Ndugu michuzi tunamshukuru Mungu kwa kuliponya LIBENEKE hili kwa ugonjwa wa kwikwi ambao uliupata.
Baada ya hapo ninaomba kupitia chombo chetu hiki niwatangazie watanzania wote popote pale walipo,kwamba yule mwalimu wa neno la Mungu ndugu DEOGLAS MMARI atakuwa mgeni wa kanisa la UMOJA hapa Dallas tarehe 19,20 mwezi huu, yaani jumamosi na jumapili ya wiki hii.
Kanisa la Umoja linawaomba kwa wale watu ambao wanajamaa zao au ndugu zao katika jiji hili la Dallas kuwaandikia email au kuwapigia simu kuwajulisha juu ya ugeni huu wa kihistoria katika kanisa hili la watu wanaozungumza kiswahili hapa Dallas.
Siku ya tarehe 19 mtumishi huyu wa Mungu atakutana na mtu mmoja mmoja kwa wale wenyeshida mbali mbali kwa ajili ajili ya ushauri na maombezi.
Tunaomba kwa wale wote wenye shida ya kuonana na mtumishi wawasiliane na uongozi wa kanisa kwa ajili ya kupangiwa muda wa kukutana nae.Jumapili itakuwa ni semina maalumu kwa watu wote kuanzia saa saa kumi na moja jioni mpaka saa mbili kamili usiku.
Kanisa la Umoja lipo;
12727 HILLCREST,
DALLAS
TEXAS 75230.
Simu;682 552 6402,
903 312 9440,
214 554 7381,
469 279 1762.
Pastor Abisalom Nasuwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...