SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUTOKANA NA AJALI YA BASI MKOANI MBEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu 10 na kujeruhi wengine 30 katika Mkoa wa Mbeya.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la Kwitumba Line na Lori la Kampuni ya Dhandoo iliyotokea jana (Jumapili, Agosti 3, 2008) katika kijiji cha Senjele mkoani Mbeya.

“Nimesikitishwa sana na jinsi maisha ya watanzania wenzetu yanavyondelea kupotea katika ajali za barabarani. Napenda kwa dhati kabisa kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu 10 waliopoteza maisha yao katika ajali ya basi la Kwitumba Line na namwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amin,” ameeleza Rais katika rambirambi hizo.

Ameongeza Rais: “ Naomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na nawaombea waliojeruhiwa kupona haraka ili warejee katika maisha ya kawaida. Mwenyezi Mungu awape imani na subira katika kipindi hiki kigumu na huku tukiwaombea ndugu zetu, mapumziko mema peponi.”

Aidha Mheshimiwa Rais amezitaka mamlaka zote zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuimarisha jitihada za kuhakikisha kwamba wasafirishaji wa abiria na mizigo wanazingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani na kuwa makini zaidi na usalama wa vyombo wanavyoviendesha, ili kuepusha ajali zinazoendelea kupoteza maisha ya watu na uharibifu wa mali hapa nchini.

Amina.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

04 Agosti, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwa nini tz kusiwe na kampeni kama nchi za wenzetu za kuzuia ajali za barabarani,naona zimekuwa nyingi.Barabarani kungekuwa na camera na speed limit ya uendeshaji wa magari.Kazi wakubwa kutia pesa mifukoni mwao tu.Pengine ingepunguza ajali barabarani.Kwani tz hata zebra crossing zimewekwa kama pambo,hazifuatiliwi kiutaratibu wake

    ReplyDelete
  2. Best way ya kuzuia hizi ajali ni kuwa na highway double lane one way. Yaani barabara moja inakwenda upande mmoja tu na nyingine inarudi upande mwingine tu. Hii itaepusha magari kukutana uso kwa uso ambapo inakuwa ni risk kubwa kama dereva anayekuja mbele yako atafanya kosa kidogo. Sio tu magari huwa yanapishana kwa speed kubwa lakini pia dereva naakuwa na poor visibility kama ku-overtake, ukungu au dharura yoyote

    ReplyDelete
  3. nafikiri tunahitaji barabara jza kupishana kwenye highways zetu yaani two lane to ways highways. vijana wa hizi phds victer,deo, na wenzako mnasemaje

    ReplyDelete
  4. Rambirambi hazitosadia Mh Rais!!! Cha msingi ni kujenga miundo mbinu ya uhakika. Barabara nyingi ni finyu mno, magari yanapishana kwa karibu sana katika one lane!Wakati umefika kwa serikali kuweka bajeti ya kutosha na kutengeneza "high ways" ambazo zitasaidia sana kupunguza ajali na pia msongamano wa magari........Jamani mpaka afe nani tena ndio tujue kuwa hili ni tatizo sugu?????!!!!

    ReplyDelete
  5. pamoja na yote madereva wanapaswa kulipwa mishahara mizuri kwani mtu anaenda kazini anamgojwa hospotal na hana hela ya matibabu unafikili hakili yake itakuwa wapi mwisho ni ajari.

    mimi nimetembea nchi nyingi sana hawana hizo njia mbili na hawana ajali za mara kwa mara kama hapo tz hivyo wafanya biashara wa usafiri wanapaswa kuangalia usalama wa wateja wao kuliko faida.

    hasara ni kubwa sana sasa aliyepoteza maisha ameacha family inayomtegemea, na aliyenusurika nae yuko hatarini kwa maambukizi ya magojwa yanayosababishwa na damu kama HIV huoni kama ni mbaya sana upate ugojwa ule kwa ajali.

    halafu uangalie sera ya nchi inakwambia mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, sikatai sasa umepata ajali umepata ugojwa guvu utazipata wapi???

    inasikitisha sana yaani ile nchi inatia huruma waliojeruhiwa hawana msaada wowote na waliopoteza maisha hakuna malipo kwa famili zao ambayo yangeweza hata kuwasukuma wafiwa kwa siku chache. utadhani ni ahela kumbe Duniani. mimi naililia sana afrika kila siku kwani watu wa MUNGU wanateseka.

