mtu au fuata messages kuripoti kadi yako imeibiwa..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2008

    HALAFU NDO MNASEMA BONGO TAMBARARE! I DON'T THINK SO

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2008

    This is rediculous, kweli Tz bado kuna njaa kubwa namna hii? what is 500 sh.??? Na hao wenye mabenki ni lini mtaanza kuendesha benki zenu kitaalamu muachane na ushamba wa Polisi ambao hawajui hata wanalofanya? hivyo vitabu vya risiti ni bei gani kiasi kwamba kuna vituo kama vinne havina? mbona Tz mnaendesha mambo kama kijiwe cha wahuni? lini tutaiinua nchi yetu hata ifikie robo ya ustaarabu wa nchi nyingine? tutaishi kishamba namna hii mpaka lini? Ndio maana wengine tunaairisha kurudi nyumbani mambo mengine hata kuyasikia tu yanatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2008

    Wewe Jinga. Lazima polisi wakuhoji umepoteza hiyo kadi ili waweze kupeleleza na kumtafuta aliye iiba kama imeibiwa au imeangukia kwenye mikono ya mtu mbaya. Halafu kupoteza kadi kunaonyesha ulivyo mzembe, Ukipewa kadi kirahisi si utapoteza tena. tatizo lingine wewe ni mjinga umezunguka vituo vyote hivyo sijui ulikuwa unatumia dala dala na nauli zimepanda kwa nini hukuwapa polisi mia tano ukamaliza mchazo. Unajua serikali haitoi risiti kwa hiyo polisi wanafanya initive zao ili kuwa saidia mnajifanya wajanja.
    Kwa heri.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2008

    Jamani unalaumu polisi bure, benki ndiyo wana matatizo, kama una vitamblisho vyako na password yako unaijua no problem.

    siku zote uangalie tatizo, polisi wameshajichokea

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2008

    pole sana ndugu..sasa nategemea response uioneshe kunako masanduku ya kura..Kila kukicha tunalalamika,ila ikifika uchaguzi tunawachagua walewale wenye sera zilizotufikisha hapa..Tubadilike waTZ na tujaribu wenye sera na muelekea tofauti.Hiyo ndiyo demokrasia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2008

    Sheria za benki za marekani na Tanzania ni tofauti.Tanzania wahuni wengi huwezi kublock tu akaunti kama wafanyavyo Marekani.Hapa hakuna hizo credit card au debit card companies usilete mbwembwe za kimarekani koko hapa bongo.Kwenda Marekani isiwe nongwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2008

    Jibu ninalo, Nenda makao makuu ya Police muulizie afande Suleiman Kova mueleze shida yako atakusaidia mara moja, akinyanyua cm tu umepata suluhisho lako. Au mpigie cm yake ya mkono alishaitoa hadharani we mpe khabari yote uone kimbembe watakavyokimbizana na matumbo yao ya rushwa watayaona mepesi kwa mbio, Tumechoshwa na uzembe uzurumwendo na rushwa za mapolisi waroho na wababaishaji.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2008

    wanachokitaka hapo ni rushwa tu.polisi rushwa,benki ukitaka mambo yako yaende express ni ujuano kama una ndugu yako mambo yangeenda vizuri tu.Hiyo ni bongo lakini kwa kweli inasikitisha.ndio maana tajiri ni tajiri na maskini,unakaa na umaskini wako.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 17, 2008

    HUKU WALA AWANA AJA YA KUKUONA UNAPIGA SIMU TUU ,KRRRI KRRII HALOO CARD YANGU IMEPOTEA OK ,TUNAKUTUMIA NYINGINE KATIKA SIKU SABA OK,OK

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 17, 2008

    Yahi ndio mjue kua TZ bila rushwa haiwezekani

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 17, 2008

    Pole. Kulikuwa hakuna uwezekano wa kutoa hiyo 500 polisi upewe hiyo loss report then ufuate hiyo risiti siku nyingine? Maana yaweza wewe ukawa tatizo kwa kudhani polisi anataka rushwa, pili mimi nimeshuhudia watu wengi sana wakifika polisi hawana lugha ya ustarabu sana wanadhani polisi wote ni wala rushwa kwani unapokuwa na shida nyeti kama hiyo yakubidi uwe mpole, uliza taratibu na alternative kama hizo za kufuata risiti baadae natumaini inawezekana lakini your first appearance hapo kituo.Pole sana. Lakini endelea kufuatilia usilalamike sana hakuna msaada nadhani umeona comments za hapo juu walipata the same problem three years back

