wadau wakijichana hapohapo dukani baada ya uzalendo wa kusubiri hadi homu kuwashinda. hakuna zawadi kwa mzalendo atakayeweza kukisia kwa usahihi uhondo wa samaki nchanga..

Picha ya kwanza ni mafungu ya panya yakiuzwa yakiwa ndani yandoo.
Picha ya pili Mama akiwa ameshika mafungu yake baada yakuwanunua kwa kitoweo.

Brother Michuzi.

Hivi karibuni nilitembelea Lukuledi wilayani Masasi mkoani Mtwara. Nikakuta wenyeji wa huko bado wanakula Panya na wanawapenda sana tu.

Nilipowauliza kama ni kwa sababu ya ukosefu wa nyama zingine,walisema Hapana, nyama zingine ikiwemo ya ng’ombe ni nyingi. Ila wanakula panyakwa ajili ya HAMU TU.

Siku hizi panya hawa hawaitwi tena “Yeila” au “Atoro”, baliwanaitwa MKANDA NJE kutokana na kambainayofungwa katika kila fungu ndio wanaifananinsha na mkanda.

Fungu moja linauzwa shilingi 200/= na kila fungu lina panya watano. Ifahamike wazi kuwa panya hawa wanaoliwa sio wale wanaokaa ndani ya nyumba bali hawa huchimba mashimo porini na hukaa huko maporini kwenye mashimo yao.
Yaani hawa ni panya mwitu a.k.a 'samaki nchanga'

Mdau
Perez.
mdau perez!
asante perez kwa nyuzzz hizi na picha. mie mwenyewe mate yananitoka. naendelea kukaribisha wadau kutuletea vitu kama hivi na vinginevyo toka kila pembe ya dunia isomwapo globu hii ya jamii. tuma kupitia issamichuzi@gmail.com. msisahau salamu, nondozz na kadhalika....
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2008

    WOW! nakumbuka mbali sana, unajuwa nafurahi sana kuona watanzania nasi tunaweza kujua milo yenye protin zakutsha,
    kulingana na taarifa za kitaalamu nikwamba panya wapo katika jamii ya wanyama wenye redmeet.
    Pia wataalamu wanasema wadudu kama SENENE, KUMBI KUMBI, MENDE, INZI, NA BUIBUI NI JAMII MOJA PIA.

    kwahiyo wazee kama mtu anakula panya kwake nisawa akila pia kima,mbuzi,kondoo na wanyama wa aina hiyo.
    nawale wanaokula kumbikumbi na senene wanatakiwa kula pia panzi, inzi, na hasa mdudu mnono mende.

    just kuproove mmonyeze mende bonyeee, then kumbi bonyeeee, then senene bonyeeee utaprove ninalolisema.

    nihayo tu,
    G7
    UK

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2008

    dah!!!, hivi vitu bana...acha niwaachie wenyewe.

    BooSt3D.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2008

    Lo ! hata mimi mate yananitoka. Nasikia ni watamu sana hasa hasa kwa kulia na ugali wa mhogo.kau kau kau,tamu sana .

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2008

    Tuache utani jamani. Hii mboga ni tamu kichizi yaani ni bora shinda nyama ya mbwa ama paka wanazokula wahehe. Kazi nzuri sana Kaka Michuzi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2008

    Yangu macho. Unajua kila kabila duniani wana mambo yao. Wa-Japan wanakula KILA KITU kinachotoka ndani ya bahari...wanakula KILA AINA YA MNYAMA WA BAHARINI, SAMAKI NA WANACHOITA "SEA WEED". Wanachukua mimea ya aina yote ya baharini mpaka ile ambayo inasadikiwa kua ni sumu lakini wao wanajua namna ya kula...Ukiiga....utapasuka msamba...!! Ukitaka usalama...kwa wale wanaotembelea "hasa nchi za Asia" huko Japan, Indonesia, Phillipines, Taiwan, China, Korea na nyinginezo; we sema tu ni Vegeterian..la sivyo.."UTAKULA SAMAKI NCHANGA"...!! Asanteni...!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2008

    Tobaaaaa! Alosema binaadamu wote ni sawa alikosea, alipaswa kufafanuwa usawa huo ni katika nyanja zipi?!!!

    Hivi jamani mnakula panya kwani kuku, mbuzi, ng'ombe au kondoo hakuna huko kwenu eeeh??
    Si naskia kuna bahari huko, au hata samaki wameisha???!!

