kibanda hujengwa asubuhi mapema na kuchomwa moto mchana katika kuhitimisha sherehe za mwaka kogwa, kwa mujibu wa mdau abdallah pandu wa ziff aliyetuwakilisha huko
makunduchi panakuwa hapatosho wakati wa mwaka kogwa
kinamama wakiimba na kucheza wakati wa kuadhimisha mwaka kogwa huko makunduchi

juu wadau wakikimbia na kuimba wakati wa sherehe za mwaka kogwa huko makunduchi wikiendi ilopita, na chini wakipigana bakora za majani ya migomba kuondoa kinyongo. hizi ni sherehe za kuhitimisha mwaka mpya wa ki-shirazi zinazofanyika kila mwezi julai. bofya hapa





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2008

    Michu, to balance this story, tafadhali elezea the other side of the coin e.g idadi ya machangudoa na malaya, condoms katika vichaka na beach, misokoto ya bangi na madawa ya kulevya nk. Plse usibane comments zangu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2008

    natamani na kwetu kungekuwa kisiwa labda mila zetu zingedumishwa, utamaduni wa kutoa watu wote nje, kushiriki katika jambo mojala jumuiya.
    nimeipenda sana hii.
    mila za Tz bara za hivi zimeishia masikini.
    Kila mtu na lake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2008

    Hizi ni imani za matambiko ya wamakunduchi na wajambiani, wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo kila mwaka ni kujilinda na mikosi na matatizo ya mwaka uliyopita na kuanza upya kwa mwaka ujao bila ya misukosuko ya majanga na matatizo ya hapa na pale. Kwa wengine wao huitumia visivyo kwa habari ya wakati wa kukimbizana na kuingia maporini na kumalizana hukohuko kwa wale ambao wakitamaniana kimapenzi, kwa tasiri ya wasukuma ni kama ngoma ya chagulaga, wengine kwa kupagawa na mapepo na kutukana matusi makubwa na madogo wakikashifiana watu wa kusini na watu wa kaskazini wa huko makunduchi, baadae hufurahi kwa ngoma na sherehe mbalimbali kwa kumaliza mwaka. MH! nisiseme sana mambongwa, nikafunua siringwa za enzi na enzi.
    Ila mimi sipati picha sana na yatendekayo huko kwani yamebase sana kwenye imani za mapokeo na matambiko ya kaushirikina kidogo,

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2008

    Misupu, Tumesikia Hao TEMAF tunaomba contact zao kama unazo timechoka wengine tunarudi bongo permit zimeshapauka huku, tumwekee post vizuri basi tuwapate hao jamaa wanaweza kutusaidia, BOngo ni ngeni lakini taasisi kama hizo huku Ulaya zipo zinasadia sana , hata mtu ukufunkuzwa kazi unakaa kwenye mali zao utalipa baadaye ili mradi una elimu hukosi kazi hata mwaka mmoja,
    Mdau East London

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2008

    MIchuzi apigwa marufuku kutangaza Castle Kagame CUp tena na watu wa Serengeti, haha! Unajifanya mjanja unachula pesa sehemu zote mbili halafu unaweka matangazo mahali pamoja watu wamemla kichwa, Misupu acha bana kuweka wapinzani mahali pamoja bana...Kama Blog hii inazaminiwa na Tigo pia sasa ukiweva Vodacom hapo jamaa hawakupi tena hako kahela kao japo ni ka ngama lakini kanakutoa hata T-shirt huwezi kununua, unakula makange ya bure tu pale break point hulipi basi ndo utatuwekea matangazo we mpaka tukome...sasa na watu hao wa TEMAF nao waweke hapo halafu watakupa offer ya kijana wako mmoja wa ulaya akae bure kwao haha!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2008

    MIchuzi apigwa marufuku kutangaza Castle Kagame CUp tena na watu wa Serengeti, haha! Unajifanya mjanja unachula pesa sehemu zote mbili halafu unaweka matangazo mahali pamoja watu wamemla kichwa, Misupu acha bana kuweka wapinzani mahali pamoja bana...Kama Blog hii inazaminiwa na Tigo pia sasa ukiweva Vodacom hapo jamaa hawakupi tena hako kahela kao japo ni ka ngama lakini kanakutoa hata T-shirt huwezi kununua, unakula makange ya bure tu pale break point hulipi basi ndo utatuwekea matangazo we mpaka tukome...sasa na watu hao wa TEMAF nao waweke hapo halafu watakupa offer ya kijana wako mmoja wa ulaya akae bure kwao haha!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2008

    Misupu Unapenda Sana Starehe Kuliko Kazi..Unajua Blog Yetu Imekua Ya Mwisho Kuweka Habari Kuliko Blog Zote Kisa Mzee Unatanua Tu Viti Virefu..Mdau Wako Mpindisha Shilingi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2008

    wow ahsante sana kama michuzi picha hizi zinanithibitishia kuwa utamaduni wa kiafrika unachanganyika na tamaduni nyingine, kama huu mwaka koga umetokana na washirazi yaani wairani au waajemi. kwani hapa iran tumekuwa tukisherehekea sherehe kama hizo kila mwanzo wa mwaka wa kiirani. Inafurahisha kuna kuwa sherehe kama hizo na Watanzania nao wanzifanya...
    Nawakilisha
    Mdau Iran

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...