RUBANI MKUU WA ATC KEPTENI GEORGE MAZULA AMEFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAKE MTAA WA NYUMBU, MIKOCHENI, DAR LEO ASUBUHI BAADA YA KUSUMBULIWA NA MATATIZO YA KUPUMUA.
MSEMAJI WA FAMILIA, DK. CHARLES LUGORA, AMESEMA KWAMBA MAREHEMU KEPTENI MAZULA ALIKUWA NCHINI INDIA KIASI CHA WIKI TATU ZILIZOPITA ALIKOKWENDA KUPATIWA MATIBABU YA ATHMA NA ALI;POREJEA ALIKUWA ANAENDELEA VYEMA HADI HALI ILIPOBADILIKA GHAFLA ASUBUHI YA LEO AMBAPO ALIFARIKI DUNIA MILANGO YA SAA NNE UNUSU ASUBUHI.
DR. LUGORA AMESEMA MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAKE NA RATIBA KAMILI ITATOLEWA KESHO.
MAREHEMU MAZULA ALIYEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 59, AMEACHA MKE NA WATOTO WAWILI (BRIAN NA GEORGE). MTOTO WAKE WA TATU, WALTER, ALIUWAWA HUKO MAREKANI SEPTEMBA 2006, AMBAPO YEYE NA MCHUMBA WAKE VONETHA NKYA WALIUWAWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI,
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. my condolescense to the mazula family for all that they are going through in this period may the almighty shine the light on them and keep them safe and strong through this hard time.God bless you all
    yillande bantu

    ReplyDelete
  2. Mungu aiweke roho yako pema anko Mazula. We'll miss you!!

    ReplyDelete
  3. R.I.P Mr Mazula and my condolences to mazula Family

    ReplyDelete
  4. This is really sad. Kazi ya Mungu haina makosa. Brian and George, be strong for your mother.Eternal rest grant to him oh Lord and perpetual light shine upon him. May he rest in peace! Loleni!

    ReplyDelete
  5. Bwana amechukua anachokipenda. Napenda kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu Mazula,Nipigo kubwa sana na pengo lisilozibika. mungu akujazeni nguvu mke na watoto wa marehemu. BWANA AILEZE PEMA ROHO YA MAREHEMU GEORGE MAZULA AMEN.

    ReplyDelete
  6. May the almighty god rest your soul in eternal life.

    ReplyDelete
  7. Sisi Tulikupenda lakini bwana amekupenda zaidi. Ucheshi wako na msaada wote ulioutoa kwa watu wote wakati wa uhai wako hauta sahaulika kamwe. Pole nyingi kwa Mrs. Mazula, Bryan and George Jr. Pole nyingi kwa wote walioguswa na msiba huu mzito. Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa na bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe. Pumziko la milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie, astarehe kwa amani, AMINA.

    ReplyDelete
  8. Jamani, poleni sana sana familia ya Mazula, Mwenyezi Mungu awazidishie nguvu. Pole sana Mama Mazula na wanao jamani.

    ReplyDelete
  9. NAPENDA KUTOA POLE ZANGU ZA THAT KWA KUFIWA NA NA MHESHIMIWA MAZULA. KUKMBUKUMBU ZANGU ZINANIONYESHA NATAKIWA KUTOA POLE KWA SCHOOL MATE WANGU JONGO PRIMARY SCHOOL IFAKARA MOROGORO BWANA STANSLAUS MAZULA AMBAYE TULISOMA NAYE HAPO MWAKA 1986/87. KWA KWELI MIMI BINAFSI NASIKITIKA KWA HALI MBYA YA YA NCHI KWA HAYA MAMBO YA ANGA AVIATION.

    ReplyDelete
  10. poleni mungu awafariji katika kipindi kigumu mungu ashukuriwe ktk kila jambo wabongo london

    ReplyDelete
  11. Pole sana wafiwa mungu awape moyo wa subira, namkumbuka huyu baba alikuwamcheshi hapo kazin hachagui wa kuongea nae ingawa yy ni kampteni lkn pia aliweza kumsaidia kila aliyeweza kumsaidia si kwa pesa bali hata ushauri... kweli vizuri havidumu mungu amlaze mahali panapo stahili...AMIN

    ReplyDelete
  12. Ni vigumu kupokea habari hizi za kusikitisha hasa kwetu siye tuliomfahamu George tangu za udogo wetu hadi kufikia umri huu. Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia ya Mazula popote ilipo.

    ReplyDelete
  13. Looh R.I.P George Mazula.Kazi ya bwana haina makosa.Pole kwa familia yote ya Mazura;
    Mazura:We will miss you George, especially on Dar-Mwz-Dar ATCL flights!.Several times uliokoa maisha ya abiria wako kwenye zile boeing chovu za ATCL.Mangu akulaze mahala pema peponi

    ReplyDelete
  14. Michuzi,my appologies kwa familia na blog,nimekosea kuandika jina la Mazula nikawa naandika Mazura.Lugha yangu ya kienyeji imeniharibu.Again,R.I.P George Mazula

    ReplyDelete
  15. Aunty Harriet pole sana, Mwenyeezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali Pema Peponi Amin

    ReplyDelete
  16. YASSIN MEMBA POPOTE ULIPO TUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MZEE MAZULA. NADHANI UNAKUMBUKA SANA KASHESHE YAKO YA KUTEKA NDEGE YA ATC ILIYOKUWA IKITOKA DAR KWENDA MWANZA NA KUJIKUTA IKITUA LONDON HEATHROW.
    SIJAMSAHAU KISODA NAYE ALIYEZAMIA NA MABOMU YA EMBE DODO AKITISHIA KULIPUA NDEGE YA MZEE MAZULA. MZEE ALIKUWA KIBOKO NA KUWEKZA KUFIKISHA SALAMA ROHO ZA ABIRIA WOTE. MOLA AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YAKE...AMIIIN

    ReplyDelete
  17. ooh this is truelly sad my condolence's to the Mazula family na mungu awape nguvu na baraka wakati huu mgumu.

    ReplyDelete
  18. RIP Captain Mazula...This is very sad news jamani...inatisha watu wanakufa sana siku hizi..too sad...he had a great sense of humour na alikua mtu wa kujichanganya jamani i am still shocked!! my condolenscenses to the mazula family.... i cant begin to imagine what they are going through...poor widow...lost a son....mother in law....now husband..tooo too sad!

    ReplyDelete
  19. poleni sana hiyo ni kazi ya mungu haina makosa

    ReplyDelete
  20. Kwa Niaba ya familia ya Marehemu Capt. Ali Abdi Lesane,tunatuma rambirambi zetu kwa Mama Mazula,Bryan and George, wafanyakazi wote wa ATC PAMOJA NA WATANZANIA WOTE. Mungu amlaze mahali pema peponi. Aamin.

    ReplyDelete
  21. Anon wa 7.47 on 02/08/08unayemwambi Memba atoe pole. Ndege iliyotekwa nyara iliendeshwa na kaka wa marehehu, Capt. Deo Mazula, na haikutua Heathrow bali Stanstead Airport. Ni katika kuweka records sawa tu.

    All the same, rest in peace, our beloved friend and brother. Amen

    ReplyDelete
  22. Natuma pole nyingi kwa Brian na George Mazula. Bwana awape faraja kwani yeye pekee ndiye mfariji wa kweli.Pamoja na familia nzima ya Mazula.
    Be comforted knowing that your father is now with your beloved brother Walter, and he finally know the truth, therefore he has finally found Peace.
    May God rest his soul in eternal peace.
    New York.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...