deus mallya anayetuhumiwa kuwa dereva wa gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha wangwe
juu mwili wa marehemu chacha wangwe ukitolewa hospitali ya wilaya ya tarime baada ya kufanyiwa uchunguzi wa pili na mtaalamu aliyeletwa na familia ya marehemu, kwa mujibu wa mdau jacob mugini aliyepiga picha hizi
ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu chacha wangwe wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa sababu ya kifo cha wangwe nje ya hospitali ya wilaya ya tarime

DEUS Mallya (27) ambaye anatuhumiwa kuwa dereva wa gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha alyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Wangwe Jumatatu usiku, jana alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuendesha gari kizembe na kuendesha gari bila kuwa na leseni.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Dodoma, Mh. Moses Mzuma.

Mwendesha mashtaka, Mrakibu Msaidizi wa polisi Polycarp Urio alidai mahakamani hapo kwamba Mallya alifanya makosa hayo Julai 28, 2008 eneo la Pandambili, kiasi cha kilomita 100 toka Dodoma, katika barabara kuu ya kuelekea Dar.

Mallya alikana mashtaka yote na amerejeshwa rumande hadi Agosti 14 kesi hiyo itaposikilizwa tena.

Utata mkubwa ulighubika ajali hiyo kutokana na madai tofauti ya nani alikuwa dereva wa gari hilo dogo. Mtuhumiwa alikana kwamba hakuendesha yeye, wakati mtoto wa marehemu Zakayo Chacha alidai ni yeye Mallya aliyekuwa dereva.

Utata huo uliepelekea kufanyika upya kwa uchunguzi wa kubaini sababu ya kifo cha Marehemu Wangwe, lakini mtaalamu aliyeletwa na familia ya marehemu alithibitisha kwamba kifo hicho hakikutokana na majeraha ya risasi kama ilivyokuwa ikidaiwa, bali kwa majeraha ya ajali hiyo.

Marehemu Chacha Wangwe hatimaye alizikwa jana huko Tarime, ikiwa ni baada ya mazishi yake kuahirishwa kwa siku moja ili kupisha uchunguzi wa kina ufanywe kwanza na mtaalamu huru aliyeletwa na familia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mtoto wa marehemu mbunge hakuwepo safarini sasa alijuwaje kuwa Mallya alikuwa anaendesha gari hilo? pia kama ni kweli mbunge gani huyu anayempa udereva mtu ambaye si dereva! hana leseni, hatuoni huo ni kama uzembe? hata KAMA ANAKOSA HASTAILI ADHABU KALI HAPO, KWANI KOSA NI USHIRIKA KATI YAKE NA MBUNGE.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na masikitiko yangu makubwa. Swali langu ni kuwa MBUNGE ataendeshwaje na DEREVA hewa..asiyekuwa na leseni? Jamani hamuoni hapa kuwa kuna uzembe mkubwa sana. Yaani Mbunge mzima anaajiri dereva asiyekuwa na Leseni? Sasa nani wa kulaumiwa kuhusu kifo chake? Hakuna background check yoyote kabla dereva hajaajiriwa? Hapa kuna jambo...!!

    ReplyDelete
  3. Jamani justice should take its course.
    While we sympathize with wafiwa we should be very careful.
    Mallya should also be treated as a Tanzanian and not as scapegoat of others' mistakes.
    kama alikuwa anamwendesha marehemu, huoni ni kosa la marehemu kukubali kuendeshwa na dereva asiyekuwa na leseni?
    watoto kumwona Malya ameondoka nyumbani akiwa anaendesha gari maanayake hawezi kutoka kwenye usukani mpaka safari iishe?
    Msisahau "what goes around comes around", mnachowafanyia wengine kitawarudia tu nanyie.
    Watch out !!!

    ReplyDelete
  4. nawapa pole sana kwa familiya ya wafiwa.

    sweet,

    Arusha.

    ReplyDelete
  5. This story about Mallya being the Driver without a Driving Lisence driving an MP as smart as Wangwe does not click in my mind!You will forgive me for that.Some of us are born that way,Very Hard Believers but not Doubting Thomases!Now that Chacha Wangwe is gone for keeps,there is nothing much that we can do about it!But what made the Hiring of Scotland Yard so difficult in the circumstances?Tusichukulie kila jambo kiholela tu,aah,ilikuwa kazi ya Mungu!Boyz,this World is so dirty and filthy!Kikulacho Ki Nguoni Mwako.Watch Out!

    ReplyDelete
  6. Nchi yetu bwana kweli kazi bado ipo.

    Ninacho jua mpaka sasa Tanzania tuna maabala ambayo wanaweza kuchunguza alama za vidole kwenye usukani wa gari na hivyo kusaidia kujua nani alikuwa anaendesha.Maana kutokana na mahojiano ya Mallya anasema hajawahi kugusa usukani wa gari ya marehemu.

