Kila mwaka kwa muda wa miaka saba sasa, shughuli hii kabambe huwa ikiandaliwa na watanzania wenyewe wenyeji wa majimbo ya New England.
Kila mwaka hafla hii huwa ikinogeshwa kwa vionjo tofauti kwa mfano mwaka jana tulikuwa na nyota wa Bongo flava Mr. II aka 'Sugu' na vikundi vya kucheza ngoma za kitanzania, maonyesho ya mavazi halisi ya mtanzania na mambo kadha wa kadha.
Nimeshikwa bega mwaka huu kutanabaisha kuwa ule mrindimo wa maonyesho ya mavazi uliotia fora sana mwaka jana umeboreshwa na kuwekwa katika kiwango cha juu hivyo mwakwetu usikose uhondo wa kuja kuona watoto, vijana na wazee wakionyesha mitindo mbali mbali ya kuvutia ya mavazi ya kitanzania huku yakitilia maanani vyombo vyetu vya asili vya kupikia kama vile vyungu, mitungi ya kubebea maji, ungo n.k. ambavyo huwa vikibebwa na kinamama pale wanapopita kuonyesha mavazi yao.
Mwakwetu "shughuli ni watu" na hao watu wenyewe ni mimi na wewe, kama hatukujishughulisha kudumisha mila,desturi na utamaduni wa kwetu sisi wenyewe nani atatufanyia?
Na watoto wetu tutakuwa tunawafunza nini? Hivyo chonde chonde fika kwenye shughuli hii muhimu ya kifamilia wewe na familia yako mapema ili uweze kuja kunywa supu ya utumbo na nyama choma.
Na kutwa nzima kutakuwa na chakula cha kila aina cha kitanzania na kuna mama mmoja kanambia ati mahanjumati ni "speciality" yetu na hii ni shughuli isio malipo.Camp Kee-wanee kuna mandhali mazuri kifamilia, kuna paki kubwa sana za magari, pia lipo bwawa la kuogelea na Life guard wa kulipwa atakuwepo kwa usalama wa watoto.
Pia kutakuwa na mchezo wa mpira wa vikapu na shindano asilia ni lile pambano la mpira wa miguu baina ya timu ya Mashariki na timu ya Magharibi ya mkoa wetu. Hichi huwa ni kuvutio cha kipekee kuona watu wazima wakishindana kusukuma gozi na pia timu za vijana.
Hivyo tafadhali usikose wewe na familia yako kuja shereheka pamoja nasi na kama ilivyo ada hatutakosa 'kuduarika' na mirindimo ya kitanzania na kiafrika kwa jumla.
Ahsante sana!
Isaac A. Kibodya,
Kwa niaba ya wanakamati wa New England Umoja
Ukihitaji mawasiliano zaidi hizi hapa chini ni baadhi tu ya namba za wanakamati:
Stephen Tomi 413.658.5253
Maria Sombe 413.364.8151
Richard Mwandemani 413.262.0400
Baraka Baraka 413.364.8151
Ahmad Mkambavange 413.221.2935
Severine Kiputa 413.306.2109
Mohamedi Kibodya 413.796.9761
Si utani ndugu zangu wa Massachusetts, nasubiri kwa hamu sana sherehe hii, tume-enjoy ile kinoma mwaka jana kuanzia party ya ijumaa mapaka liamba. Jumamosi mbuzi walikuwa kiboko - sisahau usiku wa mtanzania. Vipi mwaka huu washikaji timu yenu gani itakuwa kali?
ReplyDeleteMbongo, MN
Mimi nitakuwepo.Natafuta tiketi ya ndege sasa kutoka hapa Dar to Boston.Najua watu watakuwa wengi ila "majungu punguzeni"nyie waTZ.Mnajiabisha.
ReplyDeleteWakubwabwaja
bandugu msaada nimeona jina ..kibodya, ..mkambavange nawaomba mnisaidie email ya MBAI MDACHI mm ni dada-rafiki wa karibu tulikua nae kijitonyama
ReplyDeleteagnes
Jamani bila kusahau msisahau dawa za mbuu maana kuna mbuu si matani tena wa mchana na kwa wale wenye vitoto vidogo sana ni bora mlipie baby sitter wa huko mtokako wasijeshikwa homa ,Mzee kibodya hili nalo neno maana umewekwa chambo na kamati sasa hakikisha mambo hayaendi shoti maana utabebeshwa matusi na watu bure , uchumi wenye ndo kama unavyouona mtu akilipia mafuta ya dola $ 100 pamoja na tolls hataki kusikia uhanithi wowote sasa kaeni mkao wa kula isijetokea kama yaliyotokea Ohio halafu baadaye mkatafuta pa kuweka sura zenu.
ReplyDeleteAnonymous wa tarehe 9 Julai, pole kwa yaliokukuta huko ulikokwenda.Hii shughuli ni ya kujitolea,maandalizi yamefanywa kwa ustadi na ubora mkubwa kuliko miaka iliopita. Ushiriki wake ni wa ari na kujituma kila mtu kwa nafsi yake na mapenzi yake ikizingatiwa na imani yake ya umoja wetu wa kitaifa. Camp Kee-wanee ni camp kama camp zingine zozote za picnic hapa Marekani, huwezi kuzuia mazingira yanayokuzunguka lakini tahadhali kubwa imewekwa kwa kumwaga dawa ya mbu na taratibu zote za kiafya kama vyoo safi na kadhalika. Lakini hii haimaanishi kwamba mtu hatoumwa na mbu, wewe unaaishi hapa na hili unalielewa.Sasa basi, wee njoo na familia yako na marafiki zako, uje tufurahi, sisi tutakupokea kwa mikono miwili. Lengo la kamati ya maandalizi nikuona kila mmoja anakuja kufurahi na kujumuika na watanzania wenzake.Kukitokea kosa litakuwa la kibinadamu si la makusudi. Kamati imeboresha mapungufu yoyote yaliowahi kutokea siku za nyuma. kwa hiyo mdogo wangu, wee njoo tufurahi...maisha yenyewe mafupi haya..enjoy while you can...nina hakika tutakuwa sawa! Habari ndoo hiyo!
ReplyDeleteNawakilisha!
IK
Shime watu wote tujitokeze kwenye shughuli hii kwanza kamati nzima naiheshimu na ina watu wa hekima hivyo tusitie shaka na wale rafiki zangu na zetu wa mbali karibuni jimboni kwetu , mjomba kibodya usitie shaka kelele za za mlango hazivunji nyumba hivyo wembe uleule, naomba kuwa jaji kama kuna shindano la warembo (Joking)
ReplyDeleteFadhili