Habari za leo ndugu Issa,

Natumaini wikendi yako imetulia na wewe ni mzima.
Mie naitwa Eric Mutta, ni mtanzania, kijana mwenye miaka 25, na nina ndoto kubwa ya kujenga taifa letu kupitia sayansi na teknolojia (haswa computer and communications technology).

Mwaka huu, tarehe 25-April, nilianzisha kampuni yangu Problem Solved Limited inayo shugulika na kazi za kutatua matatizo sugu ya biashara kwa njia ya software engineering.
Web site yetu ni

Nadhani unafahamu ugumu wa kuanzisha na kuendesha kampuni, tena kwa mtu ambaye ni kijana kama mimi. Lakini hivi karibuni, kampuni yangu ilifanikiwa kuanzisha huduma mpya inaitwa SMS Tuwasiliane, inayo wezesha watu kuchat kwa njia ya SMS bila kugawiana namba za simu! Inafanya kwa simu zote na mitandao yote Tanzania.
Ni teknolojia ya kitanzania ambayo haipo sehemu nyingine yoyote duniani!

Huduma ilianzishwa kwa majaribio tarehe 10-July-2008. Leo hii, baada ya wiki mbili tu, ina watumiaji 100 wanao furahia uwezo wa kutafuta, kuwasiliana na kukutana na watanzania wenzao kwa njia rahisi ya SMS.

Naona blog yako inatumika sana kuwajulisha watu kuhusu habari mbali mbali. Nitashukuru sana kama ungeniunga mkono kuwajulisha wananchi wenzetu kuhusu huduma hii ya SMS Tuwasiliane. Mafanikio yake ni mafanikio yetu wote manaake dunia itaona kwamba watanzania sasa wako tayari kufanya makubwa!

Maelezo zaidi kwa Swahili:
Shukran Issa,
nakutakia wiki njema.
Eric Mutta,
Managing Director
Problem Solved Limited
0787-999-950

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2008

    Ongera sana Eric kwa kuanzisha hiyo kampuni, kwani naelewa kuwa umri wako ni mdogo kuwa kampuni ningependa kukushauri hiyo isiwe ni moja ya sababu itakayokuzuia ku-think big kwani ktk ulimwengu huu wa sasa, kuna vijana wadogo zaidi yako wanaofanya maajabu katika business World.
    Pili Unaposema hii kampuni inaitwa problem solving, nimejaribu kuingia katika website yako nilichoshuhudia ni ume-"create more problems", sisemi hivi kwa kukuvunja moyo mdogo wangu ila najaribu kukujenga ili ufanye home work yako vizuri. Hii sayansi na teknologia unayoisemea ulitakiwa kuidhihirisha kwa watu na watu ili wajenge imani na Kampuni yako.kwa mfano hapo katika website ya Michuzi nimeona link mbili zote ni zako, moja inanipeleka katika word doc na nyingine nanipeleka katika wesite ambayo inapingana na swala la technology.nikimaanisha hadhi ya website yako ni ya hali chini sana kulinganisha na kile unachokielezea, na kuahidi watu unaweza kuwatatulia

    jambo lingine ni kwamba unapokuwa na project nzuri kama hii ni vizuri ukaijenga kwanza polepole ili kufikia kiwango kizuri cha kukubalika na watu ndio uitangaze vizuri kwa watu kwani nivigumu sana kuwapata watu ambao utawapoteza kupitia nafasi hii kubwa iliyoipata kuitangaza Michuzi website.

    sina mengi mdogo wangu, I think you need to do more home work katika biashara yako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2008

    Asante Bro.Michuzi kutuletea hii.

    Hongera sana Bw.Eric Mutta kwa kuanzisha na kuja na teknolojia mpya kabisa ya ku-chat kwa kutumia SMS.

    Nakupongeza sana kwa kuwa na wazo ambalo ni very original.

