Hi, Michuzi
Mimi mdau wa website yako Naomba uwatangazie watanzania wenzangu kuhusu kutembelea hifadhi zetu ifuatavyo pia nime attach picha 2 moja yangu nyingine ya mai waifu wangu (chini) naomba uzitoe pia:-
Mdau wa Arusha Victor Mujwauzi Karugaba na ubavu wake Rose Kapinga Mujwauzi wakiwa ngorongoro crater. tunapenda kuwashauri watanzania wenzetu tujenge mazoea ya kutembelea hifadhi zetu, Sio tunasoma tu kwenye historia na jiografia, tunapoweza tujitahidi hasa kifamilia, kiofisi n.k. kutembelea hifadhi hizo, kupanda mlima kilimanjaro n.k .
Tuithamini nchi yetu na vivutio vyetu
--
Victor Karugaba
P.O. Box 435
Arusha
Tanzania
mujwauzivk@gmail.com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2008

    Safi sana Victor Njwauzi, una uhusiana na jamaa mmoja anaitwa Victor Mjwahuzi, alikuw pale UDSM B.Com 2005. maana naona mnafanana kwa characteristics hasa kwenye preference of Mambo fulani hivi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2008

    WAKOLA MJWAHUZI SANA NA HONGERA PAMOJA NA MKEO Lakini wizara inayohusika haitangazi sana vivutio hivyo kwa wazawa zaidi ya kusema 'gharama ni ndogo sana kwa wazawa'.
    N.B kuna baadhi ya wanablog wenye upeo mdogo wamenirushia kejeli mahala/li fulani kwenye blog.Nasisitiza mimi ni mwanaume na jina langu nd'o hilo.Binadamu hatuwezi kuwa na mawazo yanayolingana,yale yalikuwa mawazo yangu,wenye upeo mzuri walinielewa.Hii ni blog tupunguze Jazba.Yanga Oyeee

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2008

    Ni jambo zuri unalosema lakini ungeweka basi hata price range tujue ni kwa mwendo gani tunaweza kuafford kwenda huko. Wengine hizo mbuga tulizifaidi tukiwa tunasoma shule.

    Bila kujua bei na tanzania hata hawaweki vitu vyao kuonyesha bei ni kiasi gani basi mtu anakuwa hata hawazi kuwa japo siku moja anaweza kutembelea hizo mbuga.

    Ushauri kwa wafanyaboshara bongo muwekage bei kwenye vitu vyenu mnavyouza. Ndege huoni price, mbugani hata hujui package zipo za aina gani, magari, nyumba mkiuza ati bei ni maelewano. Hiyo sio biashara.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2008

    What a beautiful FAT wife you are having.She looks like she lives in the olde country buffet.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2008

    Shemeji yetu amependeza sana. Lakini nadhani hii fulana aliyovaa juu ni ya wakati wa BARIDI, na hapo inaonekana jua linachoma kidogo.

    Huku kwa wenzetu nguo/ vazi huenda na majira (Winter, Spring, Summer ...n.k.)

    Anyway, amependeza!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2008

    Dont other people think of anything else than insulting other people....Tht wasnt ur concern if the woman was fat or thin...let them enjoy their lives and let the man be proud showing off her wife goshhhh....wabongo mmejaa chuki binafsi kasageni chupa mnywe kha mnaniboa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2008

    Bwana Victor asanye lwa chagamoto uliyotupa,tutafika mbugani!!

    Mdau ATL

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2008

    Kaaaaaaaazi kweli kweli! Michu mi naona ifike mahali uwe unakata baadhi ya maoni.

    Mfano mtu anajifanya kujua nguo za kuvaa na wakati, then hajui kama sasa hivi ni baridi Tz na hapo wako ngorongoro ambapo kuna baridi sana.

    Inaudhi sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2008

    We anony 10:08pm acha ushamba wenzentu ndo nani? naona we bado upo kwenye ukoloni. I think u do what u think satisfy yourself. Are u wearing to please someone!!!!Do you want people to walk naked simply because wenzetu during summer they do the same!!!! Amka ndugu its better to shine whether feeling hot or not.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2008

    yah jamaa yupo ryt sana..unajuwa we tanzanias cjui tuna kasumba gani..unakuta ktk baadh ya mambo tunajiexclude kama hayatuhusu vile au yanapaswa kufanywa na wa2 flani kama hili alilolizungumzia aliyetalii kwenye mbuga na mywife wake...hata maeneo ya kuenjoy wd family or friends lets say steers etc unakuta wamejazana warabu na wahindi tu bt wazawa ni wachahe au hakuna kabisa af sio kwamba vi2 ni gharama sana ni kawaida 2..Lets change homies!! Mdau-Turkey!!

