Mzalendo Michuzi,
Salaam aleikum,

Nimesoma habari kama mara mbili hivi katika magazeti ya hapo kwetu zinazomnukuu katibu mkuu wa CCM, Mhe Makamba akiwaeleza watu kuwa maana ya neno 'ufisadi' ni ile tu iliyo katika kamusi ya Kiswahili (ninajua kamusi anayonukuu ni ile iliyochapishwa mwaka 1981 na kurudiwa katika miaka michache iliyopita).

Ninaomba unifikishie ujumbe wangu huu kwa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), (maana sioni kama wana tovuti wala anwani ya baruapepe), kwamba kama kitengo cha serikali kilicho na wajibu wa kushauri serikali na viongozi kama Makamba kuhusu matumizi ya lugha, wamweleweshe kuhusu tabia ya lugha (kwamba huibuka, hukua, hutanuka kama mti na matawi, na wakati mwingine huweza ikavia, au ikafa), pili wamweleweshe kuhusu maana ya kamusi (kamusi sio biblia au msaafu).

Kuhusu utunzi wa kamusi, hususan ule wa kimapokeo huwa tuna msemo mmoja kwamba "siku kamusi inapochapishwa tayari inakuwa imepitwa na wakati." Hii ni kutokana na ukweli kuwa lugha huwa haikai kusubiri kamusi. Ukiwauliza watumiaji wa Kiswahili leo hii maana ya neno 'fisadi' watakwambia bila kusita maana yake hai.

Hiyo ambayo Mhe Makamba anainukuu hata kwa watoto wa vidato vya tano na sita ni maana butu au mfu. Ninafikiri hapa ipo haja ya BAKITA kutimiza wajibu wao.

Ninatanguliza shukurani na asante sana kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha kwa mtindo wa blogu.

Charles Bwenge
Chuo Kikuu cha Florida
Gainesville,
Florida,
USA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2008

    neno fisadi limetoka kwenye kiswahili cha kenya - Mkenya

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2008

    nakupa point hapa! Kumbe kuna wakali humu ndani! Hawa jamaa wa serikali na CCM wanadhanigi wao wako right kila wakati. Huu ndo wakati wa ku-challenge hizi fikra duni!

    mtoto

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2008

    Mimi neno fisadi nimeanza kulisikia kwa wakenya!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2008

    Asante sana Prof Bwenge kwa mchango wako, inawezekana hawa CCM ndio maana mpaka leo hawajawashughulikia mafisadi kutokana na kukariri definition ya neno fisadi iliyopitwa na wakati! Na kwa kukariri huko inawezekana wakawa wanafikiri zana bora za kilimo ni kuwapelekea wakulima wetu majembe mapya ya mkono!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2008

    fisadi ni mtuu anayeiba mali ya jamii ambaye amechaguliwa au kuteuliwa na jamii hiyo,kisha akaamua kuangalia maslahi yake na kuanza kuiba bla kuheshimu wala kujali haki za wale ambao anawawakilisha,i can see why makamba is pissed off!!lol its me Makala Mluguu majuu!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2008

    Kwa muislam anayesoma quran, Fisadi linatumiwa na M/Mungu kuwa ni watu wafanyao uharibifu duniani kwa nafsi zao na za watu wote. Kwa kifupi Fisadi ni neno la kiarabu likiwalenga watu wafanyao dhambi mfano akina Firauni (Pharaos).

    Mdau
    Atlanta, Georgia USA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2008

    Fisadi kwa Kiingereza ni kleptocracy!

    Ni mimi Fisadi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 19, 2008

    Sijui Yusuf Makamba katoa ainisho gani la neno fisadi lakini nakiri kuwa mimi neno hil - sishangai kwa sababu wakati mimi naweza kumuita rafiki yangu "bwana Hamisi" kwao watashika vinywa wakinisikia - kwani wanaamini mkewe ndo wa kumuita hivyo. Kurejea kwenye neno hili fisadi pengine waandishi wa habari (si lazima wataalamu wa lugha) ndo waliolipamba kwa maana ambayo wengi tunaijua leo (si ya YusufMakamba) na kama ni hivyo labda basi watueleze maana yake halisi. Nakumbuka kwenye miaka ya 90 mfanyabiashara mmoja maarufu DSM akiongea kwenye televisheni alilitumia neno "kibaka" kumaanisha mtu "anayebaka" lakini sikumsikia mtu kumpinga pengine ningekuwa mimi ningerushiwa mawe na kuitwa wa kuja.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 19, 2008

    Mimi napenda kuondoka kama ifuatavyo neno Fisadi ni neno la kiswahili tena fasaha wala halijatoka kenya kama wakenya wamelitumia wanavofaham wao na inajulikana kwamba wakenya ni watu ambao wanazungumza kiswahili BUTU au simplified Kiswahili. In the same vein, maneno butu kama Swahili badala ya Kiswahili, Jambo badala ya Hujambo, hakuna matata badala ya hakuna matatizo. Kwahiyo bac kama wizi wao wanaita mafisadi huo uo ubutu wa kiswahili chao. Nina uhakika wakenya wa Mombasa ambao wanazungumza kiswahili fasaha wanalo neno fisadi tena wanalitumia ipaswavyo. Ila tukizungumzia kuhusu Tanzania kama wamelichukua neno ilo kutoka Kenya bac itakua wameishiwa! ni sawa na Waingereza kuchukua maneno au slang za wanaigeria na kuzitumia katika bunge lao. Ni aibu. Mimi nahisi ukweli ni kwamba watanzania wanatabia ya kuwafichia siri viongozi wao au maswahiba wao ndo maana ya kuwaita MIJIZI wanawaita mafisadi ambayo katika kiswahili fasaha fisadi na mwizi na watu wawili tofauti. Fisadi ni neno la kiswahili lenye maana ya mtu ambae ni mchonganishi, mwenye husda, mgombanishi,anaependa kuona watu wa aila moja wanagombana au wanatofautiana, mharibifu n.k. Fisadi litokanalo na lugha ya kiarabu lenye maana ya yule mwenye kufisidi, pengine kwa kufisidi fedha za umma ndo pengine waliitwa hivyo. Mimi naona Makamba atupe jina sahihi bac kama Mafisadi kaona si zuri,Mi narecommend WEZI.