    Nakushauri yafuatayo:

    1. File for patent copy rights mapema kabla wengine hawajaiuza teknolojia yako

    2. Wazo lako ni very original na napenda kukupa moyo kwamba jipange vizuri kwa sababu you might be our next millionaire. Nafikiri utakuwa unaelewa where Google and Facebook techies are.

    3. Website yako ni nzuri ila inahitaji marekebisho madogo madogo. Kwa mfano,inahitaji kuwa lugha ya kibiashara zaidi na sio tech language, na pia kurekebishwa iwe kifasaha zaidi.

    Hongera sana na unatupa fahari Watanzania wenzako, na zaidi unatupa changamoto zaidi.

    Mdau katika ICT.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2008

    Bwana Eric, i am proud of what you are trying to do and what you have achieved so far.Vijana wa bongo tunahitaji kufuata vyayo zako za kujiajiri.....
    Nimeipenda website yako, ila nimgekushauri utumie dynamic website ,hii yako we cant send you comments, or any kind of inquries about your product.Pia ningekusharui uweke a demo of one of your products ili watu waone quality ya kazi yako.

    Good luck my friend i am trying to do the same thing , ila bado niko huku kwa wazungu nakamata experience nirudi home.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2008

    Haya ndio mambo tunatakiwa kuyaona. Link technology to a Tanzanian setting. Sio kuiga tu ideas from Ulaya. Heko kijana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2008

    Hongera kijana kwa kufungua kampuni.Lakini kwa upande mwingine hiyo technolojia yako inaweza kuwa inachangia Maambukizo ya Gonjwa la ukimwi napia vitendo vya udhalilishaji(matusina hata ubadhilifu, kupitia sms ambazo hazioneshi number.Marafiki wengi huenda wakijikuta wakichonganishwa na watu wao karibu sana.Mwisho nakupongeza sana,tena sana kwa jitihada ambazo unazionesha za kujikwamua kimaisha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2008

    Bwana Eric wazo zuri sana kujiajiri na kuanzisha kampuni yako.
    Mimi pia kama mmoja ya wana teknolojia tena ya mawasiliano (IT), naomba tu nikurekebishe mambo madogo madogo ambayo kwa watu na nchi zilizoendelea huwa ni yenye mtazamo mkubwa sana kibiashara,
    1: Una website Isiyo na LINK hata moja kisha unasema wewe ni mtatuzi wa matatizo ya kiIT. Umeshindwa kutengeneza site yenye mvuto wa kiteknolojia utaweza vipi kuwa commited na kazi za watu? (ni mtazamo tu)
    2: WebHost wako hajakupa email components> iweje bado unatumia gmail kama email ya mawasiliano? wakati unaweza kutumia info@problemsolvedltd.com?
    3: Cheo chako ni Marketing & Sales Director, Kisha unasolve problems za IT?? imekaaje hiyo?
    be serious mazeee, otherwise wazo zuri, Ila tu kuwa makini na sisi wateja wenye mitazamo ya mbali na kutegemea value for money service... NB: Ukipanga budget ya sh 200 utatafuta 200, ukipanga budget ya milioni mia utatafuta milioni 100, So THINK BIG kaka.. All the best..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2008

    Kabla ya kutoa maoni yangu juu ya wazo la bro. Eric,niimejaribu kusoma mawazo ya wanajamii wengine.Ni ukweli kabisa mawazo waliyoyatoa ndugu zangu ni mazuri yenye kila faida kama yatafanyiwa kazi.Kwa bro.Eric najua ndio unaendeleza hii project yako.Nafikiri Website ni moja ya njia muhimu sana ya kuitangaza biashara yako.Hivyo basi nakushauri utengeneze webiste iliyo nzuri zaidi na yenye kurahisisha mawasialiano na wateja.Tengeneza website iliyo dyamic kama alivyosema ndugu yetu mmoja hapo awali.Pili tafuta haki miliki documents mapema kabla jamaa wengine hawajafaidika na project hii.Vilevile nakupongeza mno juu ya wazo lako zuri na lenye manufaa kwa taifa.May be ipo siku twaweza kukutembelea kujifunza mengi zaidi.
    ALL THE BEST BROTHER-wise A

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2008

    Nimefurahishwa na kutiwa moyo na mawazo ya wanaglobu kwa Eric. Eric Hongera kwa kujaribu na pia fuata ushauri uliotolewa na wengine utafika mbali
    Mdau Boston

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2008

    Kwanza namshukuru ndugu Issa kwa nafasi aliyonipa bila kudai chochote, shukran!