    ReplyDelete
  11. Huu ni ni uungwana kweli? nadhani ni ukosefu wa nidhamu, hivi mtu mwenye akili timamu anawezaje kumtukana mke wa mtu bila sababu yoyote?(sijui fat n.k) kama umekereka bora usiweke comment yoyote.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2008

    Ehhh, wee Matumbi. Kipenda roho jamani kila mtu na chake. Wengine wanapenda wanawake WANENE na wengine Nyama karibu na mfupa. Kwani wewe huyo Skeleton wako kuna mtu anakucheka? Tena unaweza kukuta hata huna mwanamke na sanasana mwendo wa REVOLA tu.
    Wee unayejifanya unajua MAVAZI, naona hujui kuwa kuna Kaprokoni, Kansa na Ikweta. Bora ukajue hivyo vitatu ni vitu gani na Wazungu wanavitumiaje katika Mavazi. Mwisho Wazungu hawavai nguo nyeupe wakati wa Winter, kwani hawataonekana. Sasa unakuta mtu Mweusi kama chungu cha makande na yeye anavaa nyeusi....COPY & PASTE.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 26, 2008

    Watanzania wachache bado wajinga na wapumbavu, hasa kwa watu ambao wanaandika ujinga na matusi kwenye Blog mbalimbali bila hata ya sababu ya msingi.

    Hasa huyo binti amekosa nini mpaka watu wamuandike ni mnene au amevaa fulana ya baridi. Na kusingizia watu wanavaa nguo kutokana na weather, Mimi nipo Uk na waulizeni watu wote ambao wanaishi Uk wakwambieni watu wanavaa vipi, sasa hivi ni summer almost 21 Celsius lakini bado utakuta watu wamevaa makoti. Tuacheni ujinga wa kusingizia wenzetu wanafanya hivi au vile.Kumbukeni kila mtu ana maisha yake na unafanya kitu kujitosheleza wewe na sio wengine na hii ndio maana bado hatutafika kwani tunafikiri wazungu wote wanafanya kazi za ofisini............mawazo ya kipuuzi


    Unene............sasa amekosa nini yeye kuwa mnene, mimi binafsi sioni kama ni mnene na hata kama ni mnene wewe inakuhusu nini wakati ni mke wa watu na yeye anamaisha yake.

    Tuacheni ujinga na upuuzi jaribuni kuchambua maisha yenu na sio ya wengine.jiangalieni wewe umefanya nni kuchangia gurudumu la Taifa. watu wanabidi waelimishwe na waache kashfa ambazo hazina msingi wowote.

    Mungu ibariki Tanzani,Mungu ibariki Afrika na mwenyezi Mungu wabariki wote wenye mawazo potufu na kashfa waweze kubadilika na wawe watu wa kuelimisha wengine

