Historia ya muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava kama unavyojulikana miongoni mwa wengi hivi leo una historia ndefu. Ni historia ndefu kiasi kwamba hivi leo wengi hatukumbuki tena hata muziki huu ambao hivi leo umetokea kuwa kipenzi cha wengi ulianzaje,ukapitia hatua na harakati gani mpaka kufikia hapa ulipo hivi leo.

Miongoni mwa mashuhuda wa mwanzo wa harakati za mwanzo kabisa za muziki wa bongo flava ni aliyewahi kuwa DJ maarufu nchini Tanzania kwa jina Mike Pesambili Mhagama(pichani).
Mike sio tu miongoni mwa mashuhuda wa mwanzo bali pia ni miongoni mwa watu wachache walioamini katika muziki wa kizazi kipya tokea mwanzo.Kumbuka hizo ni zile enzi ambapo muziki huo ulikuwa ukichukuliwa kama "uhuni" tu na sio aina mpya ya muziki au burudani.
Ni watu wachache sana walioweza kutabiri hatua ambazo muziki huo ungepiga miaka kumi au kumi na tano baadaye. Kwa hayo na mengine mengi nenda katika ule uwanja wa maselebriti wa www.bongocelebrity.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2008

    Big Mike tell 'em wapi hii kitu imetoka sio kuingia studio na kutoka na kuanza kupiga watu ovyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2008

    Ndio hiyo Picha yake rasmi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2008

    Huku kwetu kuna vibanda unavyojipiga picha mwenyewe..vinapatikana kwenye Malls..unatumbukiza tu vijisenti vyako na inakuchukua picha....ndo maana huwezi kujua kama ni Mweusi, wa Bluu au Kijani...Ila sidhani kama ndo picha yake rasmi....!! Muhimu tu ni kuwa katoa historia ya Bongo Flava..!! You Go Mike...!! Mdau USA.

    ReplyDelete
  4. Aminia, kijana makini ndani ya "Dj Show".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...