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 17, 2008

    Nashukuru kwa fundisho hilo kuwa nitunze kadi yangu la sivyo nitapata shida kama hiyo. Pole na asante

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 17, 2008

    Bongo tambarare!
    Uliepata tabu hiyo sorry sana lakini kwetu huku bara aaah! Ukienda polisi risiti kibao 10 working hours, dakika unashughulikiwa unapata ripoti yako unabaki na benki yako.

    Kila siku nawaambia acheni kubanana huko Dar njooni bara maji yapo na si ya chumvi hamsikii.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 17, 2008

    Kweli nimeamini hata mambo ya kijinga yana msemaji wake! Sasa wewe anon wa July 17, 2008 6:27 AM ndo unataka kusemaje? Mijitu mingine nadhani bongo zao zimejaa MAKAMASi tu! State failure ni pamoja na state organs kushindwa kufanya kazi zake, haiwezekani risiti ikakosekana katika vituo zaidi ya vinne. Mheshimiwa MWEMA una kazi nzito!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 17, 2008

    kama maelezo ya mtoa mada ya sahihi, kamanda Mwema unadhani falsafa yako ya "polisi jamii" itafanikiwa kwa pace unayotaka?
    kumbuka NIPA NIKUPE

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 17, 2008

    Hebu tutajie hiyo Benki tuanze kuishughulikia kupitia vyombo vya habari.You should have reported this thru this blog much earlier.Hiyo ni Benki gani ambayo bado ina operate ki 16th Century!You dont need to tell us the bank branch.Polisi usiwalaumu bure,huu ni uzembe wa hiyo benki,tungependa kuijua!Maana tatizo hilo leo wewe kesho yeyote yule laweza kumfika.Sometimes could be tha bank staff themselves are frustrated to the gutts!Who nows their 'Takeaway!'.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 17, 2008

    Pole sana mdau. Tatizo nilionalo mimi katika hili sakata ni tabia ya mabenki ya Kitanzania kukopi taratibu za kibenki za enzi hizo (chama kimoja), ambapo shughuli za kibiashara zilikua zinaendeshwa kichama. Suala la kuomba barua kutoka polisi ni mbadala tu wa kukuomba kadi ya chama enzi hizo.

    Enyi mabenki jaribuni kwenda na wakati. Mie sijajua kwanini hadi sasa NBC wanataka balance sheet kutoka katika ATM kama unataka kudraw pesa zaidi ya kiwango kinachopaswa kuchukuliwa katika ATM (namaanisha unapopaswa kuchukua pesa kupitia mhudumu wa benki - bank teller inayoendeshwa na binadamu).

    Pia hili sakata limenikumbusha pindi nilipotaka kujiunga na huduma ya internet banking. Baada ya kukamilisha masharti yote nikaelezwa kurudi baada ya siku 7 za kazi (ilishindikana kuwashawishi kupunguza idadi ya siku, ingawa niliwaeleza kua nilikua na safari ya muda mrefu nje ya nchi). Niliporudi benki baada ya hizo siku 7, nilizungushwa tena kwa wiki nzima, tena hii ilikua ya njoo kesho kila siku (ni bahati tu kua safari yangu ilihairishwa kwa wiki mbili, otherwise...).

    Kichekesho zaidi ni pale mhusika wa internet banking aliponiambia kua kitengo chake hakina uhusiano na technical department na hivyo hawezi kukadiria ni muda gani watachukua kunipatia huduma hiyo. Inasikitisha sana... Ilinibidi kwenda huko technical department, nilipofika huko nikaambiwa kua mteja haruhusiwi kufika katika hicho kitengo, na nikileta ubishi nitaripotiwa polisi.

    Baada ya hapo taratibu ziliharakishwa kidogo baada ya kuona nilikua nahitaji haki yangu kwa kuwasukuma.

