JK ameagiza huduma za kijamii zipelekwe nje ya Jiji, ili kuepusha msongamano. Aliyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika Machinga Complex Ilala, Dar (pichani).
Jengo hilo linaendelea kujengwa eneo la Ilala sehemu zilipokuwa kota za UDA mtaa wa Lindi.
Machinga Complex inayojengwa na uongozi wa Jiji la Dar pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ni wazo lake JK alilolitoa mwaka 2005 mjini Dodoma.
JK alisema kutokana na msongamano uliopo jijini, haina maana tena kufikiria kujenga jengo kubwa kama hilo tena mjini.
"Mkilazimika kubomoa nyumba, bomoeni tu, mradi utaratibu unafuatwa wa kisheria na kijamii, lakini lazima tukubali kwamba mji unakua na katika maendeleo yoyote ni lazima upande mmoja upate msukosuko, kusemwa, lakini matunda ndiyo kama haya," alisema.
Aliwataka watendaji wasiogope maneno yanayoandikwa ama yatakayoandikwa magazetini kutokana na hatua mbalimbali watakazochukua kwa ajili ya upanuzi wa mji, lakini akawaonya tabia ya kuwahamisha watu kwenda nje ya miji bila kuwapatia huduma siyo sawa.
"Mnawapeleka watu Bunju, Tuangoma, lakini hamfikirii hao watu watatibiwa wapi, maji yako vipi, umeme hampeleki halafu mnawalazimisha waondoke waende huko, hii si sawa, pelekeni huduma za kijamii nje, lakini ziambatane na miundombinu bora," alisisitiza JK.
Aliuagiza uongozi wa Jiji chini ya Meya wake Alhaj Adam Kimbisa, kuhakikisha kuwa majengo mengine madogo kuliko hilo lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 10,000 yanajengwa katika Manispaa ya Temeke na Kinondoni, pia kutaka uwazi ufanyike wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...