    Ama kweli alojisemea mwenyewe Michuzi "kizuri kwa bata mzinga hakiwi kuzuri kwa kuku"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2008

    Mashariki ya mbali huku tunakula vitu vya ajabu zaidi ya panya wa huko Ntwara.
    Kwa hiyo big up kwa wadau wanaojichana.
    Ni vile tu unavyokifikiria kitu basi kinakuwa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2008

    Huu ni udaku wa nyama uliozidi mipaka. Njaa zinatusumbua lakini saa nyingine inabidi kufa kiume. Ungetegemea mkoa kama Mtwara uko karibu na bahari kwahiyo alternative ya kula samaki ipo. Panya sio kitoweo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2008

    Michuzi, hawa YEILA ni watamu mno. Kuna watu wanadhani tunakula sababu ya kukosa nyama. Hapana, kuna ladha ambayo huwezi kuipata kokote ambayo iko kwa hawa ATORO. Niko Dar, ila huwa naletewa wa KUONJA toka Masasi kila inapowezekana - O'C

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2008

    Mimi sojawahi kuwala lakini nawaunga mkono walao.Kula tu ilimradi sio sumu.Je walao vyura, konokono. KWA AFYA YETU

    malisa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2008

    wajaju!,njomba nindikumbikila kusu namemne!ndinganje wekunogwa namene na ugwali wa magaga,niko darisalama wa porin hawapatikani leo lajima niwakamate hawa wandani,ji kazi ifanyiki nyawe ngoja nirudi nyumbani nikawatege...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2008

    Watamu sana, inanikumbusha nyumbani, I cant wait to visit.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 24, 2008

    LICHA YAKUWA LISHE BORA NI DAWA NZURI NA INAZUIA NANIHII

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 24, 2008

    Mtwara kubwa wandugu sio kila sehemu bahari imefika, hata na hivyo walipo samaki aina nyingine za nyama haziliwi? Mi ni mwenyeji wa Masasi, nikienda kijijini kwetu wenyeji wanakula samaki nchanga kwa raha zao, hawagombwi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 24, 2008

    Kusema ukweli vyakula vinatofautiana sana unapotoka sehemu unayoishi/uliyozoea. Kuna watu hapa hapa bongo hawawezi kula utumbo wa mbuzi au kondoo...utasikia ayaaaa (keshaona kinyaa). Ila pia nilishtuka kuona watu wanakula utumbo wa kuku, ilhali wa mbuzi naona sawa.
    Niliwahi kwenda Zambia, hawa panya wanaheshimika sana kama kitoweo. Pia huko wanakula madudu dizaini ya washawasha na wako radhi uwanyime mboga zote uzijuazo ila hivi viwili usiwanyime.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 24, 2008

    Haha, watu wanashangaa panya kuliwa hizi ni jamii tu amabzo zinaona panya kama chakula kingine tu, kuna watu wanawashangaa hawa watu lakini mimi nimesafiri sehemu nyingi hapo Bongo watu wanakula panya nitaanza na Mbeya maeneo ya Umalila yaani Mbeya vijijini wanakula sana pany aho, Mbozi kwa wanyiha na Wnadali wa ileje wanakula sana panya hao wakiwa shambani wanawawinda sana na kwenda kuwachoma wakati wa kula ugali mchana, wasafwa wa mbeya wanakula sana panya wa aina hiyo mitaa yote ya uyole wanakula sana hao panya, ukija wasukuma wa kule vijijini magu na kwingineko wanakula sana panya hao, maeneo ya dodoma wilaya ya kondoa kuna watu wanakula sana hao panya ,

    Huku Nchi za watu
    Maeneo ya China mashambani panya ni chakula chao ghali sana kutokana na upatikanaji kuwa mgumu lakini wanapendwa mno panya mmoja nafikia hadi $ 40

    Huku slovakia kuna sehemu wanaliwa sana hao Panya tena kwa bei kubwa sana,

    Kule kulikokuwa na Euro 2008, Viena kuna maeneo wanafuga ng'ombe kwa wingi kuna mashamba kidogo panya wanaliwa sana na kuwidwa na watu kama vile wnawinda swala kwa hapo bongo,

    Ni hayo tu najua wengi wazee wenu wanakula sana panya huko bush mnajifanya kishangaa hapa,

