PERONI NASTRO AZZURRO
BIA NAMBARI MOJA YA KIITALIANO DUNIANI YAZINDULIWA BONGO
Dar es Salaam,
Ijumaa
Julai 25, 2008:
Tanzania Breweries Limited (TBL), chini ya SABMiller plc, jana ilizindua Peroni Nastro Azzurro – bia nambari moja ya Italia duniani, jijini Dar es Salaam. Peroni Nastro Azzurro inatazamiwa kuwa kinara mpya wa mtindo wa Kiitaliano ambaye amesheheni umahiri na hisia za maisha.
Wakati hali za kiuchumi ulimwengu mzima pamoja na Tanzania zikielekea kupendelea bia za kimataifa zenye thamani ya juu, TBL inatazamia kwamba kwa kuileta Peroni kwenye soko la Tanzania, vionjo vya wanywaji wa bia nchini kote ambao kwa sasa wanatafuta ladha yenye hadhi ya juu vitaridhishwa.
Katika kusherehekea uzinduzi wa Peroni Nastro Azzurro, TBL ilifanya hafla maalum kwenye ukumbi wa The Slipway jijini Dar es Salaam.
Kimataifa, Peroni Nastro Azzurro imejijengea heshima ya kuwa bia nambari moja ya Italia na pia kuwa kinywaji cha kwanza kwa watu maarufu na wenye mvuto, ikiwa bia iliyochaguliwa kunywewa kwenye matukio ya watu kama Madonna na Giorgio Armani. Bia hii yenye kuthaminiwa itaanza kupatikana kwenye vilabu vyenye hadhi ya juu, sehemu maalum za starehe na migahawa ya Kiitaliano jijini Dar es Salaam na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Bw. David Minja alisema, “Kwa kuileta Peroni Nastro Azzurro, TBL inasisitiza jitihada yake ya kuendeleza soko la bia zenyehadhi ya juu nchini Tanzania. Kwa jinsi ilivyo na mvuto wa mtindo wa Kiitaliano, Peroni Nastro Azzurro itabadili mtazamo wa wengi juu ya unywaji wa bia hasa miongoni mwa wote wanawake na wanaume. Tunaamini kwamba Peroni itakuwa kinywaji kitakachopendwa miongoni mwa Watanzania wanaokwenda na wakati.”
“Zaidi ya hapo soko la vinywaji vyenye kileo duniani linaelekea zaidi kupendelea vinywaji vya hali ya juu. Watumiaji kila wakati wanatafuta aina za vinywaji vyenye vionjo tofauti na vile vya kawaida. Tunaamini kuwa kuileta Peroni Nastro Azzurro Tanzania kutakipatia kinywaji hiki nafasi ya kukua na kulinyanyua soko la bia kwa ujumla.”
Peroni Nastro Azzurro hutengenezwa kwa kutumia shayiri ilipandwa wakati majira ya kuchipua, kimea na mhopi na kwa pamoja viungo hivi huleta bia yenye ladha ya hali ya juu iliyonakshiwa kwa mtindo wa Kiitaliano. Peroni Nastro Azzurro, bia ambayo imekuwa ikitengenezwa kwa miaka zaidi ya arobaini, itakuwa ikiagizwa na TBL kutoka kwenye kiwanda cha SABMiller kilichopo kusini mwa Italia.
Bia hii ya hali ya juu ni sehemu ya bia nyingine zenye hadhi za SABMiller duniani ambazo ni pamoja na Pilsner Urquell na Miller Genuine Draft.
Hapa Tanzania, Peroni itaungana na bia nyingine za SABMiller kama Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Balimi Extra, Bia Bingwa, Eagle Lager, Castle Lager, Castle Milk Stout, Miller Genuine Draft na Redd’s Original.
Kuhusu Peroni Nastro Azzurro
Peroni Nastro Azzurro ni bia nambari moja ya kifahari ya Italia.
Birra Peroni ilianza kutengeneza bia mwaka 1846, na Nastro Azzurro ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1960 nchini Italia.
Peroni Nastro Azzurro ni bia nambari moja ya kifahari ya Italia.
Birra Peroni ilianza kutengeneza bia mwaka 1846, na Nastro Azzurro ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1960 nchini Italia.
Peroni Nastro Azzuro, bia nyororo iliyobuniwa kwa umakini ilizinduliwa duniani kote mwaka 2005. Peroni Nastro Azzurro inapatikana kwenye baadhi ya masoko katika chupa zenye ujazo wa 33cl na 66cl.