    BABA MUNGU UKO WAPI WATU WAKO TUNAKUFA!!!

    ReplyDelete
  6. naona mpaka afe kigogo namba moja ndo labda watastuka ah!inaudhi na kusikitisha sana kila kukicha habari ndo hizo tu ajali! ajali! salam za rambirambi mara wahusika wamesahau na hawachukui tena hatua!tumechoka kulia jamani kwa uzembe wa watu wachache!!

    ReplyDelete
  7. Pamoja na kuunga mkono maoni ya wenzangu nadhani itungwe sheria kali zaidi ya kuwabana madereva wa magari ya abiria na mizigo. Najua wanasheria watasema wazo hili ni la kibaguzi ila tuliwahi kuwa na sheria ya kuunda kampuni ktk mkoa mmoja tu na ilikubalika. Mambo yanapofikia hali mbaya masuala mengine hufumbiwa macho!!!

    ReplyDelete
  8. Michuzi kwanza natoa pole kwa wahanga wa ajali hizi na familia za marehemu.Pili,mimi siyo mtalaam sana wa mambo ya usafirishaji na barabara,lakini wachangiaji wote kuanzia mwanzo juu kama umesoma vizuri comments zao wametoa comments nzuri sana na za kweli. Sina uhakika kama viongozi wetu huwa wanasoma blogs.Inaweza kusaidia,wasidharau hizi porojo tunazotoa humu

    ReplyDelete
  9. Huku kwenye nchi zenye highways,free ways sijui na motor ways kila siku tunasikia ajali tena magari 100 yameparamiana,ishu nafikiri hapa ni kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani,na kampeni kubwa zifanyike kuwaelimisha madereva sambamba na kuweka road signs.Nchi yetu ni masikini mpaka sasa hivi less than 10 pecent ya nchi ndio kuna umeme leo hii tunasubiri highway?tutamalizana hapo mpaka hizo highway zije

    ReplyDelete
  10. Kama watu wanapanda magari hivi wanaachiwa. Basi hata ajali ikitokea asilaumiwe mtu. Niliona picha hii kwa blog ya mjengwa nikashangaa. Police wa barabarani wako wapi?????

    http://bp1.blogger.com/_1fXMXYztr0w/SItfC8AltOI/AAAAAAAAJio/MxAltFEbll0/s1600-h/6.JPG

    ReplyDelete
  11. hapa inabidi tuelewe kuwa THE CHEAP IS EXPENSIVE!madereva wengi huwa niwale waliopita njia zapanya kujifunza udereva na kupata leseni,kama dereva angekuwa anahakikiwa kuwakapita ktk chuo stahiki na kuisotea leseni yake,asingekuwa na muda wa kurisk kuipoteza leeni yake,nahii ingechangia kufanya madereva ku wamakini anapo edesha gari. lakini unakuta wikimbili tu mtu yuko ni spana boy mara anaanza kuiba gari wanazotengeneza ili akatest barabarani[hasa vipanya],mara baada ya mwezi huyo-analeseni tena daraja C YA KUSAFIRISHA ABIRIA. unategemea nini???
    wabongo tuna tendency yakujifanya hatujali lakini huwa inatugharimu maranyingi sana!!sindiyo hayo mnayo yaona ktk kila nyanja ya serikali na sekta binafsi longolongo nyingi tu!watu wana vyeti vya kugushi,utakuta kuna wanaume wana vyeti vya jangwani sec,jina la MARIA linageuzwa kuwa MARIO na mtu analamba ajira,matokeo yake ndiyo hayo!maofisa wengine serikalini walipita njia hizohizo za panya sasa mnategemea wasanue liwageukie?? haya bwana,madereva wengine ndugu zao ndiyo walikuwa na leseni lakini wakawa marehemu tayari leseni za marehemu ndizo wanazotumia!!
    KWA UFUPI NI HIVI IKIFANYIKA KUWA KOSA LA UZEMBE BARABARANI DEREVA AKAPOTEZA LESENI MIAKA 5 NA FAINI JUU,AKIHISI CHUNGU ATAKAYO PATA MTAONA AJALI ZINAPUNGUA.
    chibiriti aliwahi kutoa hoja watu wakacheka lakini ilikuwa ya msingi sana.vinginevyo funikeni kombe mwanaharamu apite,leo zamu ya aliyepatwa ajali anaugulia saahizi au kafa tayari,kesho huenda ni wewe!!au unasemaje msomaji??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...