kwa furaha na tadhima napenda kuwatambulisha wadau kwa mkatuni nathan mpangala ambaye kaibuka na globu mpya ya katuni zake motomoto. mtembelee hapa: http://nathankatuni.wordpress.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wanafunzi waandamana

    2008-08-02 09:39:22
    Na Godfrey Monyo


    Mamia ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam, jana walivamia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa maandamano wakipinga ongezeko jipya la nauli.

    Wanafunzi hao walikusanyika katika ofisi hizo kuanzia saa 4:47 asubuhi huku wakiwa wamebeba mabango yenye kulaani ongezeko hilo.

    Maandamo hayo yanakuja siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), kupandisha nauli za wanafunzi kutoka Sh. 50 hadi Sh.100 na watu wazima kati ya Sh. 400 na 600 kutegemeana na umbali.

    Ongezeko hilo kwa mujibu wa SUMATRA, linafuatia kupanda kwa gharama za mafuta na vifaa mbalimbali vya magari.

    Tukio la wanafuzi kuvamia ofisi za Mkuu wa Mkoa, limekuja siku moja kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika na kuzuiwa na polisi.

    Wengi wa wanafunzi hao walikuwa wamevalia sare zao za shule bila kujali askari waliokuwa na silaha za moto eneo hilo.

    Wanafunzi waliokuwa kwenye maandamano hayo ni wa za shule za Sekondari za Jangwani, Msimbazi, MOA, Benjamin Mkapa, Tambaza, Makongo, Gerezani na Islamic.

    Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na magari matano, walionekana kuwa tayari kudhibiti vurugu zozote ambazo zingetokea.

    Namba za magari hayo ni PT 1516, PT 0890, PT1438, PT1523, PT0886 ambalo lilokuwepo maalum kwa kumwaga maji ya kutoa machozi.

    Mabango waliyokuwa wamebeba wanafunzi hao yalisomeka ``Nyerere fufuka ufisadi is too much`` lingine lilisomeka ``Serikali gani inakaba hata penati, maisha bora kwa mafisadi.``

    Mabango mengine yalisomeka ``Tumeamini kuwa, serikali yetu haina huruma,`` lingine lilisomeka kuwa ``Kikwete tuokoe tunakufa`` na ``we need social servises``.

    Aidha, wanafunzi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumkumbuka hayati Mwalimu Nyerere ikiwemo iliyokuwa ikitumika katika migomo ya vyuo vikuu.

    ``Kama sio juhudi zako Nyerere?kama sio juhudi zako Nyereremafisadi hawa wangetoka wapiiiii ``.

    Katika hatua nyingine, uongozi wa Umoja wa Wanafunzi Tanzania (TASO), ulisema hawautambui mkusanyiko huo.

    Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Augustino Materu, alisema maandamano hayo hawayatambui kwa sababu bado walikuwa katika majadiliano na viongozi wa serikali.

    ``Sisi tulikuwa kwenye majadiliano na wakubwa ghafla tunaambiwa kuwa wapo wanafunzi wenzetu wamekusanyika hapa wakitaka kumuona mkuu wa mkoa,`` alisema.

    Aliwataka wanafunzi wenzake kuvuta subira wakati suala lao likiwa liatafutiwa ufumbuzi na hasa katika kipindi hiki walichopo katika majadiliano na serikali.

    Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na wanafunzi waliokuwa kwenye maandamano hayo wakidai kuwa ni wasanii na kamwe hawawezi kuwatetea.

    ``Hawa ni wasaliti wamekwenda huko wamelegezwa kwa kupewa kitu kidogo, sasa wanataka kutulegeza na sisi hapa ni mpaka kielewe alisema mmoja wa wanafunzi hao.

    Hata hivyo, wanafunzi hao waliondoka katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa maadamano na kuelekea katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, ambapo walijikusanya wakiwasubiri wenzao waliongia katika majadiliano.

    Akizungumzia hatua ya wanafunzi hao kuandamana, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Kova, alisema awali walipanga kuandama leo na si jana kama walivyofanya.

    Na katika hatua nyingine, nauli mpya za mabasi jijini Dar es Salaam, zimeanza kuonyesha makali yake baada ya wasafiri kulalamika kuwa imepanda kinyume na matarajio yao.

    Wananchi hao wameiomba (SUMATRA) kuangalia upya suala hilo ili kuwanasuru katika adha hiyo.

    Nauli zilizolalamikiwa ni za Kigamboni kwenda Pembamnazi ambapo wanatozwa Sh.1,500 na Kigamboni kwenda Mbutu\Kichangani, Sh. 800.

    Mbagala Rangi Tatu kwenda Mvuti nauli ni Sh. 800 wakati wasafiri wa Buguruni kwenda Mvuti walilipa Sh. 1,000.
    Njia ya Kivukoni kwenda Tabata Kimanga walitozwa Sh.700 na Kigamboni Kimbiji walitozwa Sh. 1,000.

    Nauli hizo zimeonekana kuwachanganya wasafiri wengi kutokana na kuelewa vibaya agizo la SUMATRA kuwa zingekuwa kati ya Sh. 300 hadi Sh. 600 na wanafunzi watatozwa Sh. 100 badala ya 50.

    SUMATRA imeahidi kusimamia zoezi la kubandika majedwali yenye taarifa za nauli mpya.

    ReplyDelete
  2. Hongera Nathan!!

    On a topic related to your cartoons here; wimbi la kuanguka kwa majongo katika miaka ya karibuni linatisha kwakweli, mwishowe watu tutaogopa hata kwenda katika shughuli K'koo.

    Makandarasi wazawa wamekuwa kwa miaka mingi wanalalamika kuwa hawapewi tenda na wanashindwa jinsi ya kujikwamua. Ninakubali kweli walikuwa hawathaminiwi kwa miaka mingi. Lakini hizi projekt chache walizopata baadhi yao wanatia kitumbua mchanga. Yaani watu hawafikirii mbele kabisa; mtu anaona bora aibe milioni chache kwa kubanie saruji katika zege; matokeo yake anaangusha ghorofa. Kesho na keshokutwa watu wanashindwa kukupa kazi zaidi. Yaani milioni chache unazozibania leo zinakukosesha mabilioni siku za usoni.

    Hii sio kwa wote, ila wale wachache mnaoharibu sifa ya weledi wenu na mnakosesha hata wenzenu kula. Fanyeni kazi kwa uaminifu na maadili na mafanikio yatakuja. Tamaa ya mafanikio ya haraka itawapeleka jela mwishowe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...