Hatma ya kundi la wachekeshaji maarufu kama Ze Comedy itajulikana Jumanne Mahakama itakapotoa uamuzi kama wasanii hao waendelee na shughuli zao au la.
Uamuzi huo ulikuwa utolewe jana kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, haukutolewa kutokana na Jaji Catherine Urio anayesikiliza kesi ya msingi kuwa katika safari ya kikazi.Kundi hilo liliiomba Mahakama kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao wakati kesi ya msingi inasikilizwa.
Kesi iliyofunguliwa na kundi hili ni dhidi ya Televisheni ya EATV, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) pamoja na Msajili wa Nembo za Biashara, likiomba Mahakama iwazuie kuingilia biashara zao na kuruhusu kutumia jina lao.
Pia waliitaka Mahakama kutoa tamko kuwa walalamikaji ni wamiliki wa jina la Ze Comedy kabla na baada ya kuingia makubaliano na kulipwa fidia ya Sh milioni 200 na walalamikaji kutokana na usumbufu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...