    Samahani wajumbe kwa huu waraka mrefu, ila hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu. Inatupasa tuibadili.

    Ignorant, Jeremani

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 17, 2008

    weweeee! acha kabisa.
    Police siyo wa mchezo. Rushwa kwanza, huduma baadaye. Anonymous mmoja anasema eti inategemea na first impression ulipofika kituoni. Nadhani customer service ni kitu muhimu irespective of atakuja vipi. Mbona madaktari wangetuua wote kama si uvumilivu?
    Jamaa yangu alipata ajali Shekilango, trafic alikuja na kuwashauri waelewane ili aliyemgonga amsaidie kutengeneza gari yaishe. Baadaye jamaa aliyemgonga akampigia simu kumuambia ameona aache tu traffic aendelee na kesi kwani yeye hana hela. Kufika traffic mbona kibao kimegeuka. jamaa yangu alidaiwa kuwa yeye ndiye mwenye makosa na amlipe huyo aliyesababisha ajali. Vipimo vimebadilishwa na michoro tofauti.
    Police si watu.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 17, 2008

    Kuna mtu mmoja mjinga kama wewe alipoteza kadi zake na bahati mbaya zikapokelewa na vibaka. walipoenda kwenye mission zamcargo wakadondosha hizo card. next day polisi wakamkamata kumuhusisha na wizi wa zamcargo.
    Alikataa lakini jamaa wanafacts pale. nayeye hakuwa ametowa taarifa polisi,akabaki kulaumu kama wewe.
    Munanusuriwa munatia kelele, but bank huwa wanablock account na kukupa ingine just baada ya kuwapa polisi report na hakuna mizunguo kama unavyodai. kuhusu miatano comeon.. yaani wazembe kama wewe wasipotoa hizo miatano watajifunzaje kufanya kazi? halafu hujuwi kwamba kwakufanya hivyo umechukua paper na time ya polisi pale...
    nadhani wapo sahihi, kama hutaki kutoa mia tano, then tunza kadi zako vizuri..

    G7
    UK

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 17, 2008

    anonymous 12:10 pm.G7 UK
    wewe unaleta utani wakati jamaa yupo serious na tatizo. Kama huna mchango nyamaza. Jamaa hajasema amekataa kutoa 500 polisi. Alichosema ni namna anavyozungushwa kulipia hiyo 500. Police wanachotaka ni nini kama siyo rushwa? Of course wording zako zinaonyesha wewe ni mtoa rushwa mzuri. Hongera kwa kuwa mtoa rushwa ila sisi hatutaki. Kuwa Uk si sababu.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 17, 2008

    huyo anon wa July 17, 2008 6:27 AM, naona kadata! Wewe nani kasema serikali haitoi risiti? Na kwa nini atoe rushwa kupata haki yake? Ujinga kama huu ndo unaturudisha nyuma. Kila mtu afanye kazi yake kwa haki. Tatizo sisi twapenda sana kutumia nafasi zetu za kazi kudidimiza wenzetu. Process zinafanywa kuwa ndefu kweli bongo kwa madai wanaongeza efficiency kumbe ndo wanatoa nafasi za wajinga. Education system za bongo zahitaji kubadilika watu wajue kutumia nafasi zao za kazi kuleta maendeleo sio kupata cha ziada. Sijui lini tutaelewa hilo?! Wewe fanya kazi yako bwana. Kuna mwingine tena ali-post juu ya tanesco kufanya ubabe. Huo ni ujinga kabisa! Inabidi kweli tukae tuone shida zipo wapi na jinsi ya kuzifanyia kazi. Yani kila kitu mpk kujuana? Wazungu wangefanya kujuana au kuomba hela kila saa kweli wangekuwa na maendeleo waliyonayo leo? lazima tuwe proud na kazi zetu, hata kama wewe ni mfagiaji. Kila mtu ana sehemu ya kuchangia katika maendeleo bila kuangalia ni kazi gani unafanya! Tutakapoweza kujifunza hilo ndo tutaweza kupiga hatua za maendeleo, ama sivyo tutabaki kuomba misaada na kusema masifadi, rushwa, magonjwa ndo maadui zetu! Adui wetu mkubwa ni sisi binafsi!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 17, 2008

    G7 kweli unafikra za ajabu. Sasa polisi asifanye kazi yake! Kweli kuna watu wa ajabu sana! Eti tunza kadi yako...hehehehe. Unaniacha hoi kweli! hizo tunaitaga FIKRA DUNI. Na ndo hizo twapambana nazo. Kweli elimu sumtimez haisaidii! Hapa kwanza kuna maswali kibao...