    Pili ni kiasi cha baada ya tukio kuchunguza sehemu ya kitambaa cha kiti cha mbele kulia ..nina uhakika damu za kumwaga ili vipimo vya DNA kubainisha nani alikuwa alikaa hapo.

    Mwisho ili swala lipo wazi,Mallya unaweza kuta ndio wale vijana "wapambe" wa waheshimiwa.Na ukweli utajulikana huyo dogo ni kweli ajali inatokea alikuwa anaendesha.Kaona hana leseni ndio ikabidi abadili habari.

    tutafika tu.

    RIP Ras Chacha Zakayo WANGWE

    ReplyDelete
  7. Nasaport comment zote hapo juu.

    ReplyDelete
  8. Madereva wote wa wabunge wakaguliwe kama wana leseni. Ingawa ajali haisababishwi na kuwa au kutokuwa na leseni lakini hii itasaidia kupunguza maswali yasiyo na majibu.
    Halafu nauliza, Familia ya Chacha Wangwe inaishi Dodoma?

    ReplyDelete
  9. Kifo cha mbunge huyu ni kilio kikubwa kwa family yake na jumuia nzima ya wapenda maendeleo. Ila hii tabia ya Madingi kuendeshwa na watoto/vijana ambao hawana leseni ipo sana Bongo. Enzi yetu ilikuwa fahari kwa baba zetu kuletwa St. Peters/Joseph kanisani (na katika maharusi na get together nyingine) na first borns ambao majority walikuwa hawana leseni. Na traffic police gani anaweze kuhoji dereva anaemwendesha Big Boss? Hivyo naona kosa kubwa ni la mbunge marehemu aliyempa huyu bwana mdogo gari yake ili aendeshwe. Inaonyesha hiyo haikuwa mara ya kwanza kumkabidhi gari.
    Kwa wale wanaokumbuka: Hivi Senyagwa alikuwa na leseni alipopata ajali?
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  10. kwanza ningependa kutoa pole kwa wafiwa.
    Pili ningependa kuuliza kwani wakati ajali inatokea si kuwa watu walikwenda eneo la tukio sasa walimkuta nani amekaa upande wa Dereva maana wasitake kuwatia watu wengine hatiani wakati hiyo ni mipango ya molla.sasa kumuweka kijana wa watu rrumande si kumuaribia maisha yake naona swala hilo liangaliwe kwa makini.
    Mchangiaji.

    ReplyDelete
  11. Tatizo hapa ni "U-bwana mkubwa" umezidi sana huko Bongo. Hakuna sababu yoyote ya kimsingi inayoweza kunielewesha kwanini katika nchi changa kama yetu, wabunge wasiendeshe magari yao wao wenyewe.

    ReplyDelete
  12. wanambabatiza tu kuua soo, tena hiyo inaongeza utata zaidi!

    ReplyDelete
  13. Jamani, hebu tujiulize. Hivi Mbunge anaweza kukubali kuendeshwa na dereva asiye na leseni kweli, tena safari ndefu kati ya Dar na Dodoma ? Tukumbuke hii ni safari ya masaa karibia matano.

    Hili la leseni limewekwa ikiwa ni cover-up ya real identity ya the real name of the driver. Ukipata leseni halisi ya "Malya", umepata jina lake halisi na habari zake zote nyingine.

    ReplyDelete
  14. ISSA KWANINI UNA UPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA KWA KUNGANGANIZWA ETI DEREVA ALIKUWA HANA LESENI..KAMON MEEN DON LAI TO PIPLE MEN WE NO THE TRUTH. NINA KOPY YA UJUMBE HUU KAMA HUTO UTOA.

    ReplyDelete
  15. Hivi bongo manafikiri nani ana leseni? Kutoa leseni bongo wanaona ni ujiko kweli kumbe wangeweza kucontrol madereva wenye maajali na kujua kila dereva anaelewa sheria za barabara.....

    Leseni huna hongo hupati wewe... hivyo mtu anaamua kujiendeshea tu gari. Mtu anaimport gari au anapelekewa gari zawadi na watoto wake lakini wala hawajali kuwa analeseni au la. Bora umelikomboa bandarini ni lako. Atakayeliendesha wala hawajali..

    Kama wameweza kubadili passiport...naona ingefaa kuanzisha lessen kwanza siwe hivyo hivyo za finger print. Na iwe kwa kila mtanzania anayequalify na wasiotaka kuendesha basi wapewe tu ID za mkoa .....

    Wakulaumiwa sio huyu kijana ...Ni system mbovu iliyopo

    ReplyDelete
  16. Mdau hapo juu hiyo comment ya lesseni apewe kila mtu mimi mmmmm!!

    Cha msingi sema leseni ziandaliwe utarabibu wa kudhibiti. Kwani ukiwa na kuanzia 70.000 hadi 100,000 hata kama hujui gari inawashwaje unapata leseni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...