waziri mkuu mh. mizengo pinda akiongea na wasanii wa kikundi maarufu cha uchekeshaji walipomtembelea ofisini kwake jumanne mchana. kundi hili, ambalo limeingia mkataba wa mwaka mmoja kuonesha michezo yake kupitia tbc, liko katika hekaheka ya mambo ya hakimiliki na haki shiriki baina na stesheni ya east african tv, huku kila upande likidai haki ya jina la ze comedy, pamoja na mambo mengine. sakata hili limeshazungumziwa hadi bungeni ambapo wah. walitaka kujua nini hatma yake na serikali ikajibu kwamba chombo cha kusimamia hakimiliki, cosota, wanalifanyia kazi na litapatiwa ufumbuzi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2008

    Ndugu zangu watanzania, nawaomba muwe makini sana mnapoingia mikataba ya kufanya kitu cho chote na makampuni ama watu binafsi, kwani swala la "Haki Miliki" ni muhimu kuwekwa wazi kila upande lieleweke na wahusika wote. Yawezekana Ze Comedy na EATV hawakulichukulia kuwa ni swala muhimu kisheria. Ni heri Ze Comedy na EATV waelewane. Jina la Ze Comedy kubaki kwa EATV, halitawasaidia kwa vile watu wamezoea kuwaona wasanii wahusika wakilitumia jina hilo na kuwazuia kutumia jina lao kutawarudisha nyuma katika shughuli zao za kisanii. Kwa hiyo si Wasanii wala EATV watakaopata faida kwa hilo. Naomba mwelewane tu ninyi wenyewe ili sisi wapenzi wa Ze Comedy tuendelee kufaidi.

    BLACKMANNEN

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2008

    Mpoki suti tumekubali full manager....... infact najua utakuwa umenunua URAYA..

    ReplyDelete
  3. Duh, jamaa wapo juu! Nimependa sana suti zao! Manji haongopi bwana!

    ReplyDelete
  4. Hivi ofisini kwa waziri mkuu hakuna chumba chenye nafasi ambayo ingewatosha hao wote au ze comedy ni lazima wabananebanane kwenye kochi moja?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2008

    Kuna tatizo gani kwa kikundi cha iliyokuwa Ze Comedy kuanza upya katika TBC1 kwa kutumia jina jipya la Kipindi chao na jina jipya la kikundi chao,badala ya kuendelea kung'ang'ania jina lilelile la zamani la ZeComedy ambalo lilipata umaarufu kwa kupitia EATV CHANNEL 5 na kwa hakika kipindi hicho EATV haiwezi kukubali kitumike kama kilivyokuwa katika EATV kitumike katika Televisheni nyingine labda kwa kufidiana gharama ambazo EATV iliingia katika kukipatia umaarufu hadi hapo kilipofikia?Huu ni ujinga tu.Hakuna anaye wazuia hao vijana wasiendelee na Usanii wao kwa kutumia Jina Jipya la Kisanii na la Kikundi!Mimi siyo mfanyakazi wa EATV na sina hisa katika Kampuni hiyo lakini ningependa kukiona kikundi hicho kikiendelea kazi zake za usanii kwa ktumia jina jipya jingine kabisa badala ya ya kupoteza muda wao kwenda kule na huku hakutawasaidia lolote.Tatizo ni wao na Muda haungoji mtu.Watatokea vijana wengine mahiri zaidi katika sanaa ya ucheshi wakajikuta wameachwa kwenye mataaa.Huu ni ushauri wa bure tu!Ukitaka chukua hutaki Acha!Ila nawatahadharisha tu hao vijana kwamba wakilala usingizi wako wanasiasa wajanja ambao watataka kuwatumia kijanja kujiongezea umaarufu wao hususan hivi sasa tukiwa tunaelekea kipindi cha maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa 2010.Sisi siku zote macho yetu yatakuwa kwao tuwaone kama hawatatumbukia katika mtego huo wa kutumika kisiasa kwa maslahi ya wachache wenye malengo binafsi ya kisiasa LAKINI gharama hizo zikabebwa na watanzania wote kupitia RUZUKU YAO wanayoitoa katika kukiendesha Kituo cha TBC1.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2008

    Nakuona Bwn Mpoki umetulia....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2008

    Hiyo ni roho mbaya ya EATV haswa huyo mmiliki wake kuwabania vijana ambao wanajitafutia riziki zao kutokana na vipaji vyao, inaonekana kabisa rojo imemuhuma sana kuondoka kwao lakini ajue kwamba kila mtu ana uhuru wa kufanya kazi sehemu yoyote kwa kujali maslahi yake! sasa nyie ze comedy tuwaachieni sisi wapenzi wenu tutafute jina lenu lipya muendeleze libeneke mimi nawapa zE ChEkEsha au vipi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2008

    Napenda kutoa maoni yangu nikiwa tofauti kidogo nawa-Tanzania wenzangu pamoja na kwamba sipo Tz kwa muda, unajua kinachotufanya tusiendelee ni vitu kama hivi kwani suala la the Comedy na EATV mbona limekuwa issue ya kitaifa?, kumbukumbu zangu zinanionyesha suala lao lipo mahakamani kutafuta suluhu la haki miliki na haki shiriki sasa basi kwa nini issue hii imeingizwa hadi Bungeni na baada ya wabunge kujadili mambo ya msingi kwa taifa letu badala yake wanajadili mambo binafsi ambayo kimsingi hata kama yeyote atashindwa mahakamani hakuna madhala kwa taifa.

