MAREHEMU CHACHA WANGWE, ALIYEKUWA MBUNGE WA TARIME AMBAYE ALIFARIKI DUNIA MAJUZI KWA AJALI YA GARI HUKO DODOMA, HATIMAYE AMEZIKWA RASMI LEO KIJIJINI KWAKE KEMAKORERE.
MAZISHI HAYO YAMEWEZA KUFANYIKA BAADA YA MTAALAMU WA UCHUNGUZI WA MAITI ALIYEITWA NA FAMILIA KUTHIBITISHA KWAMBA MAREHEMU CHACHA WANGWE HAKUUWAWA KWA RISASI BALI KWA MAJERAHA ALIYOYAPATA KUTOKANA NA AJALI HIYO.
WENYEVITI WA CUF, PROFESA IBRAHIM LIPUMBA, MH. JAMES MBATIA (NCCR-MAGEUZI), MH. AUGUSTINE LYATONGA MREMA NI BAADHI YA VIONGOZI WA SIASA WALIOHUDHURIA MAZISHI HAYO JIONI HII.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. afadhari imekuwa hivyo maana kama majibu yangekuwa tofauti na tulivyotarajia basi chacha wangwe angekufa na wengi maana hali inaonekana ilivyokuwa mabya toka jana kwenye mazishi .lakini pia nadhani ni wakati wa kujifunza kwa kila mmoja wetu mimi sikuona sababu ya watu kuvumisha kuwa chacha ameuwawa kwa risasi wakati mazingira yote yanonyesha kuwa ilikuwa ni ajali ya kawaida tu,ila katika moja ambalo hata mimi sikubaliani nalo ni kuwa chacha wangwe alikuwa anaendesha gari wakati hiyo ajali inatokea huyo kinaja mallya ndiye aliyekuwa anaendehs ahilo gari nadhani ni woga tu kwa kuwa labda hana leseni au pia anaogopa kusumbuliwa na vyombo vya usalama na bahati mbaya sana mtu aliyekufa ni mtu mashuhuri ,nadhani hili swala sasa limefungwa kilichobaki ni polisi kuhangaika na huyo malya kuhusu kuendesha gari bila leseni sisi wadau mjadala tunaugauzia kwa mafisadi .

    ReplyDelete
  2. Buriani Chacha!

    ReplyDelete
  3. Suala zima lina utata! Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayesema kauliwa kwa risasi hata kama ni kweli. CV ya Mallya iwekwe hadharani. Full Stop.

    ReplyDelete
  4. tumeridhisha na habari za uchunguzi kwani hicho ni kifo cha kawaida ila CCM na magazeti yake(Majira,Mwananchi,daily news na mengine mengi yanashabikia habari hii ili ionekane ni CHADEMA ila mungu mkubwa ukweli umejulikana walitaka tusahau mambo ya ufisadi sasa wadau nawaambie Wangwe katangulia sasa turudi tujajidi ufisadi
    Habari ndo hii! CCM bado tunanyie
    mpaka sera ya MAISHA BORA KWA KILA FISADI itokomee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...