Brother Michuzi Mimi nina hoja ndogo sana kwa wadau wa blog yako. Hasa maada yangu inahusu kinadada ambao mara kadhaa unapotoa picha za wanandoa or sherehe za harusi, wao hupenda kuuliza hao waume wenzao wanawatoa wapi?


Kitu kimoja ambacho nasema nikwamba hivi ni kwanini wanawake wanakaa wanasubiri mpaka wafuatwe kuombwa kuolewa badala ya wao kuchangamka tu? wengi unakuta wanawajua wanaume ambao wangependa wawaowe badala ya kuwafuata wakawaambia , wao wanakaa na kuwateg mitego ambayo sometimes badala ya kutoa picha mzuri inaonesha wewe kicheche!!


Unajuwa kulingana na jinsi ninavyoona mimi, wanaume na wanawake wengi wamebaki kutegana tu.


sometimes wanaume fulani wanamzimia binti lakini wanahisi huenda hapatikani, na utakuta same bint anamuwazia same man.. naona wanawake kama watachukua step mbele basi mafanikio yatakuwa mengi sana.. just njoo sema kaka G7 mimi nakuzimia nataka uwe wangu ... then subiri.


nadhani ukijaribu sita utafanikiwa nne then who knows!!kama kukataliwa just ni maisha tu, hata wanaume hukataliwa na huwa tunasonga mbele kwani siku hazi gandi!! nimewaambia dada zangu kama watapata mtu wakashindwa kwenda basi waniambie nitamuendea nao wanasuasua!!


haya maisha ya woga yatawaisha lini mabintiiiiiiiii?
Ni hayo tu wadau!!!

Mdau G7

UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwanamke kumuona mwanaume kwa mara ya kwanza nakumtamkia kwamba nimekupenda, kwa sisi wasambaa ni jambo la aibu.
    sijui kwa makabila mengine

    ReplyDelete
  2. kwa wanaume wengine kuambiwa anapendwa na mwanamke mwanamke unaonekana ni muhuni na hujatulia kabisa.

    ReplyDelete
  3. G7 Topic yako inaonesha haihusu wanawake ni inaonesha wewe G7 unalilia mtu humu mwambie tu basi uoe utulie G7 anahitaji mrembo kutoka michuzi jamani anashindwa kuongea moja kwa moja. msaidieni. from william UK.

    ReplyDelete
  4. kunavitu ambavyo vinaonekana ni aibu ktk baadhi ya makabila lakini havina maana wala faida kwa sasa,japo zamani ilikuwa na sababu zake.kwa mfano mnaosema ni aibu kumtamkia mwanamme kuwa unampenda je si aibu kwa mumeo kuingia jikoni kukupikia chakula kitamu? au mkuki kwa mchungu,kwa binadamu-nguruwe!!
    ilikuwa mwiko ktk kabila letu mwanamke kutizama juu wakati waume wanaezeka nyumba kwa majani wakidai nyumba itavuja wakati wa nvua,lakini unajuwa sababu ya mwiko huu ilikuwa nini?kulikuwa ngu za kuvaa ni taabu,hivyo suruali iliyochanika ilikuwa kawaida kuvaliwa,ili kuzuia kuona nyeti za muezekaji kama tahadhari ukawekwa mwiko huo.
    PIA ilikuwa ni mwiko kwa mzee kujisaidia choo kimoja na mkwe wake[mke wa mwanaye] na hii ilipelekea vinyesi kuzagaa porini na kusababisha magonjwa ya tumbo n.k lakini je kuna logic yoyote hapa?
    lazima tujifunze kuiga mambo mazuri na kuacha mila ambazo hazina msingi,nzuri tuzidumishe!
    SIONI UBAYA IKIWA BINTI YANGU ATAMPATA KIJANA ANAYEMFAA AKAMTAMKIA ANAMPENDA NA WAKAOANA.
    haya mambo ya kujificha vijana huwa yanawapeleka pabaya,ndio chanzo hata cha kuzagaa kwa HIV kwa kuwa sisi wazazi tunajifanya hatujui kuwa vijanawetu wamekuwa na wanahitaji kuwa na step muhimu ya mawasiliano na mahusiano yenye tija maishani mwao.kama mzazi ninamfahamu mwenzi wa binti yangu ni rahisi kuwasaidia namna ya kuishi,kujiheshimu,kutatua migogoro yao inapo hitajika kufanya hivyo n.k!lakini mkijificha ndio sikumbili tu mmeachana[mnaita vibuti] wala sisi wazazi hatujui uhusiano huo ulikuwepo! mabadiliko ni muhimu na hayakwepeki ktk jamii yeyote duniani ili kuelekea ktk maendeleo,japo pia sio rahisi lakini wenye moyo hujitokeza wakayaleta.

    ReplyDelete
  5. G7 ni noma na topics zako...hehehe. Watu wamenifurahisha sana na comments zao. Mimi binafsi naona haifai kwa mwanamke kumwa-approach mwanaume kwanza na kumwambia anampenda. Yani hii ni law of nature. Hata mtoe mfano sijui wa nchi zilizoendelea...bado sana. Wanawake wajifanyapo wajanja ndo unakuta wanachezewa na ndo maana divorce rates zipo juu sana katika hizi nchi.
    Nina sababu nyingi lakini ntakupa moja tu. Lazima ukumbe sisi wanaume na wanawake ni tofauti sana katika mahitaji yetu. Sisi wanaume kusema kweli hatuwezi kusema hapana mwanamke anapotu-approach na kututongoza. Mwanamke yeye katika relationship atafuta security. Sisi wanaume twapenda uroda. Ngojea nikupe mfano...wangapi hapa mtasema hapana kama msichana kama J-Lopez akikutongoza? Hata kama humpendi lazima utadai unampenda kusudi ule nae uroda tu. Kutokana na hii hali ya ubinadamu wetu, imetokea kuwa natural kwa mwanaume kumfuata mwanamke. Wewe hata ukiangalia katika makundi ya wanyama (ambao binadamu ni mmojawapo) ni wanyama gani ambao majike hufuata madume? Tena wanapigana kabisa kuona nani ni dume kweli. Kutokana na hali hii, kusudi wanawake waweze kujua kama mwanaume anampenda kweli, wame-evolve kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma wanaume na pia kutumia mbinu nyingine mbalimbali kama kuringa kusudi wale kwa kweli tu waweze kuwapata. Nadhani hapo inatoshi...sitaki kuandika kitabu hapa.

    mtoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...