Habari za kazi mheshimiwa!
Hongera sana kwa kuanzisha na kuindeleza blog yako! Hakika imekuwa ni chanzo cha habari cha uhakika kwa wengi wetu.
Naamini watumiaji wa blog hii ni pamoja na maafisa uhusiano wa wizara na idara mbalimbali za serikali.Haiingii akilini kwanini maafisa hawa hawafikirii kuanzisha blog kupitia websites zao za kiofisi au ndio kukosa ubunifu?Inawapasa kuelewa kuwa kwa kuanzisha blog kutawarahisishia kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya masuala muhimu ya kitaifa.
Ni lazima sasa waondokana na taratibu zilezile za kupata maoni kwani sasa kuna technologia kama hii ambayo ni rahisi kutumia na kufikisha ujumbe! Huu ni wakati wa kufungua vichwa na kufikiri nje ya box na kutazama mbali zaidi!
Naitwa
Ben
napatikana kwa email:
------------------------------------
Kwanza napenda nimpongeze Ndugu Ben kwa kusema kuwa serikali iwe na blog kwa ajili ya mambo yake mbalimbali,ila analaumu na kusema "Haiingii akilini kwanini maafisa hawa hawafikirii kuanzisha blog ?"
ila siwezi kumlaumu hasa hapa ila kwa kifupikabla kufanya hivyo vyote kuna mambo mengi inabidi kufukiria sio rahisi kila kwa ghafla kikatokea kitu hicho au maendeleo hayo mpaka atokee mtu kwa mfano mzuri
Mshauri akatoa ushauri sehemu inayohusika na mifano kwa nchi kadhaa kuelezea faida zake , i hope itakubalika. ila kuna vitu vingine kadhaa kabla ya kwenda kutoa ushauri inabidi pia kuangalia mfano:
Feasibility study:
system requirement: e.g. (Computer & Interenet ).
Requirements Analysis Study of present system,
collection of information etc.
Methods of investigation may include:questionnaires to staff and management;
interviewing of staff and management;
observation of procedures
Design :test plan
From A. Paul

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2008

    Ndugu yangu Ben wazo lako ni zuri lakini swali ni je hao maofisa wanao ujuzi wa kutumia ama kufungua kile unachokizungumzia hapa. Uzoefu wangu unaonyesha kuwa mpaka hivi sasa ni asilimia chini ya moja ya maofisa wa serikali wanaoweza kutumia komputa kwa ufasaha na gonjwa jingine ambalo nimeliona ni kwamba baadhi ya maofisa wetu wakishapata uwezekano wa kupeleka mkono wao kinywani bila kwa uhakika masuala mengine ya kujiendeleza kwenye ujuzi mdogo mdogo huwa halipo kabisa. Hivyo hoja yako ni ya msingi na naomba iwe changamoto kwa maofisa hawa. Hili mimi silishangai ila tu ninachokiona ni kwamba maofisa wetu wanaridhika mapema sana. Hivi karibuni nimekwenda kwenye mojawapo ya ofisi muhimu kabisa nikihitaji waraka fulani kwa ajili ya kufuatilia masuala fulani fulani, basi bosi muhusika aliandika barua kwa mkono akampatia mhudumu wake ili aipeleke ikachapwe kwenye komputa na mmoja wa wahusika katika ofisi ile, baada ya muda mfupi mhudumu alirudi na kusema kwamba mchapaji hayupo maana inaonekana anaumwa kutokana na taarifa zilizopatikana kutoka kwa ofisa mwingine. Baada ya taarifa hizo jibu nililopewa ni kwamba nirudi baada ya wiki moja maana mchapaji kwa maana ya mtu pekee mwenye uwezo wa kutumia komputa (microsoft word) hakuwepo. Ebu jaribu kufikiria kidogo kuhusu hili. Ofisi muhimu kabisa ina mtu mmoja tu anayeweza kutumia komputer. Basi nilisononeka sana na nikasema kweli tu bado.

    ReplyDelete
  2. Mdau Ben has raised a very good point. It is a shame that a lot of organizations back home do not make full use of use of what ICT has to offer. I was recently doing a certain survey, which involved me contacting people at higher learning institutions in Tanzania. You won't believe how hard it is to find their contacts! And even for the few that I managed to find; half of the emails were returned because either the system was down, or the email address (which I found on the official website) is wrong!!

    If Universities and Colleges which are supposed to be the center of knowledge and innovation can't keep up with technology, how do we expect the rest of the institutes out there to do the same?

    Most ministries and public institutions have recently opened websites; but I find that this is more of a going with a trend thing, and most of these sites don't serve their full purpose and live up to the potential, not to mention infrequent updating, occasional broken links, etc.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...