Michuzi na wadau,
naomba kuuliza, nini maana ya
1. Mgumba
2. Tasa
Na je nini tofauti yake? Michuzi hala hala mzeee wa libeneke. ukinibania ntakuroga.
Mdau Australia
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hii iliisha jadiliwa humu nenda
ReplyDeletehttp://michuzi-blog.com/2007/04/ombi.html
Utapata majibu kama ni mdau mpya
Mgumba ni mwanamume ambaye hana kizazi- mbegu za uume hazifanyi kazi wakati Tasa ni mwanamke asie na kizazi
ReplyDeleteKwanza acha kumtisha "Mkuu wa nanihii utamloga"
ReplyDeleteSasa tukija katika swali lako la TASA na MGUMBA maana zake. Mgumba ni mtu asiyebahatika kupata mtoto katika ndoa yake. Tasa pia ni mtu asiyeweza kuzaa ama kuzalisha. Maneno yote kwa mintarafu ya kuzaa yanafanana, lakini kwa wakazi wa pwani Mgumba hutumika kwa wasichana na Tasa huweza kutumika kwa msichana na mvulana. Lakini kwa wakazi wa bara yote huweza kutumika kwa jinsia zote.
Lakini Tasa hutumika pia kwa wanyama, kuwa ng'ombe huyu ni Tasa, ama Mbuzi huyu ni Tasa. Huwezi sema Ng'ombe huyu ni Mgumba.
Pia Tasa ni neno tata, waweza kulitumia kwa kuonesha kitu kisichoweza zaa ama zalisha, ama kutumika kuonesha namba zinazogawanyika kwa zenyewe na moja mfano 3,5,11,17....
Mgumba=na mwanaume asiezalisha
ReplyDeleteTasa= mwanamke asiyeweza kupata mimba
Ila wote hao ni nguvu za mwenyezimungu hazalishi hau hapati mimba mungu ndio anayejuwa kazi yake mola.
TASA MWANAMKE ALIEE KATIKA RELATION NA HASHIKI MIMBA
ReplyDeleteMGUMBA MWANAMKE ALIE HANGAIKA KUTOKA KWENYE UTASA KUJARIBU MATIBABU NA IKAHSINDIKANA ZAIDI INA ONGELEWA MGUMBA AKIWA AMEISHA FARIKI KWAMBA BIBI YULE ALIKUA MGUMBA HIVYO TASA NI HAI MGUMBA MFU
Hi,
ReplyDeleteMgumba ni mtu yeyote ambaye ameshindwa kupata mtoto kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja,akiwa nafanya mapenzi mara kwa mara bila kutumia njia yoyote ya kuzuia mimba kama vile,kondomu,Depo,pills,natural method.n.k,yaani kwa lugha ya kitahalamu inaitwa "Primary or secondary Infertility"Kama Haujawai kupata mtoto kabisa that is Primary,kama uliwai kuzaa alafu ukakaa zaidi ya mwaka bila kuzaa that is Secondaty Infertility.
Tasa maana yake ni mtu amabaeye amethibitika kitahalamu,kitabibu kuwa hawezi pata mimba kamwe kwasababu za genetic code/DNA contents,That is "Permanent Infertility"
Mdau
Tabibu.
***Tasa ni mwanamke asiye na uwezo wa kuzaa
ReplyDelete***Mgumba ni mwanamme asiye na uwezo wa kuzalisha.
biology haikutoka kwa wazungu tu.
Mimi nafikiri tasa (unbearing)ni mtu ambaye hazai kabisa na kama akiitaji mtoto hata science haiwezi kumsaidia ..Yeye shurti atumie surrogate mother au aadopt mtoto kama anataka mtoto
ReplyDeleteNa mgumba ni mtu ambaye anaweza asizae na mwanaume aliyenaye kwa vile damu hazipatani lakini akiolewa na mwingine anaweza kuzaa au akitumia science na technologia anaweza kuzaa..