    1. Kwa nini polisi stations zote hizo hazina risiti? si zifungwe tu sasa.

    2. Kwa nini ulipe polisi ku-ripoti wizi? Polisi si inalipwa na serikali? Kila mtu analipa polisi anapolipia kodi. Sijui wanaelewa mambo ya public goods?

    3. Kama kweli bank inahitaji kuhudumia wateja...kwa nini isiweke fomu hizo hapo? Unajaza, wao wanapeleka polisi wenyewe. In simple terms its called CUSTOMER CARE! hii itarahisisha mambo na kubana any loopholes za mtu kutumia hiyo kadi na rushwa kwa polisi.

    4.Piga simu kwa hao waliotoa namba zao uwaeleze kuwa polisi stations zao hazina receipt book! Mtu unanyimwa kutumia hudumu yako kisa polisi haina risiti. Kweli umaskini ni shida sana!! Alafu kuna inconsistency hapa na haya mahitaji yao...wewe umepoteza kadi ya benki...hiyo hela utatoa wapi kuweza kulipa polisi? Kama sina hiyo mia tano cash...ndo imekula kwangu au vipi? Why cant they make it easy for wananchi jamani? Unajua bwana, maendeleo ni hivi vitu vidogo vidogo viwezapo kufanya kazi kwa makini, sio kujenga mabarabara au magorofa ya NSSF, nk. Those are results lkn sio maendeleo!

    mtoto

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 17, 2008

    Nimecheka saaaaaaaaana baada ya kusoma comment ya anon wa July 17, 2008 8:42 AM.

    Kwahiyo kama marekani wanafanya vitu vizuri sisi kama watanzania hatupaswi kuvi-copy? Wapi na wapi ndugu yangu? Au na wewe ndio mmojawapo wa watu wale wanaokaa counters za benki na kuwaambia wateja waelekee polisi kufatilia kadi zao zilizopotea? What a primitive thinker!!!!

    Wenzako wanajadili namna ya kuboresha hii situation wewe unaleta longolongo.

    Nakuonea huruma. Si kosa lako. Tembea uone jinsi wenzio wanavyoendesha maisha. Pole sana mbongo mwenzangu.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 17, 2008

    Mimi ndie niliyechangia wa kwanza kwenye habari hii. Jibu kwa anon wa July 17, 2008 10:42 AM anayeuliza benki gani tuliyopata tatizo hili ni MAKAO MAKUU YA CRDB pale opposite na posta mpya.

    Ni ajabu kitu kama hiki kutokea kwenye jengo ambalo lina ofisi ya mkuu wa benki ya CRDB. Ni aibu!!!!

    Mabenki inabidi wabadilishe taratibu za kizamani za utendaji wa kazi. We are now in the 21st century. Sheria na taratibu za kibenki zinazofuata bureaucracies za ki-20th century hazi-make sense kwenye karne hii jamani. Bwana Kimei, we know you can solve this issue scientifically.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 17, 2008

    anoon wa July 17, 2008 12:10 PM; Kama mtu umeripoti umepotea kadi yako then why polisi wakukamate kadi yako ilipoangushwa kwenye huo wizi? Kuna many means za kukamata wezi, kama vile finger-printing, mahojiano, etc. Hiki kisiwe ni kisingizio cha kutumia taratibu zisizofaa.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 17, 2008

    Mambo hayawezi badlika Bongo. Kama una uwezo wa kukimbia kimbia, ukiweza pigana na upigane, kama haiwezekani kubali tu upigwe bao.

