Brother Michuzi Mimi nina hoja ndogo sana kwa wadau wa blog yako. Hasa maada yangu inahusu kinadada ambao mara kadhaa unapotoa picha za wanandoa or sherehe za harusi, wao hupenda kuuliza hao waume wenzao wanawatoa wapi?
Kitu kimoja ambacho nasema nikwamba hivi ni kwanini wanawake wanakaa wanasubiri mpaka wafuatwe kuombwa kuolewa badala ya wao kuchangamka tu? wengi unakuta wanawajua wanaume ambao wangependa wawaowe badala ya kuwafuata wakawaambia , wao wanakaa na kuwateg mitego ambayo sometimes badala ya kutoa picha mzuri inaonesha wewe kicheche!!
Unajuwa kulingana na jinsi ninavyoona mimi, wanaume na wanawake wengi wamebaki kutegana tu.
sometimes wanaume fulani wanamzimia binti lakini wanahisi huenda hapatikani, na utakuta same bint anamuwazia same man.. naona wanawake kama watachukua step mbele basi mafanikio yatakuwa mengi sana.. just njoo sema kaka G7 mimi nakuzimia nataka uwe wangu ... then subiri.
nadhani ukijaribu sita utafanikiwa nne then who knows!!kama kukataliwa just ni maisha tu, hata wanaume hukataliwa na huwa tunasonga mbele kwani siku hazi gandi!! nimewaambia dada zangu kama watapata mtu wakashindwa kwenda basi waniambie nitamuendea nao wanasuasua!!
haya maisha ya woga yatawaisha lini mabintiiiiiiiii?
Ni hayo tu wadau!!!
Ni hayo tu wadau!!!
G7
UK
Wow! this is good. Mimi naona hao wanaouliza wengine sio kuwa hawana waume. Wengine swali lao ni kuwa ni vipi mwanaume anaweza kuamua kukuoa au ni muda gani kusubiri ukiona haleti ring ukimbie?
ReplyDeleteUnajua kama sis wanamke tukipenda tunapenda kweli na mimi nina rafiki yangu but I wonder when or how long he will finally pop the question. Au ni mimi nimforce, pressurelized au just run from this.... Na kaa kimya nikifuata culture zetu lakini naona mh! Ila saa nyingine nawaza isijekua mtu ananitake for granted.
Nashangaaga kuona mtu anampata mwanaume leo mwezi ujao wanaoana lakini pia nafikiri muda wa kufahamiana vizuri ni kiasi gani ikiwa wote mmeshamaliza shule na mko kwenye career?????
HOW LONG IS TOO LONG?
salama ndugu zangu?
ReplyDeletemimi sijawahi ku-comment hata mara moja katika blog hii....japo mada nzito huwa zinawakilishwa lakini nadhani hii imenikuna na imenikuta katika mood nzuri na nikiwa na vidakika kidogo vya kubofya.
naomba nimshukuru mtoa mada....na niongeze kuwa kina dada lazima waonyeshe dhana ya "wanawake wana haki sawa na wanaume" kwa vitendo.
nwezaje kusema una haki sawa na mwanaume wakati hata haki ya ku-initiate uhusiano huna? mi nadhani hili ni jambo la msingi kabisa lakini nalo wamekuwa hawaliwezi....matokeo ni kuolewa/kuwa na mtu usiyempenda eti kwa sababu uliyempenda hakukutongoza.
mimi naamini katika nguvu ya wanawake na kwa kuwa wao hawakurupuki katika suala la kimapenzi wanaweza kuoa chaguo zuri.....unajua sisi wanaume tamaa mbele mapenzi hufuata.