Peroni Nastro Azzurro ina kiwango kidogo cha sukari na hutengenezwa kwa kutumia shayiri ilipandwa wakati majira ya kuchipua, kimea na mhopi na kwa pamoja viungo hivi huleta bia yenye ladha ya hali ya juu.
Kuhusu Birra Peroni S.p.A.
SABMiller ilinunua hisa kubwa kwenye kampuni ya Birra Peroni mwezi Mei 2003. Birra Peroni S.p.A. ina historia ndefu ilianzia mwaka 1846 wakati ilipoanzishwa na Francesco Peroni. Sasa hivi ni kampuni kubwa ya pili ya bia nchini Italia ikiwa inashikilia takriban asilimia 25 za soko na viwanda vitatu vilivyopo Bari, Roma na Padua. Bia zake ni pamoja na Peroni - bia nambari moja nchini Italia, Nastro Azzurro - bia ya hali ya juu inayoongoza na nyinginezo kama Gran Riserva, Crystall, Wuhrer na Raffo.
Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya SABMiller www.sabmiller.com
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Pilsner Ice, Pilsner Lager na Tusker Lager. Bia nyingine kubwa zinazotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Konyagi Ice.
Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vitatu vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabar matano. Bia zake ni pamoja na zila za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.
SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Maneno Mbegu
kwenye
0767 266806,
PERONI NASTRO AZZURRO
HISTORIA NA UFAHAMU
Historia
Birra Peroni ilizinduliwa zaidi ya miaka 150 iliyopita, mwaka 1846, na Francesco Peroni
Mwaka 2003 Birra Peroni ilinunuliwa naSABMiller
Bia ya ‘Peroni Nastro Azzurro’ ilitengenezwa kwa mara ya kwanza miaka ya sitini na Carlo Peroni ambaye alianza kupenda vinywaji vya hali ya juu na akataka vipatikane Italia.
Jinsi Peroni Nastro Azzurro inavyotengenezwa ni siri nab ado inatengenezwa kwa kufuata maagizo yaliyotolewa mwanzoni mwake.
Peroni Nastro Azzuro, bia nyororo iliyobuniwa kwa umakini ilizinduliwa tena duniani kote mwezi Machi 2005 ikiwa kwenye chupa yenye shingo ndefu.
Jinsi ya kuijaribu
Peroni Nastro Azzurro hutengenezwa kwa kutumia shayiri ilipandwa wakati majira ya kuchipua, kimea na mhopi.
Peroni Nastro Azzurro siyo chungu wala haijazi tumbo, hivyo kuifanya ipendwe na wanawake.
Peroni Nastro Azzurro ni bia yenye rangi nyepesi na ina kiwango kidogo cha sukari
Technical Specification
Alcohol: 5.1%
Style: Premium quality export lager
Mwenyezi Mungu atakulaani duniani na akhera.Uislamu unapiga marufuku uchocheji wa maasia na wewe unafanya wazi kwa kiburi .Lakini ujue laana ya Mungu haiko mbali.Mimi kama mwislamu nakupa nasaha kwa kuna mwenzetu unapotea.Mwenzako mwanamuziki wa Bongo Fleva ameshapata adhabu ya Mungu kwa pombe na alikanywa hakusikia.Bado wewe.
ReplyDeleteaaah hizo bia za kishua,ndo mana zinazinduliwa huko ushuani,hapa kitu NDOVU tu,ata mkituzuga na alcohol ya 5.1 hayo mabia ya kizungu gharama bwana,unakunywa bia kwa presha,nyie TBL bora mconcerntrate na local brand zetu,ka ndovu,yan alieandika hiyo fomula ya ndovu adumu milele mana najua ataendelea kuimarisha.afu inapendeza mnavyodhamini blog yetu mana nikiwa ofisini nikiingia tu kwa blog naona kitu kinavuja jasho yani kazi inaenda kabisa!!!
ReplyDeletewewe shehe hapo juu usituzuge na "extremist idealogy" zako. wewe mbona una lala na mke wa jirani yako.
ReplyDeleteWADHUNGU Wanazidi kutustopisha hawataki tuendelee hata kidogo,Wao kila siku wanavumbua iphone,mp3,bluetooth,laptop,ferrare yaani mambo mazuri tu Sisi wanatuletea mipombe,na sisi tunasherekea tunavumbua hahah TUMEKWISHA,
ReplyDeleteWADHUNGU will never walks alone wanataka hadi skeleton zetu.
Ni mimi SLAVE
SLAVE we kiboko duh ha ahahahaha lakini angalau wanatuletea pombe zilizoenda shule, sio kubaki kukumbatia gongo, pingu, wanzuki, ulanzi na ile nyingine ukinywa unakuwa kipofu... hakuna standards!!
ReplyDelete