    Fisadi Kiwembe

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 17, 2008

    Tanzania tubadilike jamani yaani kila kitu rushwa tu , njaa, ufisadi mwingi.Huku kwa kichaka ujinga kama huo hamna, nani anamda wa kwenda Bank kwanza. Just pick the phone and call your bank. Done deal. Hembu wabongo tuamke. na nyie kina Bank hembu acheni kunyanyasa mteja.Block the damn account na mmpe card nyingine then mwambie akariport kwa polisi. Inaniuma kweli kuona wabongo wenzangu tuko nyumaaa kwa ujinga tu. Au ni serikali ya Kikwete imeshindwa kazi kwa ujumla!! I wonder tutashindaje haya mambo huko. God bless Tanzania

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 17, 2008

    UK ni Ukonga, sishangai.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 17, 2008

    anon 12;10 g7 you are an idiot..watch your mouth..this is not a place for comedy,hili ni janga limekuta mtu. kama huna la kuandika,tafadhali ondoka haraka sana!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 17, 2008

    Nikisoma vitu kama hivi inaniuma sana na nalaumu sana viongozi kwa kuparamia "MAENDELEO" bila maandalizi. Kuna ATM machines lakini hakuna supporting strategies...Kuna internet banking laking hakuna technical supporting. Kila siku JK yuko nje ya nchi kuita wawekezaji wakati kubadilisha ATM Cards takes a month. Wananchi wanalipa kodi lakini kupata polisi report inabidi ulipie na polisi hawana risiti? Halafu bado kuna wapumbavu wanatetea polisi, wanatete bank, wanatetea viongozi. This is shameful to the nation...hatuwezi ku-compete in International play ground. Hata Burundi and Rwanda, not to mention Eritrea are better than us. Mababu walisema "Kikulacho ki nguoni mwako"...we are eating ourselves.
    nawakilisha

    ReplyDelete
  36. pole saana brother nipo ireland nimepoteza kadi bank ya ireland bank, nilichoambia nilete copy bank details only, na kweli nilipoleta mchezo uliisha nikiendelea na transaction mpaka hapo mambo walipo nitumia kadi.
    lakini kweli bongo kuna complication saana.
    nikijibu huyo tikiti maji G7
    wa UK, Huyo nimshamba fulani kwani anonyesha anaupeo mdogo saaana hawa ndio watu ambao wanabeba maboksi tu UK hata wakae miaka 30 hawawezi kufunuka sababu mtu yupo ulaya bado anaogopa shule, ndio maana anapunguza stress za boksi kwa kuwa namda mchafu wa kutukana watu hapa hii ni blog ya kushauriana pale tunapokuwa na matataizo sio the comedy tu.
    wadanganyika tuamke jamani tusichome mda kwa bullshit ambazo hazina mpango wowote.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 17, 2008

    MHHHH! MAKUBWA NIMEJARIBU KPITIA COMMENT ZOOOTE KUNA WATU WANAKURUPUKA WAKATI MWAENYE TATIZO AMJIELEZA ANAELEWEKA BADALA YA KUCHANGIA JINSI YA MNAMKANDIA KUOPOTEZA KADI NI KKAWAIDA MNAMWITA MZEMBE. ILA DUUU! SIKJUA KUNA PROCESS NDEFU NA ZAKIJINGA, JAMANI HATA BENK KUU??? NASHUKURU KWAKUNISHTUA MAPEMA NA POLE AMBAYE UMEKUTWA NA HAYO

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 17, 2008

    WEE ANOYMOUS WA JULLY 17 2008,1.56 HUJAMWELEWA ANOMOUS WA 172008,7.42 AMESEMA MAENDELEO BILA MAANDALIZI AKATOA HOJA YAKE NA KANDIKA VIZURI USICHOKIELEWA NINI??? UWE UNASOMA SIO KUKURUPUKA TENA MIMI NAONA AMEONGEA KWELI NA POINT

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 18, 2008

    Hebu mhishimiwa ulopoteza kadi irushe hii ishu yako katika ile website ya kero yangu tuone watafanyaje. Wasipofanya kitu na website yenyewe bora isiwepo.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 18, 2008

    brother pole sana,
    issue kama hii bank wangetakiwa kublock hiyo a/c on the spot kwa muda ndo mambo mengine yafuate. Pili, bro rushwa imetawala, yawezekana kabisa kwamba hizo risiti zipo ila kuzipata tabu.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 18, 2008