Labda wengine wanaelewa zaidia lakini hayo ndio mawazo yangu
Tasa ni mtu ambae hana uwezo kabisa wa kuzaa yaani hana mayai ya uzazi na hiyo ni tangu azaliwe anakuwa ameumbwa ivo kuwa hana kizazi kwahiyo hata afanye plantation inakuwa haiwezekani, mgumba ni mtu ambae anakuwa amekumbwa na matatizo ya kuzaa kutokana na sababu tofauti yakiwemo magonjwa ya zinaa, uvutaji sigara na bangi na ulevi kupindukia au sababu zinginezo zisizojulikana ila mgumba ana uwezo wa kushika mimba na kuzaa, mgumba anaweza kutibiwa na akapona lakini utasa ni nature
ReplyDelete1. mgumba = binadamu mwanamke asiyezaa. hakuna mwanamme asiyezaa maana kitanda kihizai haramu
ReplyDelete2. tasa = kiumbe kisichozaa.
szipChacha mwita wa Tarime unachanganya mambo sasa hapo.
ReplyDeleteyote sawa hawazai hata kidogo iwe mnyama au binadamu.
ReplyDeletesweet,
Arusha
Kisayansi mwanamke ambaye hawezi kushika/kupata mimba kwa sababu mbali mbali kama vile kukosa mfuko wa uzazi au mirija ya kupitisha mayai ya kike kuziba, au hali ya maumbile ya mfuko wa uzazi inayosababisha mimba isitunge; anaitwa tasa.
ReplyDeleteNa yule ambaye hajabahati kujifungua mtoto aliye hai, ama kwa sababu mimba zake zinaharibika mara kwa mar; au kuzaa mtoto mfu, anaitwa mgumba. yaani anauwezo wa kutungwa mimba lakini hapati mtoto kutokana na mambo niliyoyaeleza.
Blaza Michu na wadau ukumbini
ReplyDeleteMGUMBA: ni mtu nasisitiza tena ni MTU aliyefikia umri wa kuzaa lakini akwa hajazaa wala kupata mimba au kutia mimba
amma TASA; ni ni kiuknbe chochote cha kike kisichoweza kuzaa, kwa fasili hizo mbili bila shaka muulizaji na wadau wengine wanaopenda kuongeza maarifa kuhusiana na tofauti ya fasili ya maana mbili hizi watakuwa wamefahamu tofauti iliyopo. MBlaza Michu hongera kwa blogu yako lakini picha ya urembo, miziki na mengineyo ambayo faida ni kidogo mno naona zinakithiri mno kuna mambo mengi ya kuelimisha jamii kuliko kuonyesha visichana vimevaa uchi.
Anony.11:56 Explainations zako sio za kisayansi ni za mitaani sana,Sio kweli kuwa Kuziba kwa mirija ya uzazi kunasabisha mwananke kuwa Tasa..!!Umeisha sema wewe mwenyewe kuwa tasa hawezi kuzaa,sasa iweje kuzipa mirija kusababishe utasa,wakati mirija inaweza kuzibuliwa either kwa operation maalum au kwa kutumia dawa maalum...???!!
ReplyDeletePili sio kweli kuwa Mgumba uzaa mtoto mfu wakati wa kipindi cha ugumba..NO..NO,kwani maana ya ugumba ni kuwa huyo mtu hawezi kabisaa either kushika mimba au kutungisha mimba,yaani there is NO FERTILIZATION taking place for the whole period of ugumba,akisha shika mimba au akasababisha mimba huyo sio mgumba tena hata akijifungua mtoto mfu yaani,Fresh stiil birth or macerated still birth...!!
by
Mdau
kweli watu wasahaulifu...
ReplyDeleteMgumba si yule mwanamke aliyeimbwa na Muumin au?
huyu Tasa simjui labda atakuwa jirani yake Mgumba au marafiki wa kweli.