    ReplyDelete
  10. Huyo makamba wamuulize tu kuwa kwani maneno kama Kung'atuka,Ikulu,ugiligili (liquid) na mengineyo yalitoka kamusi ipi kabla ya kuanza kutumika kutumika kama kiswahili rasmi na fasaha??

    Huyu mzee bwana!!!ingekuwa hivyo anavyotaka yeye basi kiswahili kisingekuwa na misamiati ya kutosha leo hii.
    Wakodya Profesa Bhwenge.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 19, 2008

    'Kuhusu utunzi wa kamusi, hususan ule wa kimapokeo huwa tuna msemo mmoja kwamba "siku kamusi inapochapishwa tayari inakuwa imepitwa na wakati." Hii ni kutokana na ukweli kuwa lugha huwa haikai kusubiri kamusi. Ukiwauliza watumiaji wa Kiswahili leo hii maana ya neno 'fisadi' watakwambia bila kusita maana yake hai.'

    Angalizo la Charles Bwenge ni makini.Aidha wataalam wa lugha (hususan Willard Van Orman Quine)'linguists' huzungumzia 'linguistic drift' amabyo inahusu kubadilika kwa maana na matumizi ya maneno na misemo (words and expressions) katika lugha- hili linatokea katika lugha zote siku zote, tupende au tusipende.Kwa nyongeza tu labda piya tunaweza kusema kwamba kamusi huweza kuwa na athari au uwezo wa kupunguza tu kasi ya mabadiliko au 'drift' na kusaidia uelewa wa hata yaliyosemwa na kuzungumzwa wakati maneno tuyatumiyao leo yalikuwa na maana na matumizi tofauti, pamoja na kwamba mabadiliko ya matumizi na maana yanaendelea kila kukicha. Kamusi ni reference point ya kule tulikotoka na 'ikibahatika' inaweza ikawa reference point ya pale tulipo sasa katika maana na matumizi ya maneno ya lugha fulani.Naomba nimalize na swali: je, kung'ang'ania maana na matumizi ya kihistoria ya neno fulani ni dalili ya kukataa kuenda na wakati au hata kupitwa na wakati?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 19, 2008

    Miaka ya 80 tuliwaita wahujumu uchumi, miaka takribani 30 sasa wanaitwa Mafisadi. Kiswahili kina kuwa kama lugha nyingie.Chanzo likiwa neno la kidini (nimenukuliwa toka kwenye quran) lenye maana sawa na kuhujumu na limekidhi maana halisi. Mbona kung'atuta ni neno la kizanaki na tena la kimila lilitumiwa kwa maana ya kustaafu na likakubalika. Tukubali Fisadi ni msamiati mpya na hauna budi kutumika.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 19, 2008

    Hapa ukinzani ni mkubwa kwa sababu aliyesema ni mccm na labda hapendeki. Angekuwa kalisema marehemu Baba wa taifa ingekuwa kimya. Kuweni fair.

    Lugha ya kishwahili inaundwa na lugha nyingi, hata jina lake ni la kiarabu. Na misamiati mingi inatokana na kiarabu.

    Si lazima maana ya fisadi ya kiarabu iwe sawa na ya kiswahili maana kuna maneno yakikopwa hubadilika maana. Mfano: Binamu ni neno la kiswahili limekuwa likitumika kwa maana ya mtoto wa shangazi au mtoto wa mjomba.

    Binamu limetokana na lugha ya kiarabu, BIN-AMU yaani mtoto wa kiume wa AMU, AMU ikimaanisha mtu alozaliwa tumbo moja na baba (kwa kiswahili baba mdogo au baba mkubwa). Kwa kuwa kiarabu ni kikongwe na kipana, watoto wengine huwa:
    1. mtoto wa shangazi-binamah
    2. mtoto wa mjomba-binkhaal
    3. binti wa amu-bnatamu
    4. binti wa shangazi-bnatamah

    SOOTE BADO WANFUNZI WA KISHWAHI, MADAM NI KINAKOPA MANENO.

    MSIMZOGOE MWENZETU.

    Ni mimi mtanzania wa Jaxon-MS.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 20, 2008

    Naungana na mdau anayeonya kuhusu kuchukua maana ya neno katika Kiarabu kuwa sawa katika Kiswahili. Pamoja na lugha hizi kushabihiana yapo maneno mengi ambayo pamoja na kuwa na asili ya Kiarabu huwa na maana tofauti katika Kiswahili - kwa mfano neno ghorofa (ghorfa) tulitumiavyo katika Kiswahili si maana ya Kiarabu; neno safina kwetu (nikosoe) ni ile tu ya Nabii Nuhu huku Waarabu waabu lakini wakati sisi tunamaanisha chombo cha kusafiria baharini - lina maana hasa ya mashine (generic meaning). Liko neno fuska ambalo maana ya kiswahili tunawalioamini na kisha wakawa wakitenda maovu hali ya kwamba wanajua ukweli (tofauti na kaffir - ambaye haamini). Neno tarehe lina maana ya Historia kwa Kiarabu na si date kama sisi. Yapo mengi...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2008

    CHA KUSHANGAZA LUGHA HII NI YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI HALAFU INAITWA JINA LA KIARABU, TUBADILI JINA HILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...