    Mmmmmm Mimi mpotezaji mzuri wa ATM NBC toka 2001 lakini sijawahi toa taarifa polisi labda hao CRDB sijui ingawa kwa utaratibu as a lawyer nakubali nimakosa pasipo kuthibitisha wizi wa kitu, yapo mengi yanayoweza kudhaniwa, mfano unapoibiwa wengi wanafahamu kuripoti ni muhimu kama vitu vitapatikana ili uweze kutambulika kama mmiliki halali.Tatizo hapa si mabenki wala polisi bali ni mfumo mzima wa kiutawala usipobadilika hakuna kitakacho kuwa chepesi au rahisi kubadilika.na hapo sizungumzii vyama vya siasa.Mchumbangu kapoteza nitaenda mwuliza kama amepitia utaratibu huo coz yangu ilipotea two weeks ago

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 19, 2008

    KWANZA POLE SANA, HAYO NI MAMBO YA MWAKA 47, HUKU MAJUU NA UTARATIBU WA BENKI MAHALI POPOTE DUNIANI UKIPOTEZA KADI UNAENDA BENKI KUWAELEZA UMEPOTEZA KADI NA WANACHOFANYA NI KU-BLOCK HIYO ILIYOPOTEA NA KUKUPOSTIA NYUMBANI KWAKO KAMA ADDRESS INAVYOELEZA KATIKA BENKI ACCOUNT YAKO HAINA HAJA YA POLISI, NA HAO POLISI WALIKUWA WANATAKA RUSHWA KUKUAMBIA WAZI WAZI SIKU HIZI WANAOGOPA, SASA NENDA KWA SAID MWEMA SHEMEJI YAKE KIKWETE MWELEZE ILI ACHUKUWE HATUWA KWA VIJANA WAKE, WEWE ANDIKA BARUA POLISI KULALAMIKIA KITENDO HICHO COPY KWA BENKI YAKO NA BENKI KUU, ILI WAJUWE NA WAFANYE UTARATIBU WA KUBADILISHA HIYO TARATIBU YA KIJIMA, I AM A BANKER BY PROFESSION, THAT IS A THING OF THE PAST, HATA NBC YA ZAMAI UKIPOTEZA CHEQUE BOOK, AU KITABU CHA SAVINGS TULIKUWA TUNASHITISHA OPERATIONS YOYOTE KWENYE ACCOUNT HADI PALE TARATIBU ZOTE ZITAKAPO KAMILI IKIWA PAMOJA NA BARUA YA POLISI ILI IFAILIWE KWENYE FILE NA KU-ISSUE NEW ONES KAMA KINGA KWA BAADAYE KAMA KUTATOKEA KITENDO CHA WIZI, KWA VILE KULIKUWA HAKUNA COMPUTER WAKATI ULE, KWANI ANGEWEZA KUTUMIA HATA CHEQUE BOOK ILIYOPOTEA KAMA KARANI SI MAKINI NA KUTOA PESA LAKINI SASA NI COMPUTER THAT IS IMPOSSIBLE ONCE IS BLOCKED CAN NOT TAKE MONEY OUT, WAACHE UJIMA NA TRADITIONAL BANKING, MAMBO NI YA CENTURY YA 21ST THAT IS YOUR MONEY FUNGA ACCOUNT KAFUNGUWE BENK INGINE

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 19, 2008

    mie mwenyewe niliwahikupata tatizo hilo ila mie nikisumbuliwa sana nakuwaga kauzu tena sio kawaida,mie nilienda sikuhiyi wakaniambia nikafanye hivyo nilivyokwenda nikakuta usumbufu kama huo usiokuwa wa maana,kilichofuata ikabidi niingie jikoni mwenye nikasuka hiyobarua nikaizamisha kwani hata mibarua yenyewe wanaicomferm si uzushi tu wa kijinga wanataka kuona muhuri na blabla za kizushu huyu flani na chini unaweka simbo za usalama na kichwa cha tibaigana kwisha kazi unabloku akaunti yako na fitina zote unaziblok

    mapolisi ni wazushi kwakweli hawana maana kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...