    Hii kwa kweli inasikitisha, bunge lina mambo mengi ya kujadili na Mh. waziri mkuu ana mambo mengi ya kufanya si vyema kwake kujihusisha au hata kuwa muda wa kuongea na vijikundi vidogo kama hivi, kama nakosea sawa lakini Tanzania yetu ina mambo mengi sana ya msingi ya kujadili,taifa letu bado dogo matataizo hayaishi kila siku kuna majanga ,migogoro ya kitaifa lakini hatuipi kipaumbele tunajikita kwenye the comedy what is this?, i think there is a political eyes surrounding the issue.

    Mwisho ni kuwadokezea tu watanzania, hapa kila mtu anatetea maslahi yake na tumbo lake the comedy au EATV hakuna atakayejali U-taifa kesi ikiisha na pia huku Ulaya na Mashariki ya mbali sijapata kusikia suala la iwe Opra,Mr. Been, Bill Cosby au mchekeshaji au Super Star yeyote likajadiliwa na Bunge awe na mgogoro au amekufa vyombo husika vinaachiwa vifanye kazi yake na kila mtu ana nafasi yake ya ku -act.

    Asanten, Tujifunze.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2008

    simbadilishe tu jina kwani mi naona mnapoteza sana muda kwani mkibadilisha jina vichekesho si viko pale pale? nawafagilia sana

    sweet,

    Arusha

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2008

    ANON 11:46 UMEMALIZA KILA KITU...SINA LA KUONGEZA MKUU.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2008

    viongozi wa afrika nuksi sana, angalia kiongozi alivyokaa....anaongea na wananchi walioleta shinda zao kaandika nne, kakaa kwenye kiti cha watu wnne peke yake! hivyo ndivyo unavyoweza kuona uongozi uko mbali saana na shida za wananchi. if justice is not solved in small magnitute no other way will be solved......hii ni tanzania.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2008

    Nyie Kina Mpoki Utafikiri Sio Watoto Wa MIGOMIGO Bana Waachieni Hao EATV Hilo Jina Tuone Watalifanyia nini.Kama mmebadili Majina yenu maana nasikia joti anajiita JOTA basi Badilini Hio ZE Wekeni Hata We,Up,Full, kwani najua utata ni hio Ze tu na kama watashupalia comedy basi EATV wana chuki binafsi a.k.a jilasi na sio usongo...Ni mimi ....... mvunja nazi kwa ugoko a.k.a mpindisha shilingi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 16, 2008

    Sheria ni sheria na kama walisaini still EATV Wana haki ila kama wanaona wanaongwa kwingine maana wamekuwa kama nanii sasa...yote ni njaa badala ya kimili status yao njaa inawapelekesha ila haki na sheria lazima zifiatwe. hao wabunge badala ya kujadili vipi kila kijiji kitapata angalau pc moja wanajadili ze comedy wakati mjini foleni kibao na matreni na reli zipo yaani sijui lini mtaamka au mnaona kukaa kwenye foleni tow to three hours kila mtu anamchungulia mke wa mwenzake ndio issue hamka jenga roads fufua reli jenga fly over peleke miundo mbinu kote sasa madini yanatusaidia nini kama mpaka leo tuna bararaba ambazo magari yanabanana na kugongana daily. Atiii ze comedy
    inauma basi tu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 16, 2008

    Nchi ya kutaka maendeleo hiii...PM na comedies tutafika kweli......?


    Kweli hakuna burning issue za kudiscuss maendeleo ya nchi ??......labda wataleta kipengele cha hati miliki on the next BUNGE session ili ipitishwe sheria mpya

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 16, 2008

    Waziri Mkuu mwenyewe anapoamua kuwa sehemu ya ZeComedy,inanoga hiyo!Mara moja kwa Mwezi siyo kitu mbaya!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 16, 2008

    Kwa vile mmeamua kuingia katika siasa basi jiiteni 'ZE TOT MINUS'. ushauri wa bure, na baada ya miaka miwili kama kuna mtu atakayetamani kuona vichekesho vyenu zaidi ya wana sisiemu!!!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 16, 2008

    nimekasirika sana.Ze comedy wanaongeza tija gani muhimu kwa taifa hadi kuchukua muda wa watanzania.Asilimia 81% ya watanzania wote hawana umeme, hivyo nikiotea katika asilimia 19% iliyobaki huenda ni 5% tu ndio wana access kwa tv
    mimi nimetaka kumuona PM kuhusu proposal yangu ya kuzalisha umeme kwa njia ya GEOTHERMAL na Nuclear energy lakini sijapata access hata kwa katibu mkuu.Propsal yangu ingeweza kuleta impact kwa 45% ya watanzania na kuleta multiplier kubwa kama umeme kwenye zahanati na mashuleni, ili watoto wasome
    Ze comedy, please acheni malumbano na EATV, Mmechemsha na mnazidi kutupotezea muda viongozi wetu

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 16, 2008

    kweli nchi yetu inamambo,mbali namatatizo yaliyopo na mbayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka eti waziri mkuu anakaa na ze comedy, bongo ni bongo ,nchi imekua bora liende

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 16, 2008

    this is more than mchezo wa kuigiza,,,,,,,,,,,,,,

    lets be serious about maendeleo.