    Pili nawashukuru nyie wote mlio toa maoni yenu ya kunipongeza na pia kunishauri, shukran!

    Nime sikiliza kwa makini vitu vyote na website nimeifanyia marekebisho kidogo. Kadri muda unavyo enda nitaiboresha kutumia njia mbali mbali za Web 2.0 (kwa wanao fahamu mambo hayo).

    Nawaombeni wote mliopo Tanzania mjaribu kujiunga na wenzenu wote mmwaambie. Kwa mambo haya ya Social Networking, kuwa na watu wengine ndio mali!

    Nia yangu kubwa ni kuonyesha watanzania wenzangu kwamba mambo yanayo fanywa na vijana marekani kwenye vitu kama MySpace na Facebook, sasa hapa tanzania yana wezekana bila tatizo!

    Mmeisha sikia hao vijana huko ulaya wanaanzisha kampuni zao vyumbani au kwenye gereji. Yakwangu pia inaendeshwa hapa hapa chumbani kwangu nyumbani, kwenye laptop yangu!

    Tujitahidi ndugu zangu kuepuka umaskini wetu na tabu zetu kwa kutumia akili tulizo nazo na kwa kuungana mikono kama tunavyo fanya sasa hivi. Karne hii ya 21 ni karne ya Africa kusimama na kupata heshima duniani.

    Mbele bila fujo, mbele bila uoga wanainchi!

    Eric Mutta.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2008

    Mkuu nimependa sana kuweza kuanzisha kitu chako wewe mwenyewe bila kutegemea mgongo wa mtu kwa hiyo keep it up..Pia nilikuwa na mawazo kuhusu website yako sina ya kusema ila hapo juu kuna mdau kasema kuhusu email yako mimi naona haitakuwa vizuri kama utatumia GMAIL ndio ambayo itaweza kukufikishia mawasiliano katika website yako la hasha itakuwa haijatulia cha muhimu hapo kuna software ni nzuri sana na pia ni bure ila host ndio inabidi kununua sasa hapo unaweza kuweka site yako katika hadhi inayotakiwa jitahidi ufanye hivyo ili kila mtu aweza kufanikiwa na mambo yako wewe mwenyewe...Pia wadau waliokuwa nje hawawezi kuitumia hiyo SMS au ni kwa ajili ya bongo tu??

    ReplyDelete
  11. hongera kwa kuwa na idea nzuri sana ila naungana na wadau wengine wote waliosisitiza kuhusu website yako.
    ningependa kutilia mkazo technical issues 2 za website yako sababu you have to be very careful katika biashara ya IT na kwa kifupi ni kwamba inaonekana kuna mambo bado hujayafanya na ingekuwa vyema ufanye mapema.please read the following 2 issues of my concern yafanyie kazi unayoyaona yanafaa weka kapuni yasiyokufaa.
    1.Ni hatari sana kutumia plain HTML kutengeneza website yako sababu unaanika kila kitu kilichopo katika website yako na unaanika technical details za website yako haikunichukua dakika 3 kufika katika server root yako so kama ningetaka ningecopy directory yako na kuiedit then nika i upload tena - this is a security hole you are currently facing
    solution - tumia scripting language kama php,asp and connect yyour script to a database to store your info so that you can be sure that your site is secured
    hint: kama php huipendi na una haraka unaona itakupotezea muda tumia JOOMLA it is a briliant,stable,and free& it is open source of course) tumia hii kutengeneza webiste yako kuna kila kitu8components,modules,plugins) katika WEBSITE yao(download them for free).Another alternative would be TYPO3 it also a good content management system there is also DRUPALlakini kwa ushauri wangu go for joomla its very good once you know how it works you can make your own components,modules,plugins etc.nimeona watu wengi wanaojifanya wajanja wanawaibia watu hela kwa kuwatengenezea sites using joomla all they do is make their custom templates,custom components,modules,etc lakini am sure you can use this piece of info and come up with a great website.mifano ya websites zilizotengenezwa kwa kutumia joomla ni binamu13 na
    bongoUK
    2.mimi napenda sana kuona umetumia priciple ya KISS(keep it simple stupid) i also use it most of the time it is very good lakini please weka notice katika website yako eg the site is still under construction
    ni hayo tu ndugu yangu i really like your idea lakini naona umeeenda na speed sana please sit down and weka cv vizuri your website is like your cv to your clients it is very important katika IT business kuwa na reliable,consistent,robust,and dynamic website.
    unaweza kunicheki mpakakieleweke@gmail.com kama kuna lolote unataka kuuliza if i know it then i will be glad to assist ..
    it is time for african IT junkies to shine au siyo!
    stay up my bro!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2008