    Mdau, HongKong

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 24, 2008

    Wewe Kama Misupu vipi! unakuwa kama vile siyo n-zalendo wa huku
    kusini? HAPO JUU UMEKOSEA UMEANDIKA
    MTWARA badala ya NTWARA!
    Tafadhali rekebisha ondoa hiyo M na weka N yaani NTWARA

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 24, 2008

    watu bwana mnamatatizo sana kama wewe unakula panya kivyako hakuna anaekuingilia. ila usipende kuweka makabila ya watu wengie toka lini wasukuma tukala panya???

    au umedata tafadhari sana data kivyako kwanza naona kinyaa hata kuwaona harafu unatia kabila langu wee vipi??

    sisi tunakula maziwa na ugali sio wadudu kama panya koma ukomae uwe na adabu siku nyingine usirudie.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 24, 2008

    wewe ononymous wa hong kong
    wewe ni mzushi hujatembea lolote
    naunamazoea ya kitoto kama kwenu mnakula panya basi unazani wote taratibu,

    sio watu wote waroho kama wewe kuwa hong kong unakula kila ukionacho utakula na kinyesi cha watu. ila kwa tarifa yako mwanza hakuna mtu anaekula panya toa umbea wako hapa kama huna cha kuongea kaa kimya

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 24, 2008

    Hakuna ajabu au kinyaa, Wachina wanakula mbwa na nyoka, wafaransa wanakula vyura (frogs)- wengine wanakula mijusi, wadudu wa aina mbali mbali. Isipokuwa tu wanyama kama panya huwa na wanaweza kuambukiza magonjwa kama ya typhoid, rabies, n.k. hivyo idara ya afya ihakikishe kuwa hawa panya ni salama kama vile inavyofanywa kwa nyama za n'gombe, samaki n.k.
    Nyoro

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 24, 2008

    chiumbile mulungu cha kumemena, haidhuru almuradi si sumu, ukishangaa ya musa utakutana na ya firaun, kule znz Bwej... kwa kenge vipi maana mpaka mtu anaatoka mabaka ya m-ba kwa kula kenge.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 24, 2008

    Brother michuzi wacha watu waseme but this kitoweo ni bomba mno na ukionja huachi. Nawapa big up watu wa Ntwara especially kule Masasi na nnawakumbusha wanablog kuwa sio Ntwara tu!! maana hata kule Mbozi wanatafunwa kama kawa!! humuambii kitu Mnyiha kuhusu hii asusa.
    Mdau, Brasil!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 25, 2008

    Yaani na nyie wengine ati wanasupport sasa ukila panya utapata akili gani kama sio ya panya as well na kuwa mwizi tu ndio maana huko Mtwara maendeleo bao na akili za watu bado zimelala, kumbukeni kuna impact kubwa sana ya chakula unachokula na akili yako kujengeka achilia mbali mwili. Panya wana magonjwa mengi sana related na binadamu na ndio maana wanatumika kama sample katika dawa nyingi duniani. Yote hiyo njaa tu mkija hapa mtamaliza njiwa wote mjini hapa au kule uholanzi wale bata nanii kwenye zile canals ndio itakuwa watasaulika mtu yeyete anayekula panya awezi kupata akili ya maarifa hata siku moja hata kizazi chake.
    Londoner

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 25, 2008

    Kuna kabila fulani wanakunywa juisi ya kijambo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 26, 2008

    Wakipikwa kwa tui ya kolosho utazimia, ni mboga safi kwa mtandaha/ugali wa muogo. Pnya huliwa na watu wengi sana duniani, niliwahi kuwa CHAD watu wa dini zote hula panya kule tena wanawapenda sana, nyama nyingi sana za aina huliwa duniani, nimewahi kuwa Camerron, watu wa dini zote hula sana nyani, tena wanapendwa sana, London nimeona mwenyewe katika kipindi cha ready stead cook katika BBC hiki kipindi huwa kila siku jioni kama sikosei ni cha local sio BBC international hivyo watu wa huko nyumbani hamwezi kuona walipika nyama ya mamba na kenge watu wakala wakaisifu sana kuwa anafanana na ya kuku, so those things are not something not right, it okay. Chini kuna club/bar watu wanakula sehemu za siri za binadamu huzipata watu sijiuwi lakini nahisi toka hospitali watu wakifariki, nimeona mwenyewe kweye TV DOCUMENTARY watu wakichana sehemu za siri za wanaume.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...