    Hili swala lipo mahakamani,je kwa nini WHY...
    serikali kupitia kwa PM, bunge na wabunge wanaendeleza libeneke la kuishangilia wazi wazi the former Ze Komedy.

    Vinginevyo kuna maingiliano ya maslahi kwani si vikundi vyote vinapewa nafasi ya kutangazwa na serikali.

    Kazi ya serikali si hiiii...
    La sivyo...
    iwekwe ratiba ya kuitembelea bunge na PM ..hadharani ya vikundi vyote vya sanaa.

    hiki kitu sivyo ndivyo...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 16, 2008

    Kama bahati ni yako ni yako tu....tupeni hilo jina mje na jimpta material yenu si bado mnayo

    Look at p diddy, p dad, p daddy anavyobadili majina yake na kote upepo unamfuata...achaneni na hilp jina....

    But next time mkumbuke hao wanasheria wanaomaliza shule hapo mlimani kazi zao ndio hizo...Msiwe wabahili...muwe na mwanasheria wenu...Sio nyie nyie wasanii, nyie nyie wanasheria, mameneja, etc etc haiendi hivyo ndugu zangu

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 16, 2008

    nchi ya kutaka maendeleo hii, kweli yako kaka, ukiangalia kwa makini nchi inaendeshwa kama vile BET, hakuna cha maana ila kila mbongo anataka awe msanii au modo. wale wenzentu waliojiendeleza toka mashamba, vijijini hawaonyeshwi, tungeomba mifano inayoingia kichwani, kama vile wabongo wengi waliojiendeleza kwa njia za kilimo au biashara(wachapa kazi).

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 16, 2008

    Jamani, wadogo zetu wanapata taabu kwenda na kurudi shule, wafanyakazi wa kawaida hali kadhalika wanasumbuka, haya yote ukiangalia ni mijini na vijijini. Bei ya mafuta ya petroli imepanda, na gharama zimepanda. Wenye usafiri wao binafsi(daladala) wana haki ya kudai kupandishwa kwa nauli na mabasi ya abiria kwenda mikoani. Badala ya kujadili na kuyatekeleza mambo muhimu, PM anakaa kusikiliza malalamika ya ZE Comedy, tutafika kweli? Kweli nchi inapoelekea hakufai, na hawa ndio viongozi ambao hukaa na kujisifia kuwa wana PHD. Barabara kibao mbovu, toka tunazaliwa mpaka leo hakijabadilika kitu. Nimesoma kwenye blog CCM wamefungua tawi mkulanga, mkoa wa pwani, wakati njia ya Kisarawe mpaka kesho mvua ikinysha magari hayafiki Maneromango, duh! Tujifunzeni jamani watz, sio kila siku tunakua kama tupo old stone age.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 16, 2008

    Ndugu yangu wa 11:46 nakuunga mkono
    ila hii ndio Bongo yetu. kila kitu kinaenda kimzahamzaha tu. kila mtu anatafuta cheap popularity bila kutoka jasho. ndio maana mkuu wa mkoa anaacha kazi muhimu za kuendeleza nchi anaenda Airport kupokea maMiss Tanzania, wakati ana afisa utamaduni wa mkoa!! Joob true true.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 16, 2008

    UMASKINI UMASKINI UMASKINI NI KITU KIBAYA SANA WATOTO WASHAINGIA MKENGE WANANCHI ILE TEST MLIOKUWA MNAIPATA MWANZONI NDIO IMETOKA HIYO HAO VIJANA UHURU WAO WA KUONGEA YALE WANAODHANI YATAFURAHISHA JAMII NA UKWELI NI ASILIMIA 5%.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 18, 2008

    Anonymous 11;46 nakuunga mkono sana., nchi hii kuanzia bunge, serekali yote hivi sasa akili zao ni kama hao ze comedy.
    Wangekuwa ni wale wazee wa afrika mashariki wanaodai masilai yao wasingemuona huyo waziri mkuu...wangeambiwa yupo bussy sana.
    Ze comedy wenyewe upuuzi mtupu...eti wageni muhimu wa bunge tukufu la Tanzania.
    Hii nchi ni ya kuhama tu na kufuta hata uraia.
    Kuitwa mtanzania chini ya viongozi hawa ni AIBU TUPU !!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 18, 2008

    tatizo letu wabongo kila jambo tunachanganya na siasa....swala la zecomdy na eatv lilikuwa limalizwe na cosota lkn kwa ushabiki usiyo na tija ndio unakuta maswala ya kipuuzi yanafika kwa pm...that's ril bullshit.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...