    Popo
    london

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2008

    utaliwa na simba bure tafuta vitu vya maana ufanye

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2008

    Kila kitu kina utamaduni wake, kwa mimi kama mtanzania kumuambia mtu mnene si tusi ni sifa kwamba ana afya njema, lakini pia inategemea lugha uliyotumia kumuambia kuwa ni mnene inaweza kuwa matusi pia kutokana na lugha yako. Huku Ulaya hata ukitumia lugha safi kiasi gani kumuambia mtu ni mnene ni tusi kubwa na huo ndio utamaduni wao wamelelewa wakijuwa unene ni mbaya hivyo si sifa nzuri mtu kuwa nayo, kama vile si sahihi huku Ulaya kumuuliza mwanamke ana umri gani mbele za watu ni wachache sana anaweza kukuambia umri wake mbele za watu, hivyo inatubidi tuchaguwe lugha tunazotumia hasa katika zama hizi za utandawazi kwani watu wa tamaduni mbalimbali husoma hizi habari na kutokana na hilo wanaweza kusoma watanzania ni watu wa aina gani. Kuhusu nguo ni kweli watu wa huku Ulaya wanajaribu kavaa nguo tofauti kwa nyakati mbalimbali, lakini hili lilikuwepo sana zamani wakati wengi wa watu walikuwa wenyewe siku hizi kuna watu wa makabila tofauti toka duniani kote wenye vipati vya aina mbalimbali kiuchumi, na pia kuna professional tofauti za kisasa ambazo wakivaa suti basi huendandana na kazi zao, pia wageni wengi watu wa kuja huku hata hiyo 21 C bado ni baridi kwao na wanavaa makoti, kwa Africa huvaaji wa nguo unaendana na uchumi wa mtu kwani mtu hununua nguo kutokana na mfuko wake, hata hivyo maoni juu ya fulana ya huyu semeji yetu MZURI hayana msingi kwa vile katika picha vigumu kuona kama hii fulani nzuri aliyovaa ni ya baridi au ya wakati wa jua, hata hivyo mkoa wa Arusha karibu mwaka mzima huwa hauna joto sana kama Dar. Hongera sana Mr and Mrs kwa kutembelea mbuga zetu na kuwakumbusha watanzania wengine kufanya hivyo, huku Ulaya kila mtu hujaribu kwenda holiday at least once a year hata kwa kujikamua, huwa wanaenda sehemu ngeni
    ku-charge akili zao for next level ni muhimu sana kupumuzisha akili hivyo inatubidi kupumzika angalau hata mara moja kwa mwaka, unaweza kupanga kutembela mahali popote pale ambapo hujawahi kufika kwa mfano unaweza kupanga next year nataka kwenda kuona say MTWARA, siku ikifika unafungasha virago vyako na familia yako mnaenda kuona MTWARA, that's it.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2008

    Anonymous10:08 PM, GO TO HELL, na utakabaki maskini na roho yako mbaya. Bravo!!! Mr&Mrs.Victor. Pia ikiwezekana wamuvuzishie wizara ya utalii waone jinsi wasivyokuwa responsible mpaka watu wachukua personal efforts kutangaza mbuga

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2008

    Ngorongoro mwezi wa sita huwa kuna baridi sana hata kama kama jua linaangaza. Mbona huko ulaya winter time ukichungulia nje jua linawaka na temperature yaweza kuwa below zero! acheni ushamba.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 31, 2008

    we" anonymous 4;40.
    hivi kusema mtu flani ni Fat hilo ni tusi?? acha mambo yako wewe!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 31, 2008

    Sasa nyie......... wakina Karugaba(wahaya) bwana mnatabu sana,....wewe unatuwekea picha yako, mara ya my wife wako ili tuwaone nyinyi au nyie ndio vivutio vya Ngorongoro, (Sorry nauliza)????Una-act kwamba unahamasisha ila ukweli kagera mnamisifa....yaani mnakera sana tu....
    1.piga picha za wanyama, milima ili utuvutie na sisi huku .
    2. Tuambie gharama ulizotumia kwa ziara yako hiyo na my wife wako huko.Ili na sisi Tujipange.

    we vipi??
    Haya sasa tukianza kusema na shemeji yetu mnalalamika.NI VP ???

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 31, 2008

    We ananymous July 31, 2008 1:08 PM, ndo ziro kweli wewe. Misifa ya mtu unayoisema me hata siioni hapo. Kuhusu mtu katumia kiasi gani hiyo ndo misifa yenyewe ambae yeye hakuweka lakini wewe kwa kutaka sifa kivyako unataka aweke. Bukobha kwao wewe inakuhusu nini, kama huna kwenu nenda Manzese, au kamwombe Karugaba ukae kwake.

    Alafu kutulete picha za wanyama hapa bloging ndo nini sasa. Wanyama kila siku picha zao zinatoke wapo huko porini kwao. Me naona walivyotuwekea za kwao ndo safi. Coz inaonyesha kuwa kuna binadamu kaenda kutembelea mbuga. We mlugaluga kweli. Pole sana na kwa umbumbu, tongo tongo hazijakutoka.

    Kama unatofauti zako na kabila fulani, si lazima uzionyeshe kila mahali. Kwa taarifa yako hata mtu mbaya usie mpenda bado na manufaa flan flan kwako.

    Mtu we eboo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...