ladies first....hebu fanyeni hivo basi
In "MOST" cases mwanamke anayejiheshimu na kuwa mnyenyekevu anaolewa....tatizo ni kuwa wanawake wengi siku hizi wajuaji hasa baada ya kuelimika na kuona kuwa wanaweza kupata kazi nzuri kama wanaume au zaidi. Wanawake wanaojua wajibu wao na kuheshimu wanaume regardless ya elimu yao wanaolewa...ila nasisitiza "in most cases" kwavile sio wote wenye hiyo bahati. Mimi nimesikia kuwa yule Naibu katibu mkuu wa UN Asha Rose Migiro ni kati ya wanawake ambao wanaheshimu sana ndoa zao japokuwa amepata cheo cha juu sana. Inasemekana kuwa huwa anatoka kazini on time kwenda kumpikia mumewe na kazini kwake wanajua kuwa hakuna kitakachomfanya awaache ma-house girl wampikie mumewe. Well, hapa nimeenda kwenye ndoa...lakini ili mwanamke aolewe, Lazima KIBURI na MAJIVUNO yaishe....halafu..lazima kujiheshimu siyo kubadili wanaume kila siku. Kuna tofauti kubwa sana mwanamke anapobadili wanaume na mwanamme anapobadili wanawake...kama hawakubali haya nawapa muda watakubali watakapogundua wamebaki...Asante sana. Mdau...CALIFORNIA-USA
ReplyDeleteJamani wewe kaka umetoa point!!ingekuwa sijaolewa haki ya mungu ningefanya hivyo!!anyway wadada wengi wanafikiri kuuliza kuomba kuolewa ni umalaya,kumbe sivyo!kuna wanaumme wengine wako shy pia kumwambia dada nakupenda!!wapo wakaka wengi tuu maungkaren i mean bachelour wanaogopa wanawake..ebu wakina dada tuamke kuanzia leo...asanteni mdau
ReplyDeleteWe annon hapo juu kumpikia mume sio kumuheshimu!!hata wewe kama umekaa ulaya utaona haki sawa majukumu kwa wote!!kwanini na wewe usiwahi nhyumbani kumpikia mke?kwani wewe tuu ndie unaehitaji haki???acha ushamba bwana...
ReplyDeleteWewe mdau hapa juu nadhani bado hujaolewa na kama upo single ukiendelea na tabia hiyo na kama baadhi ya wanawake wengine hutaolewa. Wanaume wengi kama mdau aliyepita juu alivyosema huwa ni watu wako shy na hawapendi mwanamke mwenye kiburi. Dunia ya leo inabidi muenziane wote pande mbili na kupika ni sehemu ya mapenzi mama acha ujinga. Ujuavyo sie wanaume wengi either hajui kupika au anapenda kupikiwa na mkewe kinakuwa chakula kitamu zaidi. Jitahidi dada yangu kuwa mnyenyekevu amasivyo utakuwa msela hadi uzeeni shauri yako na mambo yako ya usawa.
ReplyDeleteNi bahati mbaya/au nzuri kwamba si wanawake wote hubahatika kuolewa. Kwa hiyo ni kama ushindani. Muonekano na tabia njema ya mwanamke ndiyo kitu ambacho wanaume hutafuta. Tabia njema za mke mzuri ni pamoja na heshima, unyenyekevu, kujitolea nk. Tukisema kila kitu anachotaka mwanaume afanyiwe na mwanamke naye amfanyie mke vivyo tutakuwa tunapotea maana maana tuko tofauti. Na kama tuko sawa (jenda ikwalite) basi HAKUNA MWANAUME ALIYETAYARI KUOA 'MWANAUME' MWENZAKE.
ReplyDeleteTangazo kwa wadada wote wanaoingiza Ubeijing kwenye mambo ya uhusiano wahesabu maumivu maana mwanaume hutaka kuoa mwanamke submissive. Hakuna mwanaume aliye tayari kuleta Olimpiki ndani ya nyumba.