    Hello, Na hiyo software yako inaweza kublock watoto wadogo mfano miaka 14 and below wasiweze kuwasiliana na watu wakubwa kuliko wao? Naona ni social network nzuri lakini kama niijuavyo madhara ya myspace kwa watoto sijui hii itakuwaje once watu wakishaanza kuelewa na kutumia hapa bongo? Kama unaweza kukarabati na hilo ni muhimu kabla hatujaanza kujilaumu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2008

    Kama kawa: naona haitakuwa vizuri kama utatumia GMAIL

    Ni kweli, hilo swala la email kupitia GMAIL wengi wamelitaja namie pia sipendi hali yenyewe. Sababu ni kwamba web host wangu amenipa email ila ina interface ambayo ni ngumu tumia kwa mawasiliano ya mara kwa mara. Ndio maana natumia GMAIL ambayo inaweza mambo mengi zaidi.

    Kama kawa: Pia wadau waliokuwa nje hawawezi kuitumia hiyo SMS au ni kwa ajili ya bongo tu??

    Wanaweza manaake kinacho hitajika ni uwezo wa kutuma na kupokea SMS tu, ila kwa sasa system haita kubali SMS zinazo toka nje ya nchi. Lakini kwa wale wanao tumia roaming kwenye nchi zingine hapa africa kama Kenya na Uganda, itafanya bila tatizo.

    Anonymous: Cheo chako ni Marketing & Sales Director, Kisha unasolve problems za IT?? imekaaje hiyo?

    Hiyo ndugu yangu ndio hali ya kampuni ndogo, kwani mimi ni engineer, managing director, sales director, marketing director...vyote nahitaji kufanya manaake nikiajiri watu wote hao kampuni itakufa mapema (kampuni yenyewe nilianzisha kwa savings zangu za $7,000 tu!).

    Sina makosa: Lakini kwa upande mwingine hiyo technolojia yako inaweza kuwa inachangia Maambukizo ya Gonjwa...

    Kama teknolojia zote zingine, hii pia inaleta faida kwa watu na madhara kwa kulingana na jinsi wanavyo amua kuitumia.

    Kitu kimoja kitakacho punguza matumizi yasiyo na ustaarabu (mfano kutukana watu usio wajua bila wao kugundua namba yako) ni swala la malipo. Kwenye internet, gharama ya kuwasiliana na watu inakaribia shilingi sifuri kwahiyo watu hawana haja ya kuzingatia ustaarabu. Ila kwenye SMS Tuwasiliane, kwa kila meseji unayo tuma unakatwa pesa. Kwa hali hiyo, mtu lazima awe amekasirika sana akubali kukatwa pesa ili amtukane mwenzie.

    Pia system inanjia mbali mbali zakuwaruhusu watu wajilinde. Mfano unaweza kublock SMS kutoka kwa watu ambao wewe mwenyewe hujawahi kuwatumia SMS. Na pia kublock SMS kwa mtu yeyote ambaye hajakuomba ruhusa ya mawasiliano. Njia ziko nyingi!

    Tabu kubwa sana ni kuwapa watu "freedom of expression" waweze kusema na kufanya wanavyo taka bila kutengeneza mazingira mabaya.

    Hili tatizo linajitokeza kwenye mambo yoyote yanayo husu binaadamu zaidi ya mmoja mwenye "free will"...na kwote lilipo tokea bado watu wanatafuta solution leo hii!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 29, 2008

    Natoa pongezi kwako Eric na kwa wadau waliochangia hii mada. Hajatokea mchafuzi wa hali ya hewa hata mmoja.
    Inawezekana tumeanza kujitoa katika usenene sasa...

    ReplyDelete
  15. email me at tgeofrey@gmail.com with ur propasal pls i failed to read all the passage.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2008

    Anonymous:Hello, Na hiyo software yako inaweza kublock watoto wadogo mfano miaka 14 and below wasiweze kuwasiliana na watu wakubwa kuliko wao?

    Ndiyo inaweza, ila tabu ni kwamba mtu anaweza kutaja umri wowote na ni ngumu kucheki kama anasema kweli bila kumwomba passport yake!

    Lakini kitu kizuri huku Africa kwetu ambacho tofauti na ulaya ni kwamba watoto wachache sana wana simu za mikononi. Mfano, mdogo wangu ana miaka 15, na anaishi kwenye nyumba yenye simu karibu 9, ila yeye hana (japokuwa computer anayo na internet anayo, na ndio maana MySpace wanapata tabu hiyo!).

    Na software yenyewe inaweza kufanya "user age prediction" ambapo inajaribu kupima umri wa mtu kwa kuangalia umri wa watu wote anaye ongea nao. Haiwezi kua 100% accurate ila inasaidia.

    Ni moja wapo wa technical challenges chungu mzima ambazo watumiaji hata hawajui zipo!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 29, 2008

    Ni wazo zuri but it is not original, watu wameshafanya tayari kitu kama hicho huku Ulaya, kama anataka kuweka hati miliki pengine huko Bongo itakubali but internationally tayari watu wanafanya hivyo. Kuhusu umri si tatizo kwani BILL GATE wa Microsoft alianza biashara akiwa kwenye 20s tena bila degree yoyote ile, yeye ni college drop out, hadi leo hana degree yoyote ile, Ford alianzisha kiwanda cha magari kwenye 20s bila degree ya mechanics, Richard Branson wa Virgin alimaliza O-level with zero division no qualification alianza kuuza magazeti mitaani kama Chinga hivi sasa ana kila biashara wewe unayoijuwa hapa duniani, hivi sasa natumia internet yake kama my internet service provider, na ukimkuta barabara ukamuongelesha anything about business utasema ana MBA. Tujaribu watanzania tunaweza fika, lakini kutokana na hali halisi ya watanzania walio wengi biashara kama hii itamchukuwa muda kupata faida kwa vile ni watu wachache sana wenye uwezo I mean financial muscles for accessing internet in Tanzania, ungekua UK au USA ungekuwa BILL GATE sasa hivi, nimeshuhudia watoto wengi wakianzisha website na kutengeneza pesa kwa siku moja kupitia matangazo tu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2008

    Anonymous:Ni wazo zuri but it is not original, watu wameshafanya tayari kitu kama hicho huku Ulaya

    Nime angalia sana kwenye internet kuona kama kuna wengine wanafanya ninacho fanya, ila sijapata. Hao unao wajua wewe wanaitwaje?

    Anonymous: Kuhusu umri si tatizo

    Kweli ndugu yangu, siku hizi mambo mengi duniani yamebadilika kiasi kwamba mtu yeyote mwenye wazo zuri na hela kidigo anaweza kufanya makuwba. Hasa ikuangalia economics za computer software utaelewa kwa nini Bill Gates anaongoza kwa utajiri duniani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 29, 2008

    Mimi sina la kuongezea ila kama wadau walivyosema hapo juu...Pia kuwa makini sana maana joomla ndio kiboko ya software hizo zote alizotaja mdau hapo juu....Na pia joomla unaweza kuitengeneza wewe mwenyewe sio mpaka utoe hela bila ina extension nyingi sana tena sana ndio maana kila mtu anatumia joomla maana ni uwakika na imara pia sasa pia hatuwezi kusema tumia joomla ila sasa hapo ni kipendacho roho chako wewe mwenyewe ni uwamuzi wako ila zaidi naona ni joomla ndio nzuri zaidi na kama template zipo za kumwaga na ni free ila kama unataka nzuri zaidi unaweza kupata kuna website inabidi ulipie utapata template nzuri tu kama utahitaji zaidi nitakuwasaidia na pia unaweza kutengeneza site yako ndani ya one week na pia inabidi uwe makini kama mdau mmoja alivyosema kuhusu website yako iweke sehemu ambayo hata mtu kama akiichek asifahamu kwamba vipi umefanya mpaka webiste iko hivyo..Zaidi nadhani MPAKA anafahamu zaidi kila kitu ila zama joomla wengi sana wabongo ndio wanaitumia na kila kitu free baadhi ya enxtensio ndio itabidi ununue Pamoja

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 29, 2008

    Eric, Msome Billi geti kama history of the past ili ikusaidie kwenda kwenye fyucha. Bizinezi model ya biligeti haifanyi kazi tena, utakolea! Kwnai hujaona Microsoft inavostrago sasa hivi kwa watoto wadogo kama google? Hadi anataka kumnunua yahoo ili ashindane na google? anawafanyia ubaya piawatengenezazaji wadogowadogo wa softiwaya mbalimbali?

    Kazi nzuri lakini angalia usisome wrong pages, wrong signal za future.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 29, 2008

    kuhusu kutumia gmail, gmail allows POP where you can set up one or more email accounts by specifying a few of your email service provider's POP settings and gmail will listen to incoming emails. that way you are not stuck with your web host's interface for emailing (sending and receiving). pretty cool stuff.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 31, 2008

    hongera kijana,lakini hii njia yako ya mawasiliano naona nicomplicated kidogo. huku niliko mimi kunahuduma ya namna inayotaka kufanana na hiyo,ila kwa kuanzia lazima mmoja katiyenu ajue namba ya mwenzie ili aanze kutuma sms,kisha unaweza kuficha nambayako isionekane na mkaendelea kuwasiliana.pia unaweza kutumia internet kutuma sms kwenda ktk mitandao yote na wao wakawa wanakujibu kama ukitaka kupokea sms hapohapo kwenye internet,au uka divert ukawa unazipokelea kwenye simu yako wakati unachat hapohapo.
    ni wazo zuri ukiliendeleza kwa huko nyumbani na utapata mbinu mpya zaidi kilakunapo kucha,cha msingi umepata wazo la kuanzia hivyo endelea kuwambunifu zaidi usilemae ukadhaninia hapo ndio mwisho,hapa kunavijana wanafanya vitu vya hatari kuliko unavyoweza imagine,sema hata nikikupa link sidhani kama utaweza kusoma maana lugha yenyewe sio ya kiingereza wala kifaransa hivyo utakuwa msala kwako maana utaona nyotanyota tu!
    othrwise keep it up!

    ReplyDelete
  23. Watanzania
    Tumaomba sisi LO wa Opportunity Tanzania ltd tusaidiwe,Tunanyanyaswa,tunafanya kazi kama punda,na hakuna haki za binadamu.
    HR toka aje,amekuwa akitunyanyasa,kutunyima haki zetu.Kwa nini anatutenda hivi nchini kwetu,Tunaomba achunguzwe,Wizara ya kazi ifuatilie swala letu.
    Yeye sio mtanzania,ni mkenya,tushaurini jamani,mbana tumefanywa manamba kwenye miji na nchi ya kwetu, Tunaomba wapenda haki waingilie kati

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...