Great topic!sijawahi kuacha ujumbe katika blogu, lakini, as a guy who sees this all the time, nimeona bora nichangie tu, nafsi iridhike.It's true kuna majamaa wengi tu ambayo wako shy, kwa hiyo uwezo wa kumwapproach mwanamke ni ndogo, unless labda mwanamke asogee kidogo kwanza.In the olden days, wazee walishajua mtoto wao yuko vipi, so waliona character type yake toka akiwa mdogo, ndipo wanaanza kazi ya kumsaka binti/mwanaume atakemfaa kijana wao; kumbuka kuoa si individual, yaani huoi mtu moja, unaoa familia nzima. Kwa hiyo, walikuwa wanachukua uamuzi mzito baada ya kufanya research ya kutosha, na kuobserve pande zote mbili kwa ujumla. You might say niko old-fashioned, but remember this: when you go to do shopping, you research price, company,quality, location, discount etc. etc. kwa kitu ambacho utatumia muda mfupi mno. Lakini katika suala zima la kuoa, how much research do you really do?
ReplyDeleteNa kuhusu mambo ya equal rights: do not confuse equal rights na equal roles! Just because you can, doesn't mean it's okay, na haina madhara kwa watoto.If we both go to work for the majority of the day, who watches the children (not watch kama mlinzi, lakini nurturing takes attention), it doesn't mean ni kazi ya kudharaurika, bali ni kazi nzito; but don't get confused kama wenzetu wa ulaya; USA: divorce rates ni 1 in 2, ie 50% ya ndoa zinishia na talaka; je na zile ambazo watu hawaelewani ndani lakini hawataki kuachana for various reasons??
mmmh hivi vi swanglish navyo mmmh,yangu macho tu.Bora mchanganye kiswahili na kiluga
ReplyDeleteHii maada mimi naona ni yauchokozi tu kwani haina maana hata kidogo kwa mfano, nyinyi wanaume mnataka muanze kutongozwa na hapo hapo mnataka mheshimiwe sasa basi itakuwa na maana gani??
ReplyDeletemimi nikutongoze na nikuowe unamaana na mahari nikaripe kisha kila siku niende mbio kukupikia hii ni mambo gani??
kwanza wanaume walio wengi hawana adabu hata akimtongza mwanamke ataishia kumtangaza ooh mara demu anajifanya mjanja nikimwabia aje haji mpaka atake mwenyewe bila kujali kuwa hao mademu wanauangalizi tofauti na wanaume makwao.
kwa ufupi ni hivi hayo maoni yako hayafai ktk jamii ila yapeleke ktk family yenu.
au kama unataka umaarufu kazana kila la kheli kwawanaokuona unamaana.
Hii maada mimi naona ni yauchokozi tu kwani haina maana hata kidogo kwa mfano, nyinyi wanaume mnataka muanze kutongozwa na hapo hapo mnataka mheshimiwe sasa basi itakuwa na maana gani??
ReplyDeletemimi nikutongoze na nikuowe unamaana na mahari nikaripe kisha kila siku niende mbio kukupikia hii ni mambo gani??
kwanza wanaume walio wengi hawana adabu hata akimtongza mwanamke ataishia kumtangaza ooh mara demu anajifanya mjanja nikimwabia aje haji mpaka atake mwenyewe bila kujali kuwa hao mademu wanauangalizi tofauti na wanaume makwao.
kwa ufupi ni hivi hayo maoni yako hayafai ktk jamii ila yapeleke ktk family yenu.
au kama unataka umaarufu kazana kila la kheli kwawanaokuona unamaana.
Nami leo naweka maoni, LIWALO NA LIWE bwana alaaa!!
ReplyDelete1. Mwanaume "smart" hahitaji sana kuambiwa na mwanamke "nioe". Wanawake wanatumia mbinu nyingine ambazo ni natural. Ni jukumu la mwanaume ku"sense" na kuelewa. Hata hivyo kuna watu tofauti, wengine wanaelewa kwa ishara tu, wengine mpaka wasikie na wengine inabidi umchoree ubaoni. kwa vyovyote, inabidi mwanamke awe mwangalifu sana kabla ya kutumia maneno.
2. Ni kweli wanaume 99% tunapenda wanawake submissive. Dalili yeyote ya "Olympic" au Ubeijing kutoka kwa Mwanamke wakati wa urafiki ni tiketi ya kuachwa. (mfano mzuri ni kuongea kwa sauti ya juu/ kumfokea mwanaume anapochelewa etc)
3. Utani ni silaha muhimu. Vitu vyote "serious" vikifichwa kwenye utani vinasemeka na kueleweka kirahisi. (Mfano wakati wa kutaniana mwanamke akataka kujua ni lini ataolewa etc) Kama mwanamume/mwanamke huna uhusiano naye kabisa na unampenda, utani pia ni approach nzuri. Ukimuita jina la utani "Mr. Wonderful" "Wife" etc ujumbe unakuwa communicated bila tafrani yeyote. Wale wenye "ndita", wanaokunja uso asubuhi hadi jioni na wasiotaniana na mtu 99% yao hukosa wenzi wa kudumu.
HUWO NI UZOEFU WANGU BINAFSI
kama mnaoa ili mpate wa kuwapikia kaoeni huko kijijini kwenu. na kama umeamua kuishi Ulaya usibebe mila zako za kishamba huku First world ukisubiria kupikiwa. watu na career zao they dont care who cooks in the house, wanachojali nani amewahi home, iwe baba/mama atakaewahi apike chakula kinachoeleweka na mboga zamajani atayarishe! na mwanaume kuingia jikoni sio kwamba unanyanganywa uume wako, ni katika kusaidiana ili kulea familia! Ulaya wanawake na wanaume wengi wana make same amount of cash kama kawa! ivo sio zile zama za ujima baba ndio analeta hela. sasa kama kila mtu analeta hela je hamwoni kuwa kuna wakati mama hatakuwa home akitafuta pesa, na kama baba yuko home, basi atasubiri hadi mama arudi hata kama ni usiku wa manane, mh na majuu makazi ya shift ya usiku ndio yanayolipa! sasa ukisema usubiri ur wife wako, utalala NJAA!
ReplyDeletekwa tuliopo tanzania baba hahitajiki jikoni maana kuna wasaidizi/maids wa bei rahisi anafanya kazi zote za ndani hadi za kumwagilia mchicha na kuangalia kuku na ngombe, na pia kuna extended family apo unakuta mnaishi na ndugu apo wanasaidia kazi. Ulaya/majuu kwa ujumla hiyo huduma haipo, ivo ni nyie wanandoa wawili mchakarike.
i for the one who could appreciate a great deal if a decent girl could just approach me and say" hi!i have a feeling for you,can't we establish a serious relationship?" then after we have known each other's past and present it won't resist me to pop up and say gently"hi!will you marry me plz" thats all, is done!!
ReplyDeleteu know why? b'se iam shy too!
inategemea na uelewa wa mwanaume pia mwingine ukimwambia hivyo atahisi wewe malaya na unawinda ila kama ni muelewa wa mambo atakuelewa
ReplyDeletemfano mzuri ni mimi niko kwenye uhusiano kwa miaka nane sasa na tuna mpango wa kufunga ndoa 2010 na mimi ndiye niliyeanza kumwonyesha jamaa kuwa nimemzimia na nampenda si lazima kutumia maneno ila matendo speaks more than words sikwambii mdada ukamwambie umpendaye waziwazi kama wenyewe wanavyotutongoza haileti picha nzuri ila mshawishi kwa matendo kama ya kumjali kwa vitu vidogo vidogo mpaka mwanaume atabwaga manyanga mwenyewe kama nilivyofanya mimi
kweli wanaume wengine wana aibu na ni wapole sana ila jaribu kumfanya ajisikie mwanaume kwa kauli zako(kauli za mwanamke zinaweza kumjenga au kumbomoa mwanaume)
ukiona hasemi kitu kauchuna tu mshukuru Mungu na uendelee na maisha yako si